Mnyika, Zitto wamchezesha kwata Naibu Spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika, Zitto wamchezesha kwata Naibu Spika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Nov 18, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0


  • Wamhenyesha kuvunja kanuni kumbeba Sophia Simba

  Na Salehe Mohamed, Dodoma

  NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai, juzi alianza kuonja machungu ya kiti chake baada ya kukaliwa kooni na wabunge wa CHADEMA kwa madai anakipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, na John Mnyika wa Ubungo, walipinga kitendo cha mbunge wa viti maalum kupitishwa bila kupingwa kuwakilisha Tanzania katika Bunge la nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).

  Mnyika aliomba mwongozo wa Naibu Spika kuhoji ni kanuni ipi iliyotumika kumpitisha Simba ilhali wenzake walijieleza kwa lugha ya Kiingereza na baadaye kupigiwa kura.

  Alisema kanuni za uchaguzi wa wabunge wanaokwenda kwenye vyombo vingine vya uwakilishi kifungu cha 5(2)c kinasema mgombea mmoja wa nafasi inayohusika wabunge watampigia kura za ndiyo au hapana.

  “Mimi napinga Sophia Simba, kutoitwa kujieleza, kuulizwa maswali na kupigiwa kura, kinyume na kanuni ametangazwa na amepita bila kupigwa,” alisema Mnyika.

  Akitoa mwangozo, juu ya jambo hilo Naibu Spika Ndugai, alisema Mnyika yuko sahihi, lakini alichelewa kutoa hoja na Spika wa Bunge, Anne Makinda ndiye aliyeanza mchakato wa uchaguzi kabla ya kumuachia kiti hicho.

  Jibu hilo lilimfanya Zitto na Mnyika kupinga hoja hiyo na kuzua mjadala ambao ulimfanya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Federick Werema kuingilia kati.

  Werema, alisema hoja iliyotolewa na Mnyika ni sahihi lakini haitoweza kujadiliwa au kubadili utaratibu uliofanyika kwa sababu ilichelewa kutolewa.

  Alisema kuwa makundi mengine yalishafanya uchaguzi huo hivyo haitokuwa rahisi kwa Sophia Simba kuitwa kujieleza, kuulizwa maswali na hatimaye kupigiwa kura.

  Maelezo hayo, yalipingwa na Zitto kwa madai kuwa kanuni zimekiukwa na Bunge haliwezi kuendeshwa kwa ukiukaji kanuni au upendeleo kwa chama fulani.

  Mjadala wa kupinga jambo hilo ulizidi kushika kasi na kumfanya Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), kusimama kutoa taarifa kwa mujibu wa kanuni ya 5 (4) inayohusu mamlaka ya Spika.

  Alisema kanuni hiyo, inamtaka mbunge ambaye hataridhika na uamuzi wa Spika kuwasilisha sababu za kutoridhika kwake kwa katibu wa Bunge, ambaye atawasilisha malalamiko hayo kwa Spika.

  Chenge alibainisha kuwa vifungu vidogo vya (5) na (6) vinaeleza Spika atawajibika kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na kulijulisha Bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa na kamati.

  Aliongeza kuwa Spika au Naibu wake hawatakuwa wenyeviti wa kikao hicho, ili kutoa nafasi na haki kwa shauri husika kusikilizwa.

  Aliongeza kuwa majibizano kati ya kiti (Spika au Naibu Spika) na baadhi ya wabunge kutokana na uamuzi wa Spika hayana nguvu.

  Zitto aliinuka na kumjibu Chenge kuwa Kamati ya Kanuni za Bunge bado haijaundwa, hivyo hawawezi kuwasilisha taarifa ya kutoridhishwa kwake.

  Akizungumzia kuhusu uadilifu kwa kiongozi wa Bunge (Spika, Naibu wake au wenyeviti wa Bunge), kwa kutumia kanuni ya nane, inayozuia upendeleo, Zitto alitaka Sophia ajieleze na apigiwe kura.

  Mjadala huo ulihitishwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ambaye aliwaonya wabunge wanaotaka kucheza na mamlaka ya Spika au Naibu Spika kujirekebisha mara moja, ili kuepuka adhabu.

  Mjadala huo, ulisababishwa na uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la SADC.

  Aliongeza kuwa mabishano hayo yanapaswa yachukuliwe na wabunge wapya kwa umakini mkubwa hasa kwa kusoma sheria na kanuni za kudumu za Bunge.

  Pamoja na Sophia, wajumbe wengine wa Bunge la SADC-PF ni Mohammed Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF), ambaye baada ya kutangazwa mshindi kwa kura 275 dhidi ya kura 47 za mgombea wa CHADEMA, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

  Mwingine ni Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (CCM) aliyepata kura 180. Waliopiga kura walikuwa wabunge 324.

  Chanzo: Tanzania Daima.
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,676
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mambo mengine yanatia hasira kuyafikiri. Ngoja kwanza nikapige Cannabis Sativa alafu ndo nirudi kuchangia. Watu wanavunja sheria kama wapendavyo
   
 3. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Haya ndo tunayoyategemea kutoka kwa wabunge wa Chadema, Hadi raha mwaka huu watakoma walio wavivu wa kusoma kanuni na wanokwenda kinyume na kanuni na sheria za nchi.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,394
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mh Sophia Simba si angejieleza tuu kwa kiswahili kwani Kiingereza siyo lugha yetu badala ya kutumia mbinu ya kupita bila kupingwa
   
 5. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  naona ubabe na kutishana kumeanza mapema sasa nani anachezea mamlaka ya spika? kuwataka wafuate kanuni inakuwa kuchezea mamlaka ya spika? wanawake nakubali wanaweza lakini anne makinda haliwezi hili bunge na ataharibu sna you just wait and see.
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0

  sophia hajui kiingereza jamani sasa atazungumza kisambaaaaaaaaaaaaa???????
   
 7. e

  ejogo JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa kama hajui kujieleza kwa kiingereza huko sadc si atakuwa bubu muda wote! Maana si muda wote watakuwa wanavaa ile vitafsiri kama kweli vipo. Au atakuwa anakula perdiem tu za sadc!! haya mambo ya upendeleo lazima yawe yanaangaliwa vizuri.
   
 8. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli ipo kwa hiyo hapo watakuwa wanaanzisha mjadala spika anaanza then anamwachia spika naibu ili amalizie kwa kuvunja kanuni...
   
 9. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,698
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Big Up Zitto na Mnyika.

  Mmewakilisha vema sana.

  This sends a very strong signals to Speaker na wasaidizi wake kuwa this time hali si shwari na hakuna kuburuzwa.

  Mzee 6 angekuwa poa katika mambo kama haya kwani hata CHADEMA wanamkubali.

  Namtabiria Spika kutokumaliza kipindi chake cha miaka 5 kabla hajaachia ngazi. Vinginevyo vilio kwake viko njiani kwa hoja za nguvu. Na hapo bado kashfa hazijaibuliwa as follows:

  1. Muungano fake na Zanzibar
  2. Kashfa ya Magereza
  3. Kashfa ya serikali kutumia pesa katika Uchaguzi kwa aajili ya CCM
  4. matokeo ya Uchaguzi kuchakachuliwa
  5. katiba mpya . . .

  Jamaa wajipange tu maana nahisi Tundu Lissu na Zitto wameshaanza kukusanya vielelezo.

  QED
   
 10. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Waheshimiwa,

  Nilileta thread ya kuhusu kumwajibisha spika lakini ioneni nimeiweka hapa na tuone ambavyo hakuna hata mmoja anayechangia:

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/88311-spika-huadhibiwa-kwa-utaratibu-gani.html

  Kama na sisi humu JF michango yetu haitaji kanuni inaonyesha jazba na utani basi bungeni tusitegemee bungeni iwe hivyo.

  Binafsi sijui spika anawajibishwa vipi ndiyo maana nikaleta hii hoja nisaidiwe kuelewa lakini inaelekea nitaendelea kutoelewa.
   
 11. m

  mbeshere Member

  #11
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhambi ya Samwel 6 inawatafuna CCM ,Hakuna jibu atakalotoa Spika wa Bunge la 10 wabunge wasihoji kila atakalo sema ni kioja...subirini muone
   
 12. k

  ktman Member

  #12
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Spika wa sasa anakariri sheria hana tofauti na Msekwa ,wote hawa hawana flexibility katika kuendesha mijadala kama alivyokuwa Mzee 6 KWA sababu hawajui sheria . Huyu Mama Makinda akiulizwa swali kuhusu Sheria na Kanuni za Bunge mpaka na yeye aliulize tena ndipo atoe jibu. Siku hao washauri wakiungua vichomi itakuwaje ? huenda PM aka Mtoto wa Mkulima atamsaidia ! haijulikaniki
   
 13. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,054
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  HAWA WATU WANAUSHANGAZA UMMA!
  MHESHIMIWA ANAWAKOSOA,NA WANASEMA YUKO SAHHI,LAKINI AMECHELEWA...JE NI KANUNI GANI WANATUMIA KUMWAMBIA AMECHELEWA....HAWANA HATA KANUNI MOJA WANAYOTUMIA.badala yake wanakuja kwa vitisho,kuwa rungu la spika litawarukia km wataendelea kukosoa....SHAME UPON THEM...VIJANA ENDELEA KUREKEBISHA TABIA ZA HAO JAMAA....WOTE WAWILI SPIKA NA NAIBU WAKE HUWA WANA MAASIRA YASIYOKUWA NA MAANA.
   
 14. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,513
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakuambia SUPERMAN unaloongea ni kweli huyu mama hamalizi miaka mitano.....wananchi tushawasoma CCM hakuna kitu...CCM inakufa CCM inakufa....Mafisadi wanakufa mafisadi wanakufa.....CCM kwishny.....CCM kwishny.......Yaani mapema kabisa Spika na naibu wake washaanza kuchemsha....Watapigwa ngumi mwaka huu....... Wajinga kabisa hawa......wanafikiria Watanzania wa sasa ni wale wa Enzi za Mwalimu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!CHADEMA kazeni buti tu. Nyie ndo Chama muafaka wananchi wameshawasoma...Hatakama wenzeni wengine wa upinzani watakuwa mamluki kazeni buti wananchi tupo nanyi...ILa chonde kama kuna viongozi wazuri CCM kama si wabinafsi msiwahikie...alimradi tu wamnaungana nanyi Kupinga Mafisadi...
   
 15. B

  BASIASI JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 2,546
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 160

  JAMANI SHUKURUNI AKUJIELEZA HUYU MAMA ANAONGEAGA UPUPU MAISHA YAKE YOTTTTTTTTEE
  SASA NAHISI MH ALIAMUA KUMHIFADHI ALAFU ANGALIA MIPUMBAVU IKIWEMO MWANASHERIA MKUU INAKIRI KUVUNJWA KWA SHERIA NA KUDAI IMECHELEWA PAMBAFU KUBWAAA NDIO MAANA WAMEAMBIWA MWAKA HUU WATATIA ADABU HILO SIO BUNGE LA WAVAA SKETI KAMA WALIVYOKUWA WAKILIZOEA,,ANGALIA HILI PUMBAFU NDUGAI LINATISHIA ATI WAWE NA ADABU HANA ADABU TENA AKOME KUCEHEZEAS WABUNGE ASITISHIE ADHABU AKAFIKIRI YUKO NA WATOTO WADOGO
  mBAFUUUUUUUUU
   
 16. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2010
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 5,822
  Likes Received: 5,334
  Trophy Points: 280
  Ila Chenge pamoja na kasfa yake jamaa Sheria imelala pale. Nafikiri kuwemo kwake bungeni kunasaidia sana kuyaweka vyema masuala mbalimbali ya kisheria.
   
 17. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani sasa kuna matatizo makubwa sana kwenye sheria na kanuni hizi za bunge. Nikirejea siku ile ya hoja ya Serikali kuhusu pendekezo la Rais kwa ajili ya jina la waziri mkuu, Mh.Tundu Lissu alitaka mwongozo wa spika katika suala la kanuni inayotaka hoja yoyote ya serikali inapowasilishwa bungeni kwamba lazima lijadiliwe bungeni na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni atoe mchango wake. Moja ya majibu ya spika yalikuwa kwamba serikali haipo(kama serikali haipo kwanini Mwanasheria Mkuu alisimama na kuwasilisha suala lile kama hoja ya serikali?)

  Leo Chenge anasema;"...kuwa vifungu vidogo vya (5) na (6) vinaeleza Spika atawajibika kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na kulijulisha Bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa na kamati."

  Kuhusu hoja ya Zitto kuhusiana na Kamati za Kanuni za Bunge kama ilivyo hapo juu ni kuwa kamati hazijaundwa. Hiyo haki ambayo wabunge wanatakiwa kuwa nayo itatolewa vipi?

  Ina maana kuwa wakati tunafanya uchaguzi na kuunda bunge haijulikani kuwa vitu gani vinatakiwa kuwepo ili utendaji wa bunge uwe sawa. Kwanini kanuni zinadai vitu ambavyo vinaonekana kuwa haviwezi kutekelezwa wakati huu? Iweje kanuni idai kuwa mbunge asiporidhika apeleke malalamiko kwenye kamati ambapo kamati yenyewe haipo?
   
 18. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,084
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  mjengoni wanasheria kibao, wengine nachuna tu
   
 19. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,200
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Pamoja na Sophia, wajumbe wengine wa Bunge la SADC-PF ni Mohammed Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF), ambaye baada ya kutangazwa mshindi kwa kura 275 dhidi ya kura 47 za mgombea wa CHADEMA, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

  jamani mmeona hili nalo, jamaa wa CUF aliungwa mkono na wabunge wote wa CCM, ni tafsiri sahihi ya ndoa ya ccm na cuf..... tafakari chukua hatua!!!!!!
   
 20. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Safi sana hii. Mnyika, Zitto, Tundu Lissu, Mdee na wengineo, haya ndio yanahitajika bungeni ili kila siku watanzania wafumbue macho na kuona huu Upupu ambao ni sehemu ya Utawala wetu. Migongano hii itawasaidia watanzania kuona aina ya viongozi wanaowatawala. leo ni 'hoja imechelewa kutolewa' utadhani kuna time frame inatubana, kesho itakuwa sababu nyingine tena lakini mwisho wa siku watakosa sababu na nina uhakika kwa asimilia Mia moja kwamba wataanza kukacha Bunge na kuwaachia wasaidizi wao kukiona cha moto! Namuunga mchangiaji alieyesema hapa kuwa mama huyu hatachukua round Bungeni. Kuna mahali atalazimika tu kujiuzulu. Hakuna binadamu (tena Mzee!) mwenye usugu wa kudumu dhidi ya 'kudhalilishwa na 'watoto' (soma, wabunge vijana!)!!
   
Loading...