Mnyika, Zitto na Regia: Tupeni mchanganuo wa hela zinazolipwa kwa Mbunge ili tujue

watanzania wanaishi under a dollar a day.....wabunge wanaishi under a thousand dollars a day.....kaazi kweli kweli
Sasa kama unajua hiko kinachokufanya u'support kuwa waendelee kulipwa hivyo ninini!..wanaishi nchi tofauti na wengine?
 
acha matusi wewe, mbunge anakazi kubwa kuliko mwalimu wa secondary......usimfananishe mkulima na daktari....sio tu kwa sababu mkulima anakaa kwenye jua siku nzima basi ndio mchapa kazi bora zaidi.

wabunge wanafanya maamuzi ambayo yana immediate effects kwa kila mwananchi.....si unaona DOWANS na mengineyo?

Sijuikitu

Nashukuru kwa kukubali mwenyewe kwamba hujui kitu na jamvi hili la siasa is too far for your understanding . Kinachojadiliwa sio maamuzi yao yana immediate effect or not bali posho zao . Hata kama wanamaamuzi ambayo yana immediate effect haiwapi rungu la kuchukua posho za kinyonyaji tena zilizokwepeshwa kodi . Na hata wanayoongea bungeni yanabaki tu kwenye kumbukumbu za bunge sioni action yeyote.Kumdharau mwalimu wa sekondari ni tusi.Kila mtu ana nafasi yake kwenye hili gurudumu la maendeleo mbunge na mwalimu halikadhalika.Na kila mtu akiwa kwenye utekelezaji wake lazima apate ujira ulio haki na ambao hataona haya kuutamka azarani.
 
JF mods huwa wanamwaga hapa mi data ya kutisha bila ya uoga wowote despite being socially recognised. hao ndio watu unaojua wana principles for what they stand for.

Sasa hawa jamaa wana nafasi ya kuwa 'Have-a-go heroes' lakini wapi. Ni maslahi tu amna hata mmoja kumbe mwenye machungu ya kweli, i for once do not believe wanashindwa kuja kusema walichoulizwa mbona huwa wanajibu vingine visivyo takiwa kusemwa: talk about hypocricy.

For gods sake! it only takes five minutes these days to be a new member, how about a new Id to answer the posed questions?

After all it is in the interest of the public they so claim to represent, why not answer then.
 
Najaribu tuu kukupa msaada kama ulivyoomba mkuu!
Nimejaribu kusoma between lines maelezo ya Mh. Regia,Kwanza nimpongeze kwa quick response. Mie, kwa kumfahamu yeye na kuongeza kidogo common sense ya siasa,naona kitu tofauti kabisa na kile ambacho wachangiaji wengi humu wameona kuwa ni WOGA wa Regia kwa hiyo kamati ya maadili. Hivi kama anaiogopa, angeuliza kwenye semina elekezi?...angeeleza humu ndani kuwa alipewa ",majibu yasiyoridhisha"?...angeonesha msimamo ule tunaouona bungeni?...Hazikutani hapa!
Ninachokiana mie ni ukomavu wa kisiasa wa huyu dada. Ametumia tu sheria na taratibu zinazotawala sasa (si lazima ziwe sahihi zote) kutoa taarifa bila kutoa telling statement prematurely. By,the way...kutaja tu maslahi hayo bila chochote kufuatia (ukizingatia awkwardness ya hayo maslahi),nadhani si jambo ambalo mwanasiasa yeyote makini angetaka kufanya. Hivyo anaelewa fika kuwa muanzisha sred alitaka zaidi ya figures tu za hayo mapesa. Naziona sababu kadhaa za kutotoa taarifa zilizoombwa hapa au kutoa KAULI thabiti kuhusiana na hilo kwa sasa,na hapa:

  1. Nafahamu hili ni suala nyeti ambalo wakati mmoja liliibua mjadala mzito bungeni kutokana na hoja fulani ya Dr. Wilbroad Slaa (heshima kwake) katika awamu iliyopita. Nafahamu hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa mpaka sasa. Nafahamu Dr. Slaa ni Katibu mkuu wa CDM na naamini suala hilo lazima litakua moja ya mambo ambayo yanaundiwa mkakati kichama. Kama hilo ni kweli au linakaribiana na ukweli basi nadhani hapa hapakua mahala sahihi kwake yeye binafsi kuchukua hatua yeyote advanced zaidi.
  2. Kama hakuna mkakati wa kichama katika hilo,na amedhamiria kulishughulikia mwenyewe (which is also fine),hahitaji kujiweka mtegoni mapema kwa "kukiuka" kanuni za kutotoa siri na kukaribisha vita nyingine isiyo ya maana juu ya vita yenyewe ya msingi . Njia sahihi zaidi ingekua ni kujenga hoja katika platform rasmi,hoja ya kulazimisha kutengua kipengele cha utaratibu wa usiri;na kwa namna hiyo angepata support kubwa zaidi na taarifa hizo zingefika tuu kwa wahusika wote (WANANCHI) ambao muanzisha thread alitaka wazipate
  3. Kama si yeye peke yake,basi namna nyingine ingekua ni ku-form a movement like in G 55,na kuwamobilize wabunge wote wenye mawazo kama yake na kulipeleka mbele baada ya kupata common stand. Hili pia lingemlazimu kutokulianzisha kwanza humu.
  4. Ili kuepuka kuambiwa amedanganya, ingemlazimu kuwa na taarifa sahihi sana za maslahi hayo,maana si wote wana maslahi sawa na si rahisi kujua details za maslahi ya wote. Angetaja za kwake tu,pamoja na suala la kukiuka taratibu,angeambiwa amesema uongo.
  5. Ni tabia fulani ya SIASA duniani kote kuwa mtu angependa ku-stand-out na kujitofautisha na wengine kwa makusudi,ili apate umaarufu.Mathalani Mtu anaweza kuamua kutaja mali zake zile kidogo,kisha anawapandia wengine wataje haraka,tena anawauliza mbele za watu wengi,ili aonekane muadilifu sana. Mwanasiasa mkomavu na mwadilifu hategwi na mtego huu. Atafanya lile analoamini kuwa lafaa kwa wakati wake,si kwa ajili tu ya "kujibu mapigo"
Mwisho naamini kiongozi mzuri atapimwa kwa uwajibikaji wake, maadili yake safi na uwezo wake wa kuonesha njia kwa usahihi.Mengine nyongeza.
Asante
Hivi kama mtu anataka kuleta mabadiliko lakini anaogopa kusemwa na kamati ya maadili, hapo nasikia kizunguzungu naomba msaada
 
na wewe unaweza kutoa mchanganuo wa mshahara wako kwanza?

huu ndio ujinga unaotumaliza Tanzania. Wewe pesa yako hutaki kujua matumizi yake? Kama kiongozi wa umma ninayemlipa mshahara mimi na hataki nijue mshahara wake, basi anapaswa kuachia ngazi!
 
Msando.Heshima Mbele!How are you?

Nimeisoma sredi yako nimekupata,nimekuelewa.Kimsingi nakubaliana na hoja yako na uko sahihi kutaka kujua maslahi ya wabunge kwakuwa sisi ni wawakilishi wa wananchi.Lakini kwakuwa nchi yetu imejengwa kwa mgumo wa usiri katika mambo mengi na ndio maana utakuta hata mke hajui mshahara wa mumewe na wako kwenye ndoa zaidi ya miaka 50 na watoto nao hivyo hivyo hawajui kipato cha wazazi wao n.k.Kumekuwa na utamaduni wa watu kutokutaka kuweka wazi vipato vyao bila sababu za msingi.Binafsi huwa sielewi hasa kwanini iwe hivi.

Binafsi napenda sana kuweka wazi vyanzo vya mapato yangu na wakati nikiomba kura Kilombero niliweka wazi jumla ya mapato ya Mbunge kwa mwezi na kimsingi nilikuwa napingana na malipo haya.Hivi sasa nimekuwa Mbunge ninafungwa na Kanuni za Bunge za kutotoa siri za Bunge.Wakati tuko kwenye Semina Elekezi Ubungo Plaza tuliwekwa wazi kuhusu mapato ya Mbunge na Spika alisisitiza sana kuhusu usiri.Nilipata nafasi ya kuhoji kwanini kuwe na usiri katika mapato yetu sikupatiwa majibu ya kuridhisha,kimsingi hakuna hoja za msingi ila ni woga tu.Spika alisisitiza kwa yeyote atakayetoa siri atawajibishwa na Kamati ya Maadili.Lema aliweka wazi kuhusu mikopo ya Magari ya Shilingi milioni 90 analaumiwa sana including baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.Kwa bahati mbaya sana sina ID nyingine humu JF zaidi ya hii ya jina alangu halisi hivyo siwezi kuweka wazi hapa mbele ya kadamnasi na kwakufahamu fika kuwa humu wako members wakila aina including wabunge na viongozi wengine hivyo nisije nikachukuliwa hatua za kinidhamu unnecessarily.Ila tukiwa nje ya jukwaa hili nitaweka wazi kila kitu iwe kwako au kwa mwingine yeyote atakayehitaji.

Naamini umenielewa na tutawasiliana kwa njia nyingine.

Aluta Continua.
Kutoka Ofisi za Bunge Dsm
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira.

Jibu lako lina ukweli. Kwa hiyo sasa unatushauri sisi wananchi tufanyaje kusudi tuweze kujua matumizi halisi ya pesa yetu. Maana sasa mnategeuza kuwa wajinga. Pesa ya kwetu mnatunyima kujua tunawapa kiasi gani? Ningependa kuona Chadema wanasimama na kupinga hili. Je wataweza kuwapeleka kwenye kamati ya maadili wote? Kwa nini msije na mtoko wa mabadiliko?
 
nimeipenda sana hii thread. Hii inaleta hatua kubwa sana ya maendeleo ya fikra Tanzania. Bwana Msando nakupa pongezi kubwa! U r my hero for today.
 
Kama mnashindwa kutetea haki ya wananchi kujua pesa wanazowalipa wawakilishi wao, mtaweza kupigania katiba mpya yenye maslahi kwa taifa?!!!
 
JF mods huwa wanamwaga hapa mi data ya kutisha bila ya uoga wowote despite being socially recognised. hao ndio watu unaojua wana principles for what they stand for.

Sasa hawa jamaa wana nafasi ya kuwa 'Have-a-go heroes' lakini wapi. Ni maslahi tu amna hata mmoja kumbe mwenye machungu ya kweli, i for once do not believe wanashindwa kuja kusema walichoulizwa mbona huwa wanajibu vingine visivyo takiwa kusemwa: talk about hypocricy.

For gods sake! it only takes five minutes these days to be a new member, how about a new Id to answer the posed questions?

After all it is in the interest of the public they so claim to represent, why not answer then.

Mh.Regia hakuwa na sababu ya kusema eti anaogopa ID yake,
je hatambui wanausalama tupo nao hapa jamvini?
Hajui wabunge tupo nao humu jamvini kwa anonymous ID?
Hajui wanataaluma wote tunao hapa jamvini kwa ID tofauti?
Hapa ni rika zote, taaluma zote, sekta zote etc...

Sikuona sababu ya eti 'ID', hapana kwa hilo umeteleza...haileti mantiki yakinifu.
 
Mmmh....... nimefatilia sana mjadala huu' baada ya kusoma coment zote kutoka kwa
wachangiaji akiwemo Dada R.Mtema,nimepata jibu moja tu -KWELI SIASA NI MCHEZO
MCHAFU SANA! Pia nafikiri baadhi ya wabunge wa CDM wako kimaslai kama wabunge
wa ccm. Kweli tunakazi kubwa sana ya kuikomboa nchi yetu! mh....hatari sana
 
Mh.Regia hakuwa na sababu ya kusema eti anaogopa ID yake,
je hatambui wanausalama tupo nao hapa jamvini?
Hajui wabunge tupo nao humu jamvini kwa anonymous ID?
Hajui wanataaluma wote tunao hapa jamvini kwa ID tofauti?
Hapa ni rika zote, taaluma zote, sekta zote etc...

Sikuona sababu ya eti 'ID', hapana kwa hilo umeteleza...haileti mantiki yakinifu.
Mkuu hapo umepigilia msumari wa mwisho na wa kweli! Hatamie sikubalianinae anaposema ID
maana anauwezo wa kumwaga hapa jamvini kilakitu kwa kutumia ID fake
 
Mh Regia kasema ukweli, wabunge wengu njaa tuu, hawana lolote..including CHADEMA, CCM etc... wote mate yanawatoka.
 
Mkombozi wa nchi hii sijui atatoka wapi?

Kila tunayemuona labda atakuwa mkombozi naye akifika huko anaonjeshwa na kuishia kuwa kama wao!

Narudia kusema tena; Wabunge wote ni wachumia tumbo na mara zote wanaungana inapofika mijadala ya masilahi yao!

Kwangu mbunge alikuwa Dr. Slaa, nakumbuka alipowaambia wabunge wenzake kuwa hela wanayolipwa ni nyingi sana alishambuliwa kutoka kila kona. Na ni kutokana na kitendo hicho, nilimwona tofauti na wengine wote wanaojiita wakombozi wetu.

Kama wanadhani hiyo hela ni halali iweje wachukie wakisikia mtu anasema wamepewa mil. 90 kwa ajili ya magari! Shame on you!
 
Ndugu zangu wanaJF. Salaam.
Nimesoma kila mchango kwenye sredi hii kwakuwa sredi hii inanihusu moja kwa moja.Ninaelewa hoja zenu na nina washukuru wote kabisa mlionielewa na msionielewa.Kuna mambo kadhaa naomba niyaweke sawa.
1.Kuna watu hapa baada ya kusoma post niliyorusha mmelaumu kwa kusema ninakwepa kusema ukweli.Kundi hili nadhani halikunielewa nilichosema,nimesema wazi kabisa nje ya jukwaa hili naweza kusema na nikampa fursa mrusha sredi anitafute kwa njia nyingine.Alberto ana access namimi kwa kiasi kikubwa tu angeweza kunipata na ningempa mchanganuo wote including access ya kiwango cha juu cha mkopo kwa Mbunge kwenye benk.

2. Kuna wengine wamesema nitumie au ningetumia ID ya siri na kuna wengine wamesema eti kutokuwa na ID nyingine ni danaganya toto lakini ukweli ni kwamba sina ID nyingine kwasababu zifuatazo ninaamini kabisa nikiwa na ID nyingine na nikawa na post sredi mbalimbali hapa ndani ya wiki mbili tu nitakuwa nimeshajulikana.Nilipokuwa natumia jina la siri enzi hizo kama Gender Sensitive kuna watu wengi tu walikuwa wameshafahamu GS ni nani.The problem niko muwazi sana na siwezi kujificha wala kupretend hivyo nitajisumbua tu kuwa na ID za siri,sioni sababu.Baada ya kuwa Mbunge kuna baadhi ya watu walinishauri niwe na hayo maID ya siri lakini nikaona nitakuwa mtumwa tu,kwnini nijifiche?namdanganya nani?naogopa nini?

3.Kuna watu hapa wanasema kuwa naogopa kuwajibishwa na Kamati ya Maadili inakuwaje naogopa kusemwa tu?ndugu zangu mnachukulia kuwa hili suala ni dogo sana,sio dogo kama mnavyodhani.Ninachokataa hapa nikuvunja kanuni kwenye forum kama hii.Nimesema wazi kuwa nje ya hapa sitaficha.

4.Kuna kitu nimejifunza hapa, kuna watu wanashangaa mimi kuogopa kuwajibishwa na kamati ya maadili lakini wengi wao wako na majina ya siri,kwanini mnajificha,manogopa nini?si angalau mimi niko na jina langu halisi na ninafahamu fika kwamba kila ninapopost kitu sio wote watakao kipokea positively,ninafahamu fika nitakumbana na changamoto mbalimbali but altleast siziogopi na ninaziface.Jamani tafakarini kwa kina.

5. Kuna watu hapa wamesema kuwa eti linapokja suala la fedha basi wote tunakuwa na sauti moja ndio maana sijasema mchanagnuo wa mapato ya Wabunge.Jamani hili si kweli.hivi mmetafakari kwa kina?hivi kwani nikisema hapa ndio hayo mapato ya wabunge yatasitishwa?kwani mjadala umeanza leo?kutosema kwangu hapa hakumaanishi kwamba eti nahofia mapato yangu la hasha.Mkumbuke maslahi ya wabunge yanaamuliwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kupitia kamati husika then Rais ndio mwamuzi wa mwisho.Tunaweza kabisa kuja na hoja za msingi kabisa za kujipangia mapato manono kabisa na wananchi wakabaki kusononeka tu,everything can be justifiable.Hivi kuna mangapi humu tumeyajadili,je yametekelezeka?kiwapi kilio chetu cha DOWANS?Mijadala yetu humu imeiondoa DOWANS?jamani tuwe tunatafakari kwa kina,msituhukumu eti kwakuwa hatujasema posho zetu hapa basi hatufai.Tusem,tusiseme haitabadilisha.Tunafuata kanuni kwenye jukwaa kama hili.Nje ya hapa mimi sifichi ndio maana wananchi wangu wa Kilombero ambao walibahatika kuhudhuria kwenye mikutano yangu wanafahamu Mbunge wao ninalipwaje.

6. Napenda kufahamu hivi humu ni wangapi wake au waume zao au watoto wao au wazazi wenu wanafahamu mishahara yao?

7. Kuna watu humu wametoa mfano niliposimamia msimamo wangu kuhusu tofauti ya PHD na First Degrees,Bungeni ninalindwa na Kanuni za Bunge,ninaweza kukubali au kukataa mwongozo wa Spika kama nilichokisema ndicho ninachokiamini na ndivyo ilivyokuwa.Hapa siwezi kuikwepa Kanuni ya kutotoa siri za Bunge.

Aluta Continua
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira
 
asante sana Regia Mtema ..nimekusoma ... kiukweli na uwazi kinachoonyesha hapa kuna uwalakini wa kanuni gandamizi za mfumo mbaya katika bunge

god bless you and your transparency towards facts and fictions
 
Ndugu zangu wanaJF. Salaam. Nimesoma kila mchango kwenye sredi hii kwakuwa sredi hii inanihusu moja kwa moja.Ninaelewa hoja zenu na nina washukuru wote kabisa mlionielewa na msionielewa.Kuna mambo kadhaa naomba niyaweke sawa. 1.Kuna watu hapa baada ya kusoma post niliyorusha mmelaumu kwa kusema ninakwepa kusema ukweli.Kundi hili nadhani halikunielewa nilichosema,nimesema wazi kabisa nje ya jukwaa hili naweza kusema na nikampa fursa mrusha sredi anitafute kwa njia nyingine.Alberto ana access namimi kwa kiasi kikubwa tu angeweza kunipata na ningempa mchanganuo wote including access ya kiwango cha juu cha mkopo kwa benk kwenye benk. 2. Kuna wengine wamesema nitumie au ningetumia ID ya siri na kuna wengine wamesema eti kutokuwa na ID nyingine ni danaganya toto lakini ukweli ni kwamba sina ID nyingine kwasababu zifuatazo ninaamini kabisa nikiwa na ID nyingine na nikawa na post sredi mbalimbali hapa ndani ya wiki mbili tu nitakuwa nimeshajulikana.Nilipokuwa natumia jina la siri enzi hizo kama Gender Sensitive kuna watu wengi tu walikuwa wameshafahamu GS ni nani.The problem niko muwazi sana na siwezi kujificha hivyo nitajisumbua tu kuwa na ID za siri,sioni sababu.Baada ya kuwa Mbunge kuna baadhi ya watu walinishauri niwe na hayo maID ya siri lakini nikaona nitakuwa mtumwa tu,kwnini nijifiche?namdanganya nani?naogopa nini? 3.Kuna watu hapa wanasema kuwa naogopa kuwajibishwa na Kamati ya Maadili inakuwaje naogopa kusemwa tu?ndugu zangu mnachukulia kuwa hili suala ni dogo sana,sio dogo kama mnavyodhani.Ninachokataa hapa nikuvunja kanuni kwenye forum kama hii.Nimesema wazi kuwa nje ya hapa sitaficha. 4.Kuna kitu nimejifunza hapa, kuna watu wanashangaa mimi kuogopa kuwajibishwa na kamati ya maadili lakini wengi wao wako na majina ya siri,kwanini mnajificha,manogopa nini?si angalau mimi niko na jina langu halisi na ninafahamu fika kwamba kila ninapopost kitu sio wote watakao kipokea positively,ninafahamu fika nitakumbana na changamoto mbalimbali but altleast siziogopi na ninaziface.Jamani tafakarini kwa kina. 5. Kuna watu hapa wamesema kuwa eti linapokja suala la fedha basi wote tunakuwa na sauti moja ndio maana sijasema mchanagnuo wa mapato ya Wabunge.Jamani hili si kweli.hivi mmetafakari kwa kina?hivi kwani nikisema hapa ndio hayo mapato ya wabunge yatasitishwa?kwani mjadala umeanza leo?kutosema kwangu hapa hakumaanishi kwamba eti nahofia mapato yangu la hasha.Mkumbuke maslahi ya wabunge yanaamuliwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kupitia kamati husika then Rais ndio mwamuzi wa mwisho.Tunaweza kabisa kuja na hoja za msingi kabisa za kujipangia mapato manono kabisa na wananchi wakabaki kusononeka tu,everything can be justifiable.Hivi kuna mangapi humu tumeyajadili,je yametekelezeka?kiwapi kilio chetu cha DOWANS?Mijadala yetu humu imeiondoa DOWANS?jamani tuwe tunatafakari kwa kina,msituhukumu eti kwakuwa hatujasema posho zetu hapa basi hatufai.Tusem,tusiseme haitabadilisha.Tunafuata kanuni kwenye jukwaa kama hili.Nje ya hapa mimi sifichi ndio maana wananchi wangu wa Kilombero ambao walibahatika kuhudhuria kwenye mikutano yangu wanafahamu Mbunge wao ninalipwaje. 6. Napenda kufahamu hivi humu ni wangapi wake au waume zao au watoto wao au wazazi wenu wanafahamu mishahara yao? 7. Kuna watu humu wametoa mfano niliposimamia msimamo wangu kuhusu tofauti ya PHD na First Degrees,Bungeni ninalindwa na Kanuni za Bunge,ninaweza kukubali au kukataa mwongozo wa Spika kama nilichokisema ndicho ninachokiamini na ndivyo ilivyokuwa.Hapa siwezi kuikwepa Kanuni ya kutotoa siri za Bunge. Aluta Continua Regia E Mtema Waziri Kivuli Kazi na Ajira
Mheshimiwa Regia umejitahidi sana kuwa muwazi juu ya jambo hili, tofauti na baadhi ya wengi wetu walivyokuelewa asubuhi ya leo...
Aksante kwa kurudi tena kufuta kiu kubwa ya wanajamii, na kupangua hoja zote zilizokuwa pending hapa...
Nadhani sasa kazi inabaki kwetu zaidi@Msando, naomba do the needful, ili tuache ku'speculate!
Yatosha Regia, binafsi nimeridhika.
 
Ndugu zangu wanaJF. Salaam. Nimesoma kila mchango kwenye sredi hii kwakuwa sredi hii inanihusu moja kwa moja.Ninaelewa hoja zenu na nina washukuru wote kabisa mlionielewa na msionielewa.Kuna mambo kadhaa naomba niyaweke sawa. 1.Kuna watu hapa baada ya kusoma post niliyorusha mmelaumu kwa kusema ninakwepa kusema ukweli.Kundi hili nadhani halikunielewa nilichosema,nimesema wazi kabisa nje ya jukwaa hili naweza kusema na nikampa fursa mrusha sredi anitafute kwa njia nyingine.Alberto ana access namimi kwa kiasi kikubwa tu angeweza kunipata na ningempa mchanganuo wote including access ya kiwango cha juu cha mkopo kwa benk kwenye benk. 2. Kuna wengine wamesema nitumie au ningetumia ID ya siri na kuna wengine wamesema eti kutokuwa na ID nyingine ni danaganya toto lakini ukweli ni kwamba sina ID nyingine kwasababu zifuatazo ninaamini kabisa nikiwa na ID nyingine na nikawa na post sredi mbalimbali hapa ndani ya wiki mbili tu nitakuwa nimeshajulikana.Nilipokuwa natumia jina la siri enzi hizo kama Gender Sensitive kuna watu wengi tu walikuwa wameshafahamu GS ni nani.The problem niko muwazi sana na siwezi kujificha hivyo nitajisumbua tu kuwa na ID za siri,sioni sababu.Baada ya kuwa Mbunge kuna baadhi ya watu walinishauri niwe na hayo maID ya siri lakini nikaona nitakuwa mtumwa tu,kwnini nijifiche?namdanganya nani?naogopa nini? 3.Kuna watu hapa wanasema kuwa naogopa kuwajibishwa na Kamati ya Maadili inakuwaje naogopa kusemwa tu?ndugu zangu mnachukulia kuwa hili suala ni dogo sana,sio dogo kama mnavyodhani.Ninachokataa hapa nikuvunja kanuni kwenye forum kama hii.Nimesema wazi kuwa nje ya hapa sitaficha. 4.Kuna kitu nimejifunza hapa, kuna watu wanashangaa mimi kuogopa kuwajibishwa na kamati ya maadili lakini wengi wao wako na majina ya siri,kwanini mnajificha,manogopa nini?si angalau mimi niko na jina langu halisi na ninafahamu fika kwamba kila ninapopost kitu sio wote watakao kipokea positively,ninafahamu fika nitakumbana na changamoto mbalimbali but altleast siziogopi na ninaziface.Jamani tafakarini kwa kina. 5. Kuna watu hapa wamesema kuwa eti linapokja suala la fedha basi wote tunakuwa na sauti moja ndio maana sijasema mchanagnuo wa mapato ya Wabunge.Jamani hili si kweli.hivi mmetafakari kwa kina?hivi kwani nikisema hapa ndio hayo mapato ya wabunge yatasitishwa?kwani mjadala umeanza leo?kutosema kwangu hapa hakumaanishi kwamba eti nahofia mapato yangu la hasha.Mkumbuke maslahi ya wabunge yanaamuliwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kupitia kamati husika then Rais ndio mwamuzi wa mwisho.Tunaweza kabisa kuja na hoja za msingi kabisa za kujipangia mapato manono kabisa na wananchi wakabaki kusononeka tu,everything can be justifiable.Hivi kuna mangapi humu tumeyajadili,je yametekelezeka?kiwapi kilio chetu cha DOWANS?Mijadala yetu humu imeiondoa DOWANS?jamani tuwe tunatafakari kwa kina,msituhukumu eti kwakuwa hatujasema posho zetu hapa basi hatufai.Tusem,tusiseme haitabadilisha.Tunafuata kanuni kwenye jukwaa kama hili.Nje ya hapa mimi sifichi ndio maana wananchi wangu wa Kilombero ambao walibahatika kuhudhuria kwenye mikutano yangu wanafahamu Mbunge wao ninalipwaje. 6. Napenda kufahamu hivi humu ni wangapi wake au waume zao au watoto wao au wazazi wenu wanafahamu mishahara yao? 7. Kuna watu humu wametoa mfano niliposimamia msimamo wangu kuhusu tofauti ya PHD na First Degrees,Bungeni ninalindwa na Kanuni za Bunge,ninaweza kukubali au kukataa mwongozo wa Spika kama nilichokisema ndicho ninachokiamini na ndivyo ilivyokuwa.Hapa siwezi kuikwepa Kanuni ya kutotoa siri za Bunge. Aluta Continua Regia E Mtema Waziri Kivuli Kazi na Ajira

Mheshimiwa Regia,

Nakushukuru sana kwa maelezo yako mazuri. Sikutaka kuingia kwa kina baada ya maelezo yako ya mwanzo kwa sababu kuu moja, bado Zitto na Mnyika hwajajibu chochote ili tujue mawazo au maoni yao. Nimekuwa mgumu kuamini haraka haraka kwamba na wao wanaweza kuwa na mawazo au msimamo kama wako.

Kwa nini nimesubiri? Zitto ninayemjua mimi amekuwa mzoefu wa kufukuzwa na kuwajibishwa kila alipopita. Zitto alifukuzwa O'level akafukuzwa A'level na akafukuzwa Chuo Kikuu. Zitto alifukizwa/simamishwa Bungeni. Kufukuzwa kote huko ilikuwa ni kwa sababu alikuwa anasema ukweli na kupinga waziwazi yale aliyoyaamini. Bado nasubiri nione katika hili inakuwaje. Inawezekana sasa hivi approach yake ni tofauti lakini bado nitasubiri nilishuhudie hilo au alitolee maelezo. Ukimya wake kwa wengine unaweza ukaonekana kama ni woga au amebadilika. Sitakuwa mwepesi kuamini hivyo mpaka mwenyewe aseme au ukimya wake umaanishe hivyo.

Kuhus Mnyika na yeye natarajia atasema neno. Endapo hatasema ataelezea kwa nin hajasema neno katika hili. Namfahamu na wengi humu ndani wamemuona ni mtu wa aina gani. Suala la Kanuni kumbana sidhani kama linamsumbua sana. Angekuwa anajali kanuni na sheria asingenipokea mimi na Zitto tulipofukuzwa chuo mwaka 2003 na kutuhifadhi chumbani kwake almost wiki tatu. Angefuata kanuni na By Laws za Chuo. Pia asingeniafirisha usiku kutoka Morogoro mpaka Dar kukimbilia Mgomo mwaka 2004 huku akiwa kiongozi wa TYVA na YUNA kwani alivunja kanuni nyingi tu. Mbona hakuogopa kipindi hicho? Kwa nini aogope sasa hivi?

Tukirudi kwako wakati nasubiri bila kuchoka kuwasikia Zitto na Mnyika, je taarifa uliyoitoa kwa wananchi wako wa kilombero ilikuwa ni kwenye hadhara au uliwapa mmoja mmoja? Uliwatangazia wakati wa mchana kwenye mwanga au usiku? Najaribu kuangalia tofauti ya eneo la kutolea taarifa hiyo i.e kwenye jukwaa la siasa kwa maandishi na kwenye mkutano wa hadhara kwa maneno.

Kwenye JF hakuna ushahidi wowote ambao unaweza kupokelewa mahakamani au kwenye kamati ya maadili kuonyesha na kuthibitisha kwamba ni wewe umesema utakachosema. Ni nani atathibitisha ni wewe? Je kama nimechukua picha yako, nikaingia nayo humu ndani pamoja na jina lako nani atajua?? nani atapinga?? Mods watathibitisha vipi ni wewe?? Lakini bado siamini kwamba kipato cha Mbunge ni siri. Nikipata muda nitasoma kanuni za Bunge.

Ila ukisimama hadharani kila mtu anakuona, mashahidi watajitokeza, usalama wa taifa watakuona, waandishi watakupiga picha uthibitisho utakuwepo kwamba ni wewe umesema mbunge analipwa kiasi gani. Hapo unatakiwa uwe muoga zaidi.

Lakini, kwa sababu ninajua tutaonana au tutazungumza nje ya hapa naamini nitapata ufafanuzi zaidi. nitakuomba kama una nakala ya Kanuni za Bunge recent unitumie kwa email ili nizipitie na nitakuwa mshauri wako kuhusu masuala yote ya kanuni. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha hazikufungi bila sababu.

Kwa sasa ninasubiri bila kuchoka kumsikia Zitto na Mnyika. Ukiwapata wafikishie salamu kwamba tunawasubiri humu.

Kila la kheri Mheshimiwa.
 
Kipendacho roho!

Yaani ile sifa ya CDM kutafuta mi-data huko maofisini leo hawawezi kuweka data za posho zao wenyewe?

Regia Mtema yuko sahihi kwa jina lake na maadili ya bunge, lakini ndio mwisho hapa?

mpaka kuna wabunge wa CDM wanamshambulia Lema kutoa siri ya mikopo ya magari (Tsh. 90m)!!

huwa tukisema tunaonekana wabaya, we have a long way towards real freedom

Upinzani haupo Tz! note this down
 
Ndugu zangu wanaJF. Salaam.
Nimesoma kila mchango kwenye sredi hii kwakuwa sredi hii inanihusu moja kwa moja.Ninaelewa hoja zenu na nina washukuru wote kabisa mlionielewa na msionielewa.Kuna mambo kadhaa naomba niyaweke sawa.
1.Kuna watu hapa baada ya kusoma post niliyorusha mmelaumu kwa kusema ninakwepa kusema ukweli.Kundi hili nadhani halikunielewa nilichosema,nimesema wazi kabisa nje ya jukwaa hili naweza kusema na nikampa fursa mrusha sredi anitafute kwa njia nyingine.Alberto ana access namimi kwa kiasi kikubwa tu angeweza kunipata na ningempa mchanganuo wote including access ya kiwango cha juu cha mkopo kwa Mbunge kwenye benk.

2. Kuna wengine wamesema nitumie au ningetumia ID ya siri na kuna wengine wamesema eti kutokuwa na ID nyingine ni danaganya toto lakini ukweli ni kwamba sina ID nyingine kwasababu zifuatazo ninaamini kabisa nikiwa na ID nyingine na nikawa na post sredi mbalimbali hapa ndani ya wiki mbili tu nitakuwa nimeshajulikana.Nilipokuwa natumia jina la siri enzi hizo kama Gender Sensitive kuna watu wengi tu walikuwa wameshafahamu GS ni nani.The problem niko muwazi sana na siwezi kujificha wala kupretend hivyo nitajisumbua tu kuwa na ID za siri,sioni sababu.Baada ya kuwa Mbunge kuna baadhi ya watu walinishauri niwe na hayo maID ya siri lakini nikaona nitakuwa mtumwa tu,kwnini nijifiche?namdanganya nani?naogopa nini?

3.Kuna watu hapa wanasema kuwa naogopa kuwajibishwa na Kamati ya Maadili inakuwaje naogopa kusemwa tu?ndugu zangu mnachukulia kuwa hili suala ni dogo sana,sio dogo kama mnavyodhani.Ninachokataa hapa nikuvunja kanuni kwenye forum kama hii.Nimesema wazi kuwa nje ya hapa sitaficha.

4.Kuna kitu nimejifunza hapa, kuna watu wanashangaa mimi kuogopa kuwajibishwa na kamati ya maadili lakini wengi wao wako na majina ya siri,kwanini mnajificha,manogopa nini?si angalau mimi niko na jina langu halisi na ninafahamu fika kwamba kila ninapopost kitu sio wote watakao kipokea positively,ninafahamu fika nitakumbana na changamoto mbalimbali but altleast siziogopi na ninaziface.Jamani tafakarini kwa kina.

5. Kuna watu hapa wamesema kuwa eti linapokja suala la fedha basi wote tunakuwa na sauti moja ndio maana sijasema mchanagnuo wa mapato ya Wabunge.Jamani hili si kweli.hivi mmetafakari kwa kina?hivi kwani nikisema hapa ndio hayo mapato ya wabunge yatasitishwa?kwani mjadala umeanza leo?kutosema kwangu hapa hakumaanishi kwamba eti nahofia mapato yangu la hasha.Mkumbuke maslahi ya wabunge yanaamuliwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kupitia kamati husika then Rais ndio mwamuzi wa mwisho.Tunaweza kabisa kuja na hoja za msingi kabisa za kujipangia mapato manono kabisa na wananchi wakabaki kusononeka tu,everything can be justifiable.Hivi kuna mangapi humu tumeyajadili,je yametekelezeka?kiwapi kilio chetu cha DOWANS?Mijadala yetu humu imeiondoa DOWANS?jamani tuwe tunatafakari kwa kina,msituhukumu eti kwakuwa hatujasema posho zetu hapa basi hatufai.Tusem,tusiseme haitabadilisha.Tunafuata kanuni kwenye jukwaa kama hili.Nje ya hapa mimi sifichi ndio maana wananchi wangu wa Kilombero ambao walibahatika kuhudhuria kwenye mikutano yangu wanafahamu Mbunge wao ninalipwaje.

6. Napenda kufahamu hivi humu ni wangapi wake au waume zao au watoto wao au wazazi wenu wanafahamu mishahara yao?

7. Kuna watu humu wametoa mfano niliposimamia msimamo wangu kuhusu tofauti ya PHD na First Degrees,Bungeni ninalindwa na Kanuni za Bunge,ninaweza kukubali au kukataa mwongozo wa Spika kama nilichokisema ndicho ninachokiamini na ndivyo ilivyokuwa.Hapa siwezi kuikwepa Kanuni ya kutotoa siri za Bunge.

Aluta Continua
Regia E Mtema
Waziri Kivuli Kazi na Ajira
Kipengele namba sita;Hutambui kuwa ukiwa kwenye public office you are accountable to the public?Sijui ni kivipi unafananisha ufahamu wa mume ama mke kuhusiana na mishahara yao vs wananchi kujua ni kiasi gani wanawalipa nyie kama viongozi wao?Ama ubunge ni private sector?
 
5. Kuna watu hapa wamesema kuwa eti linapokja suala la fedha basi wote tunakuwa na sauti moja ndio maana sijasema mchanagnuo wa mapato ya Wabunge.Jamani hili si kweli.

Mh. Mbunge, jambo pekee linalowaunganisha wabunge wetu uwa ni mjadala wa mafao ya wabunge, hilo ni kweli. Tumewaona mara nyingi, kuanzia enzi za kina Lamwai, uje katika bunge la Sitta tulishuhudia wakati wa kujadili mafao ya wabunge, ilifikia hatua hata Rais akawashangaa wabunge!

Na leo nakujuza kama kweli ulikuwa hujui, Makinda ashasema mafao yenu yataboreshwa tena na utakuwa shahidi. Kama wewe si miongoni mwao basi utasimama peke yako ka Dr. Slaa!

hivi mmetafakari kwa kina?hivi kwani nikisema hapa ndio hayo mapato ya wabunge yatasitishwa?kwani mjadala umeanza leo?kutosema kwangu hapa hakumaanishi kwamba eti nahofia mapato yangu la hasha.Mkumbuke maslahi ya wabunge yanaamuliwa kwa kiasi kikubwa na wabunge kupitia kamati husika then Rais ndio mwamuzi wa mwisho.

Mh. Mbunge unafikiri mambo ya EPA kama watu tungeyafumbia macho kuna lolote lingefanyika? Kumbuka; kuweka taarifa mbele ya umma itawafanya wabunge muone aibu ya kupata Lion share katika keki ya taifa!

Kwani mjadala umeanza leo? Hapana lakini hatuwezi kunyamaza mpaka pale tutakapoona hali imebadilika.

Tunaweza kabisa kuja na hoja za msingi kabisa za kujipangia mapato manono kabisa na wananchi wakabaki kusononeka tu,everything can be justifiable.Hivi kuna mangapi humu tumeyajadili,je yametekelezeka?kiwapi kilio chetu cha DOWANS?Mijadala yetu humu imeiondoa DOWANS?jamani tuwe tunatafakari kwa kina,msituhukumu eti kwakuwa hatujasema posho zetu hapa basi hatufai.

Hiyo ya kuja na hoja ya kujipa mapato manono na wananchi wakabaki wanasononeka hiyo ni kawaida yao/yenu, au umesahau kuhusu Mfuko wa Jimbo na uboreshaji wa mafao ya wabunge katika bunge la 9! Wananchi tulibaki tunasononeka tu.

Nitafurahi kama wewe Mh. Mbunge utakuwa tofauti na wengine!

Tusem,tusiseme haitabadilisha.Tunafuata kanuni kwenye jukwaa kama hili.Nje ya hapa mimi sifichi ndio maana wananchi wangu wa Kilombero ambao walibahatika kuhudhuria kwenye mikutano yangu wanafahamu Mbunge wao ninalipwaje.

Aluta Continua Regia E Mtema Waziri Kivuli Kazi na Ajira

Kusema kwetu naamini kutabadilisha mienendo ya wabunge, itawasukuma kubadili kanuni zisizofaa!

MWISHO;
Nakutakia mafanikio katika kazi zako kama mbunge! Aluta Continua.......!

Back
Top Bottom