Mnyika, Zitto na Regia: Tupeni mchanganuo wa hela zinazolipwa kwa Mbunge ili tujue | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika, Zitto na Regia: Tupeni mchanganuo wa hela zinazolipwa kwa Mbunge ili tujue

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 22, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Waheshimiwa Mnyika, Zitto na Regia,

  Salaam,

  Naamini kabisa mtasoma na kuitikia ombi langu. Baada ya kusikia taarifa ya Mh. Makinda kuhusu posho za wabunge na upokeaji wa posho mara mbili ni vyema mkatueleza bila kificho ni kiasi gani Mbunge anapokea kila mwezi na kwa kila kikao. Vikao ikiwa ni pamoja na vikao vya kamati, safari na kadhalika. Pia mikopo, gharama za matibabu nk.

  Tunataka mjadala wa posho za wabunge. Mjadala wa Katiba sawa, matamko kuhusu utendaji na uzembe wa serikali sawa ila kwa sasa tungependa kuanza na mjadala huu wa posho kwa wabunge.

  Tunachohitaji ni uwazi kuhusu maslahi (kama yapo) anayopata Mbunge ili tufanye maamuzi sahihi.

  Msituangushe.  Tuwekeeni hapa tujadili
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  na wewe unaweza kutoa mchanganuo wa mshahara wako kwanza?
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona nilishautoa kwenye thread yangu ya 'posho ya diwani'? Itafute utaona.
   
 4. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  jamani, kwani wewe ni mnyika, au zitto??? Si utulie, majibu yatatolewa na walioulizwa. Kama hawatakua tayari kuyatoa basi watasema wenyewe, usitake kuanza kuleta ubishi kwenye suala dogoo tu.
   
 5. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  halafu ubishi wenyewe sijui unasaidia nini! Tunachotaka ni ufahamu wa kiasi cha fedha ambazo tunatumia kuwahudumia Wabunge 350 wa Bunge letu ili tuweze kulinganisha na output ya uwakilishi wao. Kama fedha tunazotumia zina uwiano sawa na tunachokipata kutoka kwao.

  Sasa mtu anatoka huko na kuanza kutafuta ligi!
   
 6. AIZAK

  AIZAK Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  anxiously waiting
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mwaka ndio unaanza, lakini at this time I can confidently predict that this will be the best thread of the year.
  Asante sana Mh. Diwani.
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Mbona mmekaa kimya mlioulizwa swali tueleweje?u ndi swali limegusa ikulu eeehhh;tuelezeni BWANA.onyesheni tofauti yenu na wenzenu wa SISIEM,chap chap jipangeni mjibu,tena ningefurahi kama kila mmoja angejibu kivyake naamini hata Slaa yumo humu anaweza saidia hapa,Mbowe sina hakika kama yumo humu ila Mnyika,Regia,Zitto mkisaidiwa na Dr Slaa jibuni hili ni swali lenu
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Jamani embu kuweni patient kidogo...

  Hawa watu wameingia kwenye kikao kimoja tu cha 10, how come mnategemea wawe washajua mapato yote yanayowaangukia?

  Wa kumkalia koo hapo ni Zitto, naamini yeye anajua vizuri, na amekuwa kwenye kamati kwa muda mrefu.

  Lakini pia naamini kuwa hata ukijua kuwa labda net yake ni say 3000K kwa mwezi, what are you bound to do?....tutaishia kugonga keys hapa, with no substance at the end...we wont be able to reduce a penny from a sum, whatsoever!

  Mimi nijuavyo, hili siyo swali la kuwauliza hao uliowataja hapo juu, utaonekana unawaspeculate na kuwa'poke mno....Why the 3 of them..why not all MPs?...rather, why not all CDM mps, if thats what you want?

  Naamini Mapato yote ya wabunge ni wazi, na yako outlined wazi katika miongozo ya maslahi yao(bila kujali kuwa wanajiongezea kila wakipata upenyo)...https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/112613-makinda-posho-za-wabunge-hazitoshi.html

  Nikisema hivyo si kwamba naunga mkono malipo hayo...hell Noooop!, Naboreka usipime!...tu ni kwamba sioni sababu specific ya kuwabagua watatu na kudai waweke hadharani wanacholipwa!
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  unakosea sasa,hawa tunawajua ni vijana wetu ,makini na maridadi,hawana wasiwasi na wala hawapati kigugumizi kwenye KWELI,na pili tunafahamu kuwa wapo humu,kama wananchi wanataka kujua mapato yao kwa nini wasiseme,unataka kusema miaka 6 ya Zitto bungeni hajui mapato ya Mbunge,

  TULIA BWANA WAACHE WAJIBU
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  uNARUDIA NILICHOSEMA...rejea kwenye post yangu!
   
 12. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwa taarifa yako hawatajitokeza kuzungumzia mapato yao halisi, kuhusu ankara,fedha,chapaaa hiyo huwa hawazungumzi kamwee we hukumbuki mfuko wa jimbo walivyo ungana CCM na vyama vya upinzani kuutetea wakati mfuko huo ni ufisadi mwingine
   
 13. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  PakaJimmy, nakuamini sana kwa umakini katika Jamvi. Isome tena hoja yangu tafadhali.

  Kwa ufupi, nimewaomba waheshimiwa hao watuambie Mbunge analipwa shilingi ngapi, sio WAO wanalipwa shilingi ngapi. Wao kama wabunge watatusaidia kutupa habari za uhakika ili tuweze kujadili.

  Pia, nimesikitika kuwa unaamini hatuwezi kupunguza hata senti moja kwa hiyo hakuna haja ya kujadili. Ni mangapi tunayoyajadili ilhali hakuna tunaloweza kufanya? Na kwa nini hatuwezi kufanya lolote?

  Huwezi kuniambia eti Regia na Mnyika hawajui Mbunge wa Tanzania analipwa shilingi ngapi kwa mwezi na posho na marupurupu mengine kisa wamehudhuria kikao kimoja. Mbona Mnyika anajua kuhusu suala la Maji Dar na Katiba Mpya na amehudhuria kikao hicho kimoja? Au ukubwa/uchache wa posho ya Wabunge sio muhimu kwake?

  I still expect them to hold the bull by its horns. Let them come out and tell us. We need to know with certainty Mbunge analipwa kiasi gani. That isnt a hard call!
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Namwona Regia...Huenda akaweka wazi kama kanuni zinamruhusu, vinginevyo asije akaambiwa atoe ushahidi mbele ya Bunge juu ya alichosema!

  There are currently 17 users browsing this thread. (7 members and 10 guests)

   
 15. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  sahihi mkuu;ila kama DOMO ZEGE alivyosema inaweza kuwa issue sana kwa hawa ndugu kudisclose mapato yao hapa
   
 16. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Domozege, mfuko wa jimbo ni tata sana. Kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mfuko huo ni kiasi cha shilingi Milioni 84+. Kwa mwezi July 2010 mpaka Nov 2010 pesa hizo zote zilitumika kwa asilimia 96!! Ni miradi gani ilitekelezwa ni kitendawili. Ila utaona kipindi hicho kilikuwa kipindi cha kampeni. Na Mbunge ndie Mwenyekiti wa Mfuko huo. Kwa Moshi Vijijini Mbunge aliyekuwepo ndie aliyekuwa anagombea tena. So you can tell the game behind. Its clear as day light.
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Msando.Heshima Mbele!How are you?

  Nimeisoma sredi yako nimekupata,nimekuelewa.Kimsingi nakubaliana na hoja yako na uko sahihi kutaka kujua maslahi ya wabunge kwakuwa sisi ni wawakilishi wa wananchi.Lakini kwakuwa nchi yetu imejengwa kwa mgumo wa usiri katika mambo mengi na ndio maana utakuta hata mke hajui mshahara wa mumewe na wako kwenye ndoa zaidi ya miaka 50 na watoto nao hivyo hivyo hawajui kipato cha wazazi wao n.k.Kumekuwa na utamaduni wa watu kutokutaka kuweka wazi vipato vyao bila sababu za msingi.Binafsi huwa sielewi hasa kwanini iwe hivi.

  Binafsi napenda sana kuweka wazi vyanzo vya mapato yangu na wakati nikiomba kura Kilombero niliweka wazi jumla ya mapato ya Mbunge kwa mwezi na kimsingi nilikuwa napingana na malipo haya.Hivi sasa nimekuwa Mbunge ninafungwa na Kanuni za Bunge za kutotoa siri za Bunge.Wakati tuko kwenye Semina Elekezi Ubungo Plaza tuliwekwa wazi kuhusu mapato ya Mbunge na Spika alisisitiza sana kuhusu usiri.Nilipata nafasi ya kuhoji kwanini kuwe na usiri katika mapato yetu sikupatiwa majibu ya kuridhisha,kimsingi hakuna hoja za msingi ila ni woga tu.Spika alisisitiza kwa yeyote atakayetoa siri atawajibishwa na Kamati ya Maadili.Lema aliweka wazi kuhusu mikopo ya Magari ya Shilingi milioni 90 analaumiwa sana including baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.Kwa bahati mbaya sana sina ID nyingine humu JF zaidi ya hii ya jina alangu halisi hivyo siwezi kuweka wazi hapa mbele ya kadamnasi na kwakufahamu fika kuwa humu wako members wakila aina including wabunge na viongozi wengine hivyo nisije nikachukuliwa hatua za kinidhamu unnecessarily.Ila tukiwa nje ya jukwaa hili nitaweka wazi kila kitu iwe kwako au kwa mwingine yeyote atakayehitaji.

  Naamini umenielewa na tutawasiliana kwa njia nyingine.

  Aluta Continua.
  Kutoka Ofisi za Bunge Dsm
  Regia E Mtema
  Waziri Kivuli Kazi na Ajira.
   
 18. peck

  peck JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tunashukuru Da Regia tumekupata
  Aluta kontinua!
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Msando Ablert!...unaheshimika mzee!

  Majibu ndio haya, na obviously amejibu kama nilivyodokeza awali kwenye post yangu No 14 juu!
  Japokuwa mheshimiwa ameweka wazi kwamba tuwe na subira, yatakuja wekwa hadharani tu siku moja kwa namna nyingineyo tofauti na hapa.
  So currently we have to reserve our comments.
   
 20. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  Regia Mtema unaelekea kuwa mbunge bora,siamini kama Zitto na Mnyika na yale ma id yao mengine wameshindwa kutuambia ukweli
   
Loading...