Mnyika, Zitto, Januari, Kafulila, Nape kuanzisha Jukwaa la viongozi vijana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika, Zitto, Januari, Kafulila, Nape kuanzisha Jukwaa la viongozi vijana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by T. 2015 CCM, Feb 16, 2012.

 1. T

  T. 2015 CCM Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau nimeinasa mahali kuwa kuna mazungumzo yanaendelea baina ya baadhi ya Viongozi vijana kuacha tofauti zao za kiitikadi (Kivyama) na kuanzisha jukwaa la Viongozi vijana kwa lengo la kujadili mstakabari wa Tanzania sasa na baadae kiuchumi, kisiasa, kimichezo na kiutamaduni.
  Kama mjadala na mazungumzo haya yapo, naomba kuyaunga mkono, kwani ndiyo yatakayofanikisha kuleta tija kwa mstakabari wa taifa hili. Sasa hivi kinacholitesa taifa hili ni tatizo la mvutano wa kiitikadi na kivyama badala ya mvutano wa kimtazamo wenye lengo la kusukuma maendeleo ya taifa hili mbele kwa haraka.
   
 2. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wazo zuri sana.lakini kwa sisi watz kwa mawazo mazuri hatujambo, ukija kwenye utendaji ni tatizo.waangalie na wao wasiishie kujisifia tu kuwa ni viongozi vijana halafu mwisho wa siku wauage ujana wao bila lolote.Kimsingi mimi nina imani nao kwa ujumla wao kwa maana ya kujenga hoja zenye mshiko lakini bdo kwenye suala la uwajibikaji na uhamasishaji wa uwajibikaji kwa vijana bado vingozi hawa hawajafanikiwa.

  Wajitahidi kadri wawezavo walete mageuzi ya kweli tanzania mfano waendelee kuelimisha jamii na serikali kwa ujumla umhimu wa kuwa na kasi ndogo ya rural-urban migration na njia za kuzuia na kupunguza kasi hii.Kwangu mimi kama tukiweza kuzuia movement hizi kwa kadri itakavowezekana tutakuwa tumepunguza matatizo ya jamii za mjini kwa kiasi fulani

  Namna moja wapo ya kuzuia ongezeko hili mijini ni kuhamasisha na kuwezesha uzalishaji mashambani na vijijini ili watu wengi zaidi wajihusishe na uzalishaji na hatimaye waje mijini kutafuta masoko na mambo mengine na sio kuja mijini wakiwa tegemezi.

  Namna nyingine ni kuendelea kuihimiza serikali kuwa na sera ya decentralization.Sio kila mradi wa maendeleo uwe dar es salaam tu au miji hii mingine mikubwa.Serikali kadri iwezekanavo ianzishe miradi ya maendeleo mikoani hasa hii midogo kama vile Kigoma, Ruvuma, Lindi etc ili watu sasa badala ya kuona maisha ni DSM peke yake watu waone maisha na Lindi yapo .

  naomba nichangie haya kwa sasa.Ntarudi bdae
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  kwani walikuwa hawana hili jukwaa?
   
 4. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Uchafu tu wanatuletea, ccm washashindwa unavyojidanganya kuungana nao kwa kisingizio cha maslahi kwa taifa ni kifo cha cdm km ilivyokuwa cuf, zitto na kafulila ningewasifu na kuwaunga mkono km wangeunda jukwaa la vijana kwa ajili ya kuing`oa ccm ili kije chama kipya na mifumo mipya na sio ujinga na ****** huu.
  Kadri vijana wa chadema wakiongozwa na zitto wanavyodhani january na bashe ni wenzao wajue wale wanawamaliza nguvu kiana tu, km kweli bashe, nape na january wanalitakia mema taifa hili kamwe wasingekaa ccm.
   
 5. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Hao vijana wasifanye makosa ya kuambatana na vijana wa CCM. Uliona wapi giza na nuru vikakaa pamoja? Unajua lazima tukubaliane kuwa mradi walio nao watanzania kwa sasa ni kuuondoa huu mfumo mbovu uliopo, na si kuwapatia vijana nafasi za uongozi. Kama akina Januari na Nape wanataka hilo wanatakiwa waikane CCM na kujiunga na makamanda katika harakati za kuikomboa nchi yetu. Sioni namna hawa vijana wanaweza kufanya kazi pamoja, kwa lengo gani hasa?

  LENGO LA SASA NI MOJA TU KUING'OA CCM MADARAKANI. KAMA HILO NAPE NA JANUARI WANALIKUBALI NAMI NAUNGA MKONO HIYO HOJA.
   
 6. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama Mnyika yumo kwenye huo umoja wa mashaka...
  Zitto inawezekana na hawajaanza leo.
   
 7. Kisiya Jr.

  Kisiya Jr. Senior Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wazo zuri ila nina wac wac it gona affect their political confidence when we are in house of political representation
   
 8. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Ni hatua nzuri lakini nina maswali; hivi, huo umoja lazima uanzishwe na vijana walio katika dhamana za ki-siasa tu?
  Na Je, kwa milango ya kisiasa Taifa, limewahi kupiga hatua gani kubwa ya kimapinduzi, ya kimaendeleo na ya kujivunia?
   
 9. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  hii kachumbari kwa macho inaonekana ni tamu, lakini ukiitia mdomoni - imechacha!

  labda ukii-spice up kidogo na a certain lema.....inaweza kidogo kunoga.
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nape?
  uungane na nape ili iwe nini?
  huyu ni mtetezi wa mafisadi na ufisadi,ni jasiri wa kifisaadi hajawahi kushinda kwa anayoyasimamia.

  nape akikuambia hii ni rangi nyekundu ukitulia na kuichunguza vizuri unakuta ni njano.
  sijui ni hana msimamo au hajijui?
   
 11. f

  faloyce2001 Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyika nz Zito please msiingie huko. Kwanza mmepata baraka za chama? Tafadhali msijichanganye na magamba mtaharibikia ukubwani kama bamia.
   
 12. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Je, ukichanganya maji na mafuta yataitwaje?
  Umchanganye Nape na Mnyika! Ah wapi. Uchanganye ukweli na uongo, usanii na ushujaa, uchafu na usafi, magamba na magwanda, kondoo na fisi!
   
 13. S

  STIDE JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nape!!??
  Ooooh my God!!!
  Mafuta ya mawese yanachanganywa kwenye chai!!!
   
 14. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  no sense, kama wana la msingi waje jamvini
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  wakafie mbele huko, watutolee ****** hapa, wanadhani mawazo yao ni bora kuliko sisi sio? hivi nani kawaongopea kuwa tunawategemea kihiivyo!!! nyang'au wakubwa hawa. kwa hiyo kupitia makamba wezi wa ccm wajekulindwa na hilo liumoja lao, Nasema ole ole ole wao, wakome kutu-underestimate namna hiyo.
   
 16. K

  KIGIGI Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lakini hayo ni mawazo tu ya mtu mmoja sidhani kama ha vijana wametamka lolote kuhusu hilo
   
 17. February

  February Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jasiri hakimbii mpambano. Ebu wajaribu kukutanishwa kwenye mdahalo wajadili masuala ya kitaifa tuwapime wanavochuana kimawazo. Itasaidia sana. Hakuna sababu ya kuogopa mijadala. Nimuhimu vijana wa upinzani kuwapambanisha na hawa vijana wa magamba ili kuonesha tofauti za uwezo wa kukabili masuala na hoja. Leo kuna changamoto kwa mfano kati ya january makamba na john mnyika katika sekta ya nishati nani zaidi. Mjadala ya pamoja mbele ya umma inaweza kuzidi kuwapambanua na kutuonesha watanzania nani ni nani.
   
 18. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Nafikiri hii ni kitu nzuri kwa mustakali wa taifa letu
   
 19. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  unaitaji ukombozi wa fikra mkuu.bado tu,umegandana na ushabiki wa vyama?,kwa mawazo haya nchi haitasonga kamwe.cdm si chama cha malaika siku wakipewe nchi,utashabikia wp? Maana hawawezi kutimiza haja zako kwa njia za kidemokrasia.turuhusu akili zetu kufikiri sahihi na kuweka ushabiki chini,kama kuna jema ktk muungano huu ni vema.ifike mahali tujue chanzo cha umasikini wetu kimejificha kwenye vyama vya kisiasa,si rahisi kukubali ukweli huu hasa mashabiki wa vyama mtapinga sana,wanasiasa wengi ni matapeli mnavyowasoma kwenye magati sivyo walivo ndg zangu ni wanafiki wapenda umaarufu,pesa na madaraka.TUWE MAKINI NAO
   
 20. W

  Wangama guy Senior Member

  #20
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata kama wataweka pembeni tofauti zao za kiitikadi, ninamashaka na Nape, huyu sikuzote penye ukweli hujitahidi kupindisha ili mradi kutetea mafisadi wao. Laiti ningemwona Nape anapambana kupigania serikali yake ishughulikie kero lukuki za sisi wananchi mf. maisha magumu, mfumuko wa bei, n.k
   
Loading...