Mnyika: Watendaji hawaelezi ukweli tatizo la umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika: Watendaji hawaelezi ukweli tatizo la umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredrick Sanga, Oct 22, 2012.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Na Mwandishi wetu

  WAZIRI Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, ameeleza kusikitishwa na kauli za viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhusu hali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini sanjari na uboreshaji wa utendaji TANESCO.
  Amesema kauli hizo zinatoa matumaini potofu kwa wananchi na kuwasihi kuzipokea kwa tahadhari kwa kuwa hazielezi ukweli kuhusu tatizo la umeme nchini.

  Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, alitoa kauli hiyo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kusema kulingana na nyaraka alizonazo za ndani ya wizara hiyo na TANESCO kuanzia Septemba hadi Oktoba mwaka huu, hali ya uzalishaji na usafirishaji na usambazaji wa umeme imekuwa tete kwa sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa upatikanaji wa mafuta na gesi asili kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya kufua umeme na kasi ndogo ya uwekezaji kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa kudumu.
  Mnyika pia alisema amemwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, ili Wizara ya Nishati na Madini iwajibike kueleza hali halisi katika mikutano ya kamati za Bunge inayoendelea.

  "Katika barua hiyo nimependekeza pamoja na mambo mengine suala la kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme na utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa utendaji wa TANESCO lishughulikiwe na kamati nyingine kwa haraka kwa kuzingatia maelezo na maelekezo ya Spika aliyoyatoa bungeni wakati wa kuahirisha mkutano wa nane wa Bunge," alisema.

  Aidha alisema mapitio ya utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa utendaji wa shirika hilo yahusishe kamati ya kudumu ya Bunge na itakayoeleza hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa tuhuma za ufisadi kwa kuzingatia kuwa siku 60 za uchunguzi zimepita.


  My Take: Hapa kuna kitu kinafichwa maana, umeme unakatika hovyohovyo tu. Hivi kuna ubaya gani kusema ukweli, na kutupa ratiba.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ma waziri vivuli wengine vipi? mbona ni Mnyika tu anapambana hao wengine ni wasomaji wa hotubu tu ama? anywabu na wabunge wengine je?
   
 3. C

  Concrete JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Bora amesema, kwani kila siku mahali nilipo umeme lazima ukatike kwa wastani wa masaa nane katika masaa 24.

  *Tatizo hili limekuwa kwa karibu miezi miwili sasa na hakuna sababu za msingi tunazopewa kwanini hali hii itokee.
   
 4. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Tumezoea kusikia wakijugamba hakuna mgawo wa umeme, ilhali tukishuhudia kukatika kwa umeme kwa theluthi moja (1/3) ya siku.
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtu ktk awamu hii ya nne anayeweza kutatua mtatizo ya nishati nchini. Kuna matatizo makubwa sana mawili,

  1) Mosi CCM ni tatizo mama, kupitia serikali zake. Kwa CCM nishati ya umeme, mafuta, gesi ni dili za viongozi na lazima ibaki hivyo. Na ndio maana tunazo kila aina ya kashfa ktk wizara hii nyeti kila mwaka na ktk kila awamu.

  2) Pili, ni TANESCO kama shirika kimuundo, kisera, kiufanisi, viability (samahani nimekosa kiswahili chake) nk.

  Kwangu mimi haya ya miundo mbinu, uwezo, wafanyakazi nk ni petty issues. Core is ni hizo mbili kwa mpangilio (by order)
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwangu mimi binafsi, athari za kukatika umeme hovyo ni kubwa mno, Napata phisical, financial and Psychological effects. Hivi wengine sijui mnaonaje?
   
 7. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Full vishoka, kuanzia wizarani hadi tanesko.
   
 8. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,773
  Likes Received: 2,675
  Trophy Points: 280
  Nadhani wala sio vishoka, bali kuna uwezekano kuna vimemo kutoka "juu", vinavyowalazimisha watendaji hawa kusema uwongo/uongo.

  Kumbuka zile hela ambazo Tanesco ilikuwa inahangaika kuhakikisha hazilipwi, mahakama nadhani iliagiza zilipwe... waweza kuunganisha nukta hapo...
   
 9. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Vishoka waunga umeme
  Vishoka wachezea luku na mita
  Vishoka wezi wa mafuta
  Vishoka kulangua tenda

  Yaani full vishoka.
   
 10. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ili tatizo lipo,yani siku yule waziri anaongea eti kukatika umeme hakupo tena,nilitoa tusi kwakweli
  umeme apa nilipo unakatika mara nyingi sana kwa wiki ata mara 3 au 4...kweli sie ni wapole na tumelishwa nini sijui
   
 11. awp

  awp JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  kazi kwelikweli
   
 12. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Uoga wetu ndio unatufanya tunyonywe, tudanganywe, tudhalilishwe, tokoloniwe, tutabakiwe, tumaskiniswe. Tusemeeee! sasa basi kwanza kwa kuondoa hili tabaka la wakoloni weusi. Ili tuweze kugawana keki ya taifa.
   
 13. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hizi nyau zinasaidia kufukuza mapanya.
   
 14. ligendayika

  ligendayika JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 1,175
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Sawa Mnyika
   
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tuna imani na mbunge wetu, Yule mama angetuingiza chaka. Kama kuna anayeefikiria hili jimbo sahau.
   
Loading...