Mnyika: Viongozi waliokimbilia nje ya nchi sasa warudi nyumbani suala lao lilikuwa katika ajenda za Maridhiano

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,785
141,681
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema Viongozi na wanachama wao waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa na kiusalama sasa warudi nyumbani baada ya Serikali kuwa imetoa tangazo bungeni.

Mnyika amesema suala la viongozi hao wakimbizi lilikuwa moja ya ajenda ya Maridhiano.

Mnyika amewataja Tundu Lissu, Lema na Wenje kuwa ni miongoni mwa walio nje ya nchi na Chama kitawaandikia rasmi kuwapa utaratibu wa kurejea nyumbani

Chanzo: ITV habari
 
Taarifa inafikirisha ikizingatiwa kuwa karibu viongozi wote hao walikuwa wagombea wa nafasi mbalimbali za kuchaguliwa na walifanya kampeni zao kwa usalama.

Warudi tu hawatakuwa na jipya kama hawataweka bayana ni kwa namna gani walitishiwa usalama wao, na nani, kwa sababu gani.

MAAMUZI YA KIPUUZI NA UHUNI
 
Ile mikopo ya dhamana ya bunge sidbani kama waliimiza
 
Chadema wanawabagua vyama vingine vya upinzani, wanajitenga nao, wakiingia madarakani watakubali maridhiano au serikali ya mseto na vyama vingine? Hapa tu hawako madarakani, Wana ubinafsi, wanachukia vyama vingine, wakipata madaraka wanaweza kufuta mfumo wa vyama vingi vya siasa, wanachukia sana vyama vingine
 
Spika mstaafu Ana makinda

Alikua anawapenda Lissu na wenje Sana

Mtoto wangu lisu nimesema kaa chini

Wenje ,mwanangu tusaidie unajua Sana kiingereza ,kulitakiwa katika Sheria ,neno

Will na shall lipi litumike na may na can lipi litumike

Mwanangu wenje tusaidie

Bunge lilikua tamu lile ,huku Mbowe alhamos swali la kwanza kwapinda ni lake ,hapa lisu pale zito kabwe wazamani ,pale wenje hapa jirani yangu kafulila , Kati John John mnyika ,huku sugu pinda alipanda ndege Hadi mwanjelwa wakamzingua mama makinda akasema SUGU nimekuruhusu nenda alipofika akatuliza zogo

Yaaani ilikua raha Sana makinda ataish maisha marefu
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Viongozi na wanachama wao waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa na kiusalama sasa warudi nyumbani baada ya serikali kuwa imetoa tangazo bungeni

Mnyika amesema suala la viongozi hao wakimbizi lilikuwa moja ya ajenda ya Maridhiano

Mnyika amewataja Tundu Lissu, Lema na Wenje kuwa ni miongoni mwa walio nje ya nchi na Chama kitawaandikia rasmi kuwapa utaratibu wa kurejea nyumbani

Chanzo: ITV habari
Mungu wetu yu mwema, tunawasubiri kwa hamu na ujio wenu ndio chachu ya mabadiliko na maridhiano
 
Kheee, wanarudi kwa tangazo la Mnyika? Si walisema hawarudi mpaka rais autangazie ulimwengu na kuwaomba kurudi, sasa imekuwaje tena?
 
Bunge lilikua na wapinzani lilikua linavutia kusikiliza. Sasa hivi ni kibisa culture group, hapa sarakasi, pale vilio nakadhalika
 
Taarifa inafikirisha ikizingatiwa kuwa karibu viongozi wote hao walikuwa wagombea wa nafasi mbalimbali za kuchaguliwa na walifanya kampeni zao kwa usalama.

Warudi tu hawatakuwa na jipya kama hawataweka bayana ni kwa namna gani walitishiwa usalama wao, na nani, kwa sababu gani.

MAAMUZI YA KIPUUZI NA UHUNI

Kipindi cha dhalimu ukiwa mpinzani vocal kutekwa, kuuwawa ama kubambikiwa kesi ilikuwa jambo la kawaida sana.
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Viongozi na wanachama wao waliokimbia nchi kwa sababu za kisiasa na kiusalama sasa warudi nyumbani baada ya serikali kuwa imetoa tangazo bungeni

Mnyika amesema suala la viongozi hao wakimbizi lilikuwa moja ya ajenda ya Maridhiano

Mnyika amewataja Tundu Lissu, Lema na Wenje kuwa ni miongoni mwa walio nje ya nchi na Chama kitawaandikia rasmi kuwapa utaratibu wa kurejea nyumbani

Chanzo: ITV habari
asante Mungu kwa kuamua ugomvi
 
Back
Top Bottom