Mnyika: The Social Security Laws (Ammendments) Act wa mwaka 2012 kwa hati ya dharura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika: The Social Security Laws (Ammendments) Act wa mwaka 2012 kwa hati ya dharura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Communist, Oct 30, 2012.

 1. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Posted: 29 Oct 2012 05:35 AM PDT

  Awali ya yote niwatikie nyinyi wanahabari kheri ya sikukuu na kupitia kwenu nifikishe salamu kwa ndugu zetu waislam na watanzania wote katika kuadhimisha Iddi Ell-Hajj.


  Tarehe 15 Oktoba 2012 nilitoa taarifa kwa umma kuwa niliwasilisha kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuwasilisha Muswada Binafsi wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (The Social Security Laws (Ammendments) Act wa mwaka 2012 kwa hati ya dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 81 ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka 2007) iwapo Serikali haitatoa kauli kwa umma ya ratiba ya kupata mapendekezo toka kwa wadau wa hifadhi ya jamii pamoja na kamati husika ya kudumu ya Bunge na kuwasilisha muswada husika bungeni kama ilivyoazimiwa bungeni tarehe 6 Julai 2012.


  Kufuatia hatua yangu na hatua za wadau wengine Serikali kinyume na msimamo wa awali ambalo ulielezwa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga tarehe 14 October 2012 ambaye alieleza kuwa marekebisho ya kurejesha fao la kujitoa hayatafanyika mpaka mkutano wa kumi wa Bunge mwezi Februari mwaka 2013; Serikali imechapa katika gazeti la Serikali Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na. 40 Juzuu namba 93 ambao katika sehemu ya 6 vifungu vya 13, 14 na 15 imependekeza kurejesha fao la kujitoa kwa upande wa mfuko mmoja wa mashirika ya umma (PPF) hata hivyo muswada huo haujawasilishwa kwa hati ya dharura kama ilivyoazimiwa na kuahidiwa.


  Kwa upande mwingine, sehemu hiyo ya sita ya muswada huo wa marekebisho ya sheria mbalimbali haijakidhi mahitaji na matakwa ya azimio la bunge la tarehe 6 Agosti 2012 lililoungwa mkono na wabunge katika kikao cha 41 cha Mkutano wa Nane wa Bunge na itasababisha mgogoro mwingine katika ya serikali na wafanyakazi kwa upande mmoja, wafanyakazi na waajiri kwa upande mwingine na kuathiri uchumi wa nchi na maisha ya wafanyakazi katika maeneo mbalimbali nchini kwa kutoresha fao la kujitoa katika mifuko mingine ikiwemo NSSF, PSPF na LAPF.


  Kwa kuzingatia kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara imeeleza kuwa Rais ndiye mkuu wa Nchi na Kiongozi wa Serikali na Ibara ya 34 imeeleza kwamba mamlaka yote yapo mikononi mwake na kwamba madaraka hayo yanaweza kutekelezwa na watu wengine kwa niaba yake na kwamba Ibara ya 35 imeeleza bayana kwamba shughuli zote za serikali zitatekelezwa na watumishi wa serikali kwa niaba yake; wakati umefika sasa wa wafanyakazi na wadau wengine kuchukua hatua za kuwezesha Rais kuingilia kati kabla ya mkutano wa Bunge kuanza tarehe 30 Oktoba 2012 kutumia madaraka na mamlaka yake kuondoa udhaifu uliojitokeza wa Waziri wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fredrick Werema na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Irene Isaka kutokutekeleza kwa wakati na kwa ukamilifu mapendekezo na maamuzi ya Bunge pamoja na ahadi za Serikali kwa wabunge.


  Mosi; Rais azingatie masharti ya Kanuni za Kudumu za Bunge na kutia saini hati ya dharura ya kuwezesha muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali wenye vifungu vya nyongeza vinavyowezesha fao la kujitoa kurejeshwa kwa mifuko yote ikiwemo NSSF, PSPF na LAPF kuwasilishwa bungeni. Kanuni ya 80 Fasili ya 4 inaelekeza kwamba "Muswada wowote wa sheria wa Serikali wa dharura hautaingizwa kwenye shughuli za Bunge bila ya kuwa na hati iliyowekwa saini na Rais inayoelekeza kuwa muswada uliotajwa kwenye hati hiyo ni wa dharura".


  Iwapo Rais hataweka saini hati ya dharura au Serikali haitawasilisha bungeni hoja kwa mujibu wa Kanuni ya 93 fasili ya 4 bunge litabanwa na fasili ya 1 ambayo inakataza bunge kushughulikia hatua zaidi ya moja katika mkutano mmoja wa bunge; tafsiri yake ni kwamba sheria hii itasubiri kupitishwa katika mkutano wa kumi wa Bunge mwezi Februari 2012 na hivyo wafanyakazi kuendelea kunyimwa mafao ya kujitoa kinyume na azimio la Bunge.


  Pili, Rais atengue tangazo na agizo la Mamlaka ya Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kueleza kuwa "kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo (ya 13 Aprili 2012) maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili kuwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa Wadau" ambalo limesababisha mifuko yote kuacha kutoa mafao ya kujitoa hata kwa wafanyakazi .


  Hii ni kwa sababu marekebisho ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa upande wa kusitisha fao la kujitoa yaliyofanyika tarehe 13 Aprili 2012 yalihusu zaidi Mfuko wa Mashirika ya Umma (PPF); hivyo hayakupaswa kabisa kutumika kama sababu ya kusitisha mafao kwa mifuko yote ikiwemo NSSF, PSPF na LAPF na kwa upande mwingine wafanyakazi wanaodai mafao hayo kabla ya kujiunga na mifuko hiyo walijiunga wakiwa wameelezwa kama kati ya haki na stahili zao ni pamoja na kupata fao la kujitoa mazingira yakilazimisha hivyo kabla ya pensheni ya uzeeni. Hivyo, kusubiriwa kwa marekebisho ya sheria hakupaswi kuwa kisingizio cha kuendelea kusitisha mafao yao ya kujitoa, ama sivyo Rais aeleze sababu za ziada za kuzuia mafao ya kujitoa kwa kuzingatia Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali juu ya uendelevu wa mifuko katika siku chache zijazo kufuatia kushindwa kwa makampuni na Serikali yenyewe iliyokopeshwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kuheshimu matakwa ya malipo ya mikopo kutoka mifuko husika ambayo fedha zake zinatokana na makato ya pensheni toka kwa wafanyakazi na waajiri.


  Rais arejee kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard) ya tarehe 7 Agosti 2012 za kikao cha 42 cha Mkutano wa Nane wa Bunge ambao nilishika mshahara wa Waziri Bunge lilipokaa kama kamati na "nilitaka ufafanuzi wa kisera wa Serikali pamoja na uamuzi wa kuahidi kwamba kwenye mkutano wa Bunge ujao italeta Muswada wa dharura kuhusiana na Fao la Kujitoa, nilitaka kauli ya Serikali juu ya agizo lilitolewa na SSRA la kusitisha utoaji wa mafao ya kujitoa katika kipindi hiki cha miezi sita (6) na kuhusiana na wafanyakazi waliosimamishwa katika hatua ya kudai hayo mafao.


  Sasa iwapo Wizara inatoa kauli ya kutengua sitisho hilo na vilevile inatoa kauli ya kutaka kurejeshwa kwa wafanyakazi waliosimamishwa katika hatua ya madai ya fao hili la kujitoa". Waziri wa Kazi na Ajira alijibu kuwa "tutalifanyia kazi agizo hilo", hata hivyo mpaka sasa agizo hilo la SSRA halijatenguliwa na wafanyakazi waliosimamishwa wengine hawajarudishwa mpaka hivi sasa na baadhi wamefukuzwa kazi kabisa kutokana na mgogoro uliosababishwa na Serikali kusitisha fao la kujitoa bila kuzingatia haki za binadamu, mazingira ya ujira nchini na ushirikishwaji wa wafanyakazi na wadau wengine muhimu wa hifadhi ya jamii.


  Wenu katika utumishi wa umma,
  John John Mnyika (Mb)
  26/10/2012

  [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  TUNASUBIRI KWA HAMU mabadiliko ya mswada huu hasa kwa hiyo mifuko mingine ya NSSF, LAPF na PSPF!
  Wako,
  Mwathirika
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hongera sana Mnyika

  Baadae tunaomba upiganie ku-harmonize formula inayotumika kukokotoa mafao ya wastaafu. Hili ndilo lengo kuu la kuanzishwa SSRA lakini ninaona Irene Isack amerukia mambo mengine, kama hilo la kuondoa fao la kujitoa wakati wenzetu ambao hawana fao hilo hutoa fao jingine la UNEMPLOYMENT BENEFIT.

  Kama hawana pesa za kuhonga RUSHWA kwenye General Election imekula kwao! BTW 2015 tunawaweka madarakani, hawa CCM wametuchosha na vitimbwi vyao!
   
 4. e

  ezra1504 Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusaidie jembe letu maana hatuna mwingine wa kututetea. Hawa wezi wamechukua kila kitu sasa wanatunga sheria za kutuibia tena wafanyakazi masikini km sisi, hapa bora nikaajiriwe kwa wahindi, mshahara kwenye bahasha hakuna kodi wala mafao, ukipata chako unatokomea. Wengine waliacha kazi let say January or February, wakaambiwa wasubiri for 6 months ndo wafuatilie mafao yao, sheria imetungwa wakiwa nje ya kazi ila wamenyimwa pesa zao kwa sababu mpk July hawakuwa wameshfungua madai. Hii nchi imejaa wezi hasa huyo Irine sijui ni mume gani amemuweka hapo.
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Ish! Mbona LAPF wanaendelea kulipa mafao ya kujitoa kama kawaida. Mie nimelamba zangu juzip tu.
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  labda ulijaza form kabla ya hiyo sheria kupitishwa..
   
 7. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mimi nikiwa mmoja wao. Na ndo maana I will not compromise on this ishu. Halafu wao wenyewe wanaona kabisa sijachangia mfuko miezi kadhaa na bado wanataka niishi vipi hapa mjini?
   
 8. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Katika vitu vilivyotibua ubongo wangu, ni hii issue ya kukopwa kwa lazima na ccm, plz kikwete we need our money!
   
 9. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Lile deni la NSSF kwa serikali juu ya UDOM sasa ndo halilipikin kabisa aise jiandaeni kudai mafao na kuambiwa subirini michango ya mwezi huu iingie. Deci type.........
   
 10. m

  malaka JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hii ndio serikali yenye slogan ya usikivu.
   
 11. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Uli lodge lini claims? Mimi nilipeleka mwezi uliopita wakaniambia nisubiri
   
 12. T

  Technology JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  maandamano, migomo na kuchoma moto ofisi za NSSF na zingine lini?
   
 13. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huu ni udhalimu sana. Serikali inawaibia wananchi wake hadharani. Tunashukuru sana Mnyika na tunaamini kuwa hii haki yetu ya msingi tutaipata tuuuuuuuuuuuuuu............... sooooooooooooooooooo saaaaaaaaaad
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Thanks Mnyika kwa hilo
   
 15. S

  Shembago JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fedha na dhahabu ni mali ya Bwana dunia na wote wakaao ndani yake,Sasa kama ni Mali Ya Mungu na tuone kama haya magamba yataweza kudhulumu kwa uroho wa madaraka!
   
 16. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yanadhulumu tayari, Prof mmoja alistaafua akapata 30M halafu mwalimu mmoja namfahamu alilamba 160M, mifuko miwili ya serikali moja. Hapa suala la harmonization ni kizungumkuti.
   
 17. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280

  katika hili suala la fao la kujitoa mbona simsikii mh. Zitto?
   
 18. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Labda yuko PPF, Natania tu.
   
 19. Mtingaji

  Mtingaji JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 1,217
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kama wakiendelea kung'ang'ania pesa za watingaji, Dunia itashuhudia mikono ya Vasco wa Msoga imejaa damu siku si nyingi!
   
 20. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mimi hata leo nipo tayari, nipo maeneo ya Ubungo nimekuja na form zangu tayari so kwa kuwa kesho ntakuwa ofisi za NSSF Kinondoni pale maeneo ya Ubungo Bus Terminal please niambieni niende na kichupa cha petrol.Nasema kweli kama hawatataka tuchukue pesa zetu maafa zaidi yanakuja lazima hatutakubali pesa zetu wachezee hawa mambwiga, wale hizo hizo za serikali kupitia budget zao lakini chetu watupatie
   
Loading...