Mnyika, Suzan wamtaka Pinda kuweka ripoti hadharani Ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika, Suzan wamtaka Pinda kuweka ripoti hadharani Ubungo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Aug 10, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuweka hadharani ripoti aliyokabidhiwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG) kuhusu ufisadi unaofanyika katika kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo.
  Akizungumza katika mkutano mkuu wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mnyika, alisema waziri mkuu anatakiwa kuwa muwazi na kuweka hadharani ripoti ambayo amekabidhiwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hivi karibuni.
  Alisema ana taarifa za uhakika kuwa waziri mkuu ameshakabidhiwa ripoti hiyo ambayo alidai kuwa imejaa ufisadi.
  “Waziri Mkuu anatakiwa kuwa muwazi na kuelezea taarifa hiyo kwa uwazi kwa kuwa CAG amefanya ukaguzi na taarifa ni kwamba tayari amekabidhiwa ripoti hiyo siku nyingi, sijui kwa nini anashindwa kutoa ripoti hiyo,” alisema Mnyika.
  Mnyika, ambaye katika mkutano huo ndiye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa suala hilo ambalo linaonekana kufumbiwa macho, yeye tayari alishazungumza tangu mwaka 2005, lakini serikali inayoongozwa na CCM walilifumbia macho suala hilo, kwa kuwa kituo hicho kinaongozwa na watoto wa kiongozi aliyemo ndani ya CCM.
  Alisema anaamini kufumbiwa macho kwa suala hilo kunatokana pia na serikali za mitaa ya Halmashauri ya Kinondoni kuongozwa na madiwani wa CCM ambao wanashindwa hata kuwatetea wananchi wao katika masuala ya msingi kama hayo.
  “Ufisadi ndani ya Halmashauri ya Kinondoni umezidi kupita wilaya zote, ni kutokana na Kinondoni kuwa na madiwani wengi wa CCM, ambao kwa namna moja ama nyingine wanashindwa kukemea ufisadi unaofanywa na viongozi wa halmashauri, kwa kuwa watendaji wote wametoka katika chama kisichojali masilahi ya wananchi,” alisema Mnyika.
  Akizungumzia msimamo wa CHADEMA, alisema watafanya maandamano hadi katika stendi ya Ubungo ili kushinikiza waziri mkuu kutoa uwazi wa ripoti hiyo. Akizungumzia ufisadi, alisema kwa sasa taifa limegawanyika katika makundi makuu matano, ikiwa ni pamoja na kundi la wanafiki, mafisadi, la watu ambao hawapambani na hawako katika harakati za kupambana na ufisadi huku wakisubiri kundi la ushindi ndipo wawe nalo pamoja.

  Makundi mengine ni la watu ambao hawajali na wala hawapo upande wowote na wala hawajihusishi na masuala ya siasa na kundi la wapambanaji kama walivyokuwa chadema.
  Alisema kuwa suala la kupambana na ufisadi si la kitaifa, linatakiwa kuanzia katika ngazi za chini hadi kufikia ngazi za juu, hivyo aliwataka wananchi kuchagua viongozi wa serikali za mitaa kupitia chadema.
  Naye Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho, Susan Lyimo, alisema Manispaa ya Kinondoni inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi, siasa na elimu kutokana na viongozi wake kutokuwa makini na rasilimali za taifa.
  Alisema kutokana na matatizo mengi yanayokikabili chama hicho, aliwataka wajumbe kujipanga sawa sawa katika uchaguzi wa madiwani huku akiwataka wananchi kufanya mabadiliko kama ilivyokuwa kwa Karatu, Kigoma Kaskazini na Tarime.
  “Kutokana na matukio mbalimbali, ikiwa pamoja na kunyang’anywa ardhi kwa wananchi na migogoro ya viwanja, wananchi wanatakiwa kubadilika ili kuweza kuachana na CCM, kwa kuwa ni chama ambacho hakitaki maendeleo ya Watanzania, bali kinataka kuwakandamiza na kuwadumaza kiuchumi,” alisema Lyimo. Jimbo la Ubungo walifanya mkutano mkuu ukiwa na ajenda tano, ikiwamo kuzungumzia hali ya kisiasa, uchumi, jamii katika halmashauri hiyo, mikakati ya kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, uchaguzi ngazi ya jimbo wa chama hicho, kupata viongozi katika Baraza la Vijana (BAVICHA), Baraza la Wanawake (BAWACHA) na Baraza la Wazee.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ripoti si ipo humu au nyika hasomi JF?
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mheimiwa sana Game Theory kwa heshima na taadhima nakuomba uweke hiyo link hapa ili nasi tupate kuipitia asante
   
Loading...