Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Tatizo kubwa hao wanawake wana mahusiano na viongozi hii ni tatizo.

Nimeshangaa Mdee, anasema zaidi ya mara moja wana baraka za Mbowe na Mbowe yupo kimya tu.

Chadema wasipokuwa makini kwenye hii issue basi tena safari ya kuwa kama TLP au NCCR Mageuzi imewadia.
 
Ukiona kifaranga kiko juu ya mti jua kimewekwa.

Najua Mbowe na Salum Mwalimu ni marafiki sana
Na Pia Mbowe na Mdee ni marafiki sana

Hii kitu ndani ya Chadema huenda imechezwa na Mbowe, Salum Mwalimu na Halima Mdee.

Inawezekana Wamemzunguuka Mnyika kwa sababu ni kikwazo!

Kitendo cha Mdee kumshukuru Mwenyekiti kwa kuwapa baraka zake ni dhahiri kuna mchezo mchafu kutoka ofisi kubwa ndani ya CHADEMA

Salum Mwalimu na Mbowe lazima waje clean kwenye hii ishu
 
Andiko lako naliunga mkono ndugu!

Mbowe amefanya mambo mazuri mengi CHADEMA lakini kwa sasa apumzike, akae pembeni pamoja na kijana wake mtiifu Salum Mwalim.
 
Tatizo kubwa hao wanawake wana mahusiano na viongozi hii ni tatizo.

Nimeshangaa Mdee, anasema zaidi ya mara moja wana baraka za Mbowe na Mbowe yupo kimya tu.

Chadema wasipokuwa makini kwenye hii issue basi tena safari ya kuwa kama TLP au NCCR Mageuzi imewadia.
Mbowe mara nyingi sio muongeaji, ila baada ya kikao cha kamati kuu, lazima ataongea kutoa mrejesho.
 
Mkuu Una uhakika lakini na unachosema , Bora upige kimya tuu....hakuna chama palee
Kama hakuna chama mbona serikali inahitaji wabunge kutoka hapo.
Nikuache utafakari hilo kwanza huku nikifikilia uwezo wako kiakili.
 
Binafsi naamini mtu pekee anayeweza kuuelezea uhalali wa ubunge wa Nusrat Henje ni mh Spika Job Ndugai aliyemuapisha na siyo bush lawyers wa mitaani.

Kumuapisha mtu akiwa ameshika kitabu kitakatifu siyo jambo dogo.

Masaa 24 ni mengi sana kuweza kufanya mambo muhimu na yakakamilika kwa sababu tunaishi kwenye dunia ya sayansi na teknolojia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mnyika naye akili yake mbaya. Angehoji kwanza lissu kujaza fomu kwa mtandao na kuchaguliwa mgombea urais huku mkimbizi na mgonjwa wa akili😂😂. Nusrat anaweza pia amejaza fomu za NEC kwa mtandao. Hakuna kitu kingezuia Nusrat kuchaguliwa viti maalum akiwa rumande.
 
Peleka upuuzi huko.
Mimi sio mwanachama wa Chadema kama ndicho unachomaanisha.

Halafu kama hujaridhika na maelezo ya huyo katibu wao si unaweza ku-hire private investigator awachunguze.
Idiot.
Wewe ukiridhika inatosha.

Papai bovu.
 
Nimejaribu kutafakari sana kuhusu vichwa nilivyokuwa naviamini sana kwa misimamo yao ya kisiasa lakini wameamua kuchukua hatua kali ya kujitosa Bungeni aidha kwa nguvu yao au kwa kibali cha chama

Ukirejea maelezo ya katibu mkuu ni dhahiri chama hakina baraka ktk tukio hilo lakini upande wa pili m/kiti wao anaashiria kama yalikuwepo malumbano juu ya kupata muafaka

Sasa ni nini kimewasukuma kutenda hayo;-

1: Inawezekana hasara walizopata zimewachanganya gharama ya kampeni , kesi zisizokwisha, majeraha ya vipigo, kuwekwa rumande mara kwa mara na kudhalilishwa kwa ajili ya kutafuta maisha rafiki kwa wananchi

2: MREJESHO haukupatika maana yake ili tuvune mazao mazuri na mengi ni sharti tushiriki wote kuanda, kulima na kuvuna (nguvu ya pamoja)

Uchaguzi huu kila mtu kauona kwa hali kama hii iliojitokeza unadhni 2025 kunaweza kuwa na mabadiliko kwa wapiga kura hawa hawa? Ni kiongozi gani wa kisiasa atakubali kuathirika kwa ajili ya wananchi? Ambao hawana uwezo wa kujitetea?

Mm nashauri hao walioapishwa wasitengwe washirikiane na viongozi ili wajaribu kutafuta plan B waendelee kuwaelimisha wananchi naamini tukikaa nao vizuri watatufahamisha dhumuni lao la kuwa Wabunge

Nawaomba wanamageuzi wote kutokata tamaa ziko mbinu nyingi za kuleta mabadiliko tuwaamini viongozi na kuyafuata maelekezo yao
 
Back
Top Bottom