Uchaguzi 2020 Mnyika: Rufaa za madiwani ni 574 , zilizotolewa uamuzi ni 195. Wabunge 18 walioshinda rufaa hawajapewa barua, hawawezi kujinadi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,419
215,182
_Mpaka sasa, @tumeyauchaguzi_tanzania imeshuhulikia rufaa 195 tu za udiwani kuto ( 449 X 640 ).jpg

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh John Mnyika alipokuwa anaongea na wanahabari , kumbe hata wale wabunge walioshinda rufaa zao bado mpaka leo hawajapewa barua, na kwa sababu hiyo hawawezi kuanza kampeni.

Taarifa za wajuzi wa mambo zinaonyesha kwamba hii mbinu ya konokono ni mradi wa Tume yenyewe ili kuwachelewesha wagombea wa CHADEMA kuanza kampeni.
 
Mbona yule mgombea ubunge wa ACT wazalendo kashinda rufaa juzi na jana amepewa barua yake na msimamizi wa jimbo la Singida magharibi!!
 
Hii Tume ya UCHAFUZI ipo kwa maslahi ya CCM, itoshe tu kusema UHUNI, UFEDHULI, DHULMA NA UHALIFU wa namna viwe ni chachu ya kuwafurusha hawa WATEKA NYARA hapo Oktoba. Iwe kupitia sanduku la kura ama MAANDAMANO MAKUBWA SANA yasiyo na kikomo, tupate Serikali itakayoheshimu Katiba ya Wananchi.
 
Atoe majina ya wale waliopitishwa kugombea, wale ambao hawajapokea barua, wale ambao wametenguliwa na wale wanaongoja majibu.

Amandla....
 
Upinzani Nchi hii hasa Chadema wanachukuliwa kama wahaini vile ,hata zile Haki zao za kikatiba wana nyang'anywa na wanaotakiwa kuzitoa.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom