Mnyika : Ole Sabaya alihusika kuwabambikia kesi makomandoo 3 ili kumuondolea ulinzi Mbowe apate kumdhuru

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,610
141,432
Hii sasa ni mpya Katibu mkuu wa CHADEMA mh J J Mnyika amemtaka DPP kufuta kesi inayomkabili mwenyekiti Mbowe baada ya Ole sabaya kuhukumiwa kwa ujambazi.

Mnyika anasema Ole Sabaya ndiye aliyesuka mipango ya kuwabambikia kesi makomandoo watatu ili Mbowe akose walinzi aweze kumdhuru.

J J Mnyika ameandika katika page yake ya Twitter.

Sabato njema!
 
Hii sasa ni mpya Katibu mkuu wa Chadema mh J J Mnyika amemtaka DPP kufuta kesi inayomkabili mwenyekiti Mbowe baada ya Ole sabaya kuhukumiwa kwa ujambazi.

Mnyika anasema Ole sabaya ndiye aliyesuka mipango ya kuwabambikia kesi makomandoo watatu ili Mbowe akose walinzi aweze kumdhuru.

J J Mnyika ameandika katika page yake ya twitter.

Sabato njema!
Na ww sabato njem
 
Mbowe yeye anatuhumiwa kupanga mipango miovu ya kuvuruga AMANI YA nchi.
sasa wewe jiulize mtu anaye taka kuvuruga amani ya nchi unajua madhara yake ni makubwa kiasi gani?! ni hatari kubwa sana na kama akikutwa na hatia anastahili adhabu kali zaidi ili iwe fundisho kwa wanasiasa wengine wanao jaribu kuchezea amani ya nchi
yaani huwezi kulinganisha makosa ya unyanganyi, n.kna makosa ya mbowe ya kupanga njama za kuvuruga amani ya nchi, Amani ya nchi ndio inayo tufanya leo tunafurahia haki kutendeka, amani ya nchi ndio mpango mzima, leo hii Mbowe na Genge lake la kihalifu wanadaiwa kupanga njama za kuvuruga amani ya nchi iliyo tengenezwa na kulindwa kwa zaidi ya miaka 60!!
Amani ya nchi yetu ni ya thamani kubwa sana kuliko mbowe au mtu yeyote yule, atakaye bainika kuchezea amani yetu atashughulikiwa bila huruma.
 
Sabaya anatuambia akiwa mtumishi wa umma Mbowe na genge lake walikuwa wakimuwinda na taarifa alizitoa kwa mamlaka.

Mbowe anatuambia Sabaya alikuwa akimtishia maisha kiasi cha kutuonyesha CCTV footage fulani fulani....Leo Mnyika anatuambia Sabaya alisuka mipango Mbowe asiwe na ulinzi wa wale makomandoo ili aweze kumdhuru..

Mwisho wasiku Sabaya alikuwa na walinzi wake mabaunsa ambao amehukumiwa nao 30yrs..
Mwisho wa siku Mbowe anawalinzi wake makomandoo kesi iki mahakamani bado inalindima...

Kwenye kesi ya Mbowe, Jamhuri inaweza kumbebesha mzigo Sabaya na Genge lake na Mbowe akawa huru huku Jamhuri ikijivua na kumuacha Sabaya peke yake kama mhuni aka kiongozi wa umma aliyemtengenezea Mbowe mazingira na Jamhuri ikaamini mpaka pale mahakama ilipong'amua na kumtema Mbowe...
Kunaweza pia kuwepo vielelezo vinavyothibisha pasipo na shaka juu ya tuhumu za Mbowe kufanya uhalifu unaofanana na ugaidi kupitia watu wake na yeye akiwa mtoa amri na financer pia.. hapa Shahidi anaweza kuwa Sabaya pia na mahakama ikakubaliana naye na hatimaye Mbowe naye akala miaka...

Kwa hizi kauli za kina Mnyika na haya matukio kuna hatari hii inawezekana ilikuwepo dhidi ya Mbowe na intelejensia yake ikashindwa kung'amua, inawezekana alitegwa naye akategeka...
 
Kuna hatari Sabaya na viongozi wengine wa umma walitumika kumtega Mbowe kwa kumbughudhi, kumnyima amani na hatimaye naye kukosa uvumilivu na kuamua either kujibu mapigo au kupanga kujibu mapigo huku nyuma nyendo zake zikifuatiliwa ili kukusanya ushahidi, NI MTAZAMO TU, tujaribu kuwa makini kwa kucheza pande zote kumnasua kuliko kupiga makelele tu kaonewa kaonewa kumbe alitegwa akategeka....
 
Mbowe yeye anatuhumiwa kupanga mipango miovu ya kuvuruga AMANI YA nchi.
sasa wewe jiulize mtu anaye taka kuvuruga amani ya nchi unajua madhara yake ni makubwa kiasi gani?! ni hatari kubwa sana na kama akikutwa na hatia anastahili adhabu kali zaidi ili iwe fundisho kwa wanasiasa wengine wanao jaribu kuchezea amani ya nchi
yaani huwezi kulinganisha makosa ya unyanganyi, n.kna makosa ya mbowe ya kupanga njama za kuvuruga amani ya nchi, Amani ya nchi ndio inayo tufanya leo tunafurahia haki kutendeka, amani ya nchi ndio mpango mzima, leo hii Mbowe na Genge lake la kihalifu wanadaiwa kupanga njama za kuvuruga amani ya nchi iliyo tengenezwa na kulindwa kwa zaidi ya miaka 60!!
Amani ya nchi yetu ni ya thamani kubwa sana kuliko mbowe au mtu yeyote yule, atakaye bainika kuchezea amani yetu atashughulikiwa bila huruma.
Ndugu yangu BINADAMU Wana akili Sana sio Kama wanyama.
Kuna maeneo huhitaji hata kujua Sheria kuyaelewa.

HAKI huwa inaonekana na DHULUMA huwa inaonekana.

Mahakama ikiamua kwa HAKI itaonekana na Mahakama ikiamua isivyo HAKI pia itaonekana.

Kulinda Heshima yake, mahakama itabidi IAMUE kwa HAKI Kama ambavyo inapaswa IWE.
 
Back
Top Bottom