Mnyika: Nyalandu na mwenzake ni wasaliti, wameshindwa kuvumilia baada ya mateso ya kuporwa ushindi wa ubunge mwaka 2020

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,103
2,000
Ni lini mpiga scrub akaishi kwa wagumu? Kulala njaa siku moja tu anatoa siri zote za familia ili apate sahani ya ubeche na nyama....mchezo!!

Kuna watakaoumia ili Tanzania ifike inapotakiwa!!
 

Stonembag

Member
Oct 21, 2020
42
125
Chadema na nyie watu wakihamia kwenu muache kuwapa nafas za juu .Pumbaka!!!Mtu akija huko akubal kuwa mwanachama wa kawaida tu
 

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
7,660
2,000
Mnyika anashindwa kusema ' we wish them all the best' huko waendako?

Why ana invite siasa za vijembe?
Na siasa za ukamanda na uhanaarakati bado zipo?..

Huu ni mwaka 2021 na Rais ni Samia kutoka Zenji...
Kuendeleza siasa zilezile ni kujiua kisiasa
Naona kama mnawaonea wakina Mnyika. Wao wana tofauti gani na wapinzani wao ambao wanasema wazi kuwa hamna mabadiliko, kazi inaendelea? Kwa nini mabadiliko mnataka yawe ya upande mmoja tuu?

Wataachaje siasa zao za zamani wakati mpaka sasa wanazunguka nchi nzima kuwatolea dhamana na kuwatetea wanachama wao wenye kesi za ajabu ajabu? Wataachaje wakati watu ambao hawakuwateua wanapigiwa kifua ili wawakilishe bungeni? Wataachaje ikiwa mpaka leo hamna tamko la kufuta zuio la mikutano ya hadhara? Mtu anapimwa kwa vitendo vyake, sio maneno.

Amandla...
 

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
7,660
2,000
Nyalandu amesema mojawapo wa vitu vilivyomfanya arudi nyumbani ni kukosekana lugha za staha na kumchukulia unaepingana nae kuwa adui huko alikotoka.

Kwa mtazamo wake lugha ya kebehi aliyokuwa anaitoa Polepole kwa mtu aliyemzidi cheo na umri ndio staha anayoitamani? Vitendo vya watu kama Ole Sabaya dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wake vinafanywa kwa sababu wanampenda na kumheshimu sana Mbowe? Maneno ya ovyo waliokuwa wanaambiwa wabunge wao wanawake bungeni ilikuwa ni kwa sababu ya upendo? Na lugha ambayo mpaka sasa Spika na wabunge wake wanatumia dhidi ya watu ambao hata bungeni hawapo, yeye anaona ndio zinazotakiwa?

Anazungumzia uchaguzi huru na uwezo wa wajumbe wa kuwaengua vigogo lakini anasahau kuwa wengi tu walio kataliwa na wajumbe walirudishwa.

Anarudi mahali ambapo sasa hivi ushindi unaotakiwa ni 100% na sio 99%.

Nyalandu alijijengea heshima alivyotoka CCM na alivyoendesha siasa zake. Heshima hiyo angebaki nayo kama angeepuka kuwapiga vijembe aliowaacha. Kajiingiza mwenyewe kwenye ugomvi wa kwenye matope.

Amandla...
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,763
2,000
Mnyika anashindwa kusema ' we wish them all the best' huko waendako?

Why ana invite siasa za vijembe?
Na siasa za ukamanda na uhanaarakati bado zipo?..

Huu ni mwaka 2021 na Rais ni Samia kutoka Zenji...
Kuendeleza siasa zilezile ni kujiua kisiasa
Ndiyo siasa zetu Bongo! Yani nilipiga twita huko wakina Maria na Fatuma wao wanapost twite ata 20 kwa siku alafu sasa vitu vyenyewe wanavyoviandika vya kuandika wachanga na mashabiki wa siasa lakini unakuta wanaandika wao? Kwaiyo tu siasa za upinzani ni zakihanarakati zaidi.
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,095
2,000
Mnyika anashindwa kusema ' we wish them all the best' huko waendako?

Why ana invite siasa za vijembe?
Na siasa za ukamanda na uhanaarakati bado zipo?..

Huu ni mwaka 2021 na Rais ni Samia kutoka Zenji...
Kuendeleza siasa zilezile ni kujiua kisiasa
Wewe nae huna jipya,bora ungeendelea kukaa kimya tuu.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,159
2,000
Mnyika ujanja wake upo kwenye kuandika makaratasi tu
Ana uwezo mdogo sana kiuongozi
Anavyo struggle kumbomoa Mdee,huku Mdee akiwa kadindisha msuli,inaonesha kabisa KM Mnyika bado sana
Yaani hata Ado Shaibu ana uwezo mzuri kuliko huyo kikaragosi Cha Sultani Mbowe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom