Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

Hii kwenye taaluma yetu ya ujasusi tunaita fake news na disinformation,watu kama nyie ni spindoctors tu,mnajaribu kuweka mashaka kwa wananchi Ili waione Chadema haifahi.

Chadema inawatisha sana. Kwanini mambo ya ndani ya Chadema yanawakosesha sana usingizi ccm, nyie badala ya kujadiri kuhusu Nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi hakuna, wazee kuboreshewa maisha yao, big no, ila Mzee Mwinyi kuzawadiwa Benz!pesa ipo, 450Millioni zikatumika.

Kama mnyika ndio alipereka majina,wekeni fomu zao hapa, maana mnyika hakuweka sahihi yake.

Pili Barua aliyoandikiwa Spika kuhusu kufukuzwa hawa wabunge, imesainiwa na Mnyika, na ushahidi upo Bungeni,wekeni ushahidi kwamba Mnyika ndio alisaini fomu zao za kuteuliwa zilizoperekwa Kwenye tume, acheni kuweweseka kama kuku asiye na kichwa.

Tatu kusema Mbowe alitaka mkewe awe Mbunge, ni ujuha, nenda kasikilize Historia ya Mbowe, alianza siasa na biashara akiwa kijana mdogo sana, kazaliwa kwenye ukwasi, hawezi kuwa na njaa kama nyie mnaosubili kubusu makali o ya viongozi wenu Ili mpate uteuzi.
 
Kwa nini hiyo barua ya Mnyika aliyopeleka Tume haiwekwi hadharani?
Hilo lingeepusha Spika wa Bunge kukejeliwa kama ilivyo sasa na kupoteza heshima ya Bunge.
Tupunguze hadithi za kutunga
Sasa kama tumeimegoma kuiweka hadhalaniii, kwa nini chadema isichukue jukumu la kwenda mahakamani kuomba ushahidi huo?
 
TUME ya UCHAGUZI walipokea majina kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Mnyika kama sheria inavyotaka. Tatizo ni Mnyika alipogombezwa na akina Mbowe na John Mrema kuwa katika majina yale hakuna watu wao, ndipo aliamua kuwageuka akina HALIMA Mdee ili aweze kujikosha kwa akina Mbowe
Umesoma barua za Chadema kwenda kwa Speaker? Umesoma barua ya kwenda time au unahorojeka tu?
 
Mwakibinga hauna social legitimacy ya kuzungumzia swala hili
IMG-20210510-WA0058.jpg
 
Mpaka mtu anachomolewa maabusu usiku na kuapishwa asubuhi. Mahakamani hakuasaidia chochote. C19 waliteuliwa na CCM kwa maslahi yao.
Kwahiyo mumeona mahakama haifai kuwapa haki. Sasa hao vikongwe wamama bawacha wanaohangaika na ndugai watawaletea mwalobaini wa hilo tatizo huku viongozi wanaume wa chama wamestarehee??? Achani kutudanganya
 
Wewe ni tume ya uchaguzi?
Kama sio tume umejuaje kuwa Mnyika ndio kapeleka majina?
Siku nyingine usiweke namba ya simu pekee bali weka na akaunti namba kabisa
Mshauri Mnyika aende mahakamani au aite BARAZA KUU ukiona hafanyi hivyo jua anacheza na akili yako.
 
... Mkuu Erythrocyte kwenye uzi fulani alihoji hivi ni kwanini verified members wengi wa JF mara nyingi huanzisha threads "takataka"; this is another proof!

Nikuulize swali moja tu; je, ni Mnyika na Chadema walioenda kumtoa Nustrat Henje gerezani usiku na muda mfupi baadaye akaapishwa kuwa mbunge? Ujinga ni mzigo kweli kweli!
Akijibu tujulishe
 
Yamesemwa mengi kuhusu wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema. Sijui ni kwanini Chadema hawajifunzi, hawabadiliki? Viongozi wake wanafikiri migogoro kubishana bishana ndio siasa, hapana. Chadema ni chama kinachopendwa sana lkn uendeshaji wake kwa maana ya uongozi ndio shida.

Viongozi wake wamekuwa watu wanaokaza shingo muda wote, hawataki kubadilika, hawataki kukubali yaishe ili maisha yaendelee, wanashikilia jambo lile lile hata kama halina manufaa yoyote. Kilichotokea katika uchaguzi wa 2020 kila mtu mwenye macho na masikio anafahamu hii sio siri!

Maji yakimwagika hayazoleki! Baada ya uongozi wa Rais Mama SASHA (Samia Suluhu Hassan) ni ukweli ulio wazi siasa za Tanzania zimekuwa za wazi na maelewano angalau, watu wameanza kuongea mambo kwa uwazi. Ningekuwa mimi ni kiongozi wa Chadema ningepiga moyo konde na kuanza upya kuepuka mapambano ndani ya chama.

Wabunge hawa 19 mimi ningewasamehe kwani tatizo ni nini? Kwani wameua? Wote tunajua msimamo wa Chadema kuhusu tuhuma za EL kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015!

Sasa kama Chadema waliweza kumkaribisha EL na kumupatia nafasi ya kugombea nafasi ya juu kabisa ya kiti cha uraisi 2015 wanashindwa nini kuwasamehe hawa wabunge 19?

Misimamo ya baadhi ya hawa wabunge 19 inajulikana, kupambana kwao kunajulikana vizuri, wamefungwa gerezani, wamekaa sana mahabusu, wamepata kila adha ya misukosuko ya kisiasa, ni kwanini Chadema hawakumbuki yote haya na kuwasamehe hawa wabunge 19 ili maisha yaendelee na siasa nzuri na zenye hoja zianze?

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan (Mama SASHA) amekaribisha siasa za uweledi na ustaarabu na kuliunganisha taifa, ni kwanini Chadema hawajifunzi ili nao wakaleta maelewano ndani ya chama chao kwa kuzingatia ule usemi usemao "yaliyopita si ndwele tulonge yaliyopo na yajayo" sijui kama nimeukumbuka vizuri usemi huu, lakini lengo la usemi wenyewe ni kwamba tusonge mbele tuachane na yale yote yanayotukwaza!

CHADEMA ACHANA NA HAWA WABUNGE 19 TUJENGE TAIFA LETU PAMOJA.
 
Back
Top Bottom