Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,957
2,000
Kumaliza Mgogoro wa Wabunge 19 Tume ina Nafasi Muhimu ya Kuumaliza.
1 Tume ya Uchaguzi iueleze Umma wa Watanzania Utaratibu ULIVYO Kisheria Wabunge wa Viti Maalumu Mchakato wa Kuwapata Ukoje ili tujue kama hao 19 waliufuata kisheria...
Tatizo Mahela aliwekwa hapo kupokea na kutekelezwa maagizo toka juu. Inawezekana kabisa hata hizo sheria na Taratibu zilizotumika hazijui.

Actually, Kati ya watu wanaotakiwa Kuondolewa kabisa kazini kwa kuwajibidhwa kwa sababu ya ukiukwaji wa viapo vyao ni huyu bwana Mahela na Mwenyekiti wake wa Tume!!
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,399
2,000
Huu mgogoro hautaiacha salama tume
Tume na Ndugai ni wahanga tu,wameachiwa mzigo na mwendazake,ili kuzihadaa jumuia ya kumataifa,

Nusrat Hanje alikuwa Jela na hakuachiwa na mahakama,ni hakimu gani aliamlu atolewe Jela usiku wa manane?
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,399
2,000
Huu mgogoro hautaiacha salama tume
Tume na Ndugai ni wahanga tu,wameachiwa mzigo na mwendazake,ili kuzihadaa jumuia ya kumataifa,

Nusrat Hanje alikuwa Jela na hakuachiwa na mahakama,ni hakimu gani aliamlu atolewe Jela usiku wa manane?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
8,771
2,000
Kumaliza Mgogoro wa Wabunge 19 Tume ina Nafasi Muhimu ya Kuumaliza.
1 Tume ya Uchaguzi iueleze Umma wa Watanzania Utaratibu ULIVYO Kisheria Wabunge wa Viti Maalumu Mchakato wa Kuwapata Ukoje ili tujue kama hao 19 waliufuata kisheria
2.Tume ya Uchaguzi iijibu barua ya Chadema ambayo huu ni Mwezi wa 5 hawataki Kuujibu kwanini Wanasita kutoa Majibu?
3.Tume ya Uchaguzi Utufafanulie Watanzania ilikuwaje Yule Mwanachama wa Chadema alikuwa Mahabusu akatolewa Usiku na kwenda kuapishwa je Mchakato wake nae ulikuwaje

Mkuu uliyoyanena yatatokea tu katika nchi ambayo utawala wa sheria na haki umetamalaki. Huwezi kuyapata au hata kuyategemea hayo ambapo utawala wa dhuluma umetamalaki katika nyanja zote.

Hayakupatikana hayo kwenye kipindi cha awamu ya tano kwa sababu hizo hizo. Acha tuone mama anajipambanua vipi kwenye uongozi wake kwani hata hili lipo wazi likimkodolea macho.

Hiiiiii bagosha!
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,635
2,000
Kama mnajua hakuna mahakama, hakuna bunge vyote mali ya CCM wewe na Mnyika mnalialia nini mitandaoni!?.. nendeni kwa Samia ndo pa mwisho au waache akina Mdee wale pesa za ubunge.

Huku mitandaoni sisi ni eneo letu la kujidai ama unakonda? Nasema hivi, hakuna mahakama nchi hii, bali kuna majengo ya mahakama yanayosimamiwa na vilaza wa ccm fullstop.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,725
2,000
Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika ameonyesha form 19 zilizotumwa na NEC kwenda CHADEMA ili wazijaze baada ya kupendekeza wabunge 19 na kuzirudisha NEC

Kutokana na msimamo wa CHADEMA kutokubali matokeo ya uchaguzi haikukubali huo wito na hivyo hizo form hazikujazwa na bado zipo ofisini.

Sasa hao 19 wabunge walipendekezwa na nani na hizo form zilisainiwa na nani

....https://www.instagram.com/p/COklYManMr9/?igshid=173lqyfze638s
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
28,646
2,000
Hao Nec na huyo Ndugai watueleze hayo Majina 19 ya covid waliyatoa wapi?

jath.gif
 

Baikije

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
533
998
itisheni baraza kuu la chama chenu Chadema majibu mtakutana nayo huko ambako wamekata rufaa na wako tayari kuongea yote huko.Nendeni mkayaongee huko kwenye mkutano wa baraza kuu mnaoukwepa kuuitisha
Mbona unademka mkuu swali fupi tu maelezo meeeeengi, nani alipeleka majina ya uteuzi? Kwisha
 

Lutifya

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,500
2,000
Hicho ki despatch ulichoweka ni cha CHadema cha NEC kiko wapi? alichosaini mtu wa CHadema? Mnajitekenya na kujichekesha wenyewe.Hako KA DESPATCH kenu mwaweza kuwa mumejisainia ofisini kwenu

NEC wakipokea kitu huwa wana despatch yao ya NEC iko wapi
Punguzeni matumizi ya Serikali kwa kutowalipa wasiyohusika. Huo nao ni wizi dhahiri.
 

Hey

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
686
1,000
Kusema kwanini rufaa haijasikilizwa au Kwa nini chadema hawajaenda mahakamani ni kutokuwa mkweli. Chadema kwenda mahakamani haina maana Kwa sababu mbali mbali, moja ni kupoteza resources, muda, na kuwapa muda na sababu wavunja katiba kuendelea kuivunja Kwa kisingizio cha kusubiri maamuzi ya mahakama.
Pili ni kuweka precedence ya kukubali maamuzi huru ya chama kupokwa. Kama chama hakiwezi hata kuamua uanachama wa mwanachama kwa kutumia taratibu zao wenyewe wanabaki na haki gani? Hata hii wakaipiganie mahakamani? Wengine huko nyuma walipitishwa kwenye vigingi hivi walipofukuza wanachama? Kupeleka wanasheria na rasilimali nyingine za chama mahakamani ni kukubali kupokwa mamlaka, na pia ni kama wanapambana na kina Halima ambacho sidhani kama ni kweli au kina maslahi kwao. If anything, chenye maslahi zaidi ni wao kuwa na sababu ya kuonyesha uvunjwaji wa katiba, na kuhoji legitimacy ya chaguzi zilizosimamiwa na NEC, ikiwa moja ya taasisi zilizoshiriki kwenye hili pamoja na Nusrat kuachiwa huru na kuapishwa kesho yake. Mahera alifikia hatua ya kutuambia watanzania wanachotaka kwenye viongozi wa kuwachagua tukiwa kwenye uchaguzi. Kama hii haitoshi kuonyesha clear lack of credibility, hili la wabunge na Nusrat linaongezea chumvi kwenye kidonda. Kilichobaki ni kutafuta pa kuchomokea bila uwajibikaji, bila kushiriki kupaka tope chaguzi, bila kuruhusu ziibuliwe hoja za uhalali/ubatili wa vyombo na viongozi wake.
 

Philipo Mwakibinga

Verified Member
May 13, 2013
104
250
MNYIKA ALIPELEKA MAJINA 19 YA WABUNGE WANAWAKE CHADEMA.

Na: Philipo Mwakibinga.
0758910403

Uongo ukizungumzwa mara nyingi lazima unaweza kufanana na ukweli lakini kamwe hauwezi kubadilika kuwa ukweli maana bado utakua ni uongo tu.

JOHN Mnyika anajitahidi sana kuhakikisha ndugu yake Halima Mdee na Wenzake wanaonekana waovu mbele ya CHADEMA kitu ambacho hakiwezi kuwa kama anavyotaka. Mnyika anazunguka kuhakikisha kila Kiongozi wa Wanawake CHADEMA Mkoa anatoa tamko ili kutaka kuonesha kuwa HALIMA MDEE na wenzake 19 hawapendwi lakini ukweli ni kuwa ameamua kujipa kazi kwa kusaliti kazi aliyoifanya yeye mwenyewe.

John Mnyika kama katibu Mkuu wa CHADEMA alitimiza jukumu lake la kisheria kupeleka majina ya Wabunge viti maalumu 19 ambao leo wanatusiwa na kubezwa kwasababu ya ukigeugeu wa Mnyika. Hakuna Mbunge aliyejipeleka kwa SPIKA kama baadhi ya BAWACHA na BAVICHA wanavyosema bali ni janja janja ya Mnyika kutaka kuonekana yukosafi japo kwa muda mfupi maana hatodumu na uongo wake siku zote.

TUME ya UCHAGUZI walipokea majina kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Mnyika kama sheria inavyotaka. Tatizo ni Mnyika alipogombezwa na akina Mbowe na John Mrema kuwa katika majina yale hakuna watu wao, ndipo aliamua kuwageuka akina HALIMA Mdee ili aweze kujikosha kwa akina Mbowe. Mbowe anjaua, Lema anajua na Lissu anajua pia, hata Mnyika yeye mwenyewe anajua.

Mdee na wenzake 19 ni Kondoo wa weusi wa kafara tu! Kama kujipeleka kuwa Mbunge wa viti maalumu ni rahisi kiasi hicho basi Suzani Kiwanga angekua Bungeni, kwanini wengine hawajajipeleka? Mnyika anamakosa makubwa sana kama katibu Mkuu kwakuwaacha Mdee 19 Washambuliwe wakati anajua ukweli wa Mungu kuwa yeye ndiye alipeleka majina yale na wale ndiyo Wabunge sahihi wa Viti Maalumu CHADEMA.

KWANINI HAWAENDI MAHAKAMANI? Kamwe Mnyika na CHADEMA yake hawana ujanjanja wa Kwenda mahakamani hata kidogo kwakua wanajua MAHELA atawaumbua. Wataendelea kupiga sarakasi lakini hawawezi kwenda mahakamani kwani ukweli unadhihiri. Wale msiyojua acheni kuwashambulia akina Mdee 19 hawana hatia ni TAMAA za Baadhi ya viongozi wa CHADEMA zimewafikisha hapa na kinachoendelea ni MZUGO TU anaofanya Mnyika kiwaadaa WANACHAMA WA CHADEMA ila siku wakijua! Duuu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom