MNYIKA ndiye mpinzani namba 1 tishio kwa CCM na Serikali yake

na ndie mbunge pekee anayemiliki VITZ hadi sasa. wakati wengine wameshakimbilia mashangingi.
 
Sina comment mpaka atakapooa na kuwa na majukumu ya kifamilia kwanza. wote
tunajua kwamba wanasiasa wengi wazuri wamearibiwa na wake zao, watoto wao,
mashemeji na washenga.

aoe kwanza
 
Ni kweli kabisa lakini Mh Godbless Lema na Tundu Lisu tusiwasahau hawa ni wanasiasa machachari sana wanaomsumbua spika anne makinda.
 
Very true, I admire him so much! big up Mnyika fancy wako tuko nyuma yako.
 
Hakuna kijana mwenye uwezo mkubwa katika medani za kisiasa katika vyama vyote vya siasa kama Mh John Mnyika. Palipo na ukweli lazima usemwe, palipo na ukweli pia uongo hujitenga. Huwa anajua nini anachokichanganua katika kuchangia miswada mbali mbali hasa bungeni, mwepesi wa kujenga hoja nzito. Mweledi wa kisiasa ambaye huanza kuchambua mada taratibu na umakini mkubwa.

Hana papara wala hakurupuki wakati wa kujibu hoja mbalimbali, mpole anayejiamini. Hutumia busara katika maamuzi na husimamia kile anachokiamini. Jasiri mwenye kuchunguza mambo kwa undani, hana jazba. Hufichua hoja za msingi zilizojificha kiasi mara kadhaa ameweza kuthubutu kusababisha baadhi ya miswaada ya serikali kufanyiwa marekebisho makubwa bungeni.

Pamoja na umri wake mdogo, anafaa kushika nyadhifa za ngazi za juu katika chama na nchi kwa ujumla. Ana sifa nyingi ambazo ukurasa hautatosha kuzibeba kwa wingi wake. Huyu ni JEMBE la uhakika ambalo ni tishio kubwa kwa CCM na Serikali yake na LULU pevu inayopaswa kutunzwa na kuhifadhiwa na chama chake.

Tupo pamoja mkuu, mm pia namkubari sana huyu kijana.
 
hiyo title in ku-exclude wewe na ina demoralise wapambanaji wengine...

Mnyika is good , very good..kumweka number 1 kana kwamba tuna shindana kupambana na CCM umejidhalilisha sana...kibaya sana sababu unayoitoa eti anapanga hoja...na sio amefikisha maji kwa wananchi wake!! kuongea???....huku kisirisiri amefinya sh. laki mbili kibindoni na yuko kimya!!!

kupenda bwana!

wasifie wana siasa kwa uangalifu mkubwa mkuu........vijana wengi sana wako against CCM kuna wengine radical hata CDM hawawataki wala hawataki kuwapa nafasi...yaani wana hasira wamepitiliza! sema hauwajui!! wapo moyo na hao pia.........mwisho wa siku CCM ikitoka madarakani sifa ni kwa wote wala sio watu 17 kama JK! shame!

Hapo waberoya una lako? mtoa mada kazungumzia maswala ya bungeni na sio jimboni, sema ukweli Mnyika anastahili pongezi au ulitaka wamtaje Zito Kabwe? najua jinsi unavyomzimia. All in all Mnyika ni kichwa cha kuotea mbali!
 
Hizi (red) sio sifa bali ni tatizo kubwa la kiuongozi na uzalendo kwa nchi, hatuhitaji kiongozi mnyenyekevu kwa system, hatumhitaji kiongozi ambaye hayupo tayari kupingana na viongozi wake na chama chake pale wanapokosea/kinapokosea, ukimpata kiongozi mwenye sifa hizo fahamu kuwa hana uwezo wa kufanya chochote cha maana kwa ajili ya nchi kwani pull-forces za kulinda maslahi ya viongozi wake na chama chake zitamzuia...

Umenena! kuna wakati kuna kutofautiana si ndio ndio tu mkuu!
 
Kusaini kile ki toilet paper lilikuwa chaka la miba waliloingizwa viongozi wote wa CDM na msanii mkuu TZ bwana JK. We unadhani pale angefanyaje?

....kama aliweza kuingizwa chakani na vilaza wa magogoni kirahisi vile, huko kumwita tishio kunatoka wapi? tishio kwa nani, kwa wale wale waliomwingiza chakani, au?

mnyika is doing ok lakini inabidi akubali ukweli kuwa kwa kusaini kile kijikaratasi bila umakini ali-screw up big time and it's one of those political "lows" that he would love to see quickly erased!
 
namkubali sana mnyika. ni jembe la uhakika, CHADEMA itunzeni sana hazina hiyo. WATU WA UBUNGO BRAVOOOOO, KUWA NA MBUNGE MAHIRI.
 
hiyo title in ku-exclude wewe na ina demoralise wapambanaji wengine...

Mnyika is good , very good..kumweka number 1 kana kwamba tuna shindana kupambana na CCM umejidhalilisha sana...kibaya sana sababu unayoitoa eti anapanga hoja...na sio amefikisha maji kwa wananchi wake!! kuongea???....huku kisirisiri amefinya sh. laki mbili kibindoni na yuko kimya!!!

kupenda bwana!

wasifie wana siasa kwa uangalifu mkubwa mkuu........vijana wengi sana wako against CCM kuna wengine radical hata CDM hawawataki wala hawataki kuwapa nafasi...yaani wana hasira wamepitiliza! sema hauwajui!! wapo moyo na hao pia.........mwisho wa siku CCM ikitoka madarakani sifa ni kwa wote wala sio watu 17 kama JK! shame!

Mnyika namkubali because anatekeleza vizuri majukumu yake ya kuisimamia serikali. Si kazi ya mbunge(Mnyika) kupeleka maji ubungo; ni wajibu wa serikali inayoongozwa na CCM. Great thinkers ni vizuri tukawasaidia wananchi kutofautisha majukumu ya mihimili ya serikali; Executive(watendaji) wanayo kazi ya kutekeleza ilani ya Chama cha siasa kilichoshinda uchaguzi, wabunge wana kazi ya kutunga sheria na kuisimamia utendaji kazi wa watendaji wa serikali, mahakama ina kazi ya kutafsiri na kusimamia sheria. Nipo tayari kurekebishwa kama nimekosea

Hivyo basi kazi ya wabunge(including Mnyika) ni kuhakikisha serikali inafikisha huduma mbalimbali kwa wananchi wake. Hivi mbunge atapeleka huduma ya maji kwa wananchi kwa kutumia bajeti ipi?
 
myika anatisha na anajua siasa !
zito anaweza ila hufika mahala anashindwa kutofautisha siasa na utawala.
 
Nadhani ni John Shibuda
Kijana ritz; pole sana! Hivi unajuwa kuwa kujifananisha na kichaa ina ghalama kubwa? Ni sawa na mwanafunzi aliyekwenda shule ili kuandika mtihani lakini akasahau akili zake nyumbani. Unapoteza haiba, imani kwa watu, unadharaulika na kuonekana kama mtu wa mizaha tangu asubuhi hadi jioni.

Maoni yangu kuhusu wabunge wa CDM:
Wabunge makin wa CDM ni pamoja na Tundu Lisu, Zito Kabwe, Mnyika, Mbowe ...lakini wakiongozwa na mbunge mstaafu Dr W. Slaa. Lakini kwa vile hatuna kipimo sahihi ni vigumu sana kuwaweka kwenye ranking order.

Kama tukilazimisha kuwa na ranking order (very questionable) basi Mbowe, Dr W. Slaa, T. Lisu, Mnyika, Z. Kabwe, Lema, Regia Mtema, ...(na kuna mbunge mmoja ni mchungaji ila jina lake limenitoka, yeye anaweza kuchuana na Mnyika, Zito na Lema...), nk nk
 
Sidhani kama mtiririko wako umekaa fresh kwani tangia Zito anunuliwe na ccm sidhani kama anaubora wowote tena kwani mtu ukishatanguliza maslahi binafsi tena utakuwa huna jipya
Tuthibitishie alinunuliwa lini na kwa bei gani, kama ni kweli hija zake zenye uchambuzi wa kina zingepotelea mbali lakini kila siku anaibuka na hoja nzito, ila ninachojua ni kwamba ukishachoshwa na mtu hata afanye nini huoni na hivi ndivyo ilivyo, ila Zitto ni jembe la uhakika ndani ya cdm
 
Back
Top Bottom