MNYIKA ndiye mpinzani namba 1 tishio kwa CCM na Serikali yake

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Hakuna kijana mwenye uwezo mkubwa katika medani za kisiasa katika vyama vyote vya siasa kama Mh John Mnyika. Palipo na ukweli lazima usemwe, palipo na ukweli pia uongo hujitenga. Huwa anajua nini anachokichanganua katika kuchangia miswada mbali mbali hasa bungeni, mwepesi wa kujenga hoja nzito. Mweledi wa kisiasa ambaye huanza kuchambua mada taratibu na umakini mkubwa.

Hana papara wala hakurupuki wakati wa kujibu hoja mbalimbali, mpole anayejiamini. Hutumia busara katika maamuzi na husimamia kile anachokiamini. Jasiri mwenye kuchunguza mambo kwa undani, hana jazba. Hufichua hoja za msingi zilizojificha kiasi mara kadhaa ameweza kuthubutu kusababisha baadhi ya miswaada ya serikali kufanyiwa marekebisho makubwa bungeni.

Pamoja na umri wake mdogo, anafaa kushika nyadhifa za ngazi za juu katika chama na nchi kwa ujumla. Ana sifa nyingi ambazo ukurasa hautatosha kuzibeba kwa wingi wake. Huyu ni JEMBE la uhakika ambalo ni tishio kubwa kwa CCM na Serikali yake na LULU pevu inayopaswa kutunzwa na kuhifadhiwa na chama chake.
 
Kati yake na lema nani anafaa kuwa mbunge bora mwaka huu?

Mkuu kwangu mimi Mnyika hawezi kulinganishwa na Lema hata kidogo. Mnyika yuko mbali sana. Mtoa mada ametoa sifa halisi za Mnyika ambazo naamini ndani ya CDM kama wapo wenye nazo basi ni wachache mno na Lema si mmoja wao!
 
Kwa watu wanaoelewa maana ya siasa lazima wakubali kuwa Mnyika ni jembe la uhakika.Katika list yangu ya wabunge makini itakuwa hivi 1.Tundu Lisu 2.John Mnyika 3.Zitto Kabwe
 
Mimi binafsi hakuna mbunge naemkubali na makini Tanzania kama Godbless Lema
 
Kwa watu wanaoelewa maana ya siasa lazima wakubali kuwa Mnyika ni jembe la uhakika.Katika list yangu ya wabunge makini itakuwa hivi 1.Tundu Lisu 2.John Mnyika 3.Zitto Kabwe

Sidhani kama mtiririko wako umekaa fresh kwani tangia Zito anunuliwe na ccm sidhani kama anaubora wowote tena kwani mtu ukishatanguliza maslahi binafsi tena utakuwa huna jipya
 
Hakuna kijana mwenye uwezo mkubwa katika medani za kisiasa katika vyama vyote vya siasa kama Mh John Mnyika. Palipo na ukweli lazima usemwe, palipo na ukweli pia uongo hujitenga. Huwa anajua nini anachokichanganua katika kuchangia miswada mbali mbali hasa bungeni, mwepesi wa kujenga hoja nzito. Mweledi wa kisiasa ambaye huanza kuchambua mada taratibu na umakini mkubwa. Hana papara wala hakurupuki wakati wa kujibu hoja mbalimbali, mpole anayejiamini. Hutumia busara katika maamuzi na husimamia kile anachokiamini. Jasiri mwenye kuchunguza mambo kwa undani, hana jazba. Hufichua hoja za msingi zilizojificha kiasi mara kadhaa ameweza kuthubutu kusababisha baadhi ya miswaada ya serikali kufanyiwa marekebisho makubwa bungeni. Pamoja na umri wake mdogo, anafaa kushika nyadhifa za ngazi za juu katika chama na nchi kwa ujumla. Ana sifa nyingi ambazo ukurasa hautatosha kuzibeba kwa wingi wake. Huyu ni JEMBE la uhakika ambalo ni tishio kubwa kwa CCM na Serikali yake na LULU pevu inayopaswa kutunzwa na kuhifadhiwa na chama chake.


hiyo title in ku-exclude wewe na ina demoralise wapambanaji wengine...

Mnyika is good , very good..kumweka number 1 kana kwamba tuna shindana kupambana na CCM umejidhalilisha sana...kibaya sana sababu unayoitoa eti anapanga hoja...na sio amefikisha maji kwa wananchi wake!! kuongea???....huku kisirisiri amefinya sh. laki mbili kibindoni na yuko kimya!!!

kupenda bwana!

wasifie wana siasa kwa uangalifu mkubwa mkuu........vijana wengi sana wako against CCM kuna wengine radical hata CDM hawawataki wala hawataki kuwapa nafasi...yaani wana hasira wamepitiliza! sema hauwajui!! wapo moyo na hao pia.........mwisho wa siku CCM ikitoka madarakani sifa ni kwa wote wala sio watu 17 kama JK! shame!
 
Ni mnyenyekevu, ana heshima na ni msikivu kwa viongozi wake. Hakurupuku kutoa matamko yanayokigawa chama na kumpa ujiko. Yeye kwake ni chama kwanza, sifa binafsi baadae. Tofauti na wengine walio lewa sifa binafsi na kukiweka chama pembeni.
Viva JJ, Viva Chadema.
 
Ni mnyenyekevu, ana heshima na ni msikivu kwa viongozi wake. Hakurupuku kutoa matamko yanayokigawa chama na kumpa ujiko. Yeye kwake ni chama kwanza, sifa binafsi baadae. Tofauti na wengine walio lewa sifa binafsi na kukiweka chama pembeni.
Viva JJ, Viva Chadema.

Hakika umenena niliyotaka kunena. Huyu si tu ni Hazina kwa CHADEAMA ila Taifa kwa ujumla wake. Hongera JM.
 
Mimi binafsi hakuna mbunge naemkubali na makini Tanzania kama Godbless Lema
Hawezi kumzidi Livingstone Lusinde, Lusinde ni jembe la uhakika namuaminia sana, na ni yeye Lusinde ndio ataibuka kidedea kama Mbunge bora kijana 2011.
 
ni kweli kabisa kwani kijana anatumia busara zaidi ktk kuwasilisha hoja zake tofauti na wengine wanaotumia jazba.nadhani wakazi wa jimbo la ubungo wanajisikia fahari sana kuwa na mbunge kijana mwenye hekima kama babu wa miaka 70.
 
Back
Top Bottom