Mnyika naye awaita CCM panya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika naye awaita CCM panya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, Dec 25, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Dec 25, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, hakukosea kuwafananisha wanasiasa wa vyama vya upinzani na paka.

  Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kipumbwi wilayani hapa Mkoa wa Tanga katika operesheni Sangara inayoendelea.

  “Makamba huwa anatufananisha wapinzani na paka sasa sisi hatukatai, sisi kweli ni mapaka tunaotafuta mapanya ambayo ni CCM yanayotafuna fedha za umma, unajua ndani ya nyumba yako yakiingia mapanya lazima ufuge paka ya kuyaua,” alisema Mnyika na kuongeza kuwa: “ wananchi mjitahidi kuongeza idadi ya paka (wapinzani) bungeni ili yasaidie kuyatafuna mapanya (CCM) ambayo yanatafuna rasilimali za nchi.

  Aliongeza kuwa panya wa CCM wamekuwa wakitafuna michango inayotolewa na wananchi katika miradi ya maendeleo na fedha za baadhi ya miradi zinazotolewa na wahisani.

  Akiwahutubia wakazi wa Kata ya Gare wilayani Lushoto, Mnyika aliwataka Watanzania wasimfananishe hata kidogo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa na Makamba kwa uelewa wa mambo na utendaji wa kazi zao.

  “Hivi jamani kwa akili ya kawaida tu unaweza kumfananisha Makamba na Dk. Slaa kwa kitu gani, Dk. Slaa anamzidi Makamba kwa kila kitu, Makamba na mafisadi lao moja wakati Dk. Slaa amekuwa akiyaumbua mafisadi kwa kuanika majina yao,” alisema Mnyika.

  Mnyika alisema CCM ya wakulima na wafanyakazi ilikufa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na hivi sasa mafisadi yamevamia chama na wanyonge hawana chao.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni bonge ya reaction naona Makamba itabidi atafute jina lingine kwa wapinzani wake.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Not impressed, two wrongs do not make right, mmoja hapa alitakiwa kuonyesha the way badala ya kuitana majina ya wanyama, huku wanachi wakiendelea kuteseka kutokana na uongozi mbovu katika kila kona ya taifa letu!

  Respect.


  FMEs!
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Sifikirii kama kuna anything wrong there. Kama Makamba kwa akili zake timamu aliona Chadema ni Paka basi ufahamu kwamba amekunwa na ana wasi wasi hivyo Mnyika kuwaita CCM ni panya ni sawa kabisa na sioni kama kuna anything wrong. Swala hapa ni Makamba kuonekana hamnazo mbele ya wana CCM wenzake kwani katafuta jina ambalo lime-fire back.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - What is good hapo kwa wananchi na taifa, kama CCM ni panya basi ina maana wananchi wote wa Tanzania tuna something wrong kuweza kutawaliwa na Panya for 47 years na bado tunawachagua!

  - Ndio maana nikasema kwamba somebody had to show some decency here na kuachana na non produtive name calling thing! I mean wenye akili nyingi watashidnwa kutofautisha mkuu!

  Respect.


  FMEs!
   
 6. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Kwenye siasa kuna vijembe na hapo ni baadhi ya vijembe. ie CCM mmewaita Chadema paka mlitaka wao wawe kama Yesu Ukipigwa shavu la kulia geuza la kushoto? No way Chadema wamekubali hilo jina na balance yake ndiyo hiyo kwamba CCM ni panya therefore watasakwa kwenye kila uchochoro hadi wapatikane wote hiyo ndio reality kwenye maisha ya paka na Panya.

  Vile vile angalia sisimizi ni wadogo sana lakini wanajenga kichuguu ambacho huwezi kuamini. Hapa Makamba kachemsha ndio sababu tumewabatiza CCM Chama Cha Majambazi kwa sababu Mafisadi Papa wamo ndani ya CCM na CCM wameridhika kuyalea mumo ndani, mnategemea wananchi wafanye nini? Nyie kubalini tu mmekuwa panya na hivi sasa mapaka yamekuwa mengi Tanzania hivyo kelele za mlango zinamzuia mwenye nyumba kulala.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0

  - Mkuu jifunze kujadili hoja bila personal, mbona mara ya miwhso uliomba radhi si unajua kua ninaweza kujibu kwenye hiyo level pia, si unajua kwua sidanganyiki na hiyo rangi yako au nijibu? au unataka tuongelee ujambazi in the real sense yaani nani ndiye na nani siye?

  - Ninasema hivi kuita wengine paka au panya hailisaidii hili taifa on anything, ila inaonyesha tu uwezo wa viongozi wetu wa siasa ulipo na kwamba ni kwa nini hatuwezi kwenda popote tutaishia yale yale ya Yanga na Simba, kelele ubingwa wa Africa hakuna,

  - Mimi sio panya na siamini kwamba wewe ni paka na siamini kwamba kuna kiongozi yoyote wa taifa hili ambaye ni paka au panya, kama huna hoja tulia mkuu lakini acha name calling, hoja zangu ziko very clear kwamba taifa halinufaiki kabisa na this kind of politics na si kweli kwamba CCM itashindwa uchaguzi kwa sababu ya hizi name calling, ni waste of wananchi's valuable time hasa on the CCM's kujiingiza kwenye this kind of politics!

  - Halafu mwananchi au kiongozi mwenye akili timamu huwezi kutumia maneno ya Makamba as a standard for anything worthy kwa taifa, sio siri kwamba Makamba anawakilisha kikundi flani kidogo sana huko Magogoni, ambao wanaamini kwamba kila anayewakosoa ni kwa sababu either aligombea urais akakosa, au simply ana chuki na wivu sasa nilitegemea wananchi wote wa taifa hili tutamuomba Mungu wetu atusamehe dhambi ya kuwapa hawa madaraka, maana tutawaambia nini watoto na wajukuu zetu?

  - I mean wananchi wote tunahangaika na umasikini halafu somebody analeta maneno ya panya na paka, that is insane! Somebody has to step na kuonyesha njia hapa! Badala ya kuyafanya maneno shallow ya Makamba as a standard katika siasa zetu!

  Respect.


  FMEs!
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wacha1

  Nadhani the whole paka/panya thing is a bad joke... tunahitaji maendleo zaidi kuliko mipasho!
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Khe khe hii kali sana mie nimeipenda Makamba kuita wenzake paka alifikiri ni kitu kizuri yeye kuitwa panya imekuwa nongwa CCM bwana ni lazima wabadilike tena haraka sana.
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  FMES

  Huo ni uamuzi wako i.e. personal choice

  Kama Makamba aliamua kufuga panya basi Paka wako ready ku-deal na hao panya. Sijui ni lini nilikuomba radhi na kwa sababu gani, kilicho mezani ni Mkamba kuita wenzake Paka sasa ni zamu ya panya kukimbilia uchochoroni
  Mnyika nakupa tanomanake hapa umemuweka Makamba panapotakiwa, hapo itabidi panya wasakwe hadi waishe Tanzania maana wako wengi. Chama kilichojaa Majambazi hakiwezi kukubalika Tanzania. Typical of Mkamba type aanze kukimbilia kwenye vichochoro.
   
  Hizi type of politics ndizo zimezaa EPA, Richimonduli, Dowans etc. sasa kwa nini zisisakwe kama panya?

  BTW hakuna aliyesema FEMS ni panya.
   
 11. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  That's just a metaphor and nothing else. Sometimes when you try to explain something you have to use metaphor as a way to let your audience relate/understand your point.

  There's nothing wrong here, that's why there are sayings in many languages, Swahili is one of them.

  Here's one: "Samaki mkunje angali mbichi" or when someone referred the network of untouchables corrupt people as "Mafisadi papa"

  The bottom line is, I got the message from Mnyika simple and clear. Hope you did too.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu wote wawili wamekosea... Huyo makamba tunamfahamu, ni mzee wa kubwabwaja tu hana chochote chenye tija hata kwa chama chake!! sasa Mnyika sihangaike na yule babu, ni bora angekua anajibu hoja za watu wengine ndani ya CCM

  The best way ya kumfunza mtu kama makamba ni kumuacha tu, kumjibu makamba ni kumpa kichwa cha bure
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  huyo Mnyika ni hanithisi
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kibs, merry x-mass!!

  Hiyo lugha ni ipi tena?
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ni lugha ya malumbano ya kisiasa... zenj wameamua kuachana na ulofa huu, lakini huko bara naona ndio wameshikia bendera... Hivyo basi Mnyika ni lofa na hanithisi wa siasa!
   
 16. C

  Charuka Member

  #16
  Dec 26, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ilikuwa siku ile wainzani walipojidai wameungana. ndipo akaulizwa Makamba; wauonaje muungano wa cuf,chadema,nccr, na tlp? akasema; hao ni kama paka wamefungiwa mikia kwa pamoja, wakiwekewa maziwa kila mmoja atajivuta upande wake kuyafukuzia hayo maziwa. Kwani kilienda mbali!, Chacha Wangwe alivyokufa tu.... Makamba anaweza kuwa anakosea wakati mwingine, lakini katika hili, vitendo vya wapinzani wenyewe vilithibitisha alikuwa sahihi. na Mnyika kukubali kuitwa hivyo ni kwa kuwa anajua unabii wa Makamba ulitimia. Mlioua ushirikiano wa wapinzani shame on youuuuuu!
   
 17. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #17
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FMEs

  Mbona habari yenyewe unazungumzia hicho unachokitaka? Amesema kwamba kuna uongozi mbovu unaotafuana fedha za umma kupitia ufisadi kama panya. Hivyo amewataka wananchi wachague upinzani ili wawe kama panya wa kuwasaka hao mafisadi na kuwaondoa ili kuleta maendeleo

  serayamajimbo
   
 18. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kibunago, unajidhalilisha mkuu watu wanaweza sema ww ndiye Makamba, unaweza kujieleza kwa kutumia lugha ya kawaida. Walichofanya Makamba na Myika sio kama ni tatizo kwani walitumia lugha ya picha zaidi kuelimisha watu na sio matusi, kama ni matusi hakikisheni watoto wenu awaangalii Tom and Jerry kwa kuwa ndiyo lugha iliyotumika hapo

  Lakini mkuu ulichoongezea hapo kuna watu watakuuliza ndio nini maana hawajawahi kusikia kwenye maisha yao yote, rudi kundini mkuu bado tunaitaji mawazo yako ya zamani ambayo hayakuwa na matusi hata kidogo pamoja na ulikuwa unapinga
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Huyu mnyika ni so rookie kwenye siasa..
  Badala ya kujifunza siasa mpya..
  Yeye anaona bora achukue uzoefu wa siasa za kipumbavu...
   
 20. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  si ndo maana CCM itashinda tena uchaguzi huku bara,Maana upinzani wenyewe wanawaamini akina mnyika, so what do u expect dude?
   
Loading...