SOBY
JF-Expert Member
- Sep 19, 2011
- 1,268
- 457
Nadhani wewe ndiyo umechangany'a mambo. Ninachozungumzia mimi ni uingiliaji wa vyama kwenye shughuli za serikali, either kuu au za mitaa. Hii inatumiwa kama njia ya kwaadhibu wanachama wenye nafasi za uwakilishi, hawa ndiyo wanachama wnoeta hela au/na umaarufu.Kwa mfano CDM walitaka kumshughulikia Shibuda kwa kupingana na suala la sitting allowance, yaani ingawa kikatiba yao wangeweza,ingekuwa ni jambo linalokandamiza demokrasia.Kuna hoja katika dondoo yako lakini umechanganya mambo. Mtu yeyote kama ni makini basi atajiunga na chama baada ya kupitia katiba, kanuni na miongozo ya chama hicho na kujiridhisha kuwa anakubaliana nayo, bila ya kujali kuwa katiba hiyo ni nzuri au mbaya. Na ni lazima utambue kuwa utakapoenda kinyume na katiba hiyo ni lazima utapewa adhabu ikiwa pamoja na kufukuzwa. Swali la kujiuliza ni je hawa waliofukuzwa kwenye vyama vyao walikiuka au hawakukiuka katiba, kanuni na miongozo ya vyama vyao. Kama wamekiuka, basi ni halali kabisa kwao kufukuzwa. Kinachogomba hapo ni suala la kufukuzwa uanachama wa chama ukaenda automatic na kufukuzwa ubunge.
Sometimes it's not right to do something just because you have the right to.