Mnyika, Nape, Mtatiro na Mvungi wanapambana ITV ktk kipima Joto

Kwa mara ya kwanza Nape amekubali na kukiri kuwa ile orodha ya mafisadi 11 waliotangazwa na Chadema ni ndogo kwani ccm ina mafisadi wengi kuanzia ngazi za juu hadi chini.

Ni kwa kutambua hilo ndio maana ccm imeshindwa kuchukua hatua stahili dhidi ya mafisadi hao. Amewaondoa matumaini watanzania ya kuona hatua zinachukuliwa kwa manufaa ya Taifa kwa kudai kuwa kamati kuu iliyojiuzulu ni mfano mzuri wa kuchukua hatua ndani ya ccm. Kwa kauli hiyo Nape amethibisha kuwa ccm yote ni mafisadi kuanzia sekretarieti inayoongozwa na Rais Kikwete.

Source: Mjadala Kipima joto ITV
 
Tathmini yangu: Mnyika alikuwa makini sana, kaondoka na kura nyingi kuliko wote, kwani hoja zake ziliweka maslahi ya taifa mbele kuliko kitu kingine chochote; Mvungi naye amefanya vizuri sana, hasa kusisitiza kwamba hakuna mkubwa kuliko chama; Mtatiro naye amejitahidi sana to balance between chama na maslahi ya taifa; Nape hakuwa yule tunayemjua, alipwaya sana, na nina uhakika akitazama kipindi tena, atakubali hilo; hakuwa na hoja ya maana kwani hoja zote, Mnyika na Mtatiro walimfunika, tena sio kidogo. Ingekuwa jambo jema sana kuwakutanisha watu hawa kila baada ya muda fulani. Hitimisho la Mtatiro litakuwa gumzo kubwa kwa siku za usoni huko makao makuu CCM.
 
Mvungi, Mtatiro na Mnyika wamen'gara pengine wanasemea ukweli zaidi ya Nape aliyezungumzia katiba zaidi bila utekelezaji.
 
Yeye mwenyewe amekata tamaa na mienendo ndani ya ccm baada ya akina Mukama kumpiga kushoto na kuziponda papara zake!
 
Nape leo jasho limemtoka kila kona ya mwili wake, yan hakuna ktu alichoogea leo. NImemwonea huruma kweli yan alikuwa mwekunduuu halafu macho yanamtoka utafikiri alikuwa anataka kufa.
 
Tathmini yangu: Mnyika alikuwa makini sana, kaondoka na kura nyingi kuliko wote, kwani hoja zake ziliweka maslahi ya taifa mbele kuliko kitu kingine chochote; Mvungi naye amefanya vizuri sana, hasa kusisitiza kwamba hakuna mkubwa kuliko chama; Mtatiro naye amejitahidi sana to balance between chama na maslahi ya taifa; Nape hakuwa yule tunayemjua, alipwaya sana, na nina uhakika akitazama kipindi tena, atakubali hilo; hakuwa na hoja ya maana kwani hoja zote, Mnyika na Mtatiro walimfunika, tena sio kidogo. Ingekuwa jambo jema sana kuwakutanisha watu hawa kila baada ya muda fulani. Hitimisho la Mtatiro litakuwa gumzo kubwa kwa siku za usoni huko makao makuu CCM.
nakubaliana na wewe lakini hili la nape hata kama angekua malaika pale asingeweza kufanya zaidi ya nape...huo ujasiri wa mwendawazimu wa kutetea chama kilichooza anao nape tu!
 
CUF: hakuna mtu mwenye uwezo wa kukiweka chama
chetu mfukoni! Chama chetu si cha matajiri yeyote
anayeenda kinyume na katiba yetu anashughulikiwa
kwa mujibu wa katiba ya chama: by Mtatiro

CHADEMA: chama chetu kinaamini kwenye nguvu
ya umma. Katika kila jambo lifanywalo na chama
chetu masilahi ya nchi na wananchi huwekwa mbele.
Katiba yetu ina code of conducts ambazo
zinawabana madiwani na wabunge wote huku lengo
likiwa ni moja masilahi ya wananchi: Mnyika

CCM: chama chetu ni kikubwa ukilinganisha na vyama
vingine hivyo mchakato wa kuwajibishana ndani ya
chama lazima utakuwa ni mrefu ukilinganisha na
vyama vingine. Chama chetu kimeshafanya maamuzi
magumu mengi ikiwa ni pamoja na kuvunja sekretariet,
kuwapa na muda mrefu wale wote waliokiuka taratibu
na msingi ya chama kujiondo. Baada ya kushindwa
kujiondoa wenyewe sasa tumerudi ndani ya chama
kuwashughulikia. Chama chetu kimeifikisha nchi
yetu miaka hamsini kwa amani na ndio maana hata
Wapinzani leo wanaweza simama majukwaani wakahubiri
siasa Kwa uhuru hiyo yote ni kazi ya ccm: Nape

NCCR: Huku kwetu tunasimamia nidhamu! Ndiyo
maana katika cha chetu ukiota gamba hatukupi muda
Ujivue! Sisi tunakuvua wenyewe haraka iwezekanavyo.
N hii ndo imetusaidia tukapata viti vinne uchaguzi
Wa mwaka 2010: Dr Mvungi

Haya kazi kwako umependa ipi hapo.
 
nakubaliana na wewe lakini hili la nape hata kama angekua malaika pale asingeweza kufanya zaidi ya nape...huo ujasiri wa mwendawazimu wa kutetea chama kilichooza anao nape tu!

Kimsingi nakubaliana na wewe lakini still, Nape alikuwa na nafasi nzuri tu ya kujenga hoja vizuri zaidi kuliko kuwa on the defensive mode (60%) na offensive mode (40%), huku wenzake wakijadili facts. Kuna mengi ambayo angeweza kuyanzungumza kumpa uhai kwenye mjadala ule, kwa mfano, angekubaliana na wenzake kimsingi kwamba katiba ya nchi ina matatizo, na kuelekeza hoja za udhaifu wa CCM huko, kwani kimsingi, hata CUF na NCCR Mageuzi, wanaweza kudhania wameshinda katika sakata la kafulila la hamad, lakini kutokana na ubovu wa katiba ya sasa ya Tanzania, watu hawa wawili wataendelea kuwa wabunge mpaka watakapoamua kujiuzulu wenyewe. Katiba ya Tanzania, kutokana na ubovu wake, haizungumzii hatima ya mwanachama 'Kufukuzwa' ni nini, hasa akiwa pia ni mbunge, badala yake inaongelea mwanachama kuacha kuwa mwanachama (sio kuachishwa au kufukuzwa), kujiuzulu mwenyewe, pamoja na sababu nyingine. Hii ingewapeleka kina Mnyika, Mvungi, Mtatiro kwenye mjadala wa katiba ya nchi zaidi, na hivyo Nape to buy time mpaka kipindi kiishe. Vinginevyo hakuna Mjadala kwamba leo, Mnyika kamnyuka Nape.

Nimelijadili suala la mgogoro baina ya Katiba ya Tanzania na Katiba ya Vyama Vya Siasa, kwa kirefu zaidi kwenye thread yangu mapema leo:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/212034-katiba-ya-tanzania-na-migogoro-ya-uongozi.html?
 
Binafsi nimevutiwa na mazungumzo ya wachangiaji wote, sikupata bahati ya kuusikiliza ila nimesoma ulichokiandika hapo mkuu, wamejaribu kueleza taratibu za vyama vyao kwa kweli mimi binafsi baada ya kusoma naona maelezo ya wahusika wote yamejitosheleza.
 
Nape akitulia ni mzuri. Vinginevyo anasahau kwamba katiba ya CCM katika ukurasa wa wa 125, ibara ya 110 inazungumzia juu ya kazi za kamati kuu ya CCM, kamati kuu ambayo Nape ameisifia sana kwamba ilijiuzulu, na kupelekea kuundwa kwa kamati kuu mpya yeye akiwa mmoja wa wajumbe. Katika ibara ya 110, sehemu ndogo ya 7 Katiba ya CCM inasema hivi, kuhusu kazi za kamati kuu:

"Kumsimasisha uongozi kiongozi yeyote isipokuwa mwenyekiti wa CCM na Makamu wa mwenyekiti endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uongozi."

Hoja zake kuhusu vikao, taratibu n.k, taratibu hizi zingefuata baada ya Kamati Kuu kuchukua uamuzi wake, mfano iwapo wahusika wanakata rufaa n.k, vinginevyo Kamati Kuu ilitakiwa baada ya kujiridhisha, kukamilisha zoezi hili la kuwavua magamba wanachama iliyodhamiria kuwashughulikia April 2011, kwa azimio kwamba hawana sifa za uongozi, kwa mujibu wa katiba. Vinginevyo aelezee umma kwamba, wanachama husika wana nguvu kuliko wale ambao katiba inasema hawawezi vuliwa madaraka, yani Mwenyekiti na Makamu wa Mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom