Mnyika na Zambi: Hodari na makini ktk uchangiaji Muswada wa Manunuzi ya Umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika na Zambi: Hodari na makini ktk uchangiaji Muswada wa Manunuzi ya Umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tetere Enjiwa, Nov 14, 2011.

 1. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wadau kile kipengele cha kununua vifaa chakavu katika muswada wa manunuzi ya umma leo kinaelekea kupita na kuwa sheria. Magamba imemtumia mh Mnyika katika hilo, kwa kumkaimisha nafasi ya mh Zitto ya kuvikwa kilemba cha uchangiaji makini kwa kusifiwa na mwanasheria mkuu huku spika akimtengenezea mazingira.

  Alichokifanya Mnyika ni kutoa hoja za kupinga, anafatiwa na mh Zambi kuonyesha kuwa naye ana mawazo kama ya mnyika ila mwisho wa siku wanabadilisha misimamo yao ya awali kuwa wameridhishwa na ufafanuzi wa AG na serikali.

  Mambo ndio haya nchi hii wananchi hatuna watetezi, tutafute njia mbadala.
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tuone mwisho wake...
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wananchi tumeona kazi ya Mbenge John Mnyika amepambana sana ,mengine ya kusema kipengele kimeridhiwa ni kazi ya CCM na wabunge wao vilaza
   
 4. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wewe haukua makini wakati Mh Mnyika anachangia swala la kusema Magamba ati wanamtumia sio kweli na ni wazi ameibana serikali vilivyo sema uwingi wao ndio unasaidia baadhi ya vipengele kupita,je unafikiri watu wote wana uweledi wa alichokua anakichangia Mh Mnyika ? Kwa hyo ulitaka nae Mh Lusinde na Ngonyani nao wachangie? Hakika umekosa umakini na zaidi uelewa
   
 5. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa waliofatilia kipindi cha bunge leo, 14.11.2011 asubuhi wakati bunge lilipokaa kama Kamati kupitia kifungu kwa kifungu muswada wa manunuzi, hakika watakubaliana nami jinsi ambavyo wabunge wawili yaani Zambi na John Mnyika (Chadema-Ubungo) jinsi walivyoonyesha umakini, uwezo wa hali ya juu kuchangia kila kipengele na kutoa mawazo mbadala ya jinsi gani viboreshwe!

  Hakika wameonyesha ukomavu wa hali ya juu na kuonyesha bunge linahitaji wabunge wa namna gani.....walifanya "homework" yao vizuri na kushiriki ipasavyo katika zoezi la kutunga sheria kwa kuhoji, kupendekeza. Jambo ambalo liliwapa wakati mgumu sana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Warema na baadhi ya maeneo Mkullo.
   
 6. h

  hajoma Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  safi sana..............!peoples power..... kwani Zambi naye ni Chadema? jimbo gani?mbona ana mawazo mazuri kama wapambanaji au amejivua gamba?
   
 7. j

  jigoku JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mwenzenu nilikuwa kwenye umachinga sijapata kuangalia bunge wal sijui nini hasa kimetokea maana mleta thread hii nae sijamuelewa.mnijuze kimetokea nini,je mswaada umepita? na Mh Mnyika analaumika kwa lipi?
   
 8. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  nilichofurahi zaidi walikuwa wanalumbana kwa kujenga hoja na kutetea pia serikari nayo ilikuwa inajibu kwa hoja, ndio maana ya upinzani, Tunawaomba waendelee vivyo hivyo
   
 9. M

  Mr. Clean Senior Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Zambi ni Mb wa -Mbozi mashariki ccm ila nakumbuka allilivalia sana kombati swala la kiwira la BMW,YONA and company!
  Kwakeli Mnyika ni Kiboko .... hapo hana masters je angekuwa nayo si motoooooo!
   
 10. j

  jigoku JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo mswada umepita au imekuwaje?maana sikupata nafasi ya kufuatilia bunge
   
 11. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  miguubaja nakubaliana na wewe sijui wabunge wengine walikuwa wapi, unajua mwanasheria alikuwa akitumia nguvu tu lakini hawajaa wawili wamechukua posho kihalali
   
 12. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Wewe ndio hauko makini mimi nimesema kipengele na wala si vipengele kama unavyotaka watu waamini. Kipengele hiki ndio kinaondoa mazuri mengine yote ya nia njema ya mswada huu. Wakitaka fedha za kuibia kura za uchaguzi watakuwa wanapitisha kununua meli au ndege scrap wanaipiga rangi mnaambiwa imetumika.
   
 13. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakika wale posho imeenda kihalali na wamefanya uwakilishi uliotukuka!!!Wanastahili pongezi.
   
 14. g

  gkaaya Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tunamshukuru MUNGU kwa ajili ya Mnyika na mwenzake zambi ni kweli wamefanya kazi nzuri leo. Natamani tungekuwa na vichwa kama hivyo kwa wingi bungeni basi wananchi tusingeburuzwa tena na serikali kama ilivyo sasa mimi nimechoka kabisa.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mpaka wanapumzika mchana ulikuwa haujapitishwa... wamerejea jioni hii wanaendelea nao
   
 16. F

  FredKavishe Verified User

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mnyika leo amenifurahisha pamoja na zambi"safi sana wabunge wote wangekuwa wanasoma kifungu kwa kifungu tungekuwa mbal
   
 17. Stanley.

  Stanley. JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa wanaofuatilia bunge hawatashangaa mh Mnyika na mh Zambi wanachokifanya. katika mabunge yote yaliyopita kila inapofika wakati wa kamati ya bunge zima hawa jamaa wapo makini na schedule of amendiments. nakubaliana na title ya thread lakini kuwa mnyika ametumiwa hapana inaonekana jamaa ni mgeni kwa mijadala ya bunge. Magamba wakitaka kupitisha hawana haja ya kumtumia Mnyika. Mbona vifungu vingi vimepita ambavyo mnyika amevikataa.
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  vifungu vinapitisha fasta fasta!!! mamamamaamaeeee nchi hii inatia kinyaaa sana... naambiwa hapa kwamba sheria hii inapitishwa ili mtu fulani aweze kukamilisha baadhi ya ahadi zake za uchaguzi mkuu kama vile meli 3 na mengineyo,, yani kuanzia saSA NI VYUMA CHAKAVU KWA KWENDA MBELE


  MAJUHA TUTAKOMA
   
 19. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Hapo bolded ina maana wewe hujui kuwa wanaokubalika ni hao wenye uwakilishi mchache, sasa ili kuwazuga wananchi kua umeungwa mkono na wote lazima umtumie mtu kama mnyika. Kwa vile waliomtumia wako makini, basi unatakiwa uwe makini zaidi yao kujua kuwa wamemtumia.
   
 20. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Umepita ukiwa na mabadiliko ya hapa na pale.Mnyika,Zambi na Mpina wamefanya kazi nzuri sana!
   
Loading...