mnyika na ukakasi wa kupinga maendeleo ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mnyika na ukakasi wa kupinga maendeleo ubungo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Mar 21, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  DHANA ya maendeleo kwa wananchi ni moja, kwa maana kuwa maendeleo yanayopiganiwa na serikali kwa wananchi wake kupitia chama tawala, CCM ni sawasawa na maendeleo yanayopiganiwa na vyama vya upinzani katika majimbo yaliyo chini yao.

  Hii haina maana kuwa serikali inawajibika kuleta maendeleo katika majimbo ambayo yaliyo chini ya CCM tu, ambacho ndicho kilichounda serikali, bali inawajibika kuhakikisha kuwa wananchi wote, bila kuangalia kuwa ni wa jimbo gani na linaongozwa na chama gani, wanapata fursa sawa za maendeleo.

  Hivi wananchi waelewe nini pale serikali ambayo ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wananeemeka kutokana na rasilimali walizonazo, inapotaka kuwaletea maendeleo, inakumbana na vikwazo kutoka kwa baadhi ya wabunge wa upinzani, hususan wa chama kikuu cha upinzani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Hili halina ubishi, kwani mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika, amenukuliwa katika vyombo mbalimbali vya habari, kwanza akipinga utaratibu wa kuwaondoa wapiga debe katika kituo cha kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha
  Ubungo, uliowekwa na serikali ili kuwaondolea wananchi usumbufu.

  Serikali ilichukua uamuzi huo, ikizingatia ukweli ulio wazi kuwa wananchi wanapata taabu wanapofika katika kituo hicho, kwanza ya kuibiwa na wapiga debe hao ambao ni wezi wakubwa wa pesa na mali zingine.

  Pili, wapigadebe hao huwaibia wananchi kwa kuwatajia nauli, ambayo siyo sahihi. Mara nyingi wanazidisha na kile kilichozidi, wanachukua kwa makubaliano na wenye mabasi. Huu ni ufisadi wa chini chini na usiofaa kuvumiliwa.

  Serikali ilipoamua kuwaondoa wapiga debe ili kumaliza tatizo hilo, Mnyika alipinga kwa nguvu zote utaratibu huo, akidai kuwa hiyo ndiyo ajira yao, hivyo waachwe. Hii inaonyesha kuwa Mnyika anataka maendeleo yanayopatikana kwa dhuluma na manyanyaso makubwa. Hiyo haikubaliki!.

  Kama hiyo haitoshi, kwa kuzingatia sheria za barabarani na umuhimu wa kupanua barabara za jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi, ilitoa muda kwa watu waliojenga katika hifadhi ya barabara ya Morogoro eneo la Urafiki, kuondoa vibanda vyao.

  Muda uliotolewa uliisha na hatua iliyofuatia ni kuvunja kwa nguvu vibanda hivyo, baada ya
  wafanyabiashara hao kukaidi amri ya serikali. Mnyika akijua kuwa kilichofanywa na serikali ni utekelezaji wa sheria za ujenzi na barabarani; na hata kama yeye angekuwa waziri wa ujenzi angechukua hatua hizohizo, alilaani hatua hiyo.

  Aliwaambia wananchi katika mikutano yake ya hadhara katika jimbo lake, kuwa kilichofanywa
  na serikali ni makoa makubwa. Sijui Mnyika anataka maendeleo ya aina gani kwa wananchi wa Tanzania. Ni sahihi nikisema kuwa mbunge huyo, sasa anapinga wananchi hao wasiletewe maendeleo hayo.

  Wananchi wa Ubungo walimchagua kwa kishindo, wakiamini atashirikiana na serikali
  kuwaletea maendeleo, hasa katika kutatua kero kubwa za wananchi ambazo ni maji, barabara
  na usafi, lakini imekuwa kinyume.

  Mnyika unataka maendeleo ya aina gani Ubungo? Mbona ahadi zako hujatekeleza hadi moja hadi sasa? Umeng’ang’ania tu mambo makubwa ya kitaifa, kama vile Katiba Mpya, huku ukisahau kero za msingi za wapiga kura wako wa Ubungo, ulizoahidi utatatua haraka.

  Kwa mfano, Jimbo lako la Ubungo ni chafu kupindukia – tembelea Manzese, Ubungo,
  Mabibo na Tandale, uone harufu kali na takataka vilivyosambaa kila mahali. Uchafu kila
  mahali!

  Mabibo kuna uvundo na harufu kali ya maji machafu ya mabwawa ya DAWASA. Harufu hii kali, inaathiri afya za wapiga kura wako mchana na usiku. DAWASA hawaweki dawa katika mabwawa hayo kwa muda mrefu sasa.

  Mbona hufuatilii hili, wakati afya za wapiga kura wako zikiangamia? Pia, unatakiwa uwe na programu ya kusafisha jimbo lako. Lakini, hili nalo inaonekana siyo kipaumbele chako. Aidha,
  maji bado kero kubwa Kimara, Ubungo na Mbezi, lakini pia huonekani kufuatilia, wala kuwa tayari kutatua kero hii sugu.

  Kumbuka kuwa hatua ya kuvunja nyumba na mabanda ya biashara Ubungo, ni hatua moja
  katika safari ndefu ya kuwaneemesha wananchi, kwa kuondoa kero ya foleni, ambayo jimbo lako ni mhanga namba moja wa foleni hizo.

  Kwa mtazamo mmoja, mambo yote hayo yanayofanywa na Mnyika, yanalenga kujinufaisha
  kisiasa; na si kuwajali wananchi wa Ubungo, jambo ambalo ni hatari kwa Taifa. Ili
  kuthibitisha mtazamo huo wa kujinufaisha kisiasa, badala ya kujali maisha na maslahi ya
  wananchi, hebu angalia hili la Mwanza.

  Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Meya jijini Mwanza, Serikali mkoani humo iliwaamuru
  wafanyabiashara ndogo (machinga), waondoke katika maeneo yasiyoruhusiwa kufanya
  biashara ; na kwenda katika maeneo walikoelekezwa.

  Cha kushangaza, wabunge wa majimbo ya Nyamagana na Ilemela mkoa wa Mwanza kupitia Chadema, walikataa amri hiyo ya serikali; na walitaka machinga hao wasiondoke, hali iliyosababisha uvunjifu wa amani, pale polisi walipoingilia kati kutaka kuwaondoa.

  Hii inasikitisha, kwa sababu wabunge hao hawakutoa ushirikiano kwa serikali, kuwatafutia mahali wanapoweza kufanya biashara zao vizuri ili waondoke katika eneo hilo, ambalo haliruhusiwi kufanyia biashara.

  Lakini, baada ya kufanyika uchaguzi wa Meya na Chadema kushinda, walianza kuwaondoa machinga hao. Kwa nini awali, kabla ya kufanya uchaguzi wa Meya, wabunge hao wa Ilemela na Nyamagana, walikataa machinga hao wasiondolewe, lakini baada ya uchaguzi wa Meya na
  baada ya kushinda, waliamua kuwalazimisha waondoke?

  Ni dhahiri kuwa walikataa kwa maslahi yao ya kisiasa, lakini sio kwa maslahi ya wananchi. Kama ilikuwa ni kwa maslahi ya wananchi, iweje baada ya wao kukamata halmashauri ya jiji, waamue kuwaondoa?

  Nilisema awali kuwa tabia hii imejikita kwa baadhi ya wabunge wa Chama hicho, kwa kuwa sio wote wenye tabia hiyo. Wapo baadhi ya wabunge, ambao wanashirikiana vizuri na serikali, mfano ni Mbunge wa Mpanda Mjini mkoa wa Rukwa kupitia Chadema, Said Arfi.

  Arfi amesifiwa na viongozi mbalimbali wa serikali, kuwa anatoa ushirikiano wa hali ya juu
  kwa seriikali. Baadhi ya waliompongeza mbunge huyo wa Chadema ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay.
  Imeandikwa na Selemani Nzaro; Tarehe: 21st March 2011 @ 09:48
   
 2. i

  ibange JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  It is a mere crap!
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  sijaona point hapa ya kudiscuss bora upeleke kwa makamba mjadili hili sina mda wa kusoma mada isiyokuwa na tija kwangu kiuchumi au kifikra.naona hata wanaJF wameona crap hawana cha kuchangia hapa.Kashaga tunataka mada zenye mantik.
   
 4. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Serikali imeoza, haina plan hata kidogo ya kumtoa mtanzania toka point A hadi point B, ndio maana inayumba-yumba, inaogopa na kukurupuka pale hata viongozi wa vyama vingine wanapobuni au kutaka serikali itoe dira ya kuwasaidia wananchi badala ya kuwabughudhi na kuwafurusha pasipo na suluhisho lolote...
  Huu ni ujinga usioisha leo au kesho...NO PLANS, no DIRECTIONS, no EXPECTATIONS of DELIVERABLES. Ndio serikali yetu hiyo! SCRAPERS!
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni kama ulikuwa umepotea we jamaa. Asante kwa kuongeza idadi ya posts zako!
   
 6. C

  Calist Senior Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Post ndeeefu lakini haina nyama i ,mean haina mshiko.
   
 7. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndo watu wasiokuwa na hoja ambavyo huwa wanajibu hoja nzito za watu kwa majibu mepesi! Mtu anasema no point wakati point zimejieleza zenyewe hapo juu, au mtu alitaka uanze kumuambia hii ndo poin ya kwanza na hii ni point ya mwisho. Tujitahidi kuwa huru kimawazo wana jf sio inapokuja mada inayokwenda kinyume na mapenzi yetu kwa chadema tunaponda hata kama kilichoandikwa ni cha kweli, haya ndiyo wanayo fanya serikali ya ccm kuponda kila kinachosemwa na upinzani hata kama nafsi zao zinakubali kuwa ni cha kweli. Tuzipokee changamoto mbalimbali zinazohusu chama chetu na viongozi wetu ili kuangalia kwenye matatizo ni wapi na kuyarekebisha haya yatasaidia ukuaji wa chama chetu hatimaye kuchuukua dola lakini sio kuponda kila kinachosemwa kibaya ima kwa chama chetu au viongozi wenu. Tuwe huru kimawazo na kuwa tayari kupokea changamoto mbali mbali na hii ndio demokrasia ya kweli kama chama chetu kilivyo cha demokrasia na jana kwenye maazimio yetu tumesisitiza ya kwamba sisi ni chama cha demokrasia na tutafuata njia za kidemokrasia kushika madadraka na miongoni mwa demokrasia hii pia ni moja wao ya kukubai changamoto mbalmbali za wananchi wetu kwa sababu tupo hapa tulipo kwa sababu yao na tutaenda mbele kwa sababu yao na si vinginevyo.
   
 8. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kwa nini mnyika asiingie humu atujuze sababu ya yeye kutenda hivyo ? Lazima anasababu
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Jamani la kutambua hali za watanzania ni mbaya....hao wapiga debe mkiwatoa hapo bila kuwapa plan B unadhani matokeo yake yatakuwa nini? kama sio kuongezeka kwa wezi na majambazi? la msingi ni kuwawekea utaratibu mzuri waweze pata hata ya kuzuia kufa............
   
 10. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kashaga una matatizo ya kupayuka bila evidence, suala la mnyika kulaan uvunjaji wa vibanda vya machinga pale urafiki ni kutokana na makubaliano yaliyofanyika mwanzon ambapo wakala wa uendeshaj wa huo mradi wa magari yaendayo kasi alitembelea eneo hilo kabla ya uvujanji huo na kukuta kuwa ni nguzo moja tu ya umeme ndo inayotakiwa kuondolewa na si vibanda vya wamachinga hao.
  Tunafaham kama umetumwa na makamba bt uwe unakuja na hoja zenye evidence PAMBAAF
   
 11. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  evidence gani unayotaka mkuu zaidi ya huo?? au unaropoka tuu
   
 12. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Aje ajibu nini .. .... utumbo?
   
 13. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Nilishajiondoa ktk orodha ya kukujibu kama wanaJF wengi walivoidhinisha ila hapa nimefurahi kuona ufupi wako wa kufikiri. Ktk utunzi kichwa cha habari hutokana na habari yenyewe lakini kwako umeleta title ya kejeli alaf ukaishia kumsifu Mnyika. Kwa uchapa kazi umempamba. Umeeleza jinsi anavolinda wapiga kura wake ktk jimbo lake kama wapiga debe na machinga ambao serikali iliwajengea vibanda vya matete na makaratasi ya nailon pale kigogo sambusa ampako hamna huduma yoyote ya jamii,hamna raia wala miundombinu,pia hamna hata kituo cha kupanda au kushusha abiria,bora hata soko la makumbusho ambapo lilikuwa na parking na stendi,japo kweli mpaka sasa linafaa kuitwa soko la makumbusho mana limebaki kuwa makumbusho. Pia umelenga kuonesha ueledi wa Mnyika pale alipowatetea wanaBIG brother waliovunjiwa soko lao kipuuzi lakini mpaka sasa pita pale uulize ndo ujue kuwa sheria uitwa sheria. Hongera Mnyika. Pia umejaribu kumueleza mnyika aelekeze nguvu wapi,umemtajia mfupa uliomshinda fisi,harufu mbaya ya mabibo,urithi tulioupata kwa Mh.Bakampenja(MB) ccm,leo hii ukiuliza ccm imetunyanjia nini ubungo haraka haraka tutasema harufu mbaya na miundo mbinu yenye mbinu,kujenga jengo la Tanesco kwenye mamlaka ya barabara yan katikati mwa barabara,kutuletea maji mara1 kwa wiki jambo ambalo mnyika kalifuta. Kwa ujumla mnyika ni hero. Unasema wananchi wa ubungo wanadokoa na kupora,je wameanza wakati mnyika alipoingia ofsini au kipindi Kingunge Ngombale na kampuni yake ya kitapeli kukusanya mapato na kuendesha kituo cha ubungo kifisadi? Sam nujoma imejengwa kila mara inapigwa viraka wakati haijakabidhiwa,hapa Value for money iko wapi, CAG,fanya V4MA huone utapeli ktk barabara hii. Kashaga,usimtukane mtu kwa kumsifia,utasikia 'lione ili na manguvu kama tembo' au "linene kama pipa". Hapa utakuwa umedhania kutukana kumbe unamsifia. Ukitaka kumkejeli Mnyika bora usubiri japo mwaka ila kwa sasa hamna pa kumchimba ndo kaanza kazi,tofauti na hapo utakuwa unatuonesha upuuzu ulioachwa na mafisadi kabla jimbo alijatwaliwa na wapiganaji na wakombozi wa taifa,sawa mkuu? Safari hii hawajaribu,cdm wanatenda,sa sjui mtajificha wapi? Msalimu Mosha,yule uliyesema ana kampuni ya utalii Arusha na akakueleza kuwa Karatu hamna maendeleo yoyote. Mwambie kuwa wanaJF wamekujibu na kukueleza uache kuropoka bila kujielewa. Jioni njema Kashaga.
   
 14. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nikushukuru wee mtoa hoja ila umekua ukimwandama sana huyo mnyika kwa mrefu sasa jiulize wabunge wako mpaka sasa wamewafanyia nini watanzania sio myika pekee pili umeongea kuhusu bomoabomoa uoni umeongea uongo nakumbuka alichosema ni kwa kwamba kama mtu anakibali halali basi wajiunge waende kwa umoja wao kupinga na ikiwezekana wapewefidia ila kwa yeye atakua anasaidia kama mbunge kwa kufuata sheria na ikishindikana atalipeleka bungeni Tatu mbona ujamuuliza ilo swali pinda kuzuia maendeleo ya taifa ya bomoa bomoa aliyoyasitisha na kuingilia kazi ya magufuli ili apate ujiko? tatu waliotolewa stand ni vema kama serikali makini inapohamua jambo kama hilo inatakiwa itafuite njia mbada ya kuwawezesha eidha kufanya kazi na kupata kipato kingine sio kukurupuka kuwafukuza tatu kuhusu maji ukumbuke hata kama atia nguvu zake kufuatilia hilo tatizo pia kuna mkono wa serikali kuhakikisha katika jimbo hilo akuna kitukinachoendele kama ilivyofanya karatu kwa slaa na wewe mtoa mada ukadanganya uma wa wana JF na hata hivyo slaa alishinda vikwazo na maji yakapatikana pia kumbuka huduma nyingine ni halamshauri inatakiwa kuwajibika kwa kuwa na uzembe wa kutweka ubongo kuwa safi.

  Jamani huyu jamaa sidhani kama anahakili timamu. zingatia hoja zako usikurupuke
   
 15. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Umemjibu vizuri kwa hoja siyo matusi na maneno matupu kama wengine, nshakupa thanks kukubali wewe ni great thinker plus matendo
   
 16. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kaka nimefurahi sana kwa hoja zako nzuri na hivi ndivyo inavyotakiwa wana JF tuwe tujibu hoja kwa hoja,kimsingi uliyoyaongea yana mantiki na mimi nakubaliana na wewe lakini unakuta wengine hoja ziko mezani baada ya kuzipinga kwa vielelezo au kukubali wao wanakimbilia matusi! kaka tuko pamoja na wote tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kugombana! ALuta Continua
   
 17. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe
   
 18. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mkuu ukumbuke pia nimefurahi kuona unaleta post inayozungumzika,kama post utaziweka ktk mfumo wa kupunguza maneno makali wanaJF watakujibu ila tatizo linajitokeza kwenye kashfa,hapo wanashindwa kuvumilia,lakini ukijenga hoja vizuri tutakaa na kuelezana ukweli ili hata wajukuu wakija jf wakute maneno ya busara na hekima za watu wakipingana kwa hoja wala si kashfa na matusi. Mkuu matusi na maneno ya nguoni yataibomoa Jf,ila tukifuata misingi ya Demokrasia na maadili,mbona tutaleta hoja mpaka kuche,na kila atakayepita Jf ajue kuna watu walikuwepo wanaongea,asijefikiri kuwa kulikuwa na watu wanagombana. Kashaga,naomba unihaidi tu kuwa matusi na kashfa ni marufuku kwako ili tupate kujiridhisha kujibu madai yako,nihaidi mkuu!
   
 19. raybse

  raybse Senior Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kashaga Huna jipya na Wala hutskaa huwe na Jipya .....Hoja yako haina Mashiko hata kidogo Kama mtu atatulia na Kuisoma na Kuitafakali kwa Makini....Lakini Hukikurupuka Kama wenzako waweza onekana Una Hoja ya Msingi...... Ki msingi your a biased person and close minded!! Mpaka utakopo rekibisha hiii Hali....Huwezi kuja kuwa na Jipya!!
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Craps kama hizi zinakuwa tamu ikiwa zinaponda CCM. Ni juzi tu tuliletewa ya Januari makamba na mishipa ya puwa mkaitunisha kifyagilia.
  Kwa kweli kilichoandikwa hapa ni kweli na inafaa kizingatiwe unless hakuna tofauti kati ya CHADEMA na CCM.
   
Loading...