Mnyika na Mdee Mmezichoka kura zetu?

Tunataka nguvukazi ya pamoja wananchi na wabunge wetu tulete maendeleo. Tukiisubiri CCM tutakufa, haina msaada
 
Nipo Bunju A maeneo ya usalama mbaka sasa sielewi mbunge wa Bunju ni nani ( Bunju ipo wilaya ya UBUNGO Halima yupo wilaya ya kinondoni kura wananchi wa Bunju tulimpigia Halima ina maana Bunju aina mbunge mbaka hivi sasa.
Njia ya kwenda MabwePande utadhani niko Ruanda, magari yetu yanaisha Sipiringi, wanafunzi wa shule nauli imekuwa kubwa wanatumia usafiri wa Noah Dala zimegoma kwenda njia hiyo. Tegeta Soko la Nyuki na kituo cha Daladala huwezi amini ni Maeneo ya DSM!! Tope na Uchafu wa kutisha. Makusanyo hapo Huduma hakuna! Hakika tulikuchagua Ukatusemee Bungeni siyo kusemea bajeti ya Kilimo. Kama huwezi mtume basi Diwani, mtaa Na Meya wakapaone. Halafu ile Barabara ya Tegeta_Bahati BEach ina umri wa miaka Miwili imeshakua Mashimo/madimbwi. Halima iga mfano wa Mbowe Hai. Wee Binti wa Dar Jimbo lako hoi!
 
Kwa hiyo wabunge ndio wameleta mvua iharibu barabara? Wananchi mjipange muwasaidie wabunge ndio wajibu wenu. Viongozi ni wahamasishaji. Tutengeneze wenyewe. Twende halmashauri pia tukadai ni haki zetu. Ni wajibu wako kujiletea maendeleo yako.
 
Chadema Mmewasusa wapiga kura wenu wa Salasala na Kinzudi Majengo kata ya Goba.

Hebu oneni shida wanazozipata wananchi walio pigia kura chadema

Kwa mvua hizi kuna barabara za mtaa zilizopona?Kama Mwendokasi kuna maeneo imekatika kama keki ya harusi na maeneo mengine kuna mashimo madogo madogo sembuse za mtaani?

Hivi kuna bulldoza liatakalo weza kufanya kazi kwa performance yake kwenye hali ya sasa ya mvu??Tuwe wakweli siyo kila kitu mbunge,hivi ni mbunge yupi anayepokea kodi??

Umeenda Maeneo ya Mapinga au unapasikia na Mbunge wake toka achaguliwe hawajawahi kufika hata siku moja,na ni mbunge wa CCM unataka tumlaumu sababu barabara hazipitiki??
 
Njia ya kwenda MabwePande utadhani niko Ruanda, magari yetu yanaisha Sipiringi, wanafunzi wa shule nauli imekuwa kubwa wanatumia usafiri wa Noah Dala zimegoma kwenda njia hiyo. Tegeta Soko la Nyuki na kituo cha Daladala huwezi amini ni Maeneo ya DSM!! Tope na Uchafu wa kutisha. Makusanyo hapo Huduma hakuna! Hakika tulikuchagua Ukatusemee Bungeni siyo kusemea bajeti ya Kilimo. Kama huwezi mtume basi Diwani, mtaa Na Meya wakapaone. Halafu ile Barabara ya Tegeta_Bahati BEach ina umri wa miaka Miwili imeshakua Mashimo/madimbwi. Halima iga mfano wa Mbowe Hai. Wee Binti wa Dar Jimbo lako hoi!

Hivi unajua hiyo barabara ni ya TANROAD na siyo ya HALMASHAURI??Pita barabara ya Makabe haina lami ila namna ilivyoshindiliwa hata kama mvua imeharibu si sana kama hiyo ya Mbezi/Mpiji Magohe/Mabwepande,ndiyo ujue Serikali ya CCM isivyojua kufanya kazi kwa standard.
 
Yani Mdee ndio kabisa sijui mara ya mwisho alitembelea lini jimboni kwake.....very useless.....maendelea zero
Unataka akutembelee nyumbani kwako? Unamtolea macho Halima badala ya kuitolea macho serikali? Badala ya kushirikiana na mbunge kuishupalia serikali wewe unaanza kumtolea macho mbunge-hovyo kabisa na aina hii ya watu ndio inafanya serikali iwe likizo. Nadhani tunahitaji sana elimu ya uraia inaonekana wengi hatujitambui!
 
Acha porojo,nikuulize swali dogo tuu, mara ya mwisho ulimsikia lini halima akisimama bungeni kuongelea kuhusu kero na matatizo ya jimboni kwake?
Ni lini alienda jimboni kwake kuzungumza na wananchi wake kuhusu kero zinazowakabili?
Ni maendeleo gani mpaka leo yeye kama mbunge ameyaleta kawe?......
 
Usiulize maswali ya kijinga, unajua kabisa mmezuia Bunge Live halafu unaniuliza mara ya mwisho nimemsikia lini Halima akiuliza au kuzungumzia kero za jimboni kwake. Nikusaidie ingia kwenye Hansard tumia muda wako vizuri utapata michango yake kuhusu kero mbalimbali kwenye jimbo lake. Na juzi tu kashusha nondo akishauri namna gani serikali inaweza kufanya ili kupunguza mfumko wa bei ya vyakula kwa wananchi wakiwemo wakazi wa jimbo lake. Kwamba ameleta maendeleo gani siri hiyo wanayo wana Kawe ambao wamekuwa wakimchagua kwa kura nyingi licha ya nguvu kubwa kutoka CCM na serikali kuhakikisha anashindwa!
 
Halmashauri ya Ubungo ipo chini ya CDM, meya mashavu aka meya Boniface Jacob kutwa kucha kazi kuongelea mambo ya udaku udaku tu, hakuna kazi yake anayofanya, hawa wajinga wamepandisha hadi kodi ya maegesho, yaani ni kama mchwa vile halafu watakuambia hawana pesa wao.
Wewe hujaona Ruangwa kwa waziri mkuu,Kongwa kwa spika wa bunge,Bumbuli kwa January,Mtama kwa Nape na Iramba kwa Mwigulu watu wanavyokunywa maji bwawa moja na ng'ombe na barabara hakuna? Awamu hii maendeleo mtayasikia Chato tu!
 
Sisi wananchi wa Bunju mbunge wetu ni nani ,barabara zimeharibika vibaya hakuna kituo cha polisi tokea kile kilichochomwa moto na wananchi wenye hasira hakuna tena jitihada za kukirejesha kituo cha polisi kingine pale usalama,
Shule ya msingi bunju kuna michango mingi mno utadhani ni shule ya kulipia,
hakuna wa kutusemea wananchi wa Bunju ,
Bunju mbunge wetu ni nani???.
 
Acha porojo,nikuulize swali dogo tuu, mara ya mwisho ulimsikia lini halima akisimama bungeni kuongelea kuhusu kero na matatizo ya jimboni kwake?
Ni lini alienda jimboni kwake kuzungumza na wananchi wake kuhusu kero zinazowakabili?
Ni maendeleo gani mpaka leo yeye kama mbunge ameyaleta kawe?......
Halima na Mnyika wataendelea kuchaguliwa kuwa wabunge mpaka watakapochoka na kuamua kustaafu.Huko CCM sioni mtu wa kuwatoa.
 
Halima na Mnyika wataendelea kuchaguliwa kuwa wabunge mpaka watakapochoka na kuamua kustaafu.Huko CCM sioni mtu wa kuwatoa.
Endelea kujidanganya, na ule moto wote wa 2015, Mdee alipata kura 105000 dhidi ya 95000 za Kippi Warioba, hii ni sawa na 53% dhidi 47% za Kippi, kwa hali ya saivi ikiendelea Mdee 2020 anadondoka.
 
Hivi mdee ndio atakuwa na uwezo wa kujenga daraja hapo kwenye huu mto? Hapo napajua vizuri hata manispaa kujenga daraja hapo wanatakiwa wajipange haswa, ila wewe mkazi wa kinzudi mvua hizi kwanini ulazimishe kupita hapo? Nihatari, wote tunazunguka njia ya kwa mchinja kuku na sio mbali, acha lawama zisizo na msingi,
Kwa msiojua hapo kunahitaji daraja kubwa mama la mto ruvu, no papana sana, tofauti na serikali au wafadhili mbunge hana pesa za kujenga daraja hapa.
 
Huna akili mbunge pesa atapata wapi? Hiyo sio kazi yake ni kazi ya serikali, tumia akili

Kama ni kazi ya Serikali basi hakuna haja ya mbunge. Sio kila kitu lazima kussuport usionyeshe ujinga wako na ubendera fuata upepo wako. mbunge anahimiza anabana. Ndo wafanyavyo wabunge wengine. Ndo mwakilishi. Kelele zake ni kama mbunge wa Jimbo La Tanzania. Ajishushe mana anapoomba Kura anasema nini atafanya. So hapa its not about Vyama. Its about rights and responsibilities za Yeye kama Mbunge. Tatizo La wanachama wa viroba ndo Hivi. Pima hoja kwanza kabla hujaingiza uchama. Viroba vinaua
 
Back
Top Bottom