Mnyika na Daraja la mto unaotenganisha Kimara Suka na Golani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika na Daraja la mto unaotenganisha Kimara Suka na Golani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TWIZAMALLYA, Dec 22, 2011.

 1. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni miezi sasa imepita tangu mheshimiwa mnyika aongee na wakazi wa golani na kuwaambia kuwa pesa ya ujenzi wa daraja la mto unaotenganisha kimara suka na maeneo ya golani imetengwa na manispaa ya kinondoni. Na kuwa mchakato wa kumpata mkandarasi umeanza.Juhudi za mnyika kwa muda mfupi tuliziona pale alipofanyia ukarabati barabara inayoelekea golani, tofauti na watangulizi wake wote.Tatizo kubwa lililopo pale ni kutokuwepo kwa daraja ambalo linaunganisha sehemu nilizotaja. Kipindi hiki cha mvua imekuwa ni kiama ingawa hakuna aliyeripoti kiama hicho. Watu wengi wameshindwa kwenda makazini kwa kujaa kwa mto huo.Kuchelewa kwa ujenzi wa daraja hili kumeanza kututia wasiwasi wakazi wa maeneo hayo mpaka tunafikiria kuwa labda mambo ya siasa yameingia pale, maana hakuna ubishi ccm wanajua fitina, hata kama ni kuua mtu wako tayari.

  Ushauri wangu kwa mnyika apite maeneo hayo na kuwapa kinachoendelea wakazi wa maeneo haya wakati huu wa janga kubwa.Kwa taarifa tu kuna familia moja imefiwa na watu watatu maeneo ya golani, watu hawa waliangukiwa na ukuta wa nyumba yao wakati mvua kubwa za usiku wa kuamkia jana zikinyesha.
   
 2. SIMBA mtoto

  SIMBA mtoto JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 208
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Serikali ya Tanzania imefilisika !!
   
 3. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,040
  Likes Received: 7,484
  Trophy Points: 280
  Asiishie Golani, afike mpaka Salanga, kwani nako madaraja yanayounganisha Salanga na Temboni yote yamebebwa na maji.
   
 4. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mnyika tafadhali
   
 5. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yoyote aliye karibu na mnyika au mnyika mwenyewe asaidie kutoa ufafanuzi kuhusiana na hili
   
 6. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani wana JF kuna mtu ana ABC ya nini kinaendelea pale,maana Mnyika alipatia kura daraja hilo na mara ya mwisho alisema hela imepatikana ninachoshangaa muda mrefu sasa umepita hali ni kimya mno.Au Jamaa huyo anataka kutu'CCM' wakazi wa maeneo haya.
   
 7. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Najua mnyika unapatikana JF
   
 8. O

  Obonyo Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhe. Mnyika, pia tunaomba ufuatilie ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ile shortcut ya Ubungo Msewe hadi Chuo Kikuu (UDSM). Ikumbukwe kuwa fungu la mradi wa barabara hii lilipitishwa kwenye Budget ya Serikali ya mwaka 2011/2012 lakini hadi sasa hakuna ujenzi wowote hata maandalizi wakati June 2012 inakaribia. Hiki kipande kinaendelea kuwa kero kwa sababu ya ubovu wake hasa nyakati za mvua. Kutokana na umuhimu wa hii barabara katika kupunguza foleni, tunaomba Mhe. Mnyika ufuatilie swala hili.
   
 9. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Any updates please!
   
 10. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Twizamallya,

  Mwezi huu wa Aprili nimefuatilia kuhusu hatma ya daraja hilo na hatimaye mkataba wa ujenzi wa daraja husika umesainiwa kati ya Manispaa ya Kinondoni na Mkandarasi Kika Co. Ltd kwa gharama za shilingi milioni 447.

  Hata hivyo, ujenzi wa daraja husika haujaanza suala ambalo linahitaji Manispaa ya Kinondoni kumsimamia kwa karibu mkandarasi husika ili ujenzi uanze kwa haraka kwa kuwa mchakato wa zabuni ulianza kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2012.

  Izingatiwe kwamba kutokuwepo kwa daraja katika eneo hilo mwaka miaka mingi kumefanya mawasiliano katikati maeneo hayo kuwa magumu nyakati za mvua na kusababisha madhara ya kibinadamu na mali wananchi wanapovuka mto katika eneo hilo wakati wa mafuriko.

  Baada ya kuwawakilisha wananchi kutaka ujenzi wa daraja hilo lilingizwa kwenye bajeti ya Manispaa ya Kinondoni kwa mwaka wa fedha 2011/2012 hata hivyo miezi ikiwa imebaki takribani miwili kabla ya mwisho wa bajeti husika ujenzi wa daraja hilo ulikuwa haujaanza bado.

  Tathmini ya utekelezaji wa bajeti inaonyesha kwamba kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni ndogo pengo ambalo linapaswa kuzibwa kwa kusimamia kwa karibu miradi inayopaswa kuanza katika muhula uliobaki wa mwaka wa fedha 2011/2012.

  JJ


   
 11. k

  kiruavunjo Senior Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Poleni sana watu wa kimara poleni sana wakaazi wa ubungo pole sana john mnyika, ukiwa mbunge na ukose madiwani wazuri kazi ipo.
   
 12. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,967
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  JJ, you're such a smart guy. Keep it up bro, Tanzania inahitaji wawajibikaji Kama nyie.
   
 13. l

  lina Mongi Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Big up Mnyima, tunakuaminia kwa kazi nzuri, niliona kazi yako daraja la King'ongo lilivyojengwa faster. Mungu akupiganie ufanye kazi nzuri zaidi na zaidi.Peopleeeeees Powerrrrrrrrrrrrrrrrr forever.:nod:
   
 14. Lord K

  Lord K JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pamoja Sana Muheshimiwa ila kuna wakaazi wa msewe ambapo maji yanatoka maramoja kwa wiki mbili,,,Sijui unahabari juu ya hili?...na unawaambiaje wapigakura wako maana najisikia vibaya watu wanaposema bora chama kilichopita kuliko wewe....! P.P
   
 15. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli changamoto ni nyingi sana katika jimbo hili,wakati wewe wa msewe unasema maji yanatoka mara moja kwa wiki mbili, kuna mtu wa bonyokwa na golani maji ya bomba hajawahi kushuhudia yakitoka kwenye bomba yake.Kwa maana hiyo kama Mheshimiwa ataanzia na maeneo yenye kero kubwa basi msewe mtakuwa watu wa mwisho kutatuliwa kero zenu.
   
 16. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli Mh MNYIKA ni jembe kwani kazi ya ujenzi wa daraja la mto unaotenganisha Golani na suka imeanza kwa kasi kubwa sana
   
 17. m

  mbalapala Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Huna mbunge jembe kweli
   
 18. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pumbavu,huyo ninayemtaja sio mbunge?
   
 19. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hiki kitu huwa sikielewi hata kidogo.

  Mkandarasi, mfanyabiashara, amepata tenda kwa kupigania, ameshinda milioni takriban mia tano, halafu haanzi kazi mpaka eti asukumwe, asimamiwe na Manispaa. Hapa tatizo huwa ni nini mbona sielewi? Mkataba hauna ratiba ya kazi, au huwa hawalipwi down payment yao, au hizi kazi wanapewa kwa kuombwa wao hisani? Mfanyabiashara gani mpaka umbembeleze kutoa service baada ya kufunga mkataba?
   
 20. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  darja inajengwa na serkali au mbunge
   
Loading...