Mnyika Mbunge wangu, ya wengine unayajua, yako je?

Umeuliza kwanza Ccm wametekeleza ahadi zao za Rais ndio uje hapa na ubunge

Kila mnapoulizwa majukumu ya wabunge wa chadema mnatoa mfano wa ccm eti imetekelezaje ahadi zake! ni kichekesho! kwa hiyo wabunge wa chadema hawatatekeleza ahadi zao simply kwa kuwa ccm haikutekeleza baadhi ya ahadi zake! how pathetic! Kwa hiyo hata mkipewa dola mtakaa miaka mitano bila kutekeleza chochote, na mkirudi kwa wananchi mtasema, "mbona ccm wamekaa madarakani miaka 50 na hawakutimiza ahadi zote, tupeni muda tena" mtauona mtiti wake maana watanzania wa leo sio wa kudanganywa.
 
Tumekuwa tukilaumu sana safari za JK ulaya na kusahau kutembelea na kutatua matatizo ya wananchi wake, hali hii napenda niifananishe na mbunge wangu mnyika yeye kila siku kimguu na njia ila mtaani kwetu haonekani, hatujakuchagua kuwa mbunge wa magazeti, kumbuka ni sisi wana ubungo tuliokufanya ufikie hapo, nawasilisha na hii ni maalumu kwa wana ubungo

Acha majungu!
 
Tumekuwa tukilaumu sana safari za JK ulaya na kusahau kutembelea na kutatua matatizo ya wananchi wake, hali hii napenda niifananishe na mbunge wangu mnyika yeye kila siku kimguu na njia ila mtaani kwetu haonekani, hatujakuchagua kuwa mbunge wa magazeti, kumbuka ni sisi wana ubungo tuliokufanya ufikie hapo, nawasilisha na hii ni maalumu kwa wana ubungo

Watakuambia mnyika sio size ya ubungo tena ni mbunge wa kitaifa .mbowe na slaa wana mdanganya. Tusubiri tuone hiyo October Kama watampigia kampen wakati kila mtu atakuwa jimbo kwake kuwashawishi wapiga kura wake
 
jimbo maji hamna gar yangu inakaribia kukta shokap ni mashimo

Kwani mnyika ndio mkandarasi na mkusanya kodi wa serikali? Unataka ajenge barasbara kwa fedha zake za mfukoni,? Bangi mbaya sana aisee?pole sana.
 
kila mnapoulizwa majukumu ya wabunge wa chadema mnatoa mfano wa ccm eti imetekelezaje ahadi zake! Ni kichekesho! Kwa hiyo wabunge wa chadema hawatatekeleza ahadi zao simply kwa kuwa ccm haikutekeleza baadhi ya ahadi zake! How pathetic! Kwa hiyo hata mkipewa dola mtakaa miaka mitano bila kutekeleza chochote, na mkirudi kwa wananchi mtasema, "mbona ccm wamekaa madarakani miaka 50 na hawakutimiza ahadi zote, tupeni muda tena" mtauona mtiti wake maana watanzania wa leo sio wa kudanganywa.
ccm ni wajinga kama wafuasi wao, mfano mzuri ni wewe,
 
Ninaishi Ubungo.Ingawa sikatai kunaweza kuwa na changamoto za hapa na pale zinazosababishwa na serikali lakini Mnyika amefanya kazi kubwa sana kwa kipindi cha miaka 4 ya Ubunge wake.Hakuna mbunge yeyote wa CCM ameweza kuyafanya haya kwa miaka yote iliyopita.

Ukitaka kujua wabunge vimeo fanya ziara ya siku moja katika jimbo la Ukonga na ukirudi Ubungo utamuamkia Mnyika Shikamoo.
Mkuu Molemo msaidieni Mnyika. Kwa kweli wanaubungo tuna shida nyingi. Barabara ni mbovu sana. Hii inaweza kuchangiwa na mazingira ya ubungo hasa maeneo ya kimara lakini mbunge wetu haonekani huko kuja kuwahamasisha wananchi wake kujiletea marndeleo. Barabara za jirani zetu yaani jimbo la segerea ni nzuri na zinafanyiwa kazi na manispaa. Manispaa ya Kinondoni ina grader tena jipya lakini halionekani. Lingesaidia sana kuchonga barabara hata kwa wananchi kuchangia mafuta lakini halipatikani.
 
Last edited by a moderator:
Ninaishi Ubungo.Ingawa sikatai kunaweza kuwa na changamoto za hapa na pale zinazosababishwa na serikali lakini Mnyika amefanya kazi kubwa sana kwa kipindi cha miaka 4 ya Ubunge wake.Hakuna mbunge yeyote wa CCM ameweza kuyafanya haya kwa miaka yote iliyopita.

Ukitaka kujua wabunge vimeo fanya ziara ya siku moja katika jimbo la Ukonga na ukirudi Ubungo utamuamkia Mnyika Shikamoo.

amefanya mambo makubwa km yap????
 
Inafika wakati mtu unajuta kumchagua mtu fulani kuwa kiongozi wako,yaani unakaa muda wote huo huji hata kusikiliza kero zetu.Yapi uliyoahidi umetekeleza?

Nakuambia hivii,tutakutana kwenye sanduku la kura, sipigii chama napigia mtu kulingana na uwezo wake wewe naon umeshindwa.

Yani hata sasa hivi kuelekea uchaguzi mkuu umeshindwa kuja kujigonga? Tunakusikia mara mwanza mara Mtwara au hao ndio waliokuchagua.

Hivi unashindwa kuiga mfano wa Ndesamburo watu wa Moshi kwa raha zao,we kazi kupiga domo kwenye majimbo ya wengine.
 
Kwani anaisimamia serikali ya Ubungo....kama unatumia akili zako na si za lumumba ungegundua Mnyika ni kati ya wabunge wa kuigwa
 
Ni kweli kabisa Heri CCM walafi kuliko Mnyika MTENDAJI.Mnyika amalitendea haki jimbo lake.Pole zakom
 
kazi ya mbuge sio kuonekana mtaani kwako,kwani alikuadi kuwa atakuwa anaoenekana mtaani kwako?au unataka kuomba hela ya bia fanya kazi acha uvivu
 
Kuna wana-ubungo ambao hawakumchagua mwaka 2010 lakini wengi zaidi walimchagua na ndio maana alishinda !.

Kuna wana-ubungo ambao hawatamchagua 2015 (nadhani na wewe utakuwa mmoja wao) ila nakuhakikishia kuna wengi zaidi ya wale waliomchagua 2010 ambao watamchagua tena 2015 !

Sisi wengine tulimchagua mwaka 2005 (lakini Keenja akashinda), tukamchagua tena 2010 na tuko very proud na chaguo letu na tukishirikiana na wengine tutamrudisha kwa kishindo tena mwaka 2015 !

Hatujawahi kuwa na Mbunge mchapakazi Ubungo kama Mnyika !

Inafika wakati mtu unajuta kumchagua mtu fulani kuwa kiongozi wako,yaani unakaa muda wote huo huji hata kusikiliza kero zetu.Yapi uliyoahidi umetekeleza?

Nakuambia hivii,tutakutana kwenye sanduku la kura, sipigii chama napigia mtu kulingana na uwezo wake wewe naon umeshindwa.

Yani hata sasa hivi kuelekea uchaguzi mkuu umeshindwa kuja kujigonga? Tunakusikia mara mwanza mara Mtwara au hao ndio waliokuchagua.

Hivi unashindwa kuiga mfano wa Ndesamburo watu wa Moshi kwa raha zao,we kazi kupiga domo kwenye majimbo ya wengine.
 
Ninaishi Ubungo.Ingawa sikatai kunaweza kuwa na changamoto za hapa na pale zinazosababishwa na serikali lakini Mnyika amefanya kazi kubwa sana kwa kipindi cha miaka 4 ya Ubunge wake.Hakuna mbunge yeyote wa CCM ameweza kuyafanya haya kwa miaka yote iliyopita.

Ukitaka kujua wabunge vimeo fanya ziara ya siku moja katika jimbo la Ukonga na ukirudi Ubungo utamuamkia Mnyika Shikamoo.
Naishi Ubungo vilevile,sioni alichofanya,unasema amefanya mengi bila kuyataja huoni unaleta mahaba niue
 
Chadema chama langu kufa na kuzikana,mimi sio msaliti kama zzK na Act yake,sio ccm chama cha majambaz na mafsadi na cjawai fka rumumba kupewa buku 7000,ni cdm damu ata huyo mnyika akiniona ananitambua japo kwa sura na anajua mimi M4C pure.
ila wanachama wenzangu kwa majibu kama haya mnaotoa kwa mreta mada ni dhairi shairi kwamba hayatoshi kuwa sahh kwetu kumpatia mleta uzi,mengi ni majibu ya kahuni na tunaweza poteza imani kwa wageni wapya wa Jf ambao wanataka kujua mijadara ya chama inaendleaje?,na ikumbukwe kipindi hiki vijana na wazee ndo wameibukia kwenye siasa na wanapenda mabadriko.
Hivyo tujipange vyema kujibu hoja na maswali ya wachokozi wetu ili kuwapa moyo wanaokiona chama chetu cha cdm kama mkombozi wao vingnevyo ccm-A na ccm-B watatumulia vumbi hiyo oct.
 
Tumekuwa tukilaumu sana safari za J.Kikwete Ulaya na kusahau kutembelea na kutatua matatizo ya wananchi wake, hali hii napenda niifananishe na Mbunge wangu Mnyika yeye kila siku kimguu na njia ila mtaani kwetu haonekani.

Hatujakuchagua kuwa mbunge wa magazeti, kumbuka ni sisi wana Ubungo tuliokufanya ufikie hapo.

Nawasilisha na hii ni maalumu kwa wana Ubungo

MIRADI ILIYOTEKELEZWA KWA MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO TOKA 2010/2011, 2012/2013 NA 2013/2014.
S/NA KATA MRADI GHARAMA TSH. HALIHALISI YA UTEKELEZAJI
1 Kwembe Ukarabati wa jingo la kutolea huduma ya afya kwa akina mama na watoto (MCH). 27,245,433.00 Mradi umekamilika
2 Ubungo Kuchangia ujenzi wa police post eneo la Golani (awamu ya kwanza) 5,991,700.00 Mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
MRADI GHARAMA TSH HALIHALISI YA UTEKELEZAJI
Ubungo Umaliziaji wa kituo cha police msewa(awamu ya pili) 5,99,1,700.00 Mradi upo katika hatua ya umaliziaji
Kuchangia ujenzi wa kivuko cha waendao kwa miguu eneo la Mewe – Kibo kata ya Ubungo 5,000,000.00 Mradi umekamilika
Ujenzi wa kivuko cha waendao kwa miguu kwa mtaa wa kibo 4,500,000.00 Mradi umetekelezwa
3 Kibamba Ujenzi wa choo katika shule ya sekondari Hondogo 22,000,000.00 Mradi umekamilika
Umaliziaji wa choo cha shule ya sekondari Gogoni 10,000,000.00 Kazi haijatekerezwa
4 Mburahati Ununuzi wa wa madawati 200 ya shule ya sekondari Mburahati Tsh.65,000 13,000,000.00 Madawati 200 yalinunuliwa na kukabidhiwa katika shule ya sekondari Mburahati
Kuchangia Ujenzi wa Kingamaji katika eneo la Barafu kata ya Mburahati 1,659,000.00 Mradi umekamilika
Kuchangia ujenzi wa kalvati katika eneo la National Housing kata ya Mburahati(awamu ya kwanza) 4,792,000.00 Mradi umekamilika
Kuchangia ujenzi wa kalvati katika eneo la Nationl Housing kata ya Mburahati(awamu ya pili) 3,000,000.00
Kukarabati visima vya maji MBADECO,KWA BI ASIA na ANNA MKAPA na ujenzi wa kalvati eneo la National Housing 10,500,000.00 Kazi inaendelea
5 Kimara Kuchangia vifaa vya ujenzai wa kituo cha police 2,000,000.00 Mradi umepatiwa tofali 2,000 za inchi 5 na nondo za mm.16PCS 10
6 Saranga Matengenezo ya barabara ya Kibanda cha mkaa hadi kwa Abasi - Kimara B 4,000,000.00 Mradi umekamilika
S/NA KATA MRADI GHARAMA TSH. HALI HALISI YA UTEKELEZAJI
7 Mbezi Kuchangia ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu eneo la saba kata ya Mbezi 75,00,000.00 Mradi hauja tekelezwa na fedha ziko katika akaunti ya kata ya Mbezi
Kuchangia mradi wa maji wa kuweka by pass kwa ajili ya Makabe,Msakuzi na Mpiji Magohe 4,210,000.00 Kazi ya kuweka by pass imekamilika
Ununuzi wa madawati 120 kwa ajili ya shule ya msingi Msumi kata ya Mbezi 12,000,000.00 Madawati yamenunuliwa na kukuabidhiwa katika shule ya msingi Msumi
8 Makurumla Ujenzi wa kivuko cha waendao kwa miguu katika eneo la Jogingi kata ya Makurumla 7,000,000.00 Mradi umekamilika
Kuchangia uchimbaji na upanuzi wa mfereji wa maji ya mvua eneo la daraja la Mwinyi katika kata ya Makurumla 3,000,000.00 Mradi umekamilika
Kuchangia ukarabati wa madarasa 2 ya shule za msingi Mianzini kata ya Makurumla 5,000,000.00 Mradi umekamilika
Kuchangia ujenzi wa kivuko kinacho unganisha mtaa wa Kilimahewa 7,500,000.00 Mradi umekamilika
9 Mabibo Ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu Mabibo kisiwani 2,500,000.00 Mradi umekamilika
Ujenzi wa mifereji katika Zahanati ya Mabibo 2,500,000.00 Mradi umekamilika
Mradihaujatekelezeka na fedha za mradi huu zimebadilishwa matumizi.Fedha hizo zilitumika kujenga kivuko cha waenda kwa miguu katika mtaa wa Kanuni
S/NA KATA MRADI GHARAMA TSH HALI HALISI YA UTEKELEZAJI
Kuhangia mradi wa ujenzi wa daraja linalojengwa kwa nguvu za wananhi mtaa wa Kanuni 6,000,000.00 Mradi haujatekelezwa
10 Msigani Kuchangia ujenzi wa kivuko cha kudumu Msigani 3,085,000.00 Kazi imekamilika
Kuchangia mradi wa maji Msigani 3,500,000.00 Mradiumekamilika
11 Goba Kuchangia mradi wa maji Goba 3,000,000.00 Kazi ilifanyika kwa kulipa sehemu ya bill ya maji
Kuchangia ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kulangwa kata ya Goba 5,000,000.00 Mradi umekamilika
12 Makuburi Kuchangia mradi wa maji katika eneo la Makoka - Uluguluni 10,000,000.00 Mradi umekamilika
Kuchangia ujenzi wa kalvati na matengenzo ya barabara katika eneo la Ubungo Islamic sec.school mtaa wa Kibangu 10,000,000.00 Ujenzi umeanza
13 Manzese Kuwawezesha wanakikundi cha usafi wa mazingira ha mtaa wa Muungano kata ya Manzese 5,000,000.00 Kikundi kilikabidhiwa fedha kupitia uongozi wa kata ya Manzese
Ununuzi wa madawati 120 kwa ajili ya shule za msingi Ukombozi,Manzese,Uzuri na Kilimani 12,000,000.00 Madawati ya menunuliwa na kukabidhiwa katika shule za msingi Ukombozi,Manzese,Uzuri na Kilimani
14 Sinza Kuchangia ujenzi wa kituo cha Polie Sinza C 10,000,000.00 Kazi ya ujenzi inaendelea
JUMLA KUU 2333,302,796.00
S/NA KATA/MTAA JINA LA KIKUNDI MRADI VIFAA WANAVYO HITAJI MCHANGO WA WANACHI KIASI KILICHO OBWA MAONI YA OFISI YA MH:MBUNGE
1 MAKURUMLA/KINONDONI MANISPAA KINONDONI VIJAZNZA SACCOS SACCOS Komputa 3 za thamani ya tshs 1,5000,000.00 kifaa cha kuifadhia fedha (kiasi cha 600,000.00 2,100,000 1,100,000
2 UBUNGO UMOJAWA WANAWAKE UBUNGO TANESCO Kutengeneza sabuni Vifaa vya kutengeneza sabuni 2,975,000 1,500,000
Mapambo na usafiri Vifaa vya kupambia 930,000 0
3 MANZESE/KILIMANI PRUDENSI WOMAN SACCOS Kutotoa vifaranga Mashine ya kutotoa vifaranga 500,000 2,800,000 1,500,000
4 MBURAHATI JIPE MOYO WOMAN DEV(JIMOWODE) Kutengeneza sabuni za maji na vipande Vifaa vya kutengeneza sabuni 5,000,000 1,400,000
5 GOBA TUINUANE GROUP Mashine ya kutotolea vifaranga 4,000,000 1,900,000 1,500,000
6 KIMARA MELENIA YA TATU Kushona nguo na kudarizi Mashine za kushona nguo na kudarizi,mikasi na nyuzi 1,000,000 1,000,000
7 KIMARA-BARUTI-KITONGOJI CHA MATETE JUHUDI GROUP Kushona nguo na kudarizi 1,000,000 1,000,000
8 MABIBO GENDER TRAINING INSTITUTE Center for feminist leadership Printer hp 400n series (oloured) 450 and · Utp cable 20m….30,000.00 · Bookshelf 1 kubwa 200,000.00 1,000,000 1,000,000
JUMLA KUU 10,000,000
MIRADI YA JIMBO AMBAYO IMEPATIWA FEDHA KWA MWAKA 2013/2014
S/NA KATA MRADI GHARAMA
1 Mburahati Fedha kwa ajili ya malipo ya bili ya umeme kwa visima vitatu, cha Mbandeko, Bi Asia,Na cha Mama Anna Mkapa. 3,000,000.00
2 Saranga Kuhangia ujenzi wa chumba cha maktaba katika sekondari ya Mavurunza 15,000,000.00
3 Kwembe Kununua makalvati kwa ajili ya kuweka vivuko vya kuunganisha mitaa ya Mpakani,King’azi,Kisopwa,Kwembe na Luguluni 10,500,000.00
4 Sinza Ujenzi wa vivuko katika mitaa ya Sinza E(6 milion) na Sinza D(4milion) 10,000,000.00
5 Msigani Kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Malamba Mawili 10,000,000.00
6 Goba Ujenzi wa kituo cha Polisi 12,000,000.00
7 Kimara Kisima cha maji 10,000,000.00
8 Makurumla Uchimbaji wa kisima ha maji mtaa wa sisi kwa sisi
10,000,000.00
9 Makurumla Ujenzi wa kivuko ha waenda kwa miguu mtaa wa kwa jongo 7,000,000.00
JUMLA 87,000,000.00
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom