Mnyika mbona kimya?:Safari ya kifisadi Kigali.

ayatoayo mtu ni yale yaliyoujaza moyo wake, ukiona mtu anaongelea mabwabwabwabwa ujue moyoni na kichwani mwake umejaa ubwabwa tu...wewe ni bwabwa mwenyewe, huna maana. ungekuwa mwanaume halisi ungeelewa nilichoandika. siwezi kubishana na mabwabwa. sisi tunaokaa huku ubungo ndio tunaoliona joto ya jiwe, na mbunge huyu hatusaidii chochote, wala sijawahi kuona ameongelea matatizo yetu bungeni, zaidi ya kuongelea matatizo ya cdm in general kitaifa etc. ndo maana nimemshauri awaige wenzie kina tundu lisu, pamoja na kwamba ni wapambanani, wanajali kwao kwa wale waliompa kura. haiji akilini kuona mabomba yapo hadi majumbani mwetu lakini hayatoi maji...unataka matatizo yetu tumwambie nani ili atuwakilishie kwenye selikali kuu yatatulike? si kila mwanachadema anafanya kazi, wengine wapo hapo na wavivu na hawana faida kwenye chama wala kwa wananchi, zaidi ya kufurahia marupurupu, hata yale ya maendeleo ya jimbo basi tuyaone kwenye jimbo letu. kama hujaelewa hadi hapo, rudi shule kaanze chekechea.
Mkuu umenena. Watu wengine wanashabikia kitu hata hawakijui . A black box
 
keenja alijitahidi sana kutengeneza barabara, hela kidogo tu inahitajika hata kama si lami, kujaza mashimo tu ya zile barabara. fika pale kimara mwisho, nyooke either kwenda bonyokwa au upande mwingine kwenda king'ong'o kwa komba utarushwarushwa na mashimo kama huna akili nzuri. pale inahitajika hata ile hela ya mfuko wa jimbo tu kujaza mashimo kusawazisha ili tuendeshe magari na pikipiki kwa starehe. yeye hajawahi hata kufika kule tangu achaguliwe, wa nini sasa? halafu anamwita jk dhaifu, yeye pia ni dhaifu zaidi wasichekane....pia, usiseme mimi ni ccm...mimi ni chadema kwa taarifa yako...lakini inaniuma sana kununua maji wakati niko karibu na Ruvu na maji ya bomba la mchina yameingia hadi kwenye nyumba yangu lakini hayatoi maji....mbunge yupoyupo tu. barabara kwenda home ina mashimo ajabu.....anatusaidia nini sasa huyu? hivi ninavyoongea ndivyo raia wa mtaani wanavyoongea.

Ndugu yangu humu kuna watu uwezo wao wa kufikiri umefika mwisho na unawaonea kuwataka wajivue koti la ushabiki wenye upofu. Mnyika tumeshamsema na kumshitua humu ili aibuke alinde nafasi yake katika jimbo la ubungo lakini in most cases wale wanaojifanya wanampenda ndiyo wanamhujumu kwa kumpa ushauri uliojaa mabezo na yeye kupanda kichwa. HALI YA JIMBO LA UBUNGO ni mbaya sana na hakuna utakapokwenda ukasikia sifa nzuri za Mnyika.

Majuzi ametoa hoja kwamba ameacha mchango wake kwa diwani wa kimara na kuwataka watu wakakabidhi kichango huko. Ametoa tangazo hilo kwa njia ya gazeti wakati yuko hapa hapa Dar na alikuwa na uwezo wa kuwafikia wananchi. Hali ya barabara za kimara ni Mungu tu ndiye anajua na zina hali mbaya kuliko alivyozikuta wakati alipochaguliwa.
 
Huku Ludewa tangu uhuru hatujaona lami. Maji tunachota mtoni. umeme tunauona hospitali tu tena mwish saa nne usiku. Lakini tuna mbunge naitwa Filikunjommbe na tunamkubali. Sasa ndugu yangu sijui unalalamikia nini. Hali ya maisha na huduma za jamii katika nchi hii haziwezi kuja kwa kufumba na kufumbua. Inahitajika mipango ya muda wa mfupi, wa kati na mrefu, kwa kuanzia na kubadili mind set zetu kuwa mbunge atajenga miundombinu as if ana source of fund yeye kama yeye. I am sure hata ungepewa ubunge wewe usingefanya hayo unayomlaumu Mnyika.

Kwa sasa inatakiwa tujenge system ya utawala bora na uwajibikaji kama taifa. Hii itazuia ufisadi/wizi wa fedha za umma na hivyo itawezekana kujenga miundombinu hiyo unayodai ni kero. Kwa sasa nchi hii ni kama gunia lililotoboka ndugu yangu. Hata kama Mnyika akitaka kujenga hiyo miundombinu ya kijamii wakati fedha nyingi inaibwa na nyingine kutoroshewa Ulaya itawezekana wapi jamani?
 
Ni kweli hizi ziara si za muhimu? If so why MCT wafadhili hii?

[h=2]MCT yafadhili ziara ya wabunge, Wawakilishi kwenda India[/h]


BY ROMANA MALLYA



23rd September 2012


email.png

Email



printer.png

Print



comment_bubble.png

Comments





headline_bullet.jpg
Ni kujifunza sheria ya haki ya kupata habari




Baraza la Habari Tanzania (MCT) limefadhili ziara ya watu 12 wakiwemo wabunge na wawakilishi kwenda nchini India kujifunza jinsi sheria ya haki ya kupata habari zinavyofanya kazi ili kutetea suala hilo hapa nchini.
Ujumbe wa wabunge na wawakilishi hao unatarajia kuondoka leo na utaongozwa na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Juma Nkamia, Mbunge wa Viti Maalum, Rebecca Mngodo (Chadema) na Mbunge wa Bumbwini, Ramadhani Haji Saleh (CCM).
Wengine ni Mbunge wa Jang’ombe visiwani Zanzibar, Hussein Mussa Mzee (CCM), Mbunge wa Nkenge Assumpter Nshanju Mshana, mbunge wa Viti Maalum, Moza Abeid Saidy (CUF), mbunge Mchinga, Said Mtanda (CCM ).
Wajumbe wengine kwenye safari hiyo ni Wawakilishi kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ali Mzee Ali na Ismail Jussa Ladhu ambao watafuatana na maofisa watatu kutoka MCT ambao ni John Nguya na Ziada Kilobo kutoka Dar es Salaam na Shifaa Hassan kutoka Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Kajubi Mukajanga, alisema maandalizi yote ya ziara hiyo hadi kurudi kwao itagharimu kiasi cha Dola za Marekani 67,247.
Mukajanga alisema, kupelekwa kwa kundi hilo la Wabunge na Wawakilishi kwenye nchi inayoendelea ambayo ina sheria ya haki ya kupata habari ipo katika mpango wa mwaka huu wa MCT.
“Uzoefu kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano hivi katika mchakato wa kupata sheria hii umeonyesha kuwa kuna wasiwasi kuhusu sheria hii kwamba inaweza kuleta vurugu ama fujo, hivyo tumeandaa ziara hii kwa mtazamo kwamba kuona ni kuamini,” .
Aidha alisema kamati ya maendeleo ya jamii ndiyo inayoshughulikia masuala ya habari ambapo kwa Baraza la Wawakilishi kamati ya Mifugo, Utalii na Uwekezaji na Habari ndiyo inayoshughulika na mambo hayo.
Alisema ingawa pamoja na kamati hiyo Baraza la Wawakilishi limemteua mjumbe wa kamati ya Katiba na Sheria kwa ajili ya safari hiyo ya mafunzo.
Alitaja baadhi ya maeneo ambayo watu hao watatembelea kuwa ni, Ubalozi wa Tanzania nchini New Delhi, ofisi ya Tume Kuu ya Habari, Ofisi ya Tume ya Habari ya Jimbo, Kituo Kikuu cha Habari cha Umma, Idara ya Utumishi na Mafunzo na ofisi ya Taifa ya Kampuni ya Haki ya Kupata Habari.
Aidha, alisema mwaka ujao MCT inatarajia kuwapeleka waandishi wahabari kwenda nje ya nchi ili nao wapate nafasi ya kujifunza yale yanayofanywa na wenzao katika kuitekeleza sheria hiyo.
Mwenyekiti wa msafara huo, Nkamia akizungumzia kuhusu sheria hiyo, alisema mtazamo wake ni kwamba, nchi imekuwa na wasiwasi pengine usalama wa taifa unaweza kuvurugika kitu ambacho sio kweli.
Alisema ziara hiyo itawawezesha wao pindi watakaporejea nchini waweze kujenga hoja bungeni.
Pia alisema kuwepo kwa sheria hiyo itasaidia kuwalinda waandishi na kuweza kufanya kazi zao bila kuingiliwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wa msafara huo, wamesema kuwa safari hiyo inalenga taifa kwa ujumla.



SOURCE: NIPASHE JUMAPILI


 
Mnyika ni mbunge wangu kule kimara. hajafanya lolote kwenye jimbo langu tangu achaguliwe. mimi nilikuwa mmoja wapo wa watu waliopigwa na mbu na baridi kulinda kura zake zisiibiwe na magamba. lakini sasaivi maji naagiza lori lije nipandishe kwenye tank kwa pesa yangu binafsi wakati mabomba ya mchina yametandikwa hadi kwenye nyumba yangu, maji hayatoki. mbunge huyu anatusaidia nini? MWAKE 2015 NITACHAGUA MBUNGE WA CHADEMA, lakini nataka wambadilishe aje mgombea mwingine wa chadema na si mnyika, kwasababu akigombe atena, wananchi ha huku hawataki hata kumsikia...wanaona bora hata keenja. magari yanaharibika kwasababu barabara mbaya mno mitaa ya kimara...hatujawahi kuona ameongelea hilo bungeni hata siku moja ili tujue kuwa basi amehangaika kidogo, anachofanya ni kupigania chama kitaifa na kututelekeza...sisi hatuli chadema pamoja na kwamban i wanachadema, tunahitaji utujali ili tuone uzuri wa chama. amini msiamini, kama mtu mwingine wa chadema hatagombea ubungo, basi jimbo linaweza kurudi kwa magamba au kwenda cuf pamoja na kwamba kimara na ubungo tumejaa WACHAGA.

I really like wot u said
 
Huku Ludewa tangu uhuru hatujaona lami. Maji tunachota mtoni. umeme tunauona hospitali tu tena mwish saa nne usiku. Lakini tuna mbunge naitwa Filikunjommbe na tunamkubali. Sasa ndugu yangu sijui unalalamikia nini. Hali ya maisha na huduma za jamii katika nchi hii haziwezi kuja kwa kufumba na kufumbua. Inahitajika mipango ya muda wa mfupi, wa kati na mrefu, kwa kuanzia na kubadili mind set zetu kuwa mbunge atajenga miundombinu as if ana source of fund yeye kama yeye. I am sure hata ungepewa ubunge wewe usingefanya hayo unayomlaumu Mnyika.
Kwa sasa inatakiwa tujenge system ya utawala bora na uwajibikaji kama taifa. Hii itazuia ufisadi/wizi wa fedha za umma na hivyo itawezekana kujenga miundombinu hiyo unayodai ni kero. Kwa sasa nchi hii ni kama gunia lililotoboka ndugu yangu. Hata kama Mnyika akitaka kujenga hiyo miundombinu ya kijamii wakati fedha nyingi inaibwa na nyingine kutoroshewa Ulaya itawezekana wapi jamani?

heri wewe umesema,unajua kuna watu wanalaumu lakini wanakua km hawajui kuwa serikali iliyoko madarakani imeshikilia kila kitu?Na wakati mwingine wanafanya makusudi ili kuwakosanisha wabunge na wananchi.Je Mnyika kutoa hizo pesa kwa ajili ya barabara amefanya vibaya?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom