Mnyika mbona kimya?:Safari ya kifisadi Kigali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika mbona kimya?:Safari ya kifisadi Kigali.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lole Gwakisa, Sep 17, 2012.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ndugu Mnyika huwa mwepesi sana kulaani, kutoa maoni na hata mawzo mbadala katika matukio mbali mbali ya kisiasa au vinginevyo nchini, kwa kusisitiza msimamo wa chama chake, CHADEMA.

  Habari za kustua za mpango ulioandaliwa chini ya Meya wa mji wa Moshi, kwa ajili ya watendaji wake katika Halmashauri imesisimua umma, hasa katika mitandao, kulaani matumizi mbabaya ya fedha za umma.
  lMbaya zaidi kwa vile CDM imejipambanu kuwa mbadala wa CCM katika kuongoza nchi hii.

  Yale yaliyoonekana wiki hii huko Moshi, ni dhahiri ufisadi wa mali ya umma.

  Sasa wengi wetu tulitazamia msimamo wa CDM juu ya hili,lakini wiki inakatika.Moshi ni"Mecca" ya CDM na kwa haya kutokea Watanzania tunapata somo kubwa sana hapa.

  Kisemwacho majukwaani inaelekea ni maneno matupu, ndugu zetu hawa wakikamata nchi tusitegemee ufisadi kuisha.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mnyika ni mbunge wangu kule kimara. hajafanya lolote kwenye jimbo langu tangu achaguliwe. mimi nilikuwa mmoja wapo wa watu waliopigwa na mbu na baridi kulinda kura zake zisiibiwe na magamba. lakini sasaivi maji naagiza lori lije nipandishe kwenye tank kwa pesa yangu binafsi wakati mabomba ya mchina yametandikwa hadi kwenye nyumba yangu, maji hayatoki. mbunge huyu anatusaidia nini? MWAKE 2015 NITACHAGUA MBUNGE WA CHADEMA, lakini nataka wambadilishe aje mgombea mwingine wa chadema na si mnyika, kwasababu akigombe atena, wananchi ha huku hawataki hata kumsikia...wanaona bora hata keenja. magari yanaharibika kwasababu barabara mbaya mno mitaa ya kimara...hatujawahi kuona ameongelea hilo bungeni hata siku moja ili tujue kuwa basi amehangaika kidogo, anachofanya ni kupigania chama kitaifa na kututelekeza...sisi hatuli chadema pamoja na kwamban i wanachadema, tunahitaji utujali ili tuone uzuri wa chama. amini msiamini, kama mtu mwingine wa chadema hatagombea ubungo, basi jimbo linaweza kurudi kwa magamba au kwenda cuf pamoja na kwamba kimara na ubungo tumejaa WACHAGA.
   
 3. k

  kitefure2 Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani hayo majimbo ya ccm kuna nini kwenye ubora wa maisha ya walalahoi
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  tunachohitaji ni kwamba, wabunge wa chadema waonyeshe tofauti yao na wale wa ccm. waonyeshe whats so special about them, ni kwanini tusiwachague wale wa ccm tuwachague wao? onyesha utofauti wako. kama wabunge wa ccm wanatembelea na kutatua matatizo ya jimbo lako, halafu wewe wa chadema unaishia kwenye chadema taifa tu waliolinda kura zako usiku kucha umewasahau, unafikiri tutaona nani bora kati ya gamba na gwanda? hii iko wazi. hatujaingia chadema kwa kuamini kuwa walioko chadema ni malaika, wao pia wanaweza wakawepo mchele na makapi vilevile, makapi/pumba lazima tuzipepete kama si kuwashauri wakaze kamba tusijekupoteza jimbo....kwa mwenye akili ameshaelewa.
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,834
  Trophy Points: 280
  Sijapenda hapo mwisho ni bora ukapenda kutoharibu hoja zako
   
 6. m

  mliberali JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 2,888
  Likes Received: 1,518
  Trophy Points: 280
  serikari yako dhaifu ya CCM imekufanyia nini kabla ya mbunge Myika wa CDM
   
 7. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,177
  Likes Received: 1,259
  Trophy Points: 280
  Fafanua zaidi kuhusu safari za kigali!! kuna nini? mbona thread haina lolote?
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu basi angalau kumbuka ulipotoka.
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  keenja alijitahidi sana kutengeneza barabara, hela kidogo tu inahitajika hata kama si lami, kujaza mashimo tu ya zile barabara. fika pale kimara mwisho, nyooke either kwenda bonyokwa au upande mwingine kwenda king'ong'o kwa komba utarushwarushwa na mashimo kama huna akili nzuri. pale inahitajika hata ile hela ya mfuko wa jimbo tu kujaza mashimo kusawazisha ili tuendeshe magari na pikipiki kwa starehe. yeye hajawahi hata kufika kule tangu achaguliwe, wa nini sasa? halafu anamwita jk dhaifu, yeye pia ni dhaifu zaidi wasichekane....pia, usiseme mimi ni ccm...mimi ni chadema kwa taarifa yako...lakini inaniuma sana kununua maji wakati niko karibu na Ruvu na maji ya bomba la mchina yameingia hadi kwenye nyumba yangu lakini hayatoi maji....mbunge yupoyupo tu. barabara kwenda home ina mashimo ajabu.....anatusaidia nini sasa huyu? hivi ninavyoongea ndivyo raia wa mtaani wanavyoongea.
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nilikotoka ni afadhali kuliko huku kwa mnyika. hayo mabomba yalietwa na magamba, yeye hajaleta chochote, kama yupo hapa atuambie nini amefanya tangu achaguliwe...basi hata kuongea tu bungeni kuhusu matatizo yetu aongee, yeye anajikitak wenye chadema taifa tu m4c. wenzie kina tundu lisu wanapiga mzigo kitaifa na jimboni wapo...wabunge wengi wa cdm wanapiga mzigo taifani na jimboni wapo, yeye anapiga taifani peke yake jimboni anazembea haoni kama anahatarisha kura za cdm 2015.....
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  kwanini sasa hivi wapo nani katk serikali kuu?kipi bora Mnyika nayekuja na Ideas ambazo magamba wasingewahi zifikiri ila hwataki zitenda, au magamba waje na solutions zilezile zilizoshindwa huku wakiwa na sababu kibao za kujitetea.Possibly mnyika na mawazo mapya kwani ipo siku magamba watalazimishwa na raia kufanya au kutoka
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na mpiga debe wao namba 1 humu JF anaejiita Mzee Mwanakijiji, naona kaingia mitini kuhusu hilo.
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Huyo mkuu wa mkoa aseme kuwa alitegemea hiyo safari ifanyweje?kwani hapa njia pekee ni kupunguza watu au kuwaleta wataalamu wa Kigali wakiwa na video napolicises zao za usafi miji waje wafundisha moshi.Ila kama alipiga chini project na hakuwa na mbadala kachemsha.Kwa moshi Mji unaoongoza kwa usafi TZ na wana sheria kali sana, usafi ni issue ya kila siadhani kama kuna diwani ambaye ambaye angekuwa tayari kosa wakati ana jukumu la kurudi simamia usafi katk kata yake.

  Njia ya kuwaleta wataalamu au hata kupeleka madiwani wachache nighali zaidi.Kwani hao waliokwenda wangetumia hela karibu robo,na wakirudi walipwe posho kuwafundisha wengine ambao nao wangehitaji posho.Na hata kuleta wataalamu hata watatu tuu ni gharama kuwalipa na pia kuwalipa hao madiwani posho zao.Yoote haya pia haya gurantee mafanikio ya zoezi hilo.

  Kwa hiyo idadi ya watu na hiyo hela kama ingetosha kuwapa na osho bado ni matumizi yasiyoogopesha kama mawizarani:

  Million 200 si hela kama mnavyodhani.kwa watu wengi hivyo kwenda nje ya nchi.

  -hela/watu =>Mil 200/57=3.5087719mil/per person

  -mil 3.51 au 3,510,000/= 3,510,000/1600=$2,193.75/pp

  -hela kwa siku kwa kila mtu. katika week(assuming 7 days)=> $2,193.75/pp/7=$313.393per person, per day.

  Bei ya hotel yenye ubora Kigali ni around $200 per person per night. na inaweza zidi sana.Achilia mbali matumizi mengine,kama stationery,phone,internet, transport etc.Tz yenyewe hotel zinazidi $ 2,000 kwa siku,hata kama kitazidi ni kiasi kidogo ambacho mtu alistahili baki na kitu hata cha kuleta zawadi kwa familia.

  Seems ni msukumo wa kisiasa kuliko akili.

  Kwani viwango vya per diem vya serikali kuu kwa mtu akiwa nje ya nchi kwa ukanda wa africa mashariki na kati ni zipi?
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Mkuu wana CDM damu damu wako busy kuikwepa hii mada inayowaonyesha CDM in its true colours!
  Mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo!!!
   
 15. C

  Chief JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Hii safari ilifanyika au la? Nani kakuahidi kuwa CHADEMA, au chama chochote kile kikishika madaraka, ufisadi utaisha? Ufisadi ni tabia ya mtu. Ikiwa watu na dini zao wanafanya ufisadi sembuse kuwa ndani ya chama? Suala si ufisadi kwisha, bali hatua za kisheria kuchukuliwa mara moja ufisadi ukitokea. Matokeo yake ni kuupunguza tu to manageable level. China watu wanapigwa risasi bado hawakomi.
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Gama ataumbuka tuu na siasa zake..Aje na njia mbadala za kuweza unganisha hiyo ziara na mafanikio ya usafi kwa kata zote za manispaa ya Moshi bila kuwekeza hela nyingi.

  Ndio maana CCM HUCHUKUA NYINGI ZAIDI ILI ZIFIKIE KTK BILLIONS.VICHWA MAJI WAKIONA 2BN wanaona ni kidogo halafu 200mil wanaona nyingi.Hata helcopter walisema ni ghali na anasa hadi mnyika akawaumbua kwa maelezo ya Kina.Nadhani subirini chama kikifanya uchunguzi mtapewa majibu.Hizi ni dondoo tuu kuonyesha jinsi CCM wanavyoingia katk siasa finyu.
   
 17. S

  SEBM JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kweli Mh. Mnyika amewashika pabaya Magamba...kutwa, kucha mnatafuta mada yenye kumchafua; kaanza huyo wa kumtaka atoe tamko, mara akaja mwingine wa hakuna kilichofanyika Kimara...

  Mpaka siku iishe, mtakuwa na mengi ya kuongea na kuandika...

  Karibuni sana JOHN MNYIKA: Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA) mpate habari za uhakika za maendeleo ya Jimbo la Ubungo.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mifweza yote hiyo kujifunza kufagia?
   
 19. Upcoming

  Upcoming Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Ndo huo utofauti kati ya CDM na hiyo s/kali unayoita dhaifu tuone kweli magwanda hayafanani na magamba
   
 20. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  unashangaa kufagia wakati zaidi ya nusu ya watanzania wote wanaotumia vyoo vya kigeni hawajui flash wala jua ubaya wa uchafu?Nenda muhimbili katika toilets wala si za wagonjwa tuu ila watumiavyo staff,then UDOM na Mlimani.Then uje piga bla baha hapa kuwa course ya kutumia vyoo ya nini?kwani wasomi hawajui tumia vyoo?Huku nchi ikipoteza mamilioni ya hela kwa ajili ya kutengeneza ,kunjenga mifumo ya maji chafu ktik majengo.
   
Loading...