Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
Si alisema yuko bungeni toka 1975 kulikoni tena alikuwa analala?
huwezi jua labda kuna mtu alikuwa anamtafuta si yuko singo
Si alisema yuko bungeni toka 1975 kulikoni tena alikuwa analala?
Nadhani baadi yetu tuko kwenye TV zetu tukiangalia kupigwa kura za kumthibitisha Mizengo Pinda kama waziri mkuu.
Ukiacha swali zuri la Mh. JOhn Mnyika kuhusu usiri wa upigaji kura swali kali lilikuwa la Tundu Lissu ambaye alisoma kanuni za bunge kifungu 53 (6a) na (6c).
Amevisoma kwamba hasa kile (6a) kinasema kwamba hoja ikiletwa na serikali ni lazima kwanza ijadiliwe na bunge kama haikupitia kwenye kamati. Ama kiongozi wa upinzani anahusika katika mjadala.
Sasa hoja hii ya umpitisha Waziri mkuu haikupitia utaratibu huo wa vifungu hivi.
Hivyo Mhe. Tundu Lissu alichofanya ni kumuomba Mh. Spika mwongozo kuhusu hilo.
Niaona swali hilo ni kali nikasubiri kuona Mama Makinda akituthibitishia u-genious wake kwenye kanuni za bunge.
Badala yake alichofanya Makinda ni kwanza hakukana ukweli wa hoja ya Tundu Lissu na badala yake akaishia kusema "Jamani hapa tulipofikia hatuhitaji kusomeana tena Kanuni, tuendelee na utaratibu wa kuhesabu kura"
Umeona ambavyo bunge litakavyompelekesha huyu mama yetu akitafunwa na kanuni zilezile ambazo ni msahafu wao.
Ndiyo maana kuna thread niliomba kama kuna mwenye kanuni za bunge atudondoshee tuzichambue na kuhesabu point moja hadi nyingine ya ukiukaji na tuzitungie kitabu cha ukiukaji wa kanuni za bunge ifikapo 2015
Niko naednelea kupata live broadcast.
Tafadhali endeleeni kutupa uhondo. Huku mashenzini mbeya tannesco wameamua kuuchukua umeme wao - kata rudisha kata rudisha!! Ndo wawekezaji waje nchi hii!!
dah noma yani nimetune itv muda nna bahati kweli nikaanza na Mnyika.Guys are confident and flowing with vigour.
Hapa kazi ipo!..I am starting to love this Tundu Lisu guy!
Siyo kwamba wabunge CCM hawajui, lakini si unajua tena....
Tusubiri labda ataijibu kabla ya uchaguzi wa naibu spika.Kwahiyo oja ya lisu imekufa au?makinda tayari ameshaanza kuzipiga chini oja za wapinzani.
Kazi ipo msimu huu!!!!Mmemwona Spika akitafuta majibu kwa Spika aliopita!!!!!!:yield::yield::yield::yield::yield::yield: