Mnyika: Kwa mkataba mbovu wa Tanzania liquefied natural gas project kwa miaka 30 ijayo hatutakuwa na gesi

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
KWA MKATABA MBOVU WA Tanzania Liquefied Natural Gas Project KWA MIAKA 30 IJAYO HATUTAKUWA NA GESI TANZANIA."

Na, John Mnyika
#NguvuYaKusini

Songo Songo ya Lindi imewaathiri, limekuja bomba la mchina limewaathiri, Kusini hamnufaiki na rasilimali ndio maana mnakimbizana na Korosho pekee yake. Sasa kuna mradi mkubwa zaidi ya hizo, mradi wa kujenga kiwanda cha kuchakata gesi na kuigeuza kuwa kimiminika.

Nyinyi ukanda wenu huu mbele kidogo ya baharini kuna gesi futi za ujazo Trilioni 57, utajiri mkubwa sana. Huo mradi wa LNG (Tanzania Liquefied Natural Gas Project) ni mradi ambao uwekezaji wa mradi ni Dola Bilioni 30 sawa na Trilioni 60. Mradi ambao kila mwaka utaingiza kwenye mapato ya Serikali Trilioni 14, pesa nyingi sana. Lakini kwa mazingira ya kimikataba na kisheria na Sera za Serikali na mapato kupokwa na Serikali Kuu na mikataba mibovu ambayo nchi yetu inaingia watoto na watu wazima wa leo wataendelea kuwa maskini.

Ili taifa tuweze kujifunza tulikosea wapi, kwanza kabla hatujasaini, kwani tumekwisha saini mkataba wa awali na mwezi Disemba 2022 wanataka kusaini mkataba kamili wa nchi mwenyeji lakini nyinyi wananchi wa Kusini hamfahamu. katika ule mgogoro wa gesi ya Mtawara wa gesi itoke au isitoke ilikuja Kamati ya Bunge kuchunguza kujua tatizo lipo wapi na kwanini wananchi wamekuwa na msimamo huo ile ripoti ilifanywa kuwa siri, kwa kuwa wanataka kuingia mkataba mwingine hatua ya kwanza hiyo ripoti iwekwe hadharani ukweli ujulikane.

Pili, wakati tukiwa bungeni iliwahi kutungwa sheria inayosema kwamba mikataba mikubwa yenye maslahi kwa taifa baada ya kusainiwa inapaswa kupelekwa bungeni, sasa kwa kuwa mkataba huu ni mkubwa sana na ukiingiwa huu mkataba wakawekeza kwenye mradi na gesi ikachakatwa na kuanza kuuzwa, gesi itakuwa inapandishwa meli nakwenda kuuzwa nchi mbalimbali na kwa kuwa makampuni yana hisa nyingi kwa mikataba mibovu waliyoingia na Serikali, mapato yatakayopatikana yataenda nchi mbalimbali na yale kidogo yanayosailia nchini yataenda Dar es Salaam na Dodoma utasikia tu matumizi ya anasa ya Serikali na umasikini huku Kusini utabaki.

Kwa sababu ya ukubwa wa mkataba huu (Tanzania Liquefied Natural Gas Project) na kwa kuwa Bunge lililopo Dodoma kimsingi ni Bunge la chama kimoja, la ndio tu, mkataba huu nao uwekwe hadharani tuone masharti yake yanamanufaa kwa wananchi?.

Taarifa nilizonazo mimi siku tone la kwanza la Gesi hii iliyogeuzwa kuwa kimiminika litakapochukuliwa kwenda kuuzwa nje, utatumika huu utaratibu wa kuichukua na kuiuza kwa miaka 30 ambapo Gesi itakuwa imemalizika. Watu wananufaika kwa miaka 30 kwa mikataba yetu mibovu.

Watoto wa leo wakifikisha miaka 30 huko mbele kwao itabaki kwenye vitabu vya historia kwamba kulikuwa na utajiri wa haya Matrilioni kupitia Gesi. Ni lazima tuone kila kitu ili tujue haya mapato ya Gesi tunayapataje na yanabadili vipi maisha yetu.

Katika nchi ambazo ziliweka kipaombele wananchi kunufaika na rasilimali mapato wanapima kabisa, hii Gesi itakaa miaka 30 tunataka watoto watakaokuja miaka 30 ijayo hata kama Gesi itakuwa imeuzwa wakute kuna pesa za hayo mauzo ya Gesi za kuibadili maisha yao.

Kwa kuwa tunarudi tena kwenye LNG (Tanzania Liquefied Natural Gas Project) lazima tuiambie Serikali mlituahidi uchumi wa Gesi Kusini, huo uchumi wa Gesi upo wapi?. Ndugu zangu msiishie kuzungumzia Korosho tu, lazima tushughulike na pande zote.

Wakati umefika sasa wananchi wa Kusini mkumbuke 2005 Chadema tulikuja kwenu labda pengine kipindi hicho hamkutuelewa ninarudia tena mtuelewe vizuri, tuliwaambia nchi hii kuna tatizo la kisera, mamlaka kuhusu rasilimali za nchi yamechukuliwa na kulimbikizwa sana Serikali kuu, mapato yanaenda Serikali kuu na hayarudi kwenye maeneo yenye rasilimali, tukawaambia suluhisho la jambo hili ni tubadili mfumo wa utawala wa nchi yetu, tutengeneze tulichokiita Serikali za majimbo ili wananchi wa maeneo husika wapate mapato na wanufaike na rasilimali zao.

Mhe. John Mnyika
Katibu Mkuu Chadema
#NguvuYaKusini

Kusikiliza zaidi
 
Ni mjinga tu ndie atakaeweza kumwamini huyo muongo ,ni lini serikali ilasaini mkataba ambayo unaonyesha baada ya miaka thelethini hakutakuwa na gesi?
 
umeonyesha kuwa hujasoma umekimbilia ku comment ushamba wako.
Swala ni kwamba kama gesi ikiacha kuchimbwa inaweza kuisha baada ya miaka 30,ujue gesi ni rasilimali inayoisha,hapo umeona kiwango cha gesi kilichogundulika
 
Ukiona jambo linapigiwa kelele sana na Makamba ujue ameshaona fursa yake binafsi, anachofanya ni kuihusisha nafasi yake kuwa waziri husika kama kisingizio.

Lakini kwa historia ya Makamba sio mtu wa kumuamini kwenye mambo kama haya, na mtawala anapokuwa sio mfuatiliaji mzuri, basi hali ndio inakuwa mbaya zaidi.
 
Huo Mkataba tunapata Ngapi Asilimia ?, Tutakuwa na Hisa kiasi Gani ?

Hizo Trillioni 14 Kwa mwaka zitapatikana vipi, Je ni za Uhakika kupatikana au nazo ni kujazana Ujinga tu mwisho wa siku unaambiwa baada ya makato haya na yale na Gesi Kushuka Bei Duniani na gharama za uendeshaji inabidi sisi ndio tuwalipe waendeshaji
 
Huu mkataba ni siri sana wanausoma tu wakuu na wastaafu kadhaa.
 
Back
Top Bottom