Mnyika: Kuna njama zinasukwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa kuifuta CHADEMA

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,300
2,000
Sio siri CCM wameivuruga CUF na kumuua Seif Sharif ila Maalim hakukubali kufariki baada ya siku tatu akafufukia ACT (Jesus of Zanzibar).

Sasa baada ya kushindwa na Maalim Seif (Marehemu) CCM wamekusudia kuiuwa Chadema na kuivunja nguvu wakiamini ,uwanja wa siasa utakuwa mwepesi.

Suali Je CCM wataweza ? Nikiiangali CHADEMA ,Mbowe ni mwepesi sana ndani ya siasa za CHADEMA kuna vigogo vya siasa na vinatisha vibaya sana na sijawahi kuwaona watu hawa wa Chadema kucheka cheka hovyo ,wapo kikatili zaidi kwa maana wapo tayari kwa mapambano ya kisiasa .
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,356
2,000
Akizungumza na Waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye ofisi za Chadema Kinondoni, nje ya Jiji la Dar es Salaam, Katibu Mkuu huyo wa Chadema amesema yapo maandalizi ya kuifuta Chadema ili kuwaridhisha watu fulani ndani ya serikali.

Kinachosubiriwa ni timing tu, kwa maana ya wakati muafaka wa kufanya hivyo ili kupata kisingizio.

Hivyo Mh Mnyika amewaasa viongozi na wanachama wa Chadema kuwa waangalifu katika kipindi hiki ili kukwepa mtego uliowekwa na ofisi ya Msajili ikishirikiana na idara zingine.

Mungu ibariki Chadema
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,513

Aliyeasisi mpango wa kuiua Chadema kafa yeye na sasa yuko kuzimu anateseka,sasa haya masalia yake yanayoendeleza mpango mkakati huo na yenyewe kufa lazima yafe tena vifo vya mateso makali.
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,234
2,000
Pa1 na kujifanya unabalance ili uonekane na ww umeandika uzi wa kuisifu chadema, lkn uzi huu utasuswa haraka sana kwa sababu ya kumdharau mfalme wao. Kitendo cha kusema Mbowe ni mwepesi afu ukawasifia wengine hapo tayar ushaharibu uzi wako. Nyumbu wanaamini chadema ni Mbowe na Mbowe ndio chadema.
 
Inategemea msomaji ,labda niseme ule wakati wa CUF ,Marehemu Maalim Seifu alikuwa anatisha kuliko Lipumba na ndivyo ilivyo kwenye CHADEMA ,Mbowe ni Mwenyekiti hivyo huwa ni laini tu na ndivyo inavyobuniwa.
Umeona kuwa nia na lengo ni kuimaliza Chadema kwa kukata kichwa ,yaani CCM wanatenganisha kichwa na mwili kwa Chadema na kwa hali hiyo ni lazima Chadema wajipange,CCM wataweza kupangua na kushinda katika mwenendo na muundo wanaouunda,ili kwao mambo yawe mepesi.
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,244
2,000
Wameshajua kwamba kuchomoka hapa tulipo kwenye huu mkwamo wa kisiasa bila katiba mpya ni ngumu sasa kwa akili yao wanadhani njia rahisi ni kuifuta Chadema na hapo ndio wanajichimbia kaburi kabisa

Ingekuwa rahisi hivyo Mwendazake na ubabe wake wote alishindwa nini?Huyu mama asipotumia akili zake mwenyewe hafiki mbali,Na kama ni akili zake basi ajiandae sababu anaenda kushindwa vibaya.
 
digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
5,459
2,000
Wafute tuone. Nani aliwadanganya CHADEMA ipo kwenye makaratasi ya msajili wa vyama
Bure kabisa wewe,mlisema wakimtia nguvuni mwenyekiti wa chama Cha magaidi hakutakalika nchi hii,Leo Ni wiki ya pili Yuko rumande anakula na kulala kwa kupangiwa.

Chadema ukifika Wakati wa kuifuta itafutwa na kusiwepo mtu wa kulalama.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,356
2,000
Bure kabisa wewe,mlisema wakimtia nguvuni mwenyekiti wa chama Cha magaidi hakutakalika nchi hii,Leo Ni wiki ya pili Yuko rumande anakula na kulala kwa kupangiwa.

Chadema ukifika Wakati wa kuifuta itafutwa na kusiwepo mtu wa kulalama.
hivi kwa haya yanayoendelea unadhani nchi hii inatawalika ? hushangai mamaako kawa kiguu na njia ! unajua ni kwanini ?
 
lebabu11

JF-Expert Member
Mar 27, 2010
2,185
2,000
Kazi kubwa ambayo watanzania wanatakiwa kufanya bila kujali itikadi zao, vyama vyao na hata makundi yao ya kijamii na kiuchumi ni kutoa elimu ya uraia/utaifa kwa kuwashughulikia watumishi wa uma ambao kikatiba hawatakiwi kujihusisha na siasa moja kwa moja au kwa uwazi.
Mmojawapo wa watumishi hao ni msajili wa vyama ambaye anatuhumiwa hapa (sina maana kuwa tuhuma ni za kweli).
Watumishi wanaotakiwa kikatiba na kisheria kutokupendelea upande wowote wa vyama vya siasa, wakionekana wanajihusisha na upendeleo moja kwa moja, wakiwa bado ofisini, wanatakiwa wafukuzwe kazi na wajulikane kama maadui wa taifa.
Adui wa taifa/uma siyo serikali wala CCM, ni watumishi wanaonesha wazi wazi upendeleo wa kisiasa, na hii ni kwa sababu tu ya ujinga na upuuzi wa mtu mmoja mmoja na siyo taasisi yote (ofisi ya msajili, tume ya uchaguzi, majeshi yote, wataalam mbalimbali kuanzia wizarani hadi serikali za mitaa n,k).
Kimsingi watumishi hawa wakiwa na akili nzuri, na uzalendo kwa taifa, ni muhimu wajue kuwa ajira zao hawakugombea kupitia siasa na hivyo hawatakiwi kupendelea kwa kuwa wanasiasa wanapita kwa miaka mitano au kufa wakati ajira zao zitaendelea kuwepo.
Utanzania kwanza, vyama baadaye.
Kuna haja sasa ya watanzania wenye akili na uzalendo kuungana kupinga upumbavu wa kutokufuata katiba kabla hata ya kuwepo kwa katiba mpya.
 
ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,480
2,000
Akizungumza na Waandishi wa Habari wa ndani na nje ya nchi kwenye ofisi za Chadema Kinondoni, nje ya Jiji la Dar es Salaam, Katibu Mkuu huyo wa Chadema amesema yapo maandalizi ya kuifuta Chadema ili kuwaridhisha watu fulani ndani ya serikali.

Kinachosubiriwa ni timing tu, kwa maana ya wakati muafaka wa kufanya hivyo ili kupata kisingizio.

Hivyo Mh Mnyika amewaasa viongozi na wanachama wa Chadema kuwa waangalifu katika kipindi hiki ili kukwepa mtego uliowekwa na ofisi ya Msajili ikishirikiana na idara zingine.

Mungu ibariki Chadema
Hiki Chama kila siku ni kulalamika tuuu, kimeshajifia chama chenyewe nani akifute tena Mara ya pili
 
ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,480
2,000
Wameshajua kwamba kuchomoka hapa tulipo kwenye huu mkwamo wa kisiasa bila katiba mpya ni ngumu sasa kwa akili yao wanadhani njia rahisi ni kuifuta Chadema na hapo ndio wanajichimbia kaburi kabisa

Ingekuwa rahisi hivyo Mwendazake na ubabe wake wote alishindwa nini?Huyu mama asipotumia akili zake mwenyewe hafiki mbali,Na kama ni akili zake basi ajiandae sababu anaenda kushindwa vibaya.
Mnapenda kudanganyana nyie bavicha kaburi gani? Mbowe yuko mahabusi mmefanya nini zaidi ya kulalamika kama mke mdogo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom