Mnyika kufunga kampeni Vijibweni/Kigamboni kwa kishindo, CCM waikimbia kata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika kufunga kampeni Vijibweni/Kigamboni kwa kishindo, CCM waikimbia kata

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Mar 30, 2012.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Nawasalimu nyote.

  Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Kanda maalum ya Dar es salaam, kinapenda kuwajulisha yale yote yaliyojiri kwenye kampeni cha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya VIJIBWENI iliyomo jimbo la KIGAMBONI ndani ya wilaya ya Temeke.

  Zikiwa zimesalia siku mbili za mikutano ya hadhara ya kampeni tunapenda kuwapongeza wakazi wa kata ya vijibweni kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa kipindi chote tulichokuwa tunafanya kampeni, wakazi hawa wametupokea vizuri sana na kuonyesha ushirikiano wakutosha na wameonyesha nia kubwa sana ya kuichagua CHADEMA Kupitia kwa Diwani wake Bwana Isaya Mwita.

  Vile vile tunapenda kuwaomba ushirikiano wao wauendeleze katika kipindi hiki kifupi kilichosalia cha uchaguzi siku ya Tarehe 01/04/2012, Kwani tumekuwa tukifanya nao kampeni katika mazingira magumu sana ya manyanyaso na vitisho kutoka chama Tawala CCM pamoja na vyombo vya usalama vya taifa hili. Moja yavitisho hivyo ni kauli za mara kwa mara zinazotolewa kwenye mikutano ya hadhara ya chama hicho Tawala ya kuwa, Hata kama Chadema ikishinda CCM itatangazwa washindi then CHADEMA waende mahakamani kudai haki yao. Kutokana na kauli hizo za kufilisika kisiasa, CHADEMA cha makini chenye mgombea makini na hitaji la wakazi wa vijibweni, tunapenda kuwaondoa hofu wale wote wenye nia ya mabadiliko kutokatishwa tamaa na kauli hizo za kijinga. Vile vile Tunawahakikishia ulinzi wa kura zao watakazo piga kuwa zitalindwa kwa hali na mali bila kujali vitisho vya chama hicho.

  Kampeni zetu za uchaguzi zitafungwa na Mwenyekiti wa kanda hii ya Dar es salaam ambaye ni Mbunge wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania na muwakilishi wa wakazi wa ubungo Mh. John Mnyika Tarehe 31/03/2012. Vile vile mnyika ameshindwa kwenda Arumeru kutokana na Kesi ya uchaguzi Inayomkabili, Nguvu zote amezielekeza kwasasa kwenye uchaguzi huu mdogo wa udiwani kutokana na ukaribu wa eneo. Tunawaomba wakazi wote wa vijibweni na wale wote wanaopenda mabadiliko kujiunga na sisi siku ya kesho kwenye kufunga kampeni zetu, ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa kuliko chama kingine kinachoshiriki uchaguzi huwo bila kujali itikadi za vyama vyao, waje wasikilize sera na siyo matusi na kejeli, kitu ambacho wamekwisha kionyesha na kuvidharau vyama hivyo.

  Vile vile tunapenda kuwaambia wananchi kuwa kwasasa taifa linamsiba mkubwa linahitaji mabadiliko kwa haraka sana na harakati hizo za mabadiliko ni lazima zianze sasa. Katika uchaguzi huu wa udiwani CHADEMA tutashinda kwa zaidi ya 82%. Tunawatakia uchaguzi mwema wenzetu wa Arumeru na kwenye kata mbalimbali zinazorudia uchaguzi mdogo.

  AHSANTENI KWA USHIRIKIANO NA ENDELEENI KUSIMAMIA UKWELI BILA KUJALI ITIKADI ZA DINI ZENU, KABILA ZENU, HAKIKA UKWELI UTASHINDI DHULUMA, UKWELI UTASHINDA UONGO, UKWELI HAUJAWAHI KUSHINDWA.

  Imetolewa leo Tarehe 30/03/2012 na..

  HENRY J KILEWO
  KATIBU WA KANDA MAALUM YA DSM
  MRATIBU MKUU WA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI (VIJIBWENI) KIGAMBONI/DSM.
  SIMU: 0714 225960
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,848
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  Watu Wanatakiwa Wajue Ukweli Sasa!! Watu waelimishwe, Kwani hali ni Mbaya hadi Kiongozi aliyepewa dhamana anapewa Hela za Kujengea Machinjio anaamua kukimbia Nayo Hakuna wa Kumuuliza!! Anauza Shirika la Umma Hela anaweka Mfukoni kwake, Hakuna wa kumuuliza!! Duh Inasikitisha ila watu wanatakiwa wayajue Haya yote!! Wachukue Uamuzi sahihi!!
   
 4. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pa1 sana wakuu
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tutakuwepo ndio nyumbani huku
   
 6. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Tumekusoma mkuu, Napia tunapata yanayojiri huko na nimekubali kutokuwepo kwako Arumeru kulikuwa na maana, endeleza harakati kijana tulikujenga sasa fanya harakati, mpe mnyika pole zake mwambie tupo pamoja. Hakika Chadema sasa imekuwa..... pepozzzzzzzzzzzzzzzzzz
   
 7. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bravo cdm, kesho huku mza tuna kaz hyohyo pale kirumba, ya kumuondoa mkolon mweusi, zitto ndye atakayefunga kampen hzo.
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  Ccm wameingiwa kiwewew....nguvu kubwa sana inatumika kupora ushindi.....
   
 9. M

  Malova JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Vemaaa kabisa
   
 10. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante sana kwa taarifa
   
 11. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu
  mhe,JOHN SHIBUDA YUPO KWENYE KAMPENI WILAYA IPI?
   
 12. Ishina

  Ishina Senior Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtakaokuwepo eneo la tukio hapo kigamboni, pamoja na sehemu zingine kwenye chaguzi (Arumeru, Kiwira, Mwanza, etc), mjitahidi kurekodi (audio or video), hata kwa kutumia simu, yanayoendelea na kuweza ku-post hapa, angalau na sisi tusikie kinachoongelewa.

  Peeeeeoooopleeeeeees!!!!
   
 13. H

  Hard Rock Member

  #13
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 5
  Hongera sana. Lazima kieleweke mwaka huu!! vijibweni msikubali kuendelea kudhulumiwa na kurudishwa nyuma kimaendeleo. Tunahitaji kiongozi mwenye mtizamo mpya na uchungu wa nchi yetu, hatutaki mambo ya business as usual. Halla!!!!!!!
   
 14. w

  woyowoyo Senior Member

  #14
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kesho simba wa nyika seif sharif Hamadi atafunga kampeni kwa upande wa CUF vijibweni.
   
 15. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  sefu sharafu hamadi ndio nani, au ni rais wa kisiwani anzuani.
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana kamanda kwa kazi kubwa na nzuri uliyoifanya katika kata ya vijibweni kwa hizi wiki tatu.

  Kesho tuko pamoja katika kuhitimisha kampeni, na jumapili tarehe 01/04/2012 tutakuwa pamoja katika kuhakikisha kura zetu haziibiwi ama kuchakachuliwa!!

  Peoples power! Hakuna kulala hadi kitaeleweka!!
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pamoja na ukweli kwamba aliyekuwa diwani kata ya vijibweni kabla ya uchaguzi huu alikuwa mwanacuf, ambaye ametangulia mbele za haki, ukweli ni kwamba katika uchaguzi huu mdogo cuf imepotezwa vibaya, hamsikiki wala kuonekana. Tangu kampeni zimeanza hadi leo sijawahi kumuona ama kumsikia kiongozi yeyote wa kitaifa wa cuf kwenda vijibweni kufanya kampeni, sasa sijui sultani seif sharif hamad atabadili nini kesho, kama si kujitia aibu!?
   
 18. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  safi sana ipo siku tutachukua nchi nmima cha msingi tuendelee kutumia damu changa kama hizi za kina mnyika na vicenti nyerere
   
 19. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  kamanda usihofu kila kitu mtaki[atakwa wakati, tulikuwa kimya kwa sana, kwakuwa tulikuwa tunajipanga sasa tumekwisha maliza kazi , kilichobaki ni kutangazwa washindi.
   
 20. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kila kitu cheye mwanzo hakikosi mwisho, CCM ilipotoka ni mbali inapoelekea ni karibu, sioni sababu za kushindwa na ccm kwenye uchaguzi huu wa udiwani, wala sijawahi kufikiria kuwa ccm na mbinu zao za miaka hamsini wataweza kusimama na kushinda. Tumejipanga tunajiamini na tunaweza.
   
Loading...