Mnyika:Kuchukua form kutawajumuisha hata wale ambao hawakutia nia

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Mchakato wa kuchukua fomu utawajumuisha hata wale ambao hawakutia nia. Kila mwanachama anaruhusiwa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani- Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa Mnyika.

1593868565038.png
 
Kwa mtazamo wangu,kauli hii inaashiria jambo fulani kutimia, ila tunawasihi sana wajifunze kwa yaliyotokea na zaidi maamuzi yawahusishe wote kuepuka mgawanyiko.
Mbowe akishaamua jambo hamna wa kumzuia CDM. Kifupi Mbowe ndio kila kitu, mnaweza piga propaganda zote mzijuazo, ila Mwamba kawashika kweli kweli
 
Naona watu wanamtaja Lissu tu kuwa ndio pendekezo lao,sasa sijui Mbowe wanaona hafai maana sioni kutajwa kama Lissu.
 
Kwa mtazamo wangu,kauli hii licha ya kuwa ni ya kidemokrasia,lakini pia inaashiria jambo fulani kutimia, ila tunawasihi sana wajifunze kwa yaliyotokea na zaidi maamuzi yawahusishe wote kuepuka mgawanyiko.
Hiyo haina shida mkuu..wapo ambao walikuwa wanasikilizia upepo na wao sasa acha wajumuike wasije kusema walizuiwa...lkn taadhari ni muhimu pia
 
Mbowe akishaamua jambo hamna wa kumzuia CDM. Kifupi Mbowe ndio kila kitu, mnaweza piga propaganda zote mzijuazo, ila Mwamba kawashika kweli kweli
Vipi nayule anaetumia bunduki ili ichapishwe fomu moja tu
 
Zitto huchangia sana hawa jamaa kubadili gia angani na kukurupuka mazima!😁.

Ni heri Lisu abaki zake ughaibuni tu ausome mchezo la sivyo atajileta Segerea bure huku wenyewe tayari wana jina mfukoni.
 
Hii issue mbona kama inaenda kinyume na utaratibu uliozoeleka, sawa ni demokrasia lakini demokrasia inapendeza zaidi kama utaratibu uliozoeleka unafuatwa, hii issue inaweza sababisha maswali yasiyokuwa na maana.

Nahisi kuna jambo hapa wanaenda kulitengeneza ambalo kiukweli litasababisha mvurugano, na binafsi sikutegemea kama Chadema wanaweza kujaribu kulifanya tena, anyway... yangu macho.
 
Hii issue mbona kama inaenda kinyume na utaratibu uliozoeleka
Hapana mkuu, Kuna maeneo wagombea wenye sifa hawajajitokeza ndo maana wametoa huo mwanya na si vinginevyo...sidhani Kama wamefanya hvyo kwa wahamiaji...wahamiaji safar hii hawana nafas
 
Back
Top Bottom