Mnyika, ili kumaliza tatizo la uchafu tandale-sinza jaribu hili nalo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika, ili kumaliza tatizo la uchafu tandale-sinza jaribu hili nalo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, May 7, 2011.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Hi Members, Nawasalimu, heshima mbele.

  Mbunge wangu wa Ubungo ambae nilikupigia kura tangu 2005 naomba sana uchukue wazo hili na pengine kuliboresha ndio maana sikukutumia kama PM ili na wengine waweze kuweka mazwazo yao hapa japo si lazima.

  Nafikiri hivi, kwa sasa Sinza yote na dar kwa ujumla kuna vijana wengi sana wa kike na kiume ambao hawana kazi maalumu za kufanya zaidi ya kuwa ombaomba na kuwa vibaka na machanggudoa, lakini pia naamini miongoni mwa hao wapo pia ambao wako tayari kufanya kazi ili kujipatia kipato kwa ajili ya mahitaji muhimu ya binadamukama chakula.

  Tandale nayo ni kubwa na chafu sana ila pia ukubwa huu umechangiwa na uwepo wa familia nyingi ambazo makazi yake hayana mpangilio mzuri. Kila mara maji machafu yaliyobeba taka za aina mbalimbali yamekuwa yakikera wakazi wake na pamoja na kwamba kuna kampuni za Usafi bado ni kama ndoto tu.

  Baada ya utangulizi huo naomba sasa fanya haya yafuatayo.

  Kama kuna uwezekano, hakikisha kila jumba(Familia) katika eneo la Tandale wanalipa kiasi kipatacho elfu tano kwa mwezi, chaweza kuwa kiasi kikubwa lakini pia ni muhimu watoe kwa ajili ya afya zao kisha fanya mobilization ya vijana wote ambao wako tayari kufanya kazi ya kuokota na kuzibua mitaro ya maji machafu iliyoziba hapo Tandale kisha kila kijana kufuatana na kutegemeana na pesa iliyokusanywa walipwe.

  Kama kuna familia elfu moja mara 5000 unapata kiasi cha 5,000,000 au tufanye unapata kiasi cha milioni hata tatu tu bado ni kiasi tosha cha kuwalipa vijana hawa ambao una uwezo wa kuwapangia maeneo ya kufanya usafi kwa mita kadhaa kwa siku kwa bei ya elfu saba hadi nane.

  Na kama ofisi na serikali ikichangia pia kutoa vifaa vya usafi na usafiri wa kuzolea takataka hizi, je huoni tatizo litakuwa limepungua? Twaweza kuweka mawazo yetu pia kwa ajili ya kuboresha, mawazo hayo yawezasaidia hata nje ya Sinza pengine na Mbagala na kwingine.


  Faida zake ni nyingi ssana kama hili litatekelezwa bila kuweka siasa; moja, kuunda ajira kwa vijana wasio na elimu ya kuajiriwa kwenye mashirika na makampuni, pili, kupunguza tatizo la watoto wa mitaani na ombaomba, tatu, kuwa na jamii ya watu waliostaarabika kutokana na kidogo kilichopo, nne, kuwa na jamii yenye kujali usafi na mwisho matatizo ya ukosefu wa maadili na unyang'anyi yatapungua. Mawazo zaidi
  Nawakilisha
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Umeona mbali sana mkuu ...yaani unaua ndege3 kwa jiwe moja, 1)kukomesha uchafu 2)kutengeneza ajira na3)kupunguza vibaka,wala unga na machangu,Mh. Mnyika angalio hlo wazo
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Ndio Mpwa, kuliko kusema tutawaita wawekezaji waje wawekeze hapa kwetu ili tupate ajira au kule kusema eti ajira zimeongezeka kwa sababu ya Barmaids wamekuwa wengi na mahousigeli na mahausiboy wao. Ikifaa itakuwa nzuri nadhani, nasubiri maboresho, ila wasije wakaanza kuaandikia proposal za kuanzishia NGO za mfukoni..... sijui Youth Cleaness Center-Tandale (YCC-T) haya wapenda NGO, ka-NGO ndio hako, title ndo hiyo na vyanzo vya mshiko vipo kibao.....
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Hili nalo neno, hawachelewi kuovateki afu wakaingia mitini.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
 6. duda

  duda Senior Member

  #6
  May 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekukubali!!!!!
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kunikubali ila sasa hio Avatar yako tu......
   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hebu andika proposal mkuu kama hii ipeleke kwa mama tibaijuka pia naona inalipa una mawazo mazuri,yafaa kila mji wafanye hivo
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Do you think itakuwa bomba?? AAhh, nilishaandika miradi kibao nikaishia kuyeyushwa na baada ya muda nikaiona iko hewani na wajanja wachache.... Hyou Mama Tibaijuka jinsi ya kumpata sasa hadi uongee nae...
   
Loading...