Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika huwezi vita binafsi na Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zomba, Jun 20, 2012.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mbunge kijana ambae anaonesha kuwa umaarufu na madaraka ya ubunge yamemlevya amefikia hatua ya kumuingia Kikwete binafsi kwa kumwita, kwa kejeli na dharau eti ni "dhaifu".

  Kwa muono wangu, Mnyika amepotoka na amekosa heshima na adabu kwa sio tu mtu aliyemzidi umri, bali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Watanzania wote ambao tumeridhika kwa kumchagua Kikwete kwa kumpigia kura atuongoze.

  Mnyika baada ya kushindwa kuwasilisha hoja kuhusu bajeti akaamuwa kwa makusudi kabisa, kutoa lugha inayokera, si tu kwa Rais, bali kwa bunge pia, kuwa wote ni "wazembe" na CCM yote ni "upuuzi".

  Kweli kabisa, mimi ni mwana CCM na umenitukana, kwa hilo, umetangaza vita binafsi na mimi na wana CCM wote, hali kadhalika na Wabunge wote kwa kuwaita "wazembe". Jee, kijana hicho kiburi cha kututukana wote pamoja na Rais wetu mpendwa kwa ajili ya huo Ubunge? au kuna kinachokufanya ujione kuwa uko juu ya sheria, kwa kuwa upo hapo na watunga sheria wengine?

  Nakuhakikishia, vita uliyoitangaza itakugharimu kupita uwezo wa kufikiri, na majuto ni mjukuu.

  Kikwete humuwezi.
   
 2. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,926
  Trophy Points: 280
  Kama kikwete sio dhaifu, basi aonyeshe strength zake katika utendaji wa kazi ili watz wamuone hivyo, la sivyo, hakuna asiyejua kuwa tunaye rais dhaifu.
   
 3. S

  STIDE JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huna hata aibu ya kujitangaza kwamba ulimchagua Rais legelege na dhaifu!!!?

  Shame on you!!!
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Mnyika amesema ukweli ambao wanaccm wote mmeshindwa kuusema kwa kipindi kirefu sana, mara zote mnazunguka tu kuwa Rais anapotoshwa na watendaji. Je nani huwaweka watendaji hao? Udhaifu huo umejitikeza hata ndahi ya CCM kwa kushindwa kutekeleza dhana ya :Kujivua Gamba" aliyoiasisi mwenyewe. Huu kama sio udhaifu ni nini?

  mwacheni kijan wetu kasema ukweli. hii nchi sio ya wanaccm tu, ni nchi yetu sote. Hivyo tusitishane.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Childish.
  Silly Season.
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hebu soma sahihi yangu.......
   
 7. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kikwete ni dhaifu...
  Na wana CCM wote ni wazembe tu
  halafu zomba unasema Kikwete ni raisi wa Jamhuri ye muungano wa Tz, wakati Zanzibar hawataki? Ungesikiliza baraza la Wawakilishi ungeelewa hali halisi yaani mpaka wawakilishi wa CCM wanaubeza muungano na kuusifia huo Uamsho... Mpakaa nchi inafikia hapa ilipo Kikwete ni dhaifu na hajui hafanyalo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kweli ccm bado wajinga,kiongozi wa nyumba siku zote anatakiwa kuwa strong kama baba ni legelege hata na familia ni legelege,mf. Mtoto akiwa na utapiamlo sababu babaye hamletei chakula je hawa watoto pamoja na mzazi wao ukiwaita wajinga,legelege itakuwa mbaya?
   
 9. B

  Bob G JF Bronze Member

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ukiwa mjinga unawaza ujinga unaota ujinga na unasema ujinga, Pole Zomba. JJ Mnyika anawapigania watanzania mafukara waliokata tamaa na waliochoshwa na utawala dhaifu wa ccm na serikali yake, hayuko peke yake nyuma yake kuna umma wa watanzania, usihangaike nae wala hutaweza
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Siyo Mnyika tuu anasema ni Dhaifu hata mimi ambaye siyo mbunge nasema ni Dhaifu
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe anza kwa kuonesha ni lipi la maendeleo alilofanya Rais yeyote wa kabla yake, ambalo yeye hajafanya zaidi.

  Mnaleta matusi na ktukana lakini hoja za wazi kabisa zinawashinda. Mnyika kashindwa hoja ya bajeti akaamuwa awatukane wabunge wote, wana CCM wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Namwambia hvi; Kikwete asimjaribu, hamuwezi hata kidogo.
   
 12. k

  kamajana Member

  #12
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  jamaa unaonyesha ulivyolewa uccm, kwani hata wanayosema hauyaoni. kajifunze kiongozi shupavu anakuwa na sifa zipi then ndo uje kusema oooh rais katukwanwa. usipomwambia mtu ukweli na ukarudi kusema pambeni ni sawa na kuwa mshenzi. mnyika did his part so ccm muonyeshe sasa wapi mnyika hakusema ukweli. mbona mliambiwa mfanye maamuzi magumu mkashindwa.
   
 13. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zomba huwezi vita binafsi na Mnyika. Unakumbuka shuka kumeshapambazuka. Wenzako tumetangaza vita dhidi ya viongozi dhaifu siku nyingi sana. Mtu mzima hovyo hafai kuheshimiwa hata kama ni raisi wa dunia. Na kwa taarifa yako hamna sheria inayonikataza kumwita Kikwete dhaifu na ndiyo maana Mnyika hakufuta kauli na leo ametinga mjengoni. Kaa ukijua mwaka 2015 tukishachukua nchi tutawashitaki viongozi wote dhaifu kwa kulisababishia taifa hili hasara kutokana na udhaifu wao. Endeleeni na udhaifu wenu sie tunachuma fimbo za kuwachapa sawasawa.

  Mnyika humwezi.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unasema tu ni "dhaifu" lakini unashndwa kuonesha maendeleo yaliofanywa na Rais yeyote wa kabla yake ambayo Kikwete hajafanya zaidi.

  Mnaposhindwa hoja mnaanza viroja, si humu JF tu, hata bungeni.
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mickey Mouse at work

  Kikwete ni goi goi na dhaifu, does not have a spine at all.
   
 16. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Nadhani imefika wakati sasa Rais inabidi aoneshe udikteta kama wa Mkapa , enzi zile midono ya watu kama hawa ilifyata kama mikia ! Rais tunaomba uwashikishe adabu watu kama hawa ambao hawana nidhamu kabisa, hata iweje huwezi kuwa na kiburi na dharau kiasi hicho kwa kiongozi wako wa nchi! Rais tunaomba huyu aadabishwe ! na iwe fundisho kwa wengine !
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Kiukweli kwa kipaji hiki, Mnyika hamuwezi JK kabisaaaaa


  [​IMG]
   
 18. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280

  Unanchekesha - by FaizaFoxy
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Infalation iko zaidi ya 30% kubwa kuliko kipindi chote cha historia la taifa hili

  wewe ni dhaifu pia hata wa akili
   
 20. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hivi bado tunasera ya kuwa mkubwa hakosei? Sasa nani wakumrekebisha mkubwa huyu akikosea? Kama hata Mbunge aruhusiwi sasa sijui nani atamkosoa raisi. Hivi ni kweli Rais si dhaifu?
   
Loading...