Mnyika, fuatilia mmiliki na mkataba wa CO2 plant wilaya ya Rungwe - Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika, fuatilia mmiliki na mkataba wa CO2 plant wilaya ya Rungwe - Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapya, Oct 22, 2012.

 1. k

  kapya Senior Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Mnyika,

  Mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe kata ya Kabula kijiji cha Mpata na nyingine imegunduliwa maeneo ya Isebe kilomita chache kabla hujafika Katumba kuna ujenzi wa visima unaendelea mpaka sasa.

  Uvunaji hii ya gesi ya Carbon-dioxide ambao umekuwepo kwa miaka mingi chini ya kampuni nisiyoijua mmiliki kamili ni nani.

  Mheshimiwa, magari ya kubeba gesi nimekuwa nikiyaona kwa miaka mingi lakini sioni wanachotunufaisha. Tunakuomba ufuatilie na utuambie wamiliki hasa wa visima hivi vya kuchimba gesi ya Co2 ni akina nani ndani ya wilaya ya Rungwe.

  Lakini pamoja na hayo uwepo wa shughuli hii umeonekana kutokuwa na tija yoyote kwa wakazi wa wilaya na maeneo ya vijiji jirani vya mpata, kitema, kanyelele n.k. nimetembelea na kutaka kujua ni akina nani wanao miliki mradi huu lakini nimekosa ushirikiano.

  Tunaamini kuwa kutokana na umakini wako katika kufuatilia miradi ya madini na gesi tutapewa majibu ya maswali yafuatayo:
  1. Mmiliki wa mradi huo ni nani?
  2. Mkataba wake unanufaisha wananchi wa wilaya ya rungwe na maeneo jirani?
  3. Tuambiwe aliyesainisha mkataba ni nani?
  4. Ni athari gani za kiafya na mazingira ambazo wananchi wanazipata kutokana na mradi huo?
  5. Tangu umeanza mpaka sasa ni kiasi gani umeweza kusaidia shuguli za maendeleo?
  6. Je, kuna viongozi wowote waliojihusisha na utapeli katika mradi huo?
  7. Mkataba uliopo ni wa mda gani?
  8. Tuambiwe kwanini mradi huo umeshindwa kunufaisha wananchi?

  "Tunakuamini na ndo maana tumekuchagua katika hili, tufahamishe ili tujue na tuchukue hatua"
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Suguuuuuuuu.
   
 3. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Mbombo Ngafu! Mwanafyale mali zenu na mlivyokuwa watata atakuwa mwanenu tu anapiga hela tu huyo, mjanga haiwezekani jiulizeni vizuri ni nani kama sio Mwakabumbe basi Mwakyembe. Mnyika mwacheni ashughulikie majukumu mengine ya kitaifa mtampa kimeo wakati nyie ni nouma, miaka yote mpo mnakodoa mpaka mtu atoke Dar kuja kufanya upembuzi yakinifu sasa.

  Kunamaswali mengine majibu unaweza pata mwenyewe huko huko na utume ripoti ndio watu waifanyie kazi
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hivyo visima vya gesi kama ni hivyo vya Kyejo vinamilikiwa na kampuni ya TOL[ Tanzania oxygen Limited!! ] Kampuni hii inamilikiwa na wanahisa wengi yakiwemo Mashirika ya umma na watu binafsi walionunua hisa za kampuni. Kampuni kila mwaka hulipa mrahaba kwa halmashauri ya Rungwe. Waulizeni madiwani wenu hela wanazolipwa wanazitumiaje?
   
Loading...