Mnyika fanya kazi yako, la sivyo 2015 utashindwa ubunge

'Mtapoteza' jimbo.. Mwenzetu wewe ni Kama nani Na unaongea Na nani.. Kuna Blogs, tovuti Na majamvi ya kichama zaidi , mengi tu labda zungukia huko umwage ukereketwa wako ila usifunue gauni lako kwenye jamvi hili lisilofungamana Na upande mmoja wa kisiasa..
 
NYIE ENDELEENI KUBISHA NA KUMPA KICHWA ILA KWA UKWELI NI VIGUMU SANA JJ KUSHINDA 2015 KWA HALI HII NI LAZIMA ABADILIKE AFANYE KAZI ZA WANANCHI WA UBUNGO NA ASIPOTEZE MUDA MWINGI KWENYE TV NA BLOGS

NA MASWALA YA KUJENGA CHAMA NI YA SLAA YEYE SIO MBUNGE HANA KAZI ZAIDI YA KUJENGA FAMILIA YAKE NA CHAMA

JJ ANGALIA 2015 TUNAWEZA KUKUSAHAU NA HAWA WANAONIPINGA HUMU NI WANA CCM NAWAJUA HAWATAKI KUSEMA UKWELI ILI JJ ASHINDWE

acheni hizo tumshauri mbunge wetu kwa kusema UKWELI

Hebu soma JOHN MNYIKA
 
jj nakuamini na naamini uwezo wako,lakini ndugu yangu umejisahau sana na sasa unafikiri umechaguliwa na chama badala ya wananchi sikiliza
-wakati wana ubunge wakilia hakuna maji wewe uko tanga unatetea zao la mkonge
-wakati wana ubungo wakilia barabara mbovu wewe uko ujerumani unajenga chama
-wakati ubungo hakuna zahanati za kutosha wewe uko uzini unaahidi zahanati
-wakati ubungo foleni ni kuu wewe uko kigamboni unagombana na wakuu wa ilala kuhusu nauli za vivuko
na mengine mengi

braza watch out 2015 is very close u may loose,na itakuwa aibu kubwa kwako na kwa chama chetu

acha hizo sioni kwamba kuna tatizo hapo.hawa wote anaowadumia ni watanzania na watanzania hatubaguani kwa majimbo.ujerumani anakwenda kujifunza jinsi wenzetu wanavyoendesha vyama vyao kisayansi na pia urafiki wa kichana kwa pointi zako hazina mantiki zaidi ya ushabiki tu.
 
tukuulize JK ametekeleza ahadi ngapi kati ya hizo alizoahidi?
nkuulize wabunge wa CCM walioshika jimbo la Ubungo walifanya maendeleo yapi?
nkuulize ahadi zote za CCM ukiondoa vibajaji vya wagonjwa ni ahadi ipi umeona imetimia???
ni wabunge wangapi wanaotoa fidback kwa wapiga kura wao na kuwa nao karibu kufuatilia bila kuchoka maendeleo yao kama Mnyika?
walimu na wanafunzi wa UDSM na wanaubungo waliona mbali kuiondoa CCM jimboni mwao
 
NYIE ENDELEENI KUBISHA NA KUMPA KICHWA ILA KWA UKWELI NI VIGUMU SANA JJ KUSHINDA 2015 KWA HALI HII NI LAZIMA ABADILIKE AFANYE KAZI ZA WANANCHI WA UBUNGO NA ASIPOTEZE MUDA MWINGI KWENYE TV NA BLOGS

NA MASWALA YA KUJENGA CHAMA NI YA SLAA YEYE SIO MBUNGE HANA KAZI ZAIDI YA KUJENGA FAMILIA YAKE NA CHAMA

JJ ANGALIA 2015 TUNAWEZA KUKUSAHAU NA HAWA WANAONIPINGA HUMU NI WANA CCM NAWAJUA HAWATAKI KUSEMA UKWELI ILI JJ ASHINDWE

acheni hizo tumshauri mbunge wetu kwa kusema UKWELI
MAGAMBA!!!! Wakati wewe na chama chako mnawaza uchaguzi tuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!! Wanaume kazini. Kazi zinafanywa, matunda yanaonekana. Wewe pika majungu na chama chenye wenyewe cha John Komba.
 
[h=3]Hatimaye Ujenzi wa Choo cha Kituo cha Mabasi Mbezi Luis Waanza[/h]

Jana tarehe 27 Februari 2012 nimefuatilia tena kwa mamlaka husika na kujulishwa kwamba tayari ujenzi wa choo na uzio umeshaanza na kwamba sasa unafanywa na fedha za umma toka TANROADS badala ya Manispaa ya Kinondoni.

Mtakumbuka kuwa mwezi Januari 2012 nilifuatilia kwa nyakati na namna mbalimbali kutaka ujenzi wa choo katika Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis uharakishwe. Nimefanya hivyo pamoja na kutambua kwamba kituo husika kimejengwa katika eneo la hifadhi ya barabara (nitachukua hatua zingine kuhusu hili), kinaweza kutumika kwa miaka kadhaa kupunguza msongamano wa magari.

Kwa kuwa kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali nilizihoji mamlaka husika ambazo ni TANROADS na Manispaa ya Kinondoni ambazo zilikuwa zirushiana mpira kuhusu ujenzi wa choo. Hatimaye nilijulishwa kupitia bodi ya barabara na RCC kuhusu choo kitajengwa na Manispaa ambayo haikuwa imetenga bajeti husika.

Nilikwenda katika kituo husika cha Mbezi kabla ya kwenda bungeni Januari na kutoa kauli ya kutaka ndani mwezi mmoja ujenzi uwe umeanza na iwapo usingeanza nilieleza kusudio la kuunganisha nguvu ya umma baada ya kutoka bungeni mwezi Februari ili kituo hicho kianze kutumika kupunguza msongamano hata kama choo kitakuwa hakijakamilika.

Nawashukuru wananchi mlioonyesha mwamko wa kufuatilia suala hili kwa karibu na wadau wote ndani na nje ya mamlaka husika mliochukua hatua; Maslahi ya Umma Kwanza.
 
[h=3]Ratiba ya mbunge na DAWASCO kwenye kata leo, hatua zaidi zitafuata[/h]

Leo Machi Mosi nitakuwa pamoja na DAWASCO katika kata mbalimbali za jimbo la Ubungo kuchukua hatua za kuboresha upatikanaji wa maji kupitia ziara ya kikazi: Sinza (Saa 3-4 As), Mabibo/Makurumla (4-5), Makuburi (5-6), Saranga (6-7 mch), Msigani (7-8), Kwembe (8-9 jn).

Izingatiwe matatizo ya maji katika maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam ikiwemo katika Jimbo la Ubungo yamedumu kwa muda mrefu, tumepewa kazi ya kuwawakilisha kuisimamia serikali na mamlaka zake kupunguza kero husika katika kipindi cha muda mfupi; tunao wajibu wa pamoja wa kuziba pengo la miaka 50 katika kipindi cha chini ya miaka 5. Katika kipindi cha mwaka mmoja toka tupewe dhamana na dhima yapo maeneo ambayo tumewezesha yameanza kupewa mgawo wa maji, tuendelee kuunganisha nguvu ya umma zaidi katika mwaka huu wa pili wa 2012 yaongeze maeneo mengi zaidi.

Baada ya ziara hii tutawapa mrejesho kuhusu ratiba ya mgawo wa maji na hatua ambazo DAWASCO itapaswa kuendelea kuchukua. Nitawaeleza pia hatua za ziada ambazo tunapaswa kuchukua za kupanda ngazi kwenye mamlaka zingine hususan DAWASA, EWURA, Wizara ya Maji, Ofisi ya Rais na wadau wengine.

Tuendelee kushirikiana kila mmoja akichukua hatua kwa njia yake, maoni na ushauri pia unakaribishwa, wenye kutaka kuunganisha nguvu ya umma kupitia maandamano ya kuja kwa mbunge nao nawakaribisha; izingatiwe kuwa, maandamano yatayoratibiwa na ofisi ya mbunge kuwalenga wahusika wa juu zaidi yenyewe bado siku yake, tutafikia hatua hiyo iwapo serikali haitashughulikia kwa haraka masuala ambayo yanaweza kufanyika mwezi huu na kuonyesha kwa vitendo dhamira ya kutenga rasilimali za kutosha kwa mipango mingine inayoendelea kutekelezwa. Ni wakati wa mabadiliko ya kweli; tuwajibike. Maslahi ya Umma Kwanza, Twende Kazi
 
[h=3]Hatua nilizochukua kuhusu barabara ya Kibangu-Makoka na fidia ya Riverside[/h]

Nilichukua hatua kuhusu barabara Kibangu-Makoka na Januari nilikwenda Makuburi kuchangia matengenezo ya barabara husika , leo nimemweleza diwani kazi iharakishwe na kuhusu fidia ya wananchi wa Riverside Manispaa imenihakikishia kuwa italipwa mwezi Machi 2012; kesho nitakuwepo tena Makuburi kwa ajili ya kufuatilia masuala ya maji.

Kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali. Kama sehemu ya wajibu huo nilitumiwa SMS na baadhi ya wananchi wa Kibangu na Makoka katika kata ya Makuburi kuhusu ubovu wa barabara ulioongezeka mara baada ya mafuriko ya mkoa wa Dar es salaam. Pamoja na kuwa barabara hii ni ya ngazi ya mitaa kwa maana ya halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, nilichukua hatua ya kuunganisha nguvu pamoja na diwani na wananchi kwa ujumla.

Izingatiwe kwamba kuhusu barabara hii nilitimiza wajibu wa uwakilishi baada ya kukutana na wananchi wa eneo husika mwaka 2010 na kunitaka niipe kipaumbele katika bajeti, kwa kushirikiana na diwani tulifanya hivyo na hatimaye barabara hii imetengewa fedha takribani milioni 100 kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo na Manispaa ya Kinondoni katika mwaka huu wa fedha 2011/2012.

Hata hivyo, baada ya kupokea malalamiko ya siku za karibuni nilifika tena tarehe 7 Januari 2012 na kufanya mkutano na wananchi katika shule ya msingi Mabibo/Makuburi kwa ajili ya kuanza harambee ya kuunganisha nguvu ya wananchi kufanya ukarabati wa dharura wakati ambapo matengenezo makubwa ya Manispaa yakisubiriwa.

Katika mkutano huo paliundwa kamati ya wananchi wenyewe na sisi wengine tulichangia fedha na kamati ikapaswa kuwaona wadau wengine zaidi ili kazi iweze kufanyika kwa haraka. Kamati ilikuwa ni ya wananchi wenyewe lakini tulikubaliana kwamba iangaliwe kwa karibu na Diwani na Mwenyekiti wa Mtaa husika ili kuhakikisha kwamba fedha zinatumika vizuri na kazi inafanyika kwa ufanisi.

Hata hivyo, kamati haikuweza kuanza kazi kwa wakati kwa kuwa walipaswa kupata utambulisho toka kwenye mamlaka husika lakini kukawa na vikwazo kwenye ngazi ya serikali za mitaa.

Kwa maelezo niliyopewa na diwani ni kwamba pamekuwa na mvutano baina yake na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibangu kwa kuwa mwenyekiti husika amekuwa akinufaika na ukusanyaji wa fedha za "KITENGO", ambazo ana hofu kwamba mchakato huu wa kuwashirikisha wananchi unaweza kutishia maslahi hayo. Diwani amenieleza kuwa kufuatia hali hiyo mwenyekiti huyo amekuwa akitumia baadhi ya vijana kupinga harakati hizo za maendeleo suala ambalo lilimlazimu diwani kuitisha wenyeviti wa mitaa yote ya kata bila kujali vyama kwenye kikao cha kamati ya maendeleo ya kata (WDC) kufanya maamuzi ya pamoja.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa Februari wamekaa kikao husika, wenyeviti wengine wamehudhuria na kubariki kazi hiyo iendelee isipokuwa mwenyekiti wa Kibangu ambaye alitoka kwenye kikao kwa kususia.

Wenyeviti wengine na diwani wamekubaliana kuendelea na utekelezaji wa kazi hiyo ya matengenezo ya barabara, kazi ilichelewa kidogo kuanza baada ya mabadiliko ya mtendaji kata kufanyika kwenye kata ya Makuburi.

Leo tarehe 29 Februari 2012 nimemweleza diwani aendelee kusimamia kwa karibu suala hili ambalo liko kwenye ngazi yake ili ukarabati wa barabara ufanyike kwa haraka, na amenijulisha kwamba tayari walishaanza na maeneo korofi zaidi ili kupunguza adha ya usafiri.

Nimemwambia Diwani aongeze nguvu zaidi ili pamoja na michango ya wananchi kufanya ukarabati katika kipindi hiki cha mpito mpaka pale Manispaa ya Kinondoni itakapokuwa na fedha na kukamilisha mchakato wa zabuni wa matengenezo yaliyotengewa fedha.

Kwa upande mwingine, kumekuwepo na tatizo la miaka mingi la njia ya kwenda Makoka kwenye eneo la Riverside kumegwa na Mto Kibangu kwa kiwango cha barabara kutopitika na hivyo wananchi wenye magari kuzunguka umbali mrefu. Mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo nilifanya uchambuzi wa Hansards za miaka ya nyuma na kuiandikia serikali itekeleze wajibu wa kuwalipa fidia wananchi husika ili njia mbadala kuweza upatikana, suala hili nimelifuatilia kwa karibu kwa nyakati mbalimbali kwa mamlaka zote zinazohusika.

Tarehe 26 Januari 2012 nilifanya mazungumzo ya kikazi na wawakilishi wananchi toka Makuburi pamoja na Meya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na hatimaye nikafanikisha wananchi hao kukutana na watendaji wa Manispaa na fedha zao za fidia kutengwa.

Hata hivyo, kabla ya kukabidhiwa fedha hizo baadhi yao wamekataa kiwango ambacho walikuwa wamekubaliana awali kwa maelezo kwamba thamani za nyumba zao zimepanda baada ya serikali kuchelewa kuwalipa kwa miaka mingi, hawajaridhika na kiwango cha riba kilichowapa nyongeza kwa miaka husika kwa kutozingatia bei ya soko.

Nimeendelea kufuatilia suala husika kupitia mikutano ya baraza la madiwani tarehe 25 Februari na 28 Februari 2012 na Manispaa imeahidi kufanya majadiliano nao tena kuweza kutoa nyongeza inayowezekana ili malipo yafanyike mwezi Machi. Nimemwelekeza diwani afuatilie kwa karibu utekelezaji na iwapo akikwama anijulishe ili niweze kuchukua hatua za kuingilia kati.

Natoa mwito kwa wakazi wa Makuburi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa diwani katika kuhakikisha kwamba masuala husika yanafanyika kwa wakati, na iwapo hatua za kibunge zinahitajika msisite kunijulisha. Maslahi ya Umma Kwanza.
 
Kwa utendaji wake,hakuna wa kumtisha Mnyika mwaka 2015.
Nategemea wana -CCM, ambao bado wana uwezo wa kutafakari masuala kwa undani,na wenye nia ya kweli kuwa wabunge 2015, hawawezi kwenda Ubungo.
 
Kuna sehemu moja unguja inaitwa Malindi, Simba kanywa Chai, anaonekana mkaliiiiii. alipofika unguja na ukali wake woooote usio na maana wanaume wakamywesha Chai. Sasa jitu kama wewe wastahili kabisaaaaaaa......yakheeeeeeee
 
Amaridong, wasikushambulie. Uko sahihi kabisa.

Sisi wapigakura wa Ubungo tunataka kuona maendeleo ya Jimbo letu na huduma za kijamii zinapatikana. Kuangalia TV na kusikiliza ziara za Mbunge wetu ambazo hazina maslahi kwetu moja kwa moja haitusaidii. Tulimchagua atuhudumie sisi na taifa kwa ujumla. Kinachotuumiza hapa ametusahau wa nyumbani kwake. Kwa hali hii, akae tayari, 2015 tutamnyima kura kisha tuone kama ataonekana kwenye TV!

Mnyika lazima ajue kuwa anaupinzani mkubwa kwa sababu Chama Chake siyo kinachotawala, hivyo awe makini kuwahudumia waliomchagua hata ikimbidi kuhusika mwenyewe moja kwa moja.

TAKE CARE MNYIKA!
 
[h=3]Hatimaye Ujenzi wa Choo cha Kituo cha Mabasi Mbezi Luis Waanza[/h]

Jana tarehe 27 Februari 2012 nimefuatilia tena kwa mamlaka husika na kujulishwa kwamba tayari ujenzi wa choo na uzio umeshaanza na kwamba sasa unafanywa na fedha za umma toka TANROADS badala ya Manispaa ya Kinondoni.

Mtakumbuka kuwa mwezi Januari 2012 nilifuatilia kwa nyakati na namna mbalimbali kutaka ujenzi wa choo katika Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis uharakishwe. Nimefanya hivyo pamoja na kutambua kwamba kituo husika kimejengwa katika eneo la hifadhi ya barabara (nitachukua hatua zingine kuhusu hili), kinaweza kutumika kwa miaka kadhaa kupunguza msongamano wa magari.

Kwa kuwa kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali nilizihoji mamlaka husika ambazo ni TANROADS na Manispaa ya Kinondoni ambazo zilikuwa zirushiana mpira kuhusu ujenzi wa choo. Hatimaye nilijulishwa kupitia bodi ya barabara na RCC kuhusu choo kitajengwa na Manispaa ambayo haikuwa imetenga bajeti husika.

Nilikwenda katika kituo husika cha Mbezi kabla ya kwenda bungeni Januari na kutoa kauli ya kutaka ndani mwezi mmoja ujenzi uwe umeanza na iwapo usingeanza nilieleza kusudio la kuunganisha nguvu ya umma baada ya kutoka bungeni mwezi Februari ili kituo hicho kianze kutumika kupunguza msongamano hata kama choo kitakuwa hakijakamilika.

Nawashukuru wananchi mlioonyesha mwamko wa kufuatilia suala hili kwa karibu na wadau wote ndani na nje ya mamlaka husika mliochukua hatua; Maslahi ya Umma Kwanza.

Safi sana
 
Nadhani mtoa hoja hajui kazi za mbunge. Nakushauri usiwe kama Pinda anayedhani kazi za mbunge ni kuwagawia wapiga kura wake pesa.

Sasa nataka kukufahamisha kuwa moja ya kazi kubwa ya mbunge ni kuisimamia serikali na kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili maendeleo zinatumika kama zilivyokusudiwa na kuidhinishwa na bunge (Value for money). Aidha mbunge anawajibika kuwahamasisha wananchi wate katika kujiletea maendeleo.

Kazi zote ulizoziorodhesha hapo ni kazi za serikali! Serikali ikikataa kutenga fedha kwa shughuli hizo za kipaumbele kwa wananchi, mbunge hana namna anavyoweza kufanya kwa kuwa hana fedha. Hivyo hatua ambayo mbunge anaweza kuichukua ni kuishtaki serikali kwa wananchi ili wakati wa uchaguzi ukifika wananchi waweze kuiadhibu serikali iliyoko kwa kuiondoa madarakani!
 
Amaridong, wasikushambulie. Uko sahihi kabisa.

Sisi wapigakura wa Ubungo tunataka kuona maendeleo ya Jimbo letu na huduma za kijamii zinapatikana. Kuangalia TV na kusikiliza ziara za Mbunge wetu ambazo hazina maslahi kwetu moja kwa moja haitusaidii. Tulimchagua atuhudumie sisi na taifa kwa ujumla. Kinachotuumiza hapa ametusahau wa nyumbani kwake. Kwa hali hii, akae tayari, 2015 tutamnyima kura kisha tuone kama ataonekana kwenye TV!

Mnyika lazima ajue kuwa anaupinzani mkubwa kwa sababu Chama Chake siyo kinachotawala, hivyo awe makini kuwahudumia waliomchagua hata ikimbidi kuhusika mwenyewe moja kwa moja.

TAKE CARE MNYIKA!

Ukimnyima kura unampa nani badala yake? Je huyu utakayempa una hakika gani hatafanya kama anavyofanya Mnyika? Hebu niambie katika wabunge hawa waliomtangulia walifanya nini zaidi ya anayofanya Mnyika pamoja na kuwemo ndani ya cabinet?

  1. Bwana Venance Ngulla(alikuwa Naibu Waziri wa Fedha!!!!)
  2. Mzee Charles Keenja(naye alikuwa Waziri wa Chakula na bingwa wa ile tume ya Jiji)

Ubunge sio ana ana ana do bana
 
Amaridong, wasikushambulie. Uko sahihi kabisa.

Sisi wapigakura wa Ubungo tunataka kuona maendeleo ya Jimbo letu na huduma za kijamii zinapatikana. Kuangalia TV na kusikiliza ziara za Mbunge wetu ambazo hazina maslahi kwetu moja kwa moja haitusaidii. Tulimchagua atuhudumie sisi na taifa kwa ujumla. Kinachotuumiza hapa ametusahau wa nyumbani kwake. Kwa hali hii, akae tayari, 2015 tutamnyima kura kisha tuone kama ataonekana kwenye TV!

Mnyika lazima ajue kuwa anaupinzani mkubwa kwa sababu Chama Chake siyo kinachotawala, hivyo awe makini kuwahudumia waliomchagua hata ikimbidi kuhusika mwenyewe moja kwa moja.

TAKE CARE MNYIKA!

Hivi kwanza mnajua majukumu ya mbunge au mnakurupuka tu?tusije kua tunatoa somo kwa watu ambao hata wanachokijengea hoja hawakijui either kwa kutoelewa sawa sawa au kwa kukosa elimu stahiki
 
Huyo dogo Mnyika kushinda 2015 itakuwa ngumu aisee, sisi tuliompa kura kwa matumaini tunaanza ku doubt uwezo wake. Maana pale kwangu walikuja na diwani wakapiga kampeni kali wakatuambia na viwanja vya wazi ambavyo CCM wamejimilisha kimojawapo kikiwa ni hapo ambapo wao walikuwa wanafanyia mkutano wa wazi atahakikisha vinarudi kwa wananchi wote, sasa naona kimya.
 
Back
Top Bottom