Mnyika fanya kazi yako, la sivyo 2015 utashindwa ubunge

Kazi Ya Mbunge ni Kusimamia Utendaji!! Ila Tulikopeleka Kodi Zetu Ndio Hawataki Kuzirudisha ili Mbunge Aweze Kuzisimamia!! Najua ni Wachache Watanielewa!!
 
Una hakika km anafanya hicho kilichowekwa redish hapo kwenye sentenso yako?
 
Najua wenye ugonjwa wa vyama mtanuna.
Nikiwa mwana Ubungo nakuagiza mh mbunge wangu uanze kutimiza ahadi ulizotupatia. Sioni au kufahamu hata effort. Mpaka sasa hujafanya chochote zaidi ya maneno,mikutano isiyo na matunda na kuwa blogger. Hatujakutuma hicho wala malumbano. Barabara hatuna,maji kulekule,ulinzi mh haya sioni kipya cha zaidi ya mbunge aliyepita.

Nakuagiza anza kazi ili nisijutie kura yangu, mambo ya kuuza sura hayaendani na wewe. Nilikupigia kampeni ya hali na mali sitaki kujutia efforts zangu. Bado miaka 2 sababu after 2014 utakuwa busy kujipanga kurudi mjengoni. Nataka niwe na sababu tena ya kukukampenia vinginevyo umpishe NAPE mi sing'ang'anii Chama.

Wananchi tuache unafiki na siasa Tuwasukume wabunge watufanyie kazi sio kutafuta umaarufu ambao hautsaidii. tutake vitu tangible. Nchi hii ni yetu wote.

Poa. Sasa tunapokuwa na vikao vya maendeleo uwe unakuja basi. Au unataka mbunge aje kutufyekea majani viambazani mwetu?

La pili sidhani kama unakaa ubungo, unaonekana umetumwa tu. Na nikuhakikishie, bora tusiwe na Mbunge kuliko kuwa na Nape. Tunaweza kufumba macho na kujitwika lile zigo la CUF (Mtatiro) kuliko kurudisha siasa jimboni mwetu.

Halafu usikose akili kiasi ukapuuza mchango wa mbunge wetu anaoutoa nationwide. Vile vikao unavyoita havina maana ni kwa ajili ya Watanzania wote na haya unayotaka Mnyika aje kukufanyia hapo uwani kwenu ni ubinafsi.
 
Msimjibie kwa ushabiki naomba mnipe kipi cha maendeleo alichofanya so far. Mimi sio CCM kama mnavyodhani penye ukweli tuseme Mnyika fanya kazi. BADO

Jambo lolote linalofanywa kwa Tanzania linaihusu ubungo pia. Huyo Nape aliyekutuma amekosea kukutuma wewe kwani hata namna unayopresent mada ni kichekesho. Kusema Mnyika hajafanya kitu hiyo ni tamaduni ya ukuwadi wa CCM. Leo hii hata ukimuuliza Job Ndugai kati ya Wabunge waliobeba majukumu makubwa bungeni atakutajia Mnyika japo kwa shingo upande. Kazi yake ni kutuwakilisha wa-Ubungo bungeni sio kuja kukukagueni kama mmepona malaria sugu daily
 
mimi nakaa,eneo la ubungo maziwa, cjaona mchango wa mbunge wangu katika eneo leo, wimbi la wahuni, mgogoro wetu na tanesco kuhusiana na kuhamishwa kwetu na malipo kwa ujumla. Hapo ubungo stand ndo kinyaa. MNYIKA RUDI JIMBONI.
 
Niliona kama una akili timamu kumbe umedandia gari kwa mbele utaumia mkuu.
 
Mnyika naomba ushuke humu jf unishawishi kwa ulichofanya hata kama ni mipango. Usikalie tu kucheza na jukwaa tunataka magoli.

Ulitaka afanye nini? Ajenge barabara ya lami toka Msewe mpaka Golani?

Nakushauri usome waraka wake ulioambatanishwa hapa.
 
Attachments

  • waraka wa mnyika.pdf
    205.8 KB · Views: 46
Unaposema hajafanya kitu kwa huo mwaka mmoja na kiduchu unakua unalinganisha na nini/nani???
Lamwai na Keenja walikaa hapo miaka mingapi na wakafanyaje mpaka uje useme mnyika hajafanya kitu??
Tatizo gani specific unaloliona halijatekelezwa kwa muda mliokubaliana mpaka unakuja kulalamika huku Jamvini???
Kama ulimpigia kampeni kwa kiwango ulichotaja (kama kweli) utakuja unamjua kiasi, umechukua hatua gani kumuona yeye binafsi kwanza kabla ya kuja kujianika hapa???
Hayo uliyosema hajafanya unayajua, je hakuna ambayo kayafanya na unayajua pia???
Kua na shukrani ndugu, kama unaona hafai next time gombea wewe basi!!
 
Well said.
 
Sina ugomvi na Mnyika namfahamu kuliko yeyote humu na nimemfundisha mwenyewe darasani kwa miaka 4 akiwa katika ule umri wa kuaminika wa binadamu. Nasema kama ilivyokuwa kwa Deodorous Kamala na wengine walimezwa sana na ishu za kitaifa na ushabiki wakasahau majimbo yao. Hiki ndicho nakiona kwa Mnyika. Nampigia simu mwanafunzi wangu kuchangia mipango hapokei wala sms hajibu. Naona kwenye blogu na twitter. Tuache chuki za kishabiki na kushabikia makaratasi.Nimefanya tathmini ya mwaka mmoja COMPARATIVELY hakuna kitu kulinganisha na expectations za wanaubungo. Maeneo mnayosema Msewe hakuna kitu tusidanganyane. NARUDIA MNYIKA RUDI JIMBONI TUKUONYESHE TUNAYOTAKA WANA UBUNGO. Nakaa ubungo nyuma ya NBC Karibuni.
 
Subiri kidogo atarudi, ametumwa na Josephine kununua nyanya! Akirudi ataanza kushughulikia shida zenu wana Ubungo!
 
kila kitu ni kidogokidogo, tumpe muda.

Ivi mtoa mada ulitaka kwa muda aliokaa awe ametekeleza ahadi zote// alizohaidi kwenye kampeni??

huyo Keenja alikaa miaka kibaoo alifanya nini??
 
ulitaka akukameruni ndo uone kakufanya kitu, na ampishe nape kwa kuwa nape anakukameruni na ndo furaha yako, acha izo wewe mtoto
 
wewe fisi tu nathani ndo maana ya jina lako.. unawafundisha watu nini?? au ilo jina ni vijimambo tu?? na mambo ya adolescence?? aya Mr Fisi tu (fisi2)

Back
Top Bottom