Mnyika: Diwani wa Sinza amefanya maajabu ni kama mbingu na ardhi ukilinganisha na aliyekuwepo

Ili kuweka taarifa kwa usahihi, maeneo ya Kwa Mtogole ni kata ya Tandale inayoongozwa na magamba na sio Sinza.

Hivi unalijua eneo la kwa Mtogole wewe linapoanzia na kuishia? Sinza uzuri mbona nayo ipo Kata ya Tandale?
 
hongera Rena. So far kazi nzuri. Jitahidi uwezavyo!
 
hivi barabara anajenga diwani au wananchi?

Huwa ina jengwa na mkandarasi kwa fedha za wananchi.. chini ya usimamizi wa viongozi dhabiti wanye nia ya kweli yakusukuma maendeleo mbele.
Bila kuwa na DIWANI mwenye nia njema na wananchi hata fedha zikikusanywa hasitafanya yale yaliyo kusudiwa hivyo DIWANI ananafasi kubwa kufanikisha ujenzi wa barabara za mitaa.
 
Halafu jamaa aache usanii maana anajifagilia mwenyewe maana ndo jina lake mr pamba ni mwanamuziki anayejiita mr simple sasa kwann usiweke mambo hadharani kuliko kupitia mlango wa nyuma kwa kofia ya mh mbunge?acha. Hizo bana mi nakaa sinza barabara bado mbaya sana fanya kazi acha kujipaka mafuta kwa mgongo wa chupa kazi itaonekana kwa matendo c maneno...
 
Ili kuweka taarifa kwa usahihi, maeneo ya Kwa Mtogole ni kata ya Tandale inayoongozwa na magamba na sio Sinza.

tandale ilikuwa chini ya magamba sasa ipo chini ya CUF pamoja na kata ya makumbusho hizi kata nikama dada na kaka kuna maeneo mengine tayari ya meshuhudia mabadiliko makubwa baada ya kuingia wenyeviti wa mitaa wa CUF na Madiwani Wa CUF. Waliozagaa tandale na makumbusho pia na mwananyamala hivyo tandale si ya magamba
 
tehetehe tunacho taka ni utendaji wawakilishi wetu ktk mabaraza ya manisipaa na kata na mitaa kwa ujumla uwajibikaji kwa wananchi
 
hivi barabara anajenga diwani au wananchi?

Ndivyo mlivyokuwa mnafanya ee,mnachukua hela za mradi mnakula halafu mnasema watajenga wananchi?MASABULI YAKO YANAVUJA usirudie tena kulopoka ujinga kama huo.
 
Watu hatupendi kufuatilia ama kujifunza, mi Dar nina miaka mitatu na makumbusho napoishi nina mwaka mmoja. Lakini leo niulize mpaka watandale na Sinza, nitakwambia mpaka wa makumbusho Tandale, tandale magomeni, magomeni hanasasifu, kinondoni msasani, tuje mipaka yamitaa kama kwa mtogole, tandale uzuri, sinza uzuri , sinzasana , sinza palestina, mitaa mingi wa dsm.

Tuje mipaka ya majimbo ya uchaguzi ya dsm, kawe Kindoni, kinondoni ubungo ninaweza nika kwambia kwa kipindi kifupi nilichokaa dsm na sii mfanyakazi wa idara yoyote ya serikali kuu na serikali ya mitaa. Leo mtu anashindwa kutofautisha sinza na tandale na hajui kama nikata au mtaa au tarafa. Ukimuuliza hakupi jibu kamili wa tz tuwe wafuatiliaji.

Hata hizi route za madaladala ndio mwalimu wakujua mji konda huita vituo, kuna vituo huwakilisha kata, magomeni, kinondoni, jangwani, kigogo, keko, tandale, sinza, makumbusho, mbagala, tandika , buguruni, gongo la mboto, vigunguti.

Vituo vyote hivi vinakusaidia kujua jiografia ya mkoa wa dsm na wilaya zake, ndo maana utawatambua madiwani vizuri leo ukiambiwa diwani wasinza kafanya maajabu usichanganye nakata nyingine kama kijitonyama au tandale. Basi hata diwani wa vigunguti mtasema diwani wa gongo la mboto.

Kuweni makini na jiografia. Hata hivyo mnaweza mkachanganya kati ya jimbo la Mnyika ubungo na Kawe kama mtakutana maeneo ya Mbezi mwisho /Goba na Tegeta
 
hivi barabara anajenga diwani au wananchi?

Mkuu, nimelipenda swali lako. Are you also a great thinker? Hivi kabla ya diwani huyo anayezungumziwa, Sinza haikukaliwa na watu? Mbona hawakuijenga kama wao ndio wajengaji wa barabara? Acha kuchangia ili mradi tu uonekane nawe umechangia hoja. Heri ya wale wenye kuchangia kwa kuandika " nilikuwa napita tu".
 
tatizo ni kuwa wakazi wengi wa hio kata ya sinza hawaingii humu jamii forum manaake hali ya hewa ingechafuka humu.Kitu cha msingi ni viongozi wa CDM wasilipuuzie kabisa hili swala hizi ni point zetu tatu za ugenini tayari tushazichukua hivyo tunajiandaa kwenda kuzichukua nyingine tatu za ugenini 2015..kwahio tusibweteke na kuvimba kichwa anything can happen kama tabia ya diwani wetu huyu itaendelea hivi.Thread hii itakuwa ushahidi tosha wala tusijekumtafuta mchawi...naishi sinza na naijua sinza na nakijua nnachokiongea na pia naipenda CDM na Tanganyika ila siipendi CCM sana na wote wanaoiongoza na kuishabikia kwavile wao ndio adui namba moja wa nchi yng tanganyika
 
hivi barabara anajenga diwani au wananchi?

diwani anafuatilia halmashauri, hela ni za watanzania wote maana wanakusanya kodi, kama hakuna mfuatiliaji wanajenga matumbo yao tuuu, angalia halmashauri ambazi zina wapinzani halmashuri zinafanya vizuri siku zote
 
kwanza mlevi sana kutwa kuimbwa kwenye miziki akudo...ananiudhi ka nini ntafanyaje na mimi ndo nina mahaba na chadema ntavumilia tu ..ndoa ndoano
 
Mtm, kama wanachi ndo wanajenga sasa walikuwa wapi?wananchi hawajengi barabara,wanalipa tax ili wajengewe mambo kama hayo ya msingi lakini anayeweza kufacilitate hayo ni kiongozi waliyemchangua kama ni active basi atafanya kama sio ndo kama yaliyotokea sinza siku za nyuma ukilinganisha na sasa!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi unaongelea Sinza gani? Ile sinza ya kuungana na kwa Mtogore? Mbona chafu tu mifereji ya maji machafu kila kona.
Naona unampenda sana huyo diwani wa Sinza kwa Mtogore mpikie pilao takuletea na kuku wa kienyeji sawa umkaribishe aje kula

mitaro ni ishu za mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
Sasa nenda kacheki mwenyekiti ni nani?
Then utapata jibu.
 
Back
Top Bottom