Mnyika: CHADEMA haitasusia uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, amuomba Rais Magufuli kupeleka muswada wa Tume huru ya uchaguzi kwa hati ya dharura!

Mnyika anaweza kuwa na msimamo huo yeye kama kiongozi wa chama, ila tatizo liko kwetu sisi wapiga kura, bila tume huru ya uchaguzi hatutashiriki huo uhuni uitwao uchaguzi. Tutahakikisha unakuwa uchaguzi wenye wapiga kura wachache kupata kutokea hapa nchini. Uzuri ni kuwa somo limeshaeleweka hivyo tunasubiri hatua ya utekelezaji tu. Hapo ndio vyama vyote vya siasa vitagundua nguvu ya umma ni nini. Na uzuri wa nguvu yetu ya umma kwa sasa itakuwa sio ya machafuko. Nina hakika tutakuwa na serikali iliyo madarakani kisheria, lakini isiyo na uhalali wa umma.
Heti wananchi tutahakikisha utakuwa uchaguzi wenye wapiga kura wachache? Hivi unadhani watanzania wote zaidi mil 55 watakuelewa hiki unachokisema hapa.??
Kwahiyo wasipo ipata hiyo tume huru wataenda kugombea? Kama watagombea kwanini wakati tume huru hakuna, kwanini wasisusie uchaguzi ili kuonyesha nia na msimamo wao Kama walivyofanya kwa serikali za mitaa.??
 
Back
Top Bottom