Mnyika athibitisha UDHAIFU wa JK bungeni Jioni hii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika athibitisha UDHAIFU wa JK bungeni Jioni hii.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donyongijape, Jul 2, 2012.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Akichangia Hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Raisi , Mh. Mnyika ameanza kwa kunakili Ibara ya 33-50 ya katiba ya nchi. amesema katiba hii inampa raisi madaraka makubwa; raisi halazimiki kufuata ushauri wote wote.. Amesema mwaka jana Ofisi ya Raisi ilileta Bajeti na wakachangia weeeeee, mambo mazuri kabisa lakini kwa masikitiko makubwa ni kwamba mengi ya msingi hayajatekelezwa. Na ndio maana wabunge wanalazimika kuzungumza kwa ukali. Amesema kuna idara nyeti za PCCB,Maadili, Mipango,Ajira, Utumishi,TISS etc ambazo zote zipo kumshauri raisi kiuchumi, kiusalama, kiajira etc etc . Amesema huenda Idara hizi zinatoa ushauri mzuri tu kwa raisi lakini kwa kuwa raisi anaweza kuukubali au kuukataa basi huenda raisi anapuuza huo ushauri. Hivyo mwisho akaiomba serikali katika majumuisho iseme ni namna gani huu UDHAIFU unashughulikiwa!
   
 2. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Anasema serikali ilete Taarifa/ Makubaliano ya Serikali na Madaktari Bungeni ili ijadiliwe.
   
 3. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Wakujadili nani, wabunge au serikali? Maana serikali na madaktari wameamua kupimana msuli...
   
 4. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnyika ananipa raha kweli, magamba walikuwa kinywa kumsikiliza, ukiwa unatetea magamba lazima uonekane mjinga, mmh kuna huyu wa cuf naye kafunguka!
   
 5. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mnyika amejenga hoja yake vizuri leo..alikuwa akiuchambua udhaifu wa JK vizuri kweli kweli. Kwangu mimi nimeng'amua kwamba..kama kuna wataalamu wa maana serikalini na wanatoa ushauri wa maana kisha JK anapuuza kama tunavyomsikia na kumjua kuwa ni mbishi au a.k.a big headed,Basi ni sahihi kabisa kwake yeye kumuita JK Dhaifu. Mtu ambaye haki nchini kwake kupata ushauri wa wataalam, mtu anayezurura misibani na harusini etc etc... Huyo lazima atakuwa DHAIFU. Heko John Mnyika
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. chelsea fc

  chelsea fc JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 835
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  heko kijana anatuwakilisha vyema bungeni tunataka vitu km hv kwa tunaowatuma bungeni,sio mbunge flani anaomba tufunge na kuomba kwa ajili ya serikali,eti serikali ina pepo tulikemee lol
   
 7. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Namkubari sana JJM...nimekubali kauli ya msigwa "Akili ndogo inatawala akili Kubwa"
  'Vox populi,Vox dei'
   
 8. m

  majebere JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Kelele tu bungeni, hana maana yeyote huyu kijana, mwache aropoke tena halafu aje kujitetea
   
 9. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa taarifa yako waote leo wameufyata mkia, tuliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Chezea Mnyika wewe??. atakung'ata oooooh.
   
 10. MDAU JR

  MDAU JR JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu hapo unaleta ushabiki wa vyama, kwenye ukweli unatakiwa kukiri tu. Huyu kijana point zake ni constructive siyo mtu wa kelele kama ulivyosema, hata spika na watu wa serikalini wanamkubali isipokuwa tu ni kwa kuwa hayuko kwenye chama tawala na bunge letu linaendeshwa ki-siasa zaidi, ni kama vile wakala wa serikali na chama tawala na si mhimili unaojitegemea kama ambavyo lilitakiwa kuwa.
   
 11. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
   
 12. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  big up JM
   
 13. h

  hans79 JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Ukweli utabaki kuwa hivyo hata Kama huutaki, ni kheri akuambiae kosa lako kuliko akusifiae.
   
 14. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,271
  Trophy Points: 280
  ukweli ukicmama uongo hujitenga wamezomea sasa wanaona haya.
   
 15. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu huwa uwezo wake anabeba wabunge 200 wa ugambani
   
 16. K

  KALEBE JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 772
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 80
  Angekuwa mbunge wa chadema angeambiwa tunaomba utuletee ushahidi lakini kwa sababu ni wa chadema hakuna tatizo na yuko halali kusema lolote hivi ujinga wa namna hii tutauvumilia hadi lini sasa siyo tu ushahidi huo uwasilishwe bungeni bali pia na sisi wanachi tunaomba ushahidi na kama atashindwa kuuwasilisha alitake radhi bunge kwa kukidhalilisha chama cha chadema vile vile awatake radhi watanzania wote:A S-baby:
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyo huyo si ndio alikuwa anadai katiba hii mbaya na anataka ibadilishwe mpaka akawa anasusa bungeni. vipi leo imekuwa nzuri?

  Nakwambieni huyu kijana anachanganyikiwa, kama mnabisha mtanambia, maana nimem-observe, mara anacheka cheka bila sababu, mara ananuna bila sababu, mara anakasirika bila sababu, mara anaongea vitu vya ajabu.

  Mtazameni sana jamani, asije akafanya vituko vikubwa kuliko hayo mjengoni, huu ni ushauri wa bure.
   
 18. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Madaktari wamerudi kazini kwanini hamsemi walichochewa na nani? Km ni Udhaifu wa JK basi wangesaini kuacha kazi km mdhaifu alivyowaambia
   
 19. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Madaktari wamerudi kazini kwanini hamsemi walichochewa na nani? Km ni Udhaifu wa JK basi wangesaini kuacha kazi km mdhaifu alivyowaambia
   
 20. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  zomba ume confuse anayechekacheka bila sababu ni baba yenu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...