Mnyika atakiwa kujieleza kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kisa kusema Rais Samia alisema uongo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,965
2,000
Msajili wa Vyama vya Siasa amemtaka Katibu Mkuu wa CHADEMA J J Mnyika kujieleza kufuatia kauli yake kuwa katika mahojiano ya BBC Rais Samia alisema uongo.

Msajili amesema lugha hiyo dhidi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kinyume kabisa cha maadili.

Mnyika ameandika katika ukurasa wake wa twitter.

Mungu ni mwema wakati wote!

Pia soma: John Mnyika: Rais Samia "aidha amepotoshwa au ameamua kusema uongo”
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,910
2,000
Bila katiba mpya nchi hii inayumba. Wazee wa CCM jitokezeni muokoe jahazi...nchi yetu inazama.... Jaji Warioba; mzee Butiku simameni muhesabiwe...

Haiwezekani nchi inapitia
haya na nyie mpo kimya tu. Uongozi wa nchi unayumba - wananchi wanawaamini sana maana ninyi mlifanya kazi sambamba na baba wa taifa hili.
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,481
2,000
Samia kama hataki katiba mpya sisi watanganyika tunataka Tanganyika yetu. Atabaki hana nchi anayoiongoza.
Watanganyika bila katiba mpya tuhimizane kujitoa kwenye muungano wa wana ccm.
Tunataka muungano wa wananchi.
Binafsi nawakilisha mamilioni ya watanganyika na watanzania kwa ujumla ambao hatutaki katiba mpya. Laiti watanganyika au watanzania kwa uwingi wetu tungetaka katiba mpya basi nchi hii leo isingetawalika. Lkn kwa vile wengi wetu hatuhitaji katiba mpya ndio maana nchi bado inatawalika, shughuli mitaani zinaendelea na hakuna dalili ya chochote kutokea. Japo. alietaka kulazimisha hiyo katiba akiendelea kunyea debe.
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
6,930
2,000
Haoni kuwa kwa kufanya hivyo anakizana na kauli ya Mheshimiwa Rais kuwa Tanzania kuna Demokrasia kamili? Kuna watu wa kupinga hoja za Mnyika, sio yeye. Au ndio mpango wake wa kukabidhi chama kwa wale aliowarudishia uanachama?

Amandla...
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
1,716
2,000
Kama tunavyosherekea wagunduzi wa vitu mbalimbali na kuwapa tuzo, mfano akina Einstein, Tesla basi hapa Tanzania mnamo mwaka 2015 mara baada ya mzee wa nywele nyeupe kuwa mgombea wa chama fulani ambacho kilimtaja kwenye list of shame, hivyo mashabiki wa chama hicho kulazimishwa kumsafisha na kumpigia kampeni ili awe rais na wao wakakubali kwa kufuta list of shame kwenye tovuti ya chama chao na mara moja wakaanza kuzunguka nchi nzima wakiimba kwa kuzungusha mikono kuwa kama mtu huyu angekuwa fisadi kweli basi angefungwa maana yake walikiri kuwa walimsingizia tu!.

Baada ya mkengeuko huo ndipo akajitokeza mgunduzi wa jina la nyumbu akiwafananisha na mnyama nyumbu ambaye hanaga akili ya kufikiri mara mbili pale wanapokatiza mto Mara, hata mto uwe umejaa mamba, nyumbu kiongozi akishajirusha humo basi wote wanaofuatia watajirusha humo na kuliwa.

Leo miaka 5 imepita lakini jina la nyumbu linaendelea kuwafaa wafuasi hawa. Wao kila kitu ni kupinga na kutetea kila aina ya ujinga ili mradi tu huo ujinga umeungwa mkono na kiongozi wao.
Basi napendekeza aliyebuni jina la nyumbu asakwe huko aliko na apewe tuzo.
 
kipenseli2021

Senior Member
Jul 17, 2021
134
225
Samia kama hataki katiba mpya sisi watanganyika tunataka Tanganyika yetu. Atabaki hana nchi anayoiongoza.
Watanganyika bila katiba mpya tuhimizane kujitoa kwenye muungano wa wana ccm.
Tunataka muungano wa wananchi wa Tanganyika na Zanzibar.
Ichukue
 
Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
8,301
2,000
Kama tunavyosherekea wagunduzi wa vitu mbalimbali na kuwapa tuzo, mfano akina Einstein, Tesla basi hapa Tanzania mnamo mwaka 2015 mara baada ya mzee wa nywele nyeupe kuwa mgombea wa chama fulani ambacho kilimtaja kwenye list of shame, hivyo mashabiki wa chama hicho kulazimishwa kumsafisha na kumpigia kampeni ili awe rais na wao wakakubali kwa kufuta list of shame kwenye tovuti ya chama chao na mara moja wakaanza kuzunguka nchi nzima wakiimba kwa kuzungusha mikono kuwa kama mtu huyu angekuwa fisadi kweli basi angefungwa maana yake walikiri kuwa walimsingizia tu!.

Baada ya mkengeuko huo ndipo akajitokeza mgunduzi wa jina la nyumbu akiwafananisha na mnyama nyumbu ambaye hanaga akili ya kufikiri mara mbili pale wanapokatiza mto Mara, hata mto uwe umejaa mamba, nyumbu kiongozi akishajirusha humo basi wote wanaofuatia watajirusha humo na kuliwa.

Leo miaka 5 imepita lakini jina la nyumbu linaendelea kuwafaa wafuasi hawa. Wao kila kitu ni kupinga na kutetea kila aina ya ujinga ili mradi tu huo ujinga umeungwa mkono na kiongozi wao.
Basi napendekeza aliyebuni jina la nyumbu asakwe huko aliko na apewe tuzo.
Mbona nje ya mada? Au ndiyo vile tena
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
3,452
2,000
Mzee maneno yamekuchoma eee...mnatesa sana wapinzani ninyi...mmempiga risasi Lissu na kumfanya aishi kwa shida hivi kisa siasa...acheni hizo hii nchi ni ya wote. Kiongozi bora ni yule anayesikiliza mawazo tofauti toka hata kwa wachache.

Katiba mpya is the key to sort out all these.
Tatizo hao wachache hawajatulia, kila siku kukurupuka na dramas, mara kuita press kumjibu Rais na kumwita Muongo, Ukiacha tu urais anaweza kuwa hata Mama yake mzazi. Huyo Lissu alijitakia, yule Magu alikuwa anaonesha kabisa kuna fuse zimekata kichwani halafu yeye anamuita dikteta uchwara, ulitegemea matokeo gani? Watu wa akili kama ya Magu ni wa kukaa nao mbali
 
ngosha wa mwanza

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
1,456
2,000
Binafsi nawakilisha mamilioni ya watanganyika na watanzania kwa ujumla ambao hatutaki katiba mpya. Laiti watanganyika au watanzania kwa uwingi wetu tungetaka katiba mpya basi nchi hii leo isingetawalika. Lkn kwa vile wengi wetu hatuhitaji katiba mpya ndio maana nchi bado inatawalika, shughuli mitaani zinaendelea na hakuna dalili ya chochote kutokea. Japo. alietaka kulazimisha hiyo katiba akiendelea kunyea debe.
Watanzani wapi sema unawakilisha familia yako.Katiba ni muhimu sana kwa taifa lolote maana ndo injini ya taifa km sio muhimu basi hata iliyopo ifutwe km huoni umuhimu
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,910
2,000
Tatizo hao wachache hawajatulia, kila siku kukurupuka na dramas, mara kuita press kumjibu Rais na kumwita Muongo, Ukiacha tu urais anaweza kuwa hata Mama yake mzazi. Huyo Lissu alijitakia, yule Magu alikuwa anaonesha kabisa kuna fuse zimekata kichwani halafu yeye anamuita dikteta uchwara, ulitegemea matokeo gani? Watu wa akili kama ya Magu ni wa kukaa nao mbali
Hivi wewe kwa akili zako unafikiri kuna Mtanzania anayewaamini kwamba Mbowe ni Gaidi....

Acheni mambo ya kutesa watanzania wenzenu bana kisa madaraka.
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
3,452
2,000
Hivi wewe kwa akili zako unafikiri kuna Mtanzania anayewaamini kwamba Mbowe ni Gaidi....

Acheni mambo ya kutesa watanzania wenzenu bana kisa madaraka.
Watanzania siyo mahakama, na uzuri mahakama zetu ni za wazi, ukweli wote utamwagwa mezani! Kama kasingiziwa or no itajulikana, haina haja ya kuwa na haraka ndugu
 
St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,596
2,000
Sasa msajili wa vyama vya siasa anahusikaje na Mnyika kusema kama Rais ni muongo? Kwanini msajili wa vyama vya siasa anatishia wapinzani tu? Makonda aliwahi kusema Mbowe anauza unga jee alimuuliza Makonda juu ya kauli yake na ushahidi mpaka leo haujatolewa. Jee kamuhoji Sirro juu ya kusema Mbowe gaidi? Hata kama anatetea Kula yake lakini asiji dhalilishe hivi.

Lunatic
 
juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,640
2,000
Tatizo hao wachache hawajatulia, kila siku kukurupuka na dramas, mara kuita press kumjibu Rais na kumwita Muongo, Ukiacha tu urais anaweza kuwa hata Mama yake mzazi. Huyo Lissu alijitakia, yule Magu alikuwa anaonesha kabisa kuna fuse zimekata kichwani halafu yeye anamuita dikteta uchwara, ulitegemea matokeo gani? Watu wa akili kama ya Magu ni wa kukaa nao mbali

umenichekesha sana
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,910
2,000
Watanzania siyo mahakama, na uzuri mahakama zetu ni za wazi, ukweli wote utamwagwa mezani! Kama kasingiziwa or no itajulikana, haina haja ya kuwa na haraka ndugu
Waambie CCM wenzako waanze kurusha kesi ya Mh. Mbowe Live!!

Wakikubali njoo kigamboni nikupe kiwanja 40 kwa 60 kipo barabarani baada ya daraja la Mwalimu nyerere BUREEE
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom