Mnyika atakaimu hadi lini?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
John Mnyika amekaimu kiti cha Naibu Katibu Mkuu kwa kipindi kirefu sasa, Je hajakomaa tu? tunasubiri nini, nafikiri huu ni muda mwafaka kwa chama kufanya maamuzi magumu ili apewe kiti kizima.
 
John Mnyika amekaimu kiti cha Naibu Katibu Mkuu kwa kipindi kirefu sasa, Je hajakomaa tu? tunasubiri nini, nafikiri huu ni muda mwafaka kwa chama kufanya maamuzi magumu ili apewe kiti kizima.
Quinine!
Hili tunaweza tukallita wazo la mwaka. Kwa kifupi inabidi lifanyike kabla hawajachelewa kwani sasa hivi watu kama kina Zitto sio wa kuamini tena!
 
Nadhani hapa tumechanganya mambo. Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ni Zitto Kabwe. Mnyika alikaimu cheo cha Katibu Mkuu wa CHADEMA na kuwa bosi wa Zitto katika kipindi chote cha kampeni ambapo Katibu Mkuu wa chama, DK. WILLIBROD SLAA, alikuwa akigombea Urais.

Navyoelewa mimi, Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje CHADEMA na pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama. Nimepata taarifa kuwa CHADEMA watakaa chini na kupanga upya safu yake ya uongozi kabla ya uchaguzi wa 2015. Hapa tunatarajia watu kama Mnyika, Tundu Lissu, na wengine kupewa nyadhifa za juu zaidi kwenye chama kutokana na uadilifu uliotukuka na mchango wao mkubwa.

Tuvute subira.
 
John Mnyika amekaimu kiti cha Naibu Katibu Mkuu kwa kipindi kirefu sasa, Je hajakomaa tu? tunasubiri nini, nafikiri huu ni muda mwafaka kwa chama kufanya maamuzi magumu ili apewe kiti kizima.

Mhe. Quinine,

Afisa anakaimu wakati afisa aliyeteuliwa rasmi kwa nafasi yake hawezi kuifanya hiyo kazi. Nahisi John Mnyika anakaimu Naibu Katibu Mkuu wakati wowote Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu, hayuko Dar es Salaam.

John Mnyika alikaimu nafasi ya Katibu Mkuu pia wakati Dk. Slaa alipokuwa akifanya kampeni kama mgombea u-Rais wa Chadema.

Kamati Kuu ya Chadema inajua majukumu yake na hakuna dhuluma yoyote dhidi ya Mhe. John Mnyika. Hakuna jambo la "kukomaa" katika "Acting Post". Arudipo kazini substantive ofisa, "acting ofisa" ana-revert to his normal post.
 
Back
Top Bottom