Mnyika ataka bima, hifadhi za jamii kwenye vikundi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika ataka bima, hifadhi za jamii kwenye vikundi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 13, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Mnyika ataka bima, hifadhi za jamii kwenye vikundi


  na Zainabu Mlimbila


  [​IMG] MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amehimiza kupanuliwa kwa wigo wa bima na hifadhi ya jamii kwa kuwawezesha wananchi kukabiliana na athari za umaskini wa kipato na kuongeza ustawi.
  Mnyika aliyasema hayo juzi alipowahutubia wanachama wa kikundi cha Kusaidiana Kilungule Darajani (KICHAKIDA), kilichopo Kata ya Kimara, Ubungo, ambapo alikizindua rasmi kikundi hicho na ofisi yao.
  Alisema mifumo ya bima na hifadhi ya jamii (social security) inahudumia zaidi watu walio kwenye sekta rasmi na kuacha sehemu kubwa ya wananchi waliopo katika sekta isiyo rasmi, hivyo kuna haja ya kufanyika kwa mabadiliko na mifumo hiyo kurekebishwa.
  “Bima na hifadhi ya jamii inahudumia zaidi watu walio kwenye sekta rasmi na kuacha sehemu kubwa ya wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi,” alisema Mnyika.
  Aidha, aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa kuanzisha kikundi hicho, kwani kinatoa baadhi ya huduma za msingi zinazopaswa kutolewa na mifumo rasmi ya bima au hifadhi ya jamii.
  Kadhalika, mbunge huyo aliwataka wananchi wa Ubungo kuendelea kuunga mkono hoja ya kuandikwa kwa Katiba mpya na marekebisho ya kisheria ili pamoja na mambo mengine kuwepo kwa mifumo thabiti zaidi ya bima na hifadhi za kijamii kama suluhisho la kudumu.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa KICHAKIDA, alimueleza mbunge huyo kwamba kikundi hicho kina wanachama 100 ambapo kinawahudumia wategemezi zaidi ya 500 wanaotoka kwenye kaya za wanachama hao katika matatizo ya kijamii kama maradhi, misiba na mikopo ya elimu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Bima hujikita zaidi kwa wale wenye uhakika na kipato.........................hawataki utata.........................wa sekta isiyo rasmi..............
   
 3. C

  Changamoto2015 JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2015
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Lakini inatakiwa itafutwe namna ya kuwaweka hata hawa walio nje ya sekta rasmi, na ambao ni wengi kitakwimu.
   
 4. H

  Haika JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2015
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Inawezekana kabisa.
  Ni mtu kuamua kulisimamia na na wateja wenyewe kuamua na kugundua kuwa ni jambo zuri
   
Loading...