Mnyika ataja orodha ya mafisadi na wahujumu wa TANESCO

Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
2,025
1,791
ORODHA YA UFISADI NA UZEMBE TANESCO AWAMU YA KWANZA NA MWITO WA KUTOA MAONI KUHUSU KUSUDIO LA KUPANDISHA BEI YA UMEME KWA MARA NYINGINE




Shirika la Umeme (TANESCO) linakabiliwa na ufisadi na uzembe unaoongeza gharama za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme kwa upande mmoja na uendeshaji wa shirika kwa upande mwingine. Ufisadi na uzembe huo unapunguza uwezo wa TANESCO kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na unaongeza gharama na bei ya upatikanaji wa umeme hali inayoathiri uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa kuchangia katika mfumuko wa bei na ongezeko la gharama za maisha. Mzigo wa ufisadi na uzembe katika TANESCO unajitokeza zaidi katika mikataba mibovu pamoja na ukiukwaji wa sheria za ununuzi wa umma, ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.


Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 63 sehemu ya pili ya bunge (inayoundwa na wabunge) ndio chombo kikuu chenye madaraka na mamlaka kwa niaba ya wananchi ya kuisimamia serikali. Hata hivyo, katika kipindi cha kati mwaka 2008 mpaka 2012 maazimio ya Bunge kuhusu sekta ya nishati ikiwemo kuhusu umeme yamekuwa hayatekelezwi kwa wakati na kwa ukamilifu hali inayofanya tuhuma za ufisadi na uzembe kuendelea kujirudiarudia. Katika muktadha huo, ni muhimu kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara ya 8 madaraka na mamlaka ni ya umma (serikali inafanya kazi kwa niaba tu) ipo haja ya kuanza kuunganisha ‘nguvu ya umma’ katika kushinikiza hatua kuchukuliwa kwa wahusika wa ufisadi na uzembe ili kuweka misingi bora ya uwajibikaji katika sekta ya nishati.


Ili umma uweze kuungana kuchukua hatua ni muhimu masuala yote ya ufisadi na uzembe yakaelezwa kwa uwazi kwa umma hivyo, katika mfululizo huu nitaweka hadharani orodha za watuhumiwa wa ufisadi na uzembe katika sekta ya nishati. Orodha hizi zinatolewa kwa awamu zikigusa kwa kuanzia mashirika na taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati na Madini na baadaye Wizara yenyewe na hatimaye Serikali kwa ujumla. Aidha, orodha hizi zitatolewa kwa awamu masuala kwa masuala na matukio kwa matukio, ngazi kwa ngazi.


Katika orodha ya awamu ya kwanza nitaanza na TANESCO kuhusu masuala na matukio yaliyohusu kampuni ya M/S SANTA CLARA SUPPLIES COMPANY LIMITED pamoja na kampuni ya M/S McDONALD LIVE LINE TECHNOLOGY LIMITED. Orodha nyingine zitafuata katika awamu ya baadaye iwapo vyombo na mamlaka husika hazitachukua hatua ikiwemo juu ya tuhuma za ufisadi na uzembe katika matumizi ya dola milioni 54 (zaidi ya bilioni 86) katika ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme ya IPTL.


Bonyeza hapa kusoma ORODHA YA KWANZA YA WATUHUMIWA WA UFISADI NA UZEMBE KATIKA SHIRIKA LA UMEME (TANESCO)


Nimetoa majina haya hadharani ili umma uunganishe nguvu kwa njia mbalimbali kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya ufisadi na uzembe ili kuhakikisha nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria na maadili katika utumishi wa umma.


Mamlaka zinazopaswa kuchukua hatua ni pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Sekretariati ya Maadili ya Umma zote kila moja kwa nafasi yake zichunguze ukiukwaji wa sheria katika masuala yaliyo kwenye majukumu yao na kuchukua hatua za ziada kwa kuzingatia pia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo nimeitumia kama rejea kwenye baadhi ya masuala katika orodha hii.


Aidha, kwa kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeitisha Mkutano wa Taftishi Juu ya Marekebisho ya Bei ya Umeme za TANESCO ambao inakusudiwa bei ya umeme kupandishwa tena, ni muhimu masuala ya ufisadi na uzembe ndani ya TANESCO yakajadiliwa kwa upana na umma, ili kupinga gharama zinazotokana na hali hiyo zisiingizwe katika mahesabu ya kukokotoa bei.


Ikumbukwe kwamba tarehe 9 Novemba 2011 EWURA ilipokea Ombi la Dharura toka TANESCO na kupandisha bei kwa wastani wa asilimia 155 kuanzia tarehe 1 Januari 2012 na niliunganisha umma kupinga na hatimaye EWURA ikapunguza asilimia hiyo na kuruhusu nyongeza ya wastani wa asilimia 40.29 ambayo ndiyo inayotumika hivi sasa.


Hivyo, nitumie nafasi hii kuhimiza pia umma kujitokeza tarehe 10 Disemba 2012 kuanzia saa 4 asubuhi katika Ukumbi wa Karimjee Dar es salaam kwenda kutoa maoni kwa kuzingatia Taarifa ya Gharama za Huduma ya Umeme (Cost of Service Study) na zaidi kwa kupinga kuingizwa kwenye bei ya umeme gharama za uzembe na ufisadi ili kupunguza athari katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi miaka 51 baada ya Uhuru.


Wenu katika uwakilishi wa wananchi,





John Mnyika
Mbunge wa Jimbo la Ubungo
09/12/2012

Source:mnyika.blogspot.com

 
Mh. Mnyika, napongeza sana jitihada zako za kuelimisha umma katika mambo ya msingi yanayogusa maisha ya watu, hasa wenye kipato cha chini.

Hii itakuwa ni fursa pekee kwa watanzania wazalendo kupinga hatua zinazotaka kuchukuliwa na wanyonyaji ambao wamekuwa wajitumia nguvu za umma kwa manufaa binafsi kwa kipindi kirefu sana sasa. Kwa hiyo napenda kuungana na ndg Mnyika katika swala hili na kwa pamoja tuendelee kupambana na hii nguvu ya wachache; kwa hakika tutashinda maana sisi wanyonge ni wengi na wenye nguvu kwa kuwa maamuzi ya mustakabali wa nchi yetu yamo mikononi mwetu.
 
Siku zote nimekuwa nikisema kwamba utendaji kazi wa Mbunge wa aina ya Mnyika ndiyo tunaouhitaji katika nchi maskini kama hii iliyozungukwa kila kona na ufisadi. Wananchi tunapaswa kumuunga mkono mbunge kijana kwa kupaza sauti ya kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya manyang'au hao aliowaorodhesha Mhe. Mnyika. CCM ndiyo iliyofuga hayo manyang'au na kusababisha wananchi wengi kuteseka.

Hongera sana Mhe. Mnyika na sisi wakesha hoi tunakuombea uzima na afya tele ili jitihada zako zitukuomboe kutoka kwenye makucha ya wakoloni weusi ambao ni chama cha magamba.
 
Hon John John MNYIKA,ITAKAPOFIKA SIKU YA WATU KUSIMAMA WAHESABIWE KWA KUIFANYIA NCHI KAZI JUU Ya wajibu wa kawaida jina lako Historia italihifadhi katika vito aina nya marijani au rubbies!Pamoja
 
Kuna jambo moja linashangaza sana kuhusu Tanzania. Kama tunasema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, na tunafuata sheria, basi nilitegemea mara tu taarifa za ukiukwaji wa sheria zinapotolewa, law-enforcement agents wangeingia kazini mara moja na kuchukua hatua stahiki. Na hapa naamanisha Jeshi la policy, DPP na office ya mwanasheria mkuu. Hizi office tatu zilitakiwa kuwa kazini sasa hivi.

Police wa Tanzania hawajishughulishi kabisa, hata pale wanapopewa taarifa. Tuliona kwenye issue ya Dr Mwakyembe - badala ya kuchunguza wanaonekana kutaka 'victim' ndiyo afanye kazi ya upelelezi!

Hii issue ya Mhando na TANESCO wanasubiri nini? Mwanasheria mkuu yuko busy kuangalia nywele za wabunge na kubishana nao wakati nchi inageuzwa genge la walanguzi? DPP naye anakazana kufunga tai huku police wakitembeza vitambi! You wonder kwa nini tunagharamia uwepo wa hizi office?


Yote tisa, kumi, kama law-enforcement agents wanaonekana kutofanya kazi kama inavyotarajiwa, ni kwanini kamati ya bunge inasimamia hivi vyombo haijawaita wakuu wa hizi office na kujua shida iko wapi?
 
Hon John John
MNYIKA,ITAKAPOFIKA SIKU YA WATU KUSIMAMA WAHESABIWE KWA KUIFANYIA NCHI
KAZI JUU Ya wajibu wa kawaida jina lako Historia italihifadhi katika
vito aina nya marijani au rubbies!Pamoja

ivi hawa watu si ndio waliosimamishwa na Serikali kwa uchunguzi. Mnyika anatumika na watu wa TISS kuiamplyfy. Hongera zake kwa kuaminiwa
 
Yani haya manyang'au ndiyo yanasababisha nilipe pesa nyingi kwenye umeme?

Naomba CHADEMA muhamasishe maandamano nifie barabarani. Niko tayari kuwategea polisi kifua waniue
 
Siku hiyo hataulizwa mtu kwa dhambi zake wala jini. Watajulikana waovu kwa alama zake; basi watakamatwa kwa nywele zautosi na kwa miguu. (Al-Rahman: 39,41).

'Sivyo hivyo! Kama haachi tutamkokota kwa nywele za utosi. Utosi mwongo, wenye madhambi. Basi na awaite wanachama wenzake (wawasaidie). Na sisi tutawaita Malaika wa Motoni. Sivyo! Usimtii, lakini Sujudu na kuwa karibu (na Mwenyezi Mungu). (Alaq: 15 - 18).

Napenda kuanza na maneno hayo kutoka kwenye Quraan kwa kuwa hawa mafisadi wamekuwa hawana uwoga wowote kwenye roho zao kwa kule kujitengenezea utawala wao wa kulindana kwa yale maovu wanayotufanyia lakini wafahamu wana muda mfupi sana wa kuishi hapa duniani na baada ya hapo watakutana na yeye aliye mkuu, mmiliki wa aridhi saba na mbingu saba na kila kilichopo kwenye ulimwengu huu.
 
Myika kama una ushahidi sheria si inakuruhusu kama mtu binafsi kupeleka kesi mahakamani? maana naona tu kila siku mnanukuu katiba ambayo kimsingi ulishasema mbovu! ingawa nafahamu ubovu wake ni pamoja na kuwapatia wabunge mianya ya kuliibia taifa letu.
 
siku zote nimekuwa nikisema kwamba utendaji kazi wa mbunge wa aina ya mnyika ndiyo tunaouhitaji katika nchi maskini kama hii iliyozungukwa kila kona na ufisadi. Wananchi tunapaswa kumuunga mkono mbunge kijana kwa kupaza sauti ya kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya manyang'au hao aliowaorodhesha mhe. Mnyika. Ccm ndiyo iliyofuga hayo manyang'au na kusababisha wananchi wengi kuteseka.

Hongera sana mhe. Mnyika na sisi wakesha hoi tunakuombea uzima na afya tele ili jitihada zako zitukuomboe kutoka kwenye makucha ya wakoloni weusi ambao ni chama cha magamba.

kipi kikufurahishacho!!! Kwa watu wasemaovyo? Kama hawa hata kwetu wapo ila tumewachoka
 
Myika kama una ushahidi sheria si inakuruhusu kama mtu binafsi kupeleka kesi mahakamani? maana naona tu kila siku mnanukuu katiba ambayo kimsingi ulishasema mbovu! ingawa nafahamu ubovu wake ni pamoja na kuwapatia wabunge mianya ya kuliibia taifa letu.

Sheria ZA tanzania haina kifungu hicho, katiba Iweke kifungu cha kuruhusu Public Interest litigation
 
Safi sana John Mnyika kwa taarifa hii! Lakini nchii hii ilivyo ya ajabu tutaona hakifanyiki chochote kuhusu walio tajwa na tutaambiwa tume itaundwa na hili jambo litaisha vivyo hivyo!

Nategemea tusihishie kutaja majina tu bali tuone hatua stahiki na za kisheria zinachukuliwa zidi ya hao mafisadi!.

Asante John Mnyika kwa kazi nzuri!
 
Last edited by a moderator:
kipi kikufurahishacho!!! Kwa watu wasemaovyo? Kama hawa hata kwetu wapo ila tumewachoka

Mkuu hebu nijuze unanufaika vipi gharama za umeme zinapopanda na mzigo wote kudondokea kwa consumers..? Hivi huna hata ndugu zako wanaotabika na umaskini ambao wanashindwa kupata huduma hiyo..? Wakati mwingine icikilize nafci yako uciendekeze tamaa ya mwili...
 
Kwenye thread kama hizi misukule wa CCM huwa hawaonekani kabisa, naona comments zote ni za wapinzani.NAPE endelea kukomaa na Slaa wanaCCM na CUF wapate la kusema humu jamvini
 
Mbunge wetu tuanashukuru kwa kutufungua macho!!!
Hizi ndiyo hoja zenye mashiko kwa hatma ya nchi.......sio kadi iliyo sandukuni!!
 
Ninayo mengi yakuzungumza juu ya Mnyika, lakini simahali pake!

Mnyika wewe ni alama ya siasa za kijana wa kiafrika na dunia ya leo, Hongera sana mkuu!
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Similar Discussions

Back
Top Bottom