Mnyika asema bomoabomoa iliyofanyika barabara ya Morogoro ni haramu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252

Dodoma. Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema bomoabomoa iliyofanyika katika barabara ya Morogoro ni haramu kwa sababu sheria ya barabara iliyotumika ilitungwa mwaka 1932 na ilishafutwa.

Akiuliza swali bungeni leo Jumatatu Mnyika amesema Rais John Magufuli akiwa katika ziara Mwanza alitoa kauli ya kibaguzi na kwamba kama si ya kibaguzi basi Serikali itoe kauli ya kuwalipa fidia wakazi hao waliobomolewa nyumba zao.

"Kwa sababu Serikali ilisingizia sheria mimi kama mbunge nilichukua hatua nilileta marekebisho bungeni ili barabara yote iwe mita 60 lakini Serikali ikafanya njama na Katibu wa Bunge aliyeondoka(Thomas Kashililah) kuzuia huo muswada ni lini hasa ikaachana na hizi njama ikakubaliana na Rais na muswada ukaletwa hapa bungeni ili barabara hii iwe na upana wa mita 60? Amehoji.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukizi na Mawasiliano, Elias Kuandikwa amesema sheria mbalimbali za barabara zilipokuwa zikitungwa zilikuwa zikizingatia maendeleo na kwamba Sheria ya Barabara ya Mwaka 1932 ilianisha ukubwa wa barabara katika maeneo yote inapojengwa.

Alimtaka mbunge huyo kuwasiliana na mamlaka za halmashauri za serikali za mitaa ambazo ndio wasimamizi kuona kama kuna mahitaji ya baadhi ya maeneo kufanyiwa marekebisho kwenye sheria hiyo.

"Hakuna njama yoyote na suala la fidia litakwenda kwa mujibu wa sheria," amesema.

Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema Kanuni za Bunge sehemu ya nne inaonyesha jinsi shughuli za Bunge zinavyopangwa na sehemu ya tano inaonyesha namna majadiliano yatakavyofanywa ndani ya Bunge.

"Si kweli kwamba Serikali ilipanga njama na Bunge kuzuia muswada wowote uliokuwa uletwe ndani ya Bunge, suala liloelezwa na Mnyika katika swali la nyongeza si kweli ni suala lililojitokeza katika muswada wake," amesema.

Mhagama amesema Serikali haina utaratibu wowote wa kula njama na Bunge.

Katika swali la msingi Mnyika alitaka kujua ni lini Serikali itawasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya barabara ili eneo la hifadhi ya barabara iwiane na barabara nyingine.

Akijibu swali hilo Kuandikwa amesema Serikali haina mpango wa kufanya marekebisho sheria ili kufanya barabara ya Morogoro kuwiana na barabara kuu nyingine kwa kuwa eneo la hifadhi la barabara hiyo lilotengwa linahitajika kwa ajili ya upanuzi wa barabara ili kuwiana na mahitaji ya sasa na ya miaka ijayo.

Chanzo: Mwananchi
 
Wabunge hawa wanakuwa wapi kipind cha mapumziko mana hajasikika akifanya kazi yoyote jimboni leo anaenda kupiga kelele bungeni. ...pia kuna mwenzio saidi kubenea huku jimboni kwake toka kapigiwa kura 2015 sijawah muona tena kwenye shughuli za maendeleo
.
.
Tuonane 2020
 
Yumani feisi vs Sheria za Nchi.

Narudia tena zoezi lile la bomoabomoa lilikuwa na hata sasa bado ni haramu, la kikatili na lilikiuka sheria za nchi kwa kiwango kikubwa.

Wengi wa wahanga wanastahili fidia bila usumbufu.

Halafu huwa najiuliza kama Sheria za Hifadhi ya Barabara ya mwaka 1932 au ile ya magazeti ya miaka 1950 ni nzuri kwetu mpaka sasa je kulikuwa na haja gani ya kudai uhuru? Je si afadhali wakoloni basi wangeendelea tu maana inaonekana walikuwa na maono na ni nia nzuri hadi kututungia sheria nzuri zenye kudumu kwa muda mrefu?
 
kwenye ahadi ya chama 2020 lazima ahadi moja wapo itakuwa kuwalipa fidia wote waliobomolewa na Maku.. na ahadi nyingine itakuwa kuwalipa wazee wa EAC
 
Ila Mnyika nae alikuwa wapi muda wote huo ndo leo atoe kilio cha waliobomolewa nyumba Morogoro Road? Kuna ugumu gani kuchukua laki mbili kutoka ktk mshahara wake, kuziweka ktk bahasha za kaki 10 na kuwaita waandishi wa habari kama 10 na kukemea kitendo cha serikali kubomoa nyumba wakat kuna zuio la mahakama kwa baadhi yao?

Au ndo anajiandaa kuwa Sales Officer pale Game Mlimani City kama Baba yake wa kisiasa Dr. Mihogo? Unawezaje kusaidia kujenga chama, halafu linatokea jambo usilolipenda ktk chama bas unasusa na kuhujumu chama? Ukimya wa Mnyika unahujumu chama, nilitegemea chadema wajipange kuwasemea wana kimara kupitia viongozi wa chama wilaya ya Ubungo na Kata za maeneo yaliyoathirika maana mbunge amekuwa bubu.
 
Wabunge hawa wanakuwa wapi kipind cha mapumziko mana hajasikika akifanya kazi yoyote jimboni leo anaenda kupiga kelele bungeni. ...pia kuna mwenzio saidi kubenea huku jimboni kwake toka kapigiwa kura 2015 sijawah muona tena kwenye shughuli za maendeleo
.
.
Tuonane 2020
Mbona sisi wa mjini tunawaona?? Hii bomoa bomoa mbona iliruka kwa mama Mkapa???
 
Wabunge hawa wanakuwa wapi kipind cha mapumziko mana hajasikika akifanya kazi yoyote jimboni leo anaenda kupiga kelele bungeni. ...pia kuna mwenzio saidi kubenea huku jimboni kwake toka kapigiwa kura 2015 sijawah muona tena kwenye shughuli za maendeleo
.
.
Tuonane 2020
Utamuona wapi na wewe kutwa unashinda Lumumba kuvizia buku tano
 
Wabunge hawa wanakuwa wapi kipind cha mapumziko mana hajasikika akifanya kazi yoyote jimboni leo anaenda kupiga kelele bungeni. ...pia kuna mwenzio saidi kubenea huku jimboni kwake toka kapigiwa kura 2015 sijawah muona tena kwenye shughuli za maendeleo
.
.
Tuonane 2020
Nitajie faida 3 tu za uongo ulizopata tangu uanze kuongopa .
 
Ila Mnyika nae alikuwa wapi muda wote huo ndo leo atoe kilio cha waliobomolewa nyumba Morogoro Road? Kuna ugumu gani kuchukua laki mbili kutoka ktk mshahara wake, kuziweka ktk bahasha za kaki 10 na kuwaita waandishi wa habari kama 10 na kukemea kitendo cha serikali kubomoa nyumba wakat kuna zuio la mahakama kwa baadhi yao?

Au ndo anajiandaa kuwa Sales Officer pale Game Mlimani City kama Baba yake wa kisiasa Dr. Mihogo? Unawezaje kusaidia kujenga chama, halafu linatokea jambo usilolipenda ktk chama bas unasusa na kuhujumu chama? Ukimya wa Mnyika unahujumu chama, nilitegemea chadema wajipange kuwasemea wana kimara kupitia viongozi wa chama wilaya ya Ubungo na Kata za maeneo yaliyoathirika maana mbunge amekuwa bubu.
Huyu mnyika ndo wale wale wanasiasa uchwara.

Anataka kutumia janga la bomoa bomoa kujijenga kisiasa yeye na chama chake kuwarubuni wapiga kura wa saranga na jimbo la kibamba

Sasa watu wameshabolewa hata akiongea bungeni itasaidia nini
 
HUYU MNYIKA NDO WALE WALE WANASIASA UCHWARA.

ANATAKA KUTUMIA JANGA LA BOMOA BOMOA KUJIJENGA KISIASA YEYE NA CHAMA CHAKE KUWARUBUNI WAPIGA KURA WA SARANGA NA JIMBO LA KIBAMBA

SASA WATU WAMESHABOLEWA HATA AKIONGEA BUNGENI ITASAIDIA NINI
Akili za aina hii anazo bata tu, kwa vile Kanumba keshakufa basi hamna haja ya kesi. Yaani kwa ufinyu wako Wa akili ulitaka Mnyika akodi majeshi Uganda kuja kuzia bomoa bomoa hiyo HARAMU?

Maana kulikuwa na watu wana zuio la mahakama lakini wamebomolewa kwa ubabe. Unataka wakasemee wapi? Yaani hata Kazi za mbunge huzijui lakini kwa post hii unasubiri bk.7?
 
Mimi binafsi 2020 sitampa Mnyika kura yangu, kwa vipindi vyote vilivyopita nimempa jamaa kura, hata ile aliyoshindwa na Keenja.

Leo hii nasema mimi na Mnyika basi tena.
 
Akili za aina hii anazo bata tu, kwa vile Kanumba keshakufa basi hamna haja ya kesi. Yaani kwa ufinyu wako Wa akili ulitaka Mnyika akodi majeshi Uganda kuja kuzia bomoa bomoa hiyo HARAMU? Maana kulikuwa na watu wana zuio la mahakama lakini wamebomolewa kwa ubabe. Unataka wakasemee wapi? Yaani hata Kazi za mbunge huzijui lakini kwa post hii unasubiri bk.7?
Hahahaaaaaa ati jeshi la UGANDA
 
Ila Mnyika nae alikuwa wapi muda wote huo ndo leo atoe kilio cha waliobomolewa nyumba Morogoro Road? Kuna ugumu gani kuchukua laki mbili kutoka ktk mshahara wake, kuziweka ktk bahasha za kaki 10 na kuwaita waandishi wa habari kama 10 na kukemea kitendo cha serikali kubomoa nyumba wakat kuna zuio la mahakama kwa baadhi yao?

Au ndo anajiandaa kuwa Sales Officer pale Game Mlimani City kama Baba yake wa kisiasa Dr. Mihogo? Unawezaje kusaidia kujenga chama, halafu linatokea jambo usilolipenda ktk chama bas unasusa na kuhujumu chama? Ukimya wa Mnyika unahujumu chama, nilitegemea chadema wajipange kuwasemea wana kimara kupitia viongozi wa chama wilaya ya Ubungo na Kata za maeneo yaliyoathirika maana mbunge amekuwa bubu.

Watu wengine munapenda sifa mnyika na wananchi hadi waliandamana
 
Back
Top Bottom