Mnyika apitishwa kwa 100% Ubungo, amtangaza Dr Slaa kuwa Shujaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika apitishwa kwa 100% Ubungo, amtangaza Dr Slaa kuwa Shujaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Serayamajimbo, Jul 26, 2010.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MGOMBEA wa Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika amepitishwa na na chama chake kugombea jimbo hilo kwa asilima 100.
  Bw. Mnyika alipitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa jimbo hilo baada ya wajumbe wote 62 kumpa kura ya ndiyo.
  Wajumnbe waliohudhuria katika mkutano huo ni Wenyeviti na makatibu wote wa jimbo hilo, wageni waalikwa 60 na wawakilishi wa vyuo vikuu walioko Ubungo na wawakilishi wa matawi ya CHADEMA katika jimbo hilo.

  Wakati huo huo, Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limemtaja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa kuwa shujaa baada ya kukubalia maombi ya Kamati Kuu ya kugombea urais wakati baado alikuwa anahitajika katika jimbo lake.
  Akizungumza katika mkutano wa wakilishi wa vyuo vikuu Mweyekiti wa Kamati ya baraza hilo, Bw. John Mnyika alisema kitendo alichofanya Dkt. Slaa cha kuachia jimbo ambalo alikuwa na uhakika wa kushinda katika Uchaguzi Mkuu ni la kishujaa.
  "Tunakutana leo kwa kuwa tendo alilofanya Mtanzania mwenzetu, Dkt. Slaa kukubali kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni la kishujaa," alisema Bw. Mnyika
  Alisema Dkt. Slaa ni sawa mashujaa waliokubali kupoteza maisha yao na kulilinda na kuliteta taifa na hivyo ni shujaa wa demokarsia na maendeleo.
  Alisema mashujaa wa namna ya Dkt. Slaa hawafii kwa kuwa fikra zao zitakumbukwa milele uamuzi wa huo utandika historia mpya kwa taifa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo misingi ya CHADEMA
  Alisema Bendera ya chama hicho ni rangi ya nyekundu, nyeupe bluu, bahari na nyeusi uwepo kwa rangi nyekundu unatoka na kuthamini mashujaa wa nchi walipigana vita ili kulikomboa taifa hili.
  Alisema maadhimisho yanayofanywa na serikali Julai 25 kila mwaka kuwakumbuka mashujaa ni unafiki kwa kuwa hufanywa kwa maneno na si wa kivitendo
  Alisema tunu ya taifa hili ziko kwenye ngao ya taifa ambayo ni Uhuru na Umoja lakini uhuru umetoweka na nchi imekuwa tegemezi kwa kuwa sehemu kubwa ya rasilimli zake zimeuzwa kwa bei ya kutupwa kwa wageni na sehenu kubwa ya Watanzania hawafaidi nayo
  Alisema umoja umetelemshwa kutokana na kupuuzwa utawala wa sheria kumea kwa ubaguzi na kupanuka kwa matabaka katika jimii kwenye sekta mbalimbali za afya, elimu na hata mifumo ya haki hali ambayo ni tishio la ustawi na usalama wa nchi.
  Alisema Dkt. Slaa ametimiza wajibu huo kwa kusimamia ukweli, uwazi, uadilifu na amani kama rangi nyeupe katika bendera ya CHADEMA inayowakilishwa hususani kupitia ngazi ya ubungeni katika jamii na jimboni kwake karatu
  Bw Mnyika alisema umefika wakati wa Dkt. Slaa kuinuliwa na kupewa wajibu mkuu zaidi katika nchi wa ili kuunda serikali na kusimamia utekelezaji ilikurudisha nchi kwa wananchi.

  Source: Mnyika apitishwa kwa 100% Ubungo
   
 2. minda

  minda JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  lakin kumbk uchagz bado
   
 3. R

  Ramos JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hongera sana bw Mnyika, kuwa makini usipigwe tena changa la macho hapo kwa wajanja...
   
 4. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh...yaaan ata Mnyika haamini kuwa Dr Slaa anaweza kumshinda Kikwete mwaka huu?kaaazi kwelikweli!!
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  I'm now doubting your objectivity since you seem to hate everything Chadema. Anyway ni vichwa gani hao unaowajua ili na sisi tuwa fahamu na kuwa pima?
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Go mnyika go its our time now achana na wasotaka kukuelewa waloamua kufumba macho ili wasiuone ukweli. Keep going you will make it!
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ni walewale tu yaani huachi kuangalia kwa kutumia UDINI, bado narudia umekuwa oriented na elimu yako ya utotoni ndo maana waangalia DINI tu!
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Do you have problem with priests? By the way kusema wagombea vichwa wata tangazwa na tume ya uchaguzi ni unasema kwamba tume ya uchaguzi ndiyo ina halalisha na kichwa au nani siyo kichwa au una maanisha Tanzania tuna mfumi wa kisiasa na wa kijamii uliyo kamili sana kiasi kwamba kigezo pekee cha mtu kushinda ni kuwa kichwa au la? Maana kuna wanaoshindwa kwa rushwa nk na wana tangazwa na tume....je wao ni vichwa? Na pia huyo "padre" unayempinga kuwa hawezi kuwa raisi na yeye ni mbunge aliye tangazwa na tume ya uchaguzi kwa hiyo je mkuu ni sawa niki chukulia kwamba unamkubali Mh. Slaa ni kichwa?
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tumain anahaha sasa hivi kwenye JF akihama thread hadi thread kumtukana Slaa.

  Wenye akili zao sasa hivi wameshaacha kumjibu.

  Acheni kupoteza muda na umeme/nguvu zenu kumjibu.

  Hata Malaria Sugu jana alimuonya ila jamaa ngangari.

  Usibishane na ....... watu hawataona tofauti.

  Kila mkisoma ujumbe wa Tumain, mumhurumie Masikini wa watu. Sijui kalipwa au anafanya kazi ya bure?
   
 10. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  " Fear and Surrender are not the options for me" it does not sound like it comes from your heart! it looks like itis ctrl + P, ctrl+ v. no wonder unajiita tumain! endelea kuwatumain hao unaowatumaini labda miaka mingine 50 wataleta maendeleo, miaka 50 tuliyowapa wametuzalishia mafisadi tu! Na sasa wanasema wanakuja kwa kasi zaidi! Mwaka huu hawachomoki!
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu wapi hapo aliposema au mimi nina Makengeza?
   
 12. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  CDM HUREEEEEEE, najua ushindi upo kama tutakuwa makini
   
 13. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kijana anastahili hiyo heshima aliyopewa,hakika hili jimbo ni lake kama uchaguzi ukiwa free n fair binafsi siami kama LAST TIME alishindwa kihali!Ila wote wenye nia njema tuamua kwa busara hatma ya nchi yetu tuachana na hawa wenye hoja zisizo na mashiko za udini tujipange kupoka madaraka kistaarabu kwa NGUVU YA UMMA,mnyika aluta cntnue mpaka kieleke hapo ubungo oct.
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Butola hebu acha uvivu Hotuba ya Mnnyika ipo sasa kwa nini unakariri Magazeti?

  Hapo Mnnyika alikuwa anawakosoa wale wote wenye Fikra kama zako kwamba kwa kuwania Urais basi Amejiua Kisiasa

  Hapa Chini Mnyika anazidi kupiga Nondo

  Na hapa anamaliza kabisa

   
 15. M

  Mwanitu JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 635
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 80
  hongera Mnyika, lakini ingefurahisha zaidi ungepata pungufu kidogo ya mia.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu hakikisha unaweza kuyakoga maji haya..Ni fikra kama hizi zinazowafanya nchi za kiarabu kuendelea kuibiwa uchumi wao wakilinda dini badala ya ardhi, matokeo yake wote wamemezwa na dini inapotea ktk matendo yao walichobakia nacho ni imani tu..Dini inalindwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe kwani ni swala la imani na sii binadamu walioileta wala kutakiwa kuilinda imani iliyosetirika ktk mioyo ya watu..

  Hivyo jaribu sana kutofautisha siasa na Dini. Dr.Slaa anaweza kuwa Padre lakini kwa nia na dhamira yake ni mbora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko huwa wanaothaminisha haramu zote. Uislaam sio jina la mtu wala elimu ya mtu isipokuwa ni imani inayofuatiwa na Ibada. Sii Mwinyi wala JK wanafuata mafundisho ya dini zaidi ya majina yao..Na hakika hakuna Waislaam din - Bongo, ni unafiki mtupu..
   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Safi sana kwa Maneno yako yenye Busara Tele, tuwaache hawa wanaopiga kampeni za kidini! Hazina Nafasi
   
 18. A

  Audax JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  dini- tena imeingiaje kweye siasa? Hawajapata urais wameanza udini wakipata itakuwaje? Afghanstan jamani!!
   
 19. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  All is good but what I seeing is no sense message from another suppoter of left wing politician!

  Kama udini basi CCM ndiye namba one maana mgombea wa Urais TZ ni Mwislam,Makamu wake ni Mwislam,mgombea wao Urais ZNZ ni mwislam!Tumaini iweje umeweza kuona kibanzi kwenye"macho"ya CHADEMA lkn ukashindwa kuona boriti kwenye"macho"ya CCM?Cheapest ever CCM propagandist indeed!
   
 20. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 770
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 180
  Tunaopeda demokrasia ya kweli tukiona mtu anashinda 100% tunashtuka, tunasikitika. Binadamu, na zaidi wanasiasa, wana shabaha na matamanio ya uongozi. Kundi la wanasiasa linapokutana na wote kukubaliana kitu 100%, inawezekana kuna wengine hawaruhusiwi kufikiri au wameoshwa ubongo.


  Kwa nini mpaka Kamati ndio iteue? Kwa nini kila mwananchi mwenye kadi ya CHADEMA asiwe na uwezo wa kusimama peke yake, kivyake, asema "nataka kugombea urais" halafu wapigiwe kura?

  Utakuwaje na mgombea urais ambae yeye mwenyewe hakuomba, hakutaka, hakunyoosha mkono juu kusema "nataka kuwa rais", ameteuliwa?

   
Loading...