Mnyika apingana na Pinda kuhusu katiba: Katiba Mpya Kuzinduliwa April 2014 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika apingana na Pinda kuhusu katiba: Katiba Mpya Kuzinduliwa April 2014

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PascalFlx, Jun 28, 2011.

 1. P

  PascalFlx Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amesema haitoshi kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuweka ukomo wa kukamilika kwa katiba mpya ifikapo mwaka 2014 ,bila kuweka ratiba ya mchakato wa kupata katiba hiyo.

  Amesema wananchi wanapaswa kupokea kwa tahadhari taarifa ya Pinda kwa kuwa alipaswa kuitoa bungeni na si katika mkutano nje ya Bunge.

  Mnyika alisema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kufuatia kauli ya Waziri Mkuu kwamba katiba mpya itazinduliwa Aprili 26 mwaka 2014.


  Pinda alisema hayo juzi wakati akifungua semina ya wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu tawala, mjini Dodoma.


  "Wananchi wawe makini kuhusu kauli ya Waziri Mkuu Pinda, ameweka ukomo lakini hatoi ratiba ya mchakato, ili wananchi wafahamu wanashiriki vipi,"alisema Mnyika.


  Alisema hotuba ya Pinda inaonyesha uwa serikali haina uhakika wa lini muswada wa mapitio ya sheria ya marekebisho ya katiba wa mwaka 2011, utawasilishwa bungeni.

  "Ni muhimu ukomo huo ukawasilishwa rasmi bungeni kupitia kauli ya serikali kabla muswada wa sheria utakaozingatia ratiba, mipango , maazimio na sheria, " alisema Mnyika.

  Mnyika alisema mwanzoni mwa mwaka huu, aliwasilisha hoja binafsi bungeni, kutaka wananchi kuhusishwa katika mchakato wa katiba kuanzia mwanzoni.

  Mbunge huyo alisema Pinda alipaswa kutoa kauli bungeni kueleza bayana kama hati ya dharura ya muswada huo iliyowahi kuwasilishwa na serikali kama ilifutwa, ili muswada mwingine uweze kuwasilishwa kwa kufuata taratibu za kawaida kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

  "Pia kitendo cha wakuu wa mikoa na wilaya kuelekezwa kusimamia mchakato huo wakati sheria haijapitishwa na Bunge kinaonyesha wazi kuwa serikali tayari ina msimamo wake na inataka kulitumia Bunge kuidhinisha uamuzi wake,"alisema Mnyika.

  "ikumbukwe kwamba watendaji wamekuwa wakilalamikiwa kwa kutumia madaraka yao vibaya, leo hao ndio wanapewa nafasi za kusimamia katiba mpya, serikali haina dhamira ya kweli katika suala hili," alisisitiza.

  Mbunge huyo wa Ubungo, alisema kati ya mambo ambayo wananchi wameanza kuyatolea maoni kuhusu katika mpya ni kutaka kupunguzwa kwa madaraka ya wakuu wa mikoa na wilaya.

  "Hawa wakiwa wasimamizi hawatatenda haki," alisema Mnyika.

  by Raymond Kaminyoge

  Source: Mnyika apingana na Pinda kuhusu katiba
   
 2. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  bomu jingine amabalo litaimaliza kabisa sisiemu ni hili hapa. kuamua mambo bila kufikiria kwa umakini sasa inakuwaje waseme katiba mpya 2014? wametumia gani vigezo?
   
 3. m

  mkalachaka Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2007
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ukweli hata mimi nadhani Waziri mkuu Mheshimiwa mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda hatutendei haki kabisa watanzania kwa ujumla wetu. Suala la Katiba nadhani hata mjadala haujaanza wa nini kifanyike na kifanyike vipi. Inakuwaje Waziri mkuu anakuja na hoja hadi kuthubutu kuitolea tarehe itakapozinduliwa wakati mjadala haujaanza? Yeye kama msemaji mkuu wa Serikali Bungeni kama alikuwa na uhakika kiasi hicho basi ilibidi hayo ayasemee huko huko bungeni ili wabunge wenzie wachangie na wampe changamoto. Labda yeye mwenyewe sasa ili mradi tayari anaijua tarehe ya kuzinduliwa kwa Katiba hiyo basi awaeleze waheshimiwa wabunge wenziye ili mjadala rasmi uweze kuanza na mchakato mzima uwekwe wazi.
   
 4. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Mhariri wa jambo katoa hayo maoni katika gazeti la leo. Nashukuru wamekiri kwamba hoja zote za Mnyika zina mashiko maana hata wanaodai kwamba Mungu hayupo huwa wanathibitisha uwepo wake. Mnyika-CDM mwendo mdundo, mpaka kieleweke.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu mbona heading haiendani na content!? Au umezoea magazeti ya udaku!
   
 6. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakushauri uanze upya thread yako
   
 7. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  we ulitakaje? Sugua kichwa, kilaza wewe
   
 8. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  inajitosheleza hiyo, labda useme nini hujakielewa?
   
 9. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hamjaelewa nin?gazati la jambo leo Mhariri wake amemkosoa Mnyika na kusema s kila ki2 anachoongea n point..amekosoa hasa mchango wake wa jana alpo2mia nafas ya "Muongozo wa Mwenyekt" kufksha maswal matatu kwa Wazir mkuu...sbb 2naenda wik ya pili bla kuwa na kipnd cha Maswal kwa PM!jana alisema kuna mambo meng yanahtaj kauli ya Serikali via PM,zivnjwe kanuni PM ajibu!Jambo Leo limekosoa!Lakn kwa "wanafnz wa Logic" unapata picha kmbe Mnyka n m2 wa point mda wote!kama Jambo Leo(gazeti kaka la Uhuru na Habar Leo) linasema ivo,bas kimantk uko mda wooote Mnyka n m2 wa point2!wamempa "Promo" bla kujijua
   
 10. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  ni ukweli usiopingika kuwa watu waa ubungo walizitendea haki kura zao kwa kumchagua mnyika kuwa mwakilishi wao.
   
 11. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  mkuu mbona mkali mithili ya tindikali.lol. Hata me naona heading na content haziendani
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kuna thread humu ndani inayozungumzia gazeti la jambo leo jinsi linavyoripoti habari za chadema.
   
 13. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kuna watu akili zao zimekaa kukosoa na kukejeli wengine, mimi nimeipa "logic meaning" ya huyo mhariri,, mwingine anakurupuka eti nimezoea magazeti ya udaku alafu naye anajiita GT, Nashukuru kwa kuelewa logic yangu.
   
 14. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  sio wote wameudhuria darasa la Logic and Argument
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ntamwondoa lini huyu??[​IMG]
   
 16. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  wapunguze kukurupuka basi kwani hata JF ni darasa tosha.
   
 17. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, jana kwa mara ya pili mfululizo ameshindwa kujibu Maswali ya Papo kwa Hapo bungeni kwa madai ya kukabiliwa na mjadala wa hotuba ya bajeti ya ofisi yake.

  Wakati kanuni zikitumika kumlinda Pinda, asijibu maswali ya papo hapo, Mbunge wa Viti Maalum, Ritha Kabati (CCM), amesema anakusudia kupeleka hoja binafsi ili kukifuta kipindi hicho kinachofanyika kila siku ya Alhamisi kwa madai kuwa kina maswali ya kumdhalilisha Waziri Mkuu.

  Hatua ya Pinda kukwepa maswali jana, imemlazimisha Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika, kumshtaki Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene, kwa Katibu wa Bunge ili aitishe kikao cha dharula cha Kamati ya Kanuni za Bunge kurejea kanuni 5(5) anayodai kwamba imevunjwa na mwenyekiti huyo wa Bunge ili kumlinda Pinda.

  Mara baada ya Simbachawene kuzuia maswali na majibu kwa Pinda, Mnyika aliomba mwongozo wa kanuni bungeni kutaka zisipindishwe kumlinda Pinda kwa kuwa kifungu cha 38 (5) kinaeleza bayana kwamba hakutakuwa na maswali kwa Waziri Mkuu iwapo hatakuwepo kwa sababu maalum, lakini kiongozi huyo jana alikuwepo bungeni.

  Mnyika, alisema hata baada ya kuomba mwongozo wa kiti cha Spika, Simbachawene aliendelea kutoa miongozo yenye kukiuka kanuni za Bunge hususan vifungu 5(1), 7(3), 30(6), 38(5), 150 (1) na 150 (4).

  Taarifa ya Mnyika, iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, ilisema hajaridhika na maamuzi ya Simbachawene, kupindisha kanuni kwa ajili ya kumlinda Waziri Mkuu kutekeleza wajibu wa kujibu maswali ya papo kwa papo ya wabunge kama kanuni zinavyohitaji.

  “Nilitaka muongozo kanuni za Bunge zisipindishwe kumlinda Pinda kwa kuwa kifungu cha 38 (5) kinaeleza bayana kwamba hakutakuwa na maswali kwa Waziri Mkuu iwapo hayupo kwa sababu maalum na kwamba siku ya leo ya Alhamisi Juni 30, 2011 Waziri Mkuu Pinda alikuwepo bungeni katika kipindi husika cha maswali.

  “Hata hivyo, pamoja na maelezo hayo Simbachawene aliendelea kutoa miongozo yenye kukiuka kanuni za Bunge hususan vifungu 5(1), 7(3), 30(6), 38(5), 150 (1) na 150 (4).

  “Jana, niliomba muongozo wa mwenyekiti kwa mujibu wa kanuni 68 (7) baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Simbachawene kutoa taarifa ya Bunge kuwa hakutakuwepo na maswali na majibu kwa Waziri Mkuu kwa kuwa kanuni zilitenguliwa Juni 22, 2011 kumruhusu Waziri Mkuu kujiandaa kuwasilisha hotuba yake Juni 23 mwaka huu.”

  “Niliomba mwenyekiti atoe muongozo kuwa kanuni za Bunge zilikiukwa kwa kutoa taarifa ya kupindisha kanuni kumlinda Waziri Pinda, asijibu maswali ya wabunge wa papo kwa hapo bila kufuata utaratibu wa kutengua kanuni.”

  “Nikalieleza Bunge kuwa kanuni ya 150 imekiukwa ambayo kipengele cha 150(1) ambacho kinaelekeza bayana kwamba ili kanuni itenguliwe kwa madhumuni mahsusi ni lazima Waziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali au mbunge yeyote, atoe hoja hiyo na kifungu cha 150 (3) kinataka maelezo ya hoja hiyo yakiwemo madhumuni, yatolewe jambo ambalo halikufanyika,” alisema Mnyika.

  Mnyika mmoja wa wabunge vijana machachari wa CHADEMA, alisisitiza kwamba kwa kuwa kuna masuala tata na tete yanayoendelea nchini ambayo yanahitaji kauli za serikali ni muhimu kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu kuendelea kama kanuni zinavyohitaji ili kuyatolea ufafanuzi.

  Alitaja baadhi ya mambo yanayohitaji ufafanuzi wa serikali kupitia Waziri Mkuu kuwa ni pamoja na kauli tata kuhusu Katiba, tatizo sugu la umeme, tatizo la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

  “Mathalani nililieza Bunge kwamba vyombo vya habari vimemnukuu Waziri Mkuu Pinda akitoa maelekezo potofu kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhusu mchakato wa Katiba kabla ya sheria kupitishwa.

  “Maelekezo hayo yalifuatiwa na uamuzi wa kuondolewa kwa muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba katika ratiba ya mkutano wa nne wa Bunge kinyume na mipango iliyotangazwa awali.”

  “Pia, nililieza Bunge kuwa serikali inapaswa kutoa kauli bungeni ya kumaliza mgawo wa umeme unaoendelea na kuathiri taifa ikiwemo wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. Nililieleza Bunge kuwa wananchi wanakusudia kuandamana hivyo majibu kwa Waziri Mkuu Pinda kupitia maswali ya papo kwa hapo yangeweza kuelezea ufumbuzi wa suala hilo,” alisema Mnyika.

  Kadhalika, mbunge huyo alilieleza Bunge kuwa vyombo vya habari vimewanukuu wakuu wa wilaya wakitoa maelekezo kwa UDOM kuwabagua wanafunzi kwa misingi ya vyama vyao wakati wa kuwarejesha chuoni kwa kuanza kuwarejesha kwanza wanachuo wanachama wa CCM.

  Alisema kauli hiyo ilifuatiwa na waraka wa Wizara ya Elimu na Ufundi ambayo imetoa maelekezo maalum ya ubaguzi kwa bodi ya mikopo na UDOM.

  Kwa mujibu wa Mnyika, matokeo ya maelekezo hayo ni UDOM kutoa taarifa yenye masharti magumu ya kuwataka wanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii waliosimamishwa masomo kuripoti chuoni huku ikiwabagua wanafunzi 15 ambao wametajwa kwa majina.

  “Kutokana na masuala hayo na mengine toka kwa wabunge wengine yanayohitaji majibu toka kwa Waziri Mkuu Pinda kama kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, niliomba muongozo kwa mwenyekiti ili kanuni ya 30 (6) itumike kuagiza utaratibu wa kuwezesha shughuli ya maswali kwa Waziri Mkuu kuweza kuendelea kama kawaida,’ alisema Mnyika.

  Mbunge huyo alisema kwa kuwa kanuni zilipindishwa kuondoa kipindi cha maswali kwa Pinda, atumie kipindi cha majumuisho ya bajeti ya ofisi yake leo kutoa majibu ya kina kuhusu kauli zake juu ya mchakato wa Katiba mpya, kauli ya serikali kumaliza mgawo wa umeme na hatma ya wanafunzi 15 wa UDOM waliobaguliwa katika taratibu za kurejeshwa chuoni.

  Kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, kilianzishwa na Spika wa Bunge lililopita, Samuel Sitta, wakati wa mabadiliko ya kanuni za Bunge.
   
 18. MANI

  MANI Platinum Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Viwavi wa Nape ?
   
 19. MANI

  MANI Platinum Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  MS jibu swali sio kulalama !
   
 20. F

  FUSO JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa mwenye suti nyeusi kashapewa barua ya kutimuliwa umagamba? Napeeeeee!!!!!
   
Loading...