Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Mnyika amwaga radhi Magu
na Osoro Nyawangah, Magu
MKURUGENZI wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameitaka serikali kufuta jeshi la jadi, maarufu kama sungusungu na lile la mgambo kwa sababu hayapo kisheria.
Mnyika, alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Baraza la Vijana wa CHADEMA wilayani hapa na kuongeza kuwa sungusungu na mgambo wamekuwa wakitumika kuwanyanyasa wananchi.
Kutokana na malalamiko yaliyotolewa na uongozi wa vijana wilayani hapa, Mnyika alisema ni wakati muafaka kwa serikali kusimamia kwa dhati ulinzi na usalama wa raia na mali zao, badala ya kuacha jukumu hilo mikononi mwa vyombo visivyo vya kisheria na kuangalia uvunjaji wa haki za binadamu ukiendelea katika jamii.
Alisema sungusungu hawana taaluma yoyote ya sheria, wanatumia mabavu kuwakamata wanaotuhumiwa kwa uhalifu na kuwahukumu bila kuwapeleka mahakamani.
Nimesikia sungusungu wanawasumbua vijana hapa na kusababisha mauaji ya watu, uharibifu wa mali na unyanganyi bila ya kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria, huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, hatutalikubali na tunataka serikali ichukue hatua za kuvunja vyombo hivi ambavyo vinafanya kazi za kiitikadi, alisema Mnyika.
Alisema sungusungu na mgambo ni vyombo vilivyoundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nia ya kuwaogopesha wananchi na kuwanyanyasa kwa malengo ya kisiasa na ndiyo maana idadi kubwa ya watu walio katika majeshi hayo ni wanachama wa chama hicho.
Akizungumzia umuhimu wa vijana katika maendeleo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Chacha Wangwe, aliwataka vijana wilayani hapa kutokubali kunyanyaswa na kuwataka kutoa taarifa ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu kwenye ofisi hiyo ili wapate misaada ya kisheria.
Alisema CCM iliahidi katika ilani yake ya uchaguzi kuwapatia vijana ajira lukuki na imeshindwa kutimiza azima hiyo badala yake wameanza kuwanyanyasa vijana wanaojiajiri kwa kuendesha miradi ya usafirishaji wa baiskeli na kunyanganywa baiskeli zao kwa madai kuwa wao ni wahalifu.