Mnyika amwaga radhi Magu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika amwaga radhi Magu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, May 22, 2008.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2008
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mnyika amwaga radhi Magu

  na Osoro Nyawangah, Magu

  MKURUGENZI wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameitaka serikali kufuta jeshi la jadi, maarufu kama sungusungu na lile la mgambo kwa sababu hayapo kisheria.
  Mnyika, alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Baraza la Vijana wa CHADEMA wilayani hapa na kuongeza kuwa sungusungu na mgambo wamekuwa wakitumika kuwanyanyasa wananchi.
  Kutokana na malalamiko yaliyotolewa na uongozi wa vijana wilayani hapa, Mnyika alisema ni wakati muafaka kwa serikali kusimamia kwa dhati ulinzi na usalama wa raia na mali zao, badala ya kuacha jukumu hilo mikononi mwa vyombo visivyo vya kisheria na kuangalia uvunjaji wa haki za binadamu ukiendelea katika jamii.
  Alisema sungusungu hawana taaluma yoyote ya sheria, wanatumia mabavu kuwakamata wanaotuhumiwa kwa uhalifu na kuwahukumu bila kuwapeleka mahakamani.
  “Nimesikia sungusungu wanawasumbua vijana hapa na kusababisha mauaji ya watu, uharibifu wa mali na unyang’anyi bila ya kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria, huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, hatutalikubali na tunataka serikali ichukue hatua za kuvunja vyombo hivi ambavyo vinafanya kazi za kiitikadi,” alisema Mnyika.
  Alisema sungusungu na mgambo ni vyombo vilivyoundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nia ya kuwaogopesha wananchi na kuwanyanyasa kwa malengo ya kisiasa na ndiyo maana idadi kubwa ya watu walio katika majeshi hayo ni wanachama wa chama hicho.
  Akizungumzia umuhimu wa vijana katika maendeleo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Chacha Wangwe, aliwataka vijana wilayani hapa kutokubali kunyanyaswa na kuwataka kutoa taarifa ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu kwenye ofisi hiyo ili wapate misaada ya kisheria.
  Alisema CCM iliahidi katika ilani yake ya uchaguzi kuwapatia vijana ajira lukuki na imeshindwa kutimiza azima hiyo badala yake wameanza kuwanyanyasa vijana wanaojiajiri kwa kuendesha miradi ya usafirishaji wa baiskeli na kunyang’anywa baiskeli zao kwa madai kuwa wao ni wahalifu.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Big Up Mnyika,

  Hili tulishalijadili hapa pamoja na mgambo/Sungusungu kunyanyasa raia kwa misingi ya kutafuta wasiolipa kodi.

  Vyombo vyetu vilivyo kisheria tu vina matatizo makubwa yanayohitaji kurekebishwa, sembuse hivi vinavyoelea kwa whims za viongozi wa chama?

  I support Mnyika/CHADEMA on this.
   
 3. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #3
  May 22, 2008
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Pundit

  Thanks, lakini sidhani kama hicho kichwa hapo juu ndio habari ilivyo.

  Pili; uhalali niliokuwa nauzungumzia ni uhalali wa kimaadili, na pia kutokujua sheria. Naona mwandishi amechukulia angle nyingine kidogo.

  Unajua dhana ya community policing na suala na neighbourhood security kimantiki ni mambo mazuri, lakini utekelezaji wake Tanzania unafanyika ndivyo sivyo.

  Nilizungumza mambo kadhaa siku hiyo, bahati mbaya ilikuwa impromtu!

  JJ
   
 4. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2008
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Polisi Wenyewe Hawana Elimu Ya Uraia Sasa Hawa Wanazengo Ndiyo Kabisa Wao Opposition Party Ni Enemy Of The People,so We Need Talk Loudlyabout This, Big Up Manyika.
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  May 22, 2008
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Sentesi "Hayapo Kisheria", inaweza kuwa tata kama mtu atakuwa hajapata mazungumzo yangu kwa ukamilifu wake, maana najua kwamba zipo sheria ambazo zimetoa mianya kwa watawala kuunda vikosi vya mgambo. Lakini mipaka ya kazi yako iko bayana. Vikosi hivi vimevuka mipaka hiyo na sasa katika maeneo mbalimbali vinalekea kuwa kero kwa wananchi

  JJ
   
 6. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mnyika,

  Fanyeni mipango ya kurekodi hizi speeches halafu mnaweka mp3 mtandaoni kiasi kwamba hata kama kuna mtu ana distort au kunahitajika clarifications mnampa link ya mp3 tu anapata verbatim.

  Ila hatuwezi kuwa na neighbourhood watch iliyo effective kama elimu ya uraia ipo chini, hapo utakuwa una invite human rights abuses tu, kitu kinachotokea sasa hivi katika hizi militias za Sungusungu na Mgambo.
   
 7. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2008
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  PUNDIT KICHWA WEWE HASWA WAWEKE TUPAKUE WENYEWE
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Hivi hapo tatizo ni mgambo au ni sheria zetu? Ukiondoa Mgambo bado polisi wataendelea kunyanyasa raia. Ukiondoa polisi jeshi nao wataendelea.

  Huwezi kutatua hilo tatizo kwa kufuta Mgambo au Sungusunga. Kinachotakiwa ni kutunga sheria zinazolinda haki za raia wetu na kuwaelemisha raia juu ya haki zao.

  Mgambo na Sungusungu wakitumika vizuri wana faida kubwa sana.
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mtanzania,

  Zaidi ya sheria ni elimu ya uraia na mfumo wa haki.Hata ukiwa na sheria nzuri kiasi gani, kama wananchi hawazijui au hawana access nazo itakuwa bora.

  Ndiyo maana napigia kelele sana elimu ya uraia na mfumo mzima wa haki za kimahakama kuwawezesha wananchi kupata haki zao zaidi na kwa gharama nafuu ya hali, mali na muda.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapa tatizo no sheria nakumbuka Mgambo hutumika sana kuiba kura zetu wakai chaguzi nk .
   
 11. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,594
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Sungusungu kwa dhana ya kinadharia ni dhana nzuri lakini tatizo kwa Tanzania ni kwamba hao sungusungu wanafanya baadhi ya mambo ambayo ni kinyume kabisa ya dhana iliyokusudiwa ya kuwepo kwao. Wakati mwingine wana wa"torture" watu, wanajichukulia sheria mkononi wa kuwaadhibu watuhumiwa,

  kama sungusungu wangekuwa hawajihusishi na mambo kama hayo ya uvunjivu wa haki za binadamu wanafaa sana katika kupunguza wimbi la ujambazi. labda serikali iweke ethics kwa sungusungu nchini ili ziwe mwongozo wa wafanyeje shughuli zao
   
 12. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Lunyungu,

  Sasa kama raia wana elimu yao ya uraia na wamehamasika hapa ndipo wanapoandamana mji mzima kupinga wizi wa kura wa mgambo.

  Nobody can play with an educated and motivated electorate, even a poor (materially) one.

  Tatizo sisi ni maskini materially mpaka kwenye hiyo civic education.
   
 13. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  tatizo la Mnyika ni kwamba kila kitu anaiblame ccm, yaani hadi nacheka saa nyingine ! pengine hajui sungusungu waliundwa na nani kwa ajili ya nini na wakati gani ! nitafurahi kama atakuja kujibu yeye mwenyewe mnyika !
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama Mnyika amesema kuwa Sungusungu hawajui sheria basi yeye ndio hajui maana ya sungusungu. Prof. Shivji anaweza kuwa sungusungu mtaani kwake, je hajui sheria!!!

  Ni kweli kuna mapungufu katika jinsi askari wanavyofanya kazi wakati fulani lakini kuondoa askari ndio kuleta mapungufu zaidi. Labda nimshauri ndugu Mnyika aende kwenye wodi ya wazazi akaone jinsi akinamama wanavyolalamika jinsi wanavyosumbuliwa na wauguzi - rushwa, matusi, masimango nk.- Sasa kwa style aliyoionyesha Mnyika hapa napo atashauri wauguzi waondolewe.Matokeo yake nini?

  Cha muhimu ni kuwafundisha wananchi haki zao na kuwahamasisha kuchukua hatua za kisheria pale wanapoona kudhurumiwa haki zao.
   
 15. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  napenda the way Mnyika anavyotoa lawama zake (kulialia as usual, tena kulalamikia ccm) na wakati huo huo hatoi solution ya nini kifanyike instead ! ooh he's playing the "boss player".!
   
 16. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Sioni kama ni jambo la busara kutoa hoja kama hiyo. Hakuna sababu ya kufuta utaratibu wa Sungusungu, hoja ya maana ingekuwa ni namna ya kuboresha utaratibu wa Sungusungu. Hapa Tanzania tunaupungufu mkubwa wa polisi, na hata polisi wengine waliowengi hawana uelewa wa sheria kama ilivyo kwa sungusungu.
  Sungu sungu wameweza kufika kwenye maeneo ambayo hata polisi hawawezi kufika, wanajitahidi kufanya kazi nzuri sana, kama hata hilo ambalo ni jadi ya watanzania mkitaka kulifanya siasa itakuwa ni jambo la ajabu sana.
   
 17. C

  Chuma JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  1. Pundit ushauri wako ni mzuri juu ya MP3 lkn tujiulize ina maana IT Team ya Chadema imeshindwa juu ya Hili? au hata Mnyika mwenyewe ambae kwa muda sasa yupo hapa JF ameshindwa hata kuwa plan ya juu ya vitu tu-dogo namna hii? ambavyo bei yake dola 100?...
  Alau basi angekuja na kusema aliandaa na kurekodi, bahati mbaya virus imeharibu wakati anahamisha ktk Laptop yake...if that is the case, JJ Mnyika tafuta short kozi ingine ktk IT ili uweze fanya vema kt publicity ya Chama chako.

  2. Kuwepo Sungusungu ni kufeli kwa Polisi. pia si vema kusema eti polisi ni wachache, kwanini serikali isiwaajiri rasmi sungusungu na ikawapeleka monduli kusomea. Mtu anaweza sema hao darasa la saba....so what..kimsingi hata kama wote std 7 au hawakusoma hata std 1, lkn wana ABC za Ulinzi basi still waingizwe Polisi na kuwepo na grades...kama vilivyo vyeo vyao.vya sasa..

  3. Hatuwezi kuwalaumu wengine zaid ya serikali. kwani mambo ya ulinzi ni ya serikali. bahati mbaya serikali au viongozi wa serikali wameshindwa kukaa chini na kufikiri kazi ULEVI...Safari zao Nje ya TZ wameshindwa kujifunza namna Usalama wa raia unavyotakiwa Kuwa 40yrs baada ya Uhuru hatuna enough qualified Polis....Ikiwa wapo baadhi ya Polisi wenye mafunzo, lkn bado tu ni kero kwa watu....
   
 18. I

  Ipole JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao Chadema hawana mpya maana huyo Mbowe naye ni KAFISADI na hatuwezi kumpa nchi mcheza disco
   
 19. Mchola

  Mchola Member

  #19
  May 23, 2008
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe Ipole mbona unaropoka? watu wanatoapoint za maana wewe unakurupuka, oh, Mbowe ni kifisadi!!!! Toa point kwanza kisha umalizie na bifu lako na Mbowe. Hoja kwanza kama huna kaa kimya!!! Umeniudhi sana. By the way mimi si mshabiki wa Mbowe if you need to know
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hiyo "hoja" unayoisema ni distortions za waandishi wetu,

  Mwenyewe Mnyika kaja hapa, this very thread, ka-clarify alichosema vizuri tu, mpaka wengine tukashauri wawe wanaweka mp3 kwenye site yao ili kuzuia upotishaji huu.

  Na bado watu wanapotoka na muandishi aliyeripoti vibaya wakati clarification imetolewa na Mnyika ameelezea appreciation yake kwa dhana ya ulinzi wa wananchi kwa ajili ya wananchi na ku point out matatizo yanayotokana na elimu duni ya uraia.
   
Loading...