Mnyika amuweka Pinda kitanzini; Adaiwa kutumia Bunge kukwepa maswali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika amuweka Pinda kitanzini; Adaiwa kutumia Bunge kukwepa maswali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]• Adaiwa kutumia Bunge kukwepa maswali

  na Martin Malera
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]WAZIRI MKUU Mizengo Pinda, jana kwa mara ya pili mfululizo ameshindwa kujibu Maswali ya Papo kwa Hapo bungeni kwa madai ya kukabiliwa na mjadala wa hotuba ya bajeti ya ofisi yake.

  Wakati kanuni zikitumika kumlinda Pinda, asijibu maswali ya papo hapo, Mbunge wa Viti Maalum, Ritha Kabati (CCM), amesema anakusudia kupeleka hoja binafsi ili kukifuta kipindi hicho kinachofanyika kila siku ya Alhamisi kwa madai kuwa kina maswali ya kumdhalilisha Waziri Mkuu.
  Hatua ya Pinda kukwepa maswali jana, imemlazimisha Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika, kumshtaki Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene, kwa Katibu wa Bunge ili aitishe kikao cha dharula cha Kamati ya Kanuni za Bunge kurejea kanuni 5(5) anayodai kwamba imevunjwa na mwenyekiti huyo wa Bunge ili kumlinda Pinda.

  Mara baada ya Simbachawene kuzuia maswali na majibu kwa Pinda, Mnyika aliomba mwongozo wa kanuni bungeni kutaka zisipindishwe kumlinda Pinda kwa kuwa kifungu cha 38 (5) kinaeleza bayana kwamba hakutakuwa na maswali kwa Waziri Mkuu iwapo hatakuwepo kwa sababu maalum, lakini kiongozi huyo jana alikuwepo bungeni.

  Mnyika, alisema hata baada ya kuomba mwongozo wa kiti cha Spika, Simbachawene aliendelea kutoa miongozo yenye kukiuka kanuni za Bunge hususan vifungu 5(1), 7(3), 30(6), 38(5), 150 (1) na 150 (4).

  Taarifa ya Mnyika, iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, ilisema hajaridhika na maamuzi ya Simbachawene, kupindisha kanuni kwa ajili ya kumlinda Waziri Mkuu kutekeleza wajibu wa kujibu maswali ya papo kwa papo ya wabunge kama kanuni zinavyohitaji.

  "Nilitaka muongozo kanuni za Bunge zisipindishwe kumlinda Pinda kwa kuwa kifungu cha 38 (5) kinaeleza bayana kwamba hakutakuwa na maswali kwa Waziri Mkuu iwapo hayupo kwa sababu maalum na kwamba siku ya leo ya Alhamisi Juni 30, 2011 Waziri Mkuu Pinda alikuwepo bungeni katika kipindi husika cha maswali.

  "Hata hivyo, pamoja na maelezo hayo Simbachawene aliendelea kutoa miongozo yenye kukiuka kanuni za Bunge hususan vifungu 5(1), 7(3), 30(6), 38(5), 150 (1) na 150 (4).

  "Jana, niliomba muongozo wa mwenyekiti kwa mujibu wa kanuni 68 (7) baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Simbachawene kutoa taarifa ya Bunge kuwa hakutakuwepo na maswali na majibu kwa Waziri Mkuu kwa kuwa kanuni zilitenguliwa Juni 22, 2011 kumruhusu Waziri Mkuu kujiandaa kuwasilisha hotuba yake Juni 23 mwaka huu."

  "Niliomba mwenyekiti atoe muongozo kuwa kanuni za Bunge zilikiukwa kwa kutoa taarifa ya kupindisha kanuni kumlinda Waziri Pinda, asijibu maswali ya wabunge wa papo kwa hapo bila kufuata utaratibu wa kutengua kanuni."

  "Nikalieleza Bunge kuwa kanuni ya 150 imekiukwa ambayo kipengele cha 150(1) ambacho kinaelekeza bayana kwamba ili kanuni itenguliwe kwa madhumuni mahsusi ni lazima Waziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali au mbunge yeyote, atoe hoja hiyo na kifungu cha 150 (3) kinataka maelezo ya hoja hiyo yakiwemo madhumuni, yatolewe jambo ambalo halikufanyika," alisema Mnyika.

  Mnyika mmoja wa wabunge vijana machachari wa CHADEMA, alisisitiza kwamba kwa kuwa kuna masuala tata na tete yanayoendelea nchini ambayo yanahitaji kauli za serikali ni muhimu kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu kuendelea kama kanuni zinavyohitaji ili kuyatolea ufafanuzi.

  Alitaja baadhi ya mambo yanayohitaji ufafanuzi wa serikali kupitia Waziri Mkuu kuwa ni pamoja na kauli tata kuhusu Katiba, tatizo sugu la umeme, tatizo la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

  "Mathalani nililieza Bunge kwamba vyombo vya habari vimemnukuu Waziri Mkuu Pinda akitoa maelekezo potofu kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhusu mchakato wa Katiba kabla ya sheria kupitishwa.
  "Maelekezo hayo yalifuatiwa na uamuzi wa kuondolewa kwa muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba katika ratiba ya mkutano wa nne wa Bunge kinyume na mipango iliyotangazwa awali."

  "Pia, nililieza Bunge kuwa serikali inapaswa kutoa kauli bungeni ya kumaliza mgawo wa umeme unaoendelea na kuathiri taifa ikiwemo wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. Nililieleza Bunge kuwa wananchi wanakusudia kuandamana hivyo majibu kwa Waziri Mkuu Pinda kupitia maswali ya papo kwa hapo yangeweza kuelezea ufumbuzi wa suala hilo," alisema Mnyika.

  Kadhalika, mbunge huyo alilieleza Bunge kuwa vyombo vya habari vimewanukuu wakuu wa wilaya wakitoa maelekezo kwa UDOM kuwabagua wanafunzi kwa misingi ya vyama vyao wakati wa kuwarejesha chuoni kwa kuanza kuwarejesha kwanza wanachuo wanachama wa CCM.

  Alisema kauli hiyo ilifuatiwa na waraka wa Wizara ya Elimu na Ufundi ambayo imetoa maelekezo maalum ya ubaguzi kwa bodi ya mikopo na UDOM.

  Kwa mujibu wa Mnyika, matokeo ya maelekezo hayo ni UDOM kutoa taarifa yenye masharti magumu ya kuwataka wanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo cha Sanaa na Sayansi za Jamii waliosimamishwa masomo kuripoti chuoni huku ikiwabagua wanafunzi 15 ambao wametajwa kwa majina.

  "Kutokana na masuala hayo na mengine toka kwa wabunge wengine yanayohitaji majibu toka kwa Waziri Mkuu Pinda kama kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, niliomba muongozo kwa mwenyekiti ili kanuni ya 30 (6) itumike kuagiza utaratibu wa kuwezesha shughuli ya maswali kwa Waziri Mkuu kuweza kuendelea kama kawaida,' alisema Mnyika.

  Mbunge huyo alisema kwa kuwa kanuni zilipindishwa kuondoa kipindi cha maswali kwa Pinda, atumie kipindi cha majumuisho ya bajeti ya ofisi yake leo kutoa majibu ya kina kuhusu kauli zake juu ya mchakato wa Katiba mpya, kauli ya serikali kumaliza mgawo wa umeme na hatma ya wanafunzi 15 wa UDOM waliobaguliwa katika taratibu za kurejeshwa chuoni. Kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, kilianzishwa na Spika wa Bunge lililopita, Samuel Sitta, wakati wa mabadiliko ya kanuni za Bunge.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Wakati kanuni zikitumika kumlinda Pinda, asijibu maswali ya papo hapo, Mbunge wa Viti Maalum, Ritha Kabati (CCM), amesema anakusudia kupeleka hoja binafsi ili kukifuta kipindi hicho kinachofanyika kila siku ya Alhamisi kwa madai kuwa kina maswali ya kumdhalilisha Waziri Mkuu

  Huo ndo unafiki wa wabunge wa CCM!
   
 3. m

  mbeshere Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo kweli kabati ya mbeo!! Viti maaluum ni upuuzi mtupu angalia utumbo wa huyu binti hajui wananchi ndio tunataka kujuwa serikali yetu inafanya nn!!! kama anaona anaulizwa maswali ya kuzalilishwa si awapishe wenzie......
   
 4. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  swali linawezaje kuwa la kumdhalilisha waziri mkuu?
  bunge linatumia kanuni na kila siku tunaona wabunge wanabanwa sasa hii kumdhalilisha waziri mkuu inatoka wapi?

  kama hiki kipindi watakifuta CCM itazidi kupolomoka na hii tutaitumia kama mtaji kwenye kampeni 2015
  hakuna kufichana hapa
  wananchi tumechoka na kila siku tunachoshuhudia ni waziri mkuu kupingwa maswali ya moto kutoka upinzania na kuweuzo wake mdogo wa kujua mambo ndio maana anaonekana kudhaliliswa

  yeye kapewa uwaziri mkuu kufanya ushushu na hilo ni kosa la kikwete kuwa wapa watu vyeo ili wamletee umbeya badala ya kufanya kazi
  sio credibility kwa kupinda kuwa waziri mkuu labda ukuu wa wilaya kidogo
  kwa CCM ya sasa wanaofaa kuwa mawaziri wakuu ni MAGUFURI, SITTA, MWAKYEMBE au NUNDU

  kwa kuzingatia viwango ki- ccm
   
 5. K

  Kitoile New Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri huyu Dada yangu anaogopa uwazi!!. Na huu nafikiri ni unafiki. Nikimnukuu Mbunge toka Iringa( Mchungaji) " Sipendi tabia ya Wabunge wa kusema ninaiomba Serikali kushughulikia jambo fulani".

  Ni kweli Wabunge wengi wamekuwa wanafiki wa kutafuta kupendwa sijui ni ili wapewe vyeo. Ila hajui kuwa wale wanaoibana Serikali ndio hupewa vyeo ili kunyamazishwa?

  Mimi nafikiri Wabunge Wakiibana serikali kwa mambo yanayokwenda mrama nafikiri uwajibikaji utatiliwa mkazo na wananchi tutapata mafaniko tunayotarajia nchi yetu kuyafika.
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,876
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  hawa mawaziri walizoea kupumzika baada ya uchaguzi, mwaka huu ni mchaka mchaka tu - mtu anaona bora miaka mitano imalizike haraka aachane na uwaziri. hongera wabunge wa chadema kututetea sisi wananchi wanyonge.
   
 7. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hakuna kukifuta, tunataka hata marais wajao wawe wanachagua waziri Mkuu ambaye ni intelligent, na mchapa kazi mzuri kwa kujua kuwa atakuwa anawajibika kujibu maswali ya papo kwa hapo bungeni. Hivyo kama ana uwezo mdogo asipewe kazi hiyo
   
 8. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hawa wabunge wa viti maalum wanajidhalilisha sana. Mi nilidhani wanawake wakiwezeshwa wanaweza kumbe wengine wanajidhalilisha. Anataka kunufaika na ile sera ya magamba ya jikombe ukombolewe. Kuna siku niliona hoja katika tv kumbe wengine huwa wanahonga chini ya kitovu ili wapewe viti maalum
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huyu Pinda alizoea kutumiwa maswali na Hamad Rashid in advance na kuandaa majibu,
  lakini sasa hali imegeuka baada ya kuingia wabunge makini wa CDM, hivyo Pinda sasa anaona
  kiti cha moto ndiyo maana CCM wanapindisha kanuni za bunge kumuokoa PM. BTW, bado
  tunasubiri matokeo ya tuhuma za Lema kuhusu Pinda kusema uongo, mbona Makinda anakalia
  uthibitisho wa Lema. CCM mtaendeleana kulindana lakini la kuvunda halina ubani.

  Halafu wabunge kama huyo Kabati ndiyo wanatufanya watanzania tuchukie hivi vinavyoitwa
  VITI MAALUM. Dawa yenu ni katiba mpya hatutaki upuuzi tena wa viti maalumu kama wabunge
  wenyewe ndiyo hawa wa aina ya akina Kabati shame on you.

  Bunge linalo kanuni n taratibu zake, kama PM anaulizwa swali la kuzalilishwa, spika anaweza kuzuia swali
  hilo. Sasa wewe Kabati leo eti unajigeuza spika na mujibu swali? Go to hell big mama Kabati. Kwa IQ yake
  ilivyo ndogo I'm sure huna uwezo wa kuleta HOJA binafsi ya kufuta hicho kipindi unless usaidiwe na CCM
  wenzako wachache wenye akili. Lakini kabla ya kuleta hiyo hoja angalia historia ya mabunge ya jumuiya
  ya madola then utafahamu origin ya kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo. Ninafahamu hii ni
  hoja nzito ambayo Mh. kabati huwezi ku comprehense in your brain lakini tafuta msaada, ELIMU HAINA MWISHO.
   
 10. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyu dada wa Viti Maalum ovyo sana! Kanuni isitungwe na/au kuondolewa kwa ajili ya mtu fulani! Tunaweza kusema kipindi cha Maswali kwa PM kiondolewe kwa sababu ya udhaifu wa Pinda, sasa akija PM asiyelialia Bungeni ndio tuseme kwamba Kipindi kirudishwe? Tukiwa na mitazamo finyu namna hii tutafika kweli?
   
 11. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Hapo kwenye red...is it ??????
   
 12. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Awamu hii tunawabana kona zote; Kitaeleweka tuuu
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Imbombo ngafu
   
 14. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,878
  Likes Received: 2,827
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu sister naye mbona mchovu wa akili ki-hivyo?

  Yaani anapoona Pindo anashindwa kuyajibu kiufasaha maswali ya wabunge yeye anaona kuwa anadhalilishwa? Hebu atuondolee upum***v hapa! Kama Waziri wake hana uwezo wa kujibu maswali ya papo kwa papo si aachie ngazi?!!

  Wachovu wakubwa na Pindo wake!!! Au ni chakula ya wazee nini???
   
 15. N

  Ntandalilo Member

  #15
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao ndo wabunge wa vitu maalum jamani ................ crap!!
   
 16. d

  dotto JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kabati? Kabati? No. may be Kabata kawajamaa!
   
 17. Fisadi Mkuu

  Fisadi Mkuu Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B1C3D9, colspan: 3"]GENERAL[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Salutation[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Honourable[/TD]
  [TD="width: 42%, bgcolor: #E9F0F0, align: center"]Member picture
  [​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]First Name:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Ritta[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Middle Name:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Enesper[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Last Name:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Kabati[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="width: 20%, bgcolor: #E9F0F0"]Member Type:[/TD]
  [TD="width: 38%, bgcolor: #E9F0F0"]Special Seat[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Constituent:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]No Constituency[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Political Party:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]CCM[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office Location:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office Phone:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Ext.:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office Fax:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office E-mail:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Member Status:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Date of Birth[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 5"]EDUCATIONS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 35%, bgcolor: #B4C6DB"]School Name/Location[/TD]
  [TD="width: 27%, bgcolor: #B4C6DB"]Course/Degree/Award[/TD]
  [TD="width: 15%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Start Date[/TD]
  [TD="width: 13%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]End Date[/TD]
  [TD="width: 10%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Level[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]CERTIFICATIONS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Certification Name or Type[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Certification No.[/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Issued[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Expires[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]EMPLOYMENT HISTORY[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB"]Company Name[/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Position[/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]From Date[/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]To Date[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]POLITICAL EXPERIENCE[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu, width: 47%, bgcolor: #B4C6DB"]Ministry/Political Party/Location[/TD]
  [TD="class: text_menu, width: 31%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Position[/TD]
  [TD="class: text_menu, width: 12%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]From[/TD]
  [TD="class: text_menu, width: 10%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]To[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 2"]PUBLICATIONS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Description[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Published Date[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]SPECIAL SKILLS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB"]Skill Name or Description[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Years Experience[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Acquired Through[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Skill Level[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 5"]RECOGNITIONS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Recognition Type[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Recognition Date[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Reason[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Action Taken[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Issued by[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Huyu kweli ni kabati,hata CV hana
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
   
 19. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  the best post of the day.
   
 20. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mimi naweza kuamini hivyo angawa inaweza kuwa sivyo. Kwani ndo mara ya kwanza kuwa waziri mkuu leo? Ana miaka mingapi bungeni kama waziri mkuu na mara ngapi amekuwa akijibu maswali, au unataka niamini kuwa IQ ya Pinda imepungua kipindi hiki na kama ni hivyo kwa nini asiombe kupumzishwa au hakuna mbadala wake? Hapa ni kwamba amekutana na HIGH DIFINITION THINKING CAPACITY MP's kutoka upinzani na ndio maana vilaza kama huyo mama na vilaza wengine wa CCM wanaamini kuwa anadhalilishwa. Ukweli paha utabakia kuwa serikali ya CCM ni prakatumba, hakuna waziri anayejua waziri mwenzake anafanya nini, hata ndani ya wizara inawezakana waziri hajui katibu wake anafanya nini, ukienda kuuliza takwimu, waulize kila mtu kivyake na kila mtu atakujibu kivyake, sembuse Pinda atajua nini kinaendelea kwenye wizara hizo! Laiti Pinda angekuwa na information za kutosha kutoka kwenye wizara zake asingekuwa anababaika vile, na ndio maana anaamua kujibu jinsi anavyojua yeye bila kuwa na takwimu kutoka kwa mawaziri wake.
   
Loading...