Mnyika ambana Kikwete nyumbani kwake

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA John Mnyika amembana Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwake Bagamoyo kuhusu utekelezaji wa ahadi za CCM za maisha bora kwa kila mtanzania, wanawake kuwezeshwa na ajira kwa vijana.

Mnyika alifanya hivyo wakati akimnadi mgombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA katika kata ya Magomeni kwenye halmashauri ya Bagamoyo ambapo alisema kwamba badala ya maisha bora wananchi wana maisha magumu kutokana na kasi ya mfumuko wa bei huku ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wa kike na wa kiume ukizidi kuongezeka.

Mnyika amewaomba wananchi kuchagua CHADEMA ili kazi ya kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za taifa kwa sera mbadala iendelee katika halmashauri hiyo ya Bagamoyo yenye tuhuma mbalimbali ambayo madiwani wake wote ni wa CCM.

Mara baada ya mkutano huo wananchi walimsindikiza Mnyika kwa miguu toka kata hiyo ya Magomeni mpaka ofisi za chama hicho za wilaya umbali mrefu kutoka mkutano uliopita ambapo mratibu wa kampeni za CHADEMA katika kata hiyo alitahadharisha rushwa iliyoanza kusambazwa na CCM katika kata hiyo.
serayamajimbo

Kasi ya mfumuko wa bei anao usema mnyika ni upi ? mfumuko wa bei umetoka 19% mpaka sasa 13% , kasi hiyo iko wapi? au yeye hesabu zake anahesabu kinyume nyume? kijana mnyika acha kujitafutia umaarufu wa kisiasa kwa cheap politics
 
Kikwete alikabidhiwa uchumi wenye mfumuko wa bei wa asilimia 4.9 tu. Ameupandisha kwa uongozi mbovu mpaka umefika asilimia 19. Hata kama umeshuka kidogo hadi asilimia 13 bado ameharibu sana. Unataka tumsifu?
 
Ukisoma michango mingine ya Pro-Chadema JF unabaki kucheka tu, hivi Mnyika ana uwezo gani wa kumbana Jk, wameshindwa viongozi wake Dr Slaa na Mbowe, Mnyika ndio ataweza endeleeni kujifariji na kujiliwadha.

Uzuri hata Jk anakitambua hicho kichwa.
 
Unajua kwenye siasa Kila mtu anajaribu kufanya kitu ambacho aliwahi kudream, always MNyika amekuwa role model kwa vijana wengi waipendao nchi yetu, i like his ideas and his revolutionary mind set na nafikiri tuachane na mambo ya itikadi, sijawahi sikia kijana toka UVCCM akiongelea positive ideas za Kujenga nchi yetu zaidi ya majungu na kejeli. In the past Zitto Alitokea kuwa kijana mwenye positive and constructive ideas, ila sijui kimetokea nini hapa katikati. Lakini nafikiri siasa zina kipindi especially kwa new emerging individuals, hasa wale ambao baba zao hawakuwahi kuwa viongozi wa nchi hii. But I would say, let them fullfil their dreams, we will support and endorse them as youths. God Bless all.
 
Pamoja na mnyika lakini makamanda wengine inabidi wawepo na kuhamasisha kwa nguvu maeneo hayo
 
hivi hao watu wa bagamoyo wana akili kweli?? miaka nenda rudi wapo nyumaaaaaaa, halafu bado watakiweka chama cha ccm mbele!! watu wengine unatamani uwahamishe wahamie somalia au southern sudan!!
 
hivi najiuliza kwani kumnadi mgombea wa udiwan kwenye kata ya raisi ni ishu kubwa sana hadi ionekane kwamba mnyika kafanya jipya?
 
ubungo imemshinda,kero kibao za maji na barabara anaenda kujidhalilisha bagamoyo
 
hivi hao watu wa bagamoyo wana akili kweli?? miaka nenda rudi wapo nyumaaaaaaa, halafu bado watakiweka chama cha ccm mbele!! watu wengine unatamani uwahamishe wahamie somalia au southern sudan!!

hata watu wa huko kwenu hamna akili kwa kuchagua wazinifu na disko joka
 
Ukisoma michango mingine ya Pro-Chadema JF unabaki kucheka tu, hivi Mnyika ana uwezo gani wa kumbana Jk, wameshindwa viongozi wake Dr Slaa na Mbowe, Mnyika ndio ataweza endeleeni kujifariji na kujiliwadha.

Ni heri Dr Slaa awe Rais kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge by Dr 1,Dr 2,Dr 3,Kikwete.
 
Khaa!..
Kuna wakumshindwa Dhaifu?..
Watu wanamuonea huruma tu asije akajifia hata kabla ya kumaliza muda wake,ngoja aendelee kubwabwaja tu maneno na watu kama nyie ambao mnachukua za kwake tu hamchanganyi na zenu mnaona naye kiongozi,yule msanii tu,full kuuza sura,shit!..........
Ukisoma michango mingine ya Pro-Chadema JF unabaki kucheka tu, hivi Mnyika ana uwezo gani wa kumbana Jk, wameshindwa viongozi wake Dr Slaa na Mbowe, Mnyika ndio ataweza endeleeni kujifariji na kujiliwadha.
 
Ukisoma michango mingine ya Pro-Chadema JF unabaki kucheka tu, hivi Mnyika ana uwezo gani wa kumbana Jk, wameshindwa viongozi wake Dr Slaa na Mbowe, Mnyika ndio ataweza endeleeni kujifariji na kujiliwadha.
weweseka na ccm yako,imebakia history
 
pro-chadema = pro-uamsho
ndio maana viongozi na wafuasi wao huishia rumande..

pro ccm always ni wajinga wasiokubali mabadiliko akili zao mgando wako tayari waendelee kulala na njaa wao na watoto wao wakati jumuia zote zikishikwa na watoto wa vigogo
 
Back
Top Bottom